ZANZIBAR – Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeipongeza Benki ya NMB kwa kusaini mkataba mnono wa udhamini wa Mashindano ya Mapinduzi Cup, hatua iliyobadili rasmi jina la mashindano hayo na sasa kuitwa NMB Mapinduzi Cup.
Udhamini huo unaanza rasmi na mashindano ya NMB Mapinduzi Cup 2026, yatakayoshirikisha timu 10 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Uganda.
Timu Zitakazoshiriki NMB Mapinduzi Cup 2026
Mashindano hayo yatashirikisha:
- Tanzania Bara: Yanga, Simba SC, Azam FC, Singida Black Stars na TRA United
- Zanzibar: Mlandege, KVZ, Fufuni FC na Muembe Makumbi City
- Timu mwalikwa: URA FC ya Uganda
Michuano hiyo inatarajiwa kufikia tamati Januari 13, siku moja baada ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
SMZ Yasifu Uzalendo na Ushirikiano wa NMB
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wa SMZ, Riziki Pembe Juma, aliishukuru Benki ya NMB kwa kuyapa hadhi na thamani mashindano hayo, akieleza kuwa udhamini huo ni kielelezo cha uzalendo na ushirikiano wa kweli kati ya sekta binafsi na Serikali.
Alisema mkataba huo ni muendelezo wa ushirikiano uliodumu kwa muda mrefu kati ya NMB na SMZ, huku Serikali ikiahidi kuudumisha kwa manufaa ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla.
“NMB mmetuonesha uzalendo mkubwa kwa kukubali kusaini mkataba huu kwa niaba ya Serikali. Udhamini huu si tu kubadili taswira ya mashindano, bali ni mkubwa na mnono zaidi kuwahi kutolewa,” alisema Waziri Pembe.
Aliongeza kuwa hata tuzo za Fair Play kwa wachezaji zitakazotolewa katika hatua mbalimbali za mashindano zinaonesha dhamira ya NMB ya kuyaimarisha na kuyaongezea mvuto mashindano hayo.
.jpeg)



.jpeg)




.jpeg)


.jpeg)












.jpeg)






.jpeg)



.jpeg)
.jpeg)