Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 30 November 2020

KIVUMBI CHA #EPL BADO KINAENDELEA LEO USIKU NDANI YA DStv


Kivumbi cha #EPL⚽⚽ bado kinaendelea usiku leo ndani ya DStv, hakikisha unalipia kifurushi chako cha Compact TShs 49,000 kwa kupiga *150*53#  tu uweze kutazama mechi hizi au 0659 07 07 07 kujiunga kwa gharama nafuu TShs 79,000 tu upate kifurushi cha Family mwezi mmoja bure.

#VibeLaSikukuunaDStv

#SokaLisilopimika

TIGO YAENDELEA KUKABIDHI ZAWADI ZA SIMU KWA WASHINDI MBALIMBALI WA #JazaTukujazeTena

TunakabidhiTena: Tigo yaendelea kukabidhi zawadi za Simu kwa washindi mbalimbali wa #JazaTukujazeTena ambapo wateja hujishindia pia bonus za dakika, MB na SMS na kubwa zaidi kupata Simu Janja.

"Bado tunaendelea kutoa simu kwa wateja wetu ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kuwa pamoja nasi katika kipindi chote. Wanachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi wapate bonus na zaidi wanaingia kwenye droo ambapo wanaweza kushinda simu janja mbalimbali" Joseph Mutalemwa-Mkurugenzi wa Tigo kanda ya pwani. @jotiofficial


"Mbali na Bonus wanazojipatia wateja wetu kila siku pindi wakijiunga kifurushi pia wanajiwekea nafasi ya kushinda simu janja ikiwemo Samsung Note 20 yenye thamani ya zaidi ya milioni 2" Joseph Mutalemwa - Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani.
Amani Adami kutoka Kiwalani Dar es salaam ndiye mshindi wa Samsung Note 20. Mshindi mmoja kati ya watatu wa wiku hii. Ukiwa na Tigo wewe ni mshindi.

Nunua kifurushi chochote na Tigo itakupa Bonus za Dakika, SMS na Mb's na kubwa zaidi utajiwekea nafasi ya kushinda smartphone kila siku. #ItelT20 #TecnoKitochi4G kumi kila siku na #SamsungNote20 Tatu kila wiki. Joseph Mutalemwa - Mkurigenzi wa Tigo kanda ya Pwani pamoja na @jotiofficial wakimkabidhi simu.
"Huu mzigo ukiibiwa huu lazima uweke msiba huu maana ni balaa, bei yake ni balaa" @jotiofficial

Ukinunua kifurushi Tigo unapata Bonus za Dakika, SMS na MB's na zaidi unajiwekea nafasi ya kushinda smartphone #ItelT20 #TecnoKitochi4G kumi kila siku na #SamsungNote20 tatu kila wiki.
#JazaTukujazeTena

Mama Kashinda! Hongera wewe ni mmoja wa washindi wa Itel T20 wiki hii @jotiofficial Bado wengine Wengi.

Nunua kifurushi chochote na Tigo itakupa Bonus za Dakika, SMS na Mb's na kubwa zaidi utajiwekea nafasi ya kushinda smartphone kila siku. #ItelT20 #TecnoKitochi4G kumi kila siku na #SamsungNote20 Tatu kila wiki.

BURE: Ukinunua kifurushi kutoka Tigo unapata Bonus ya MB, SMS au Dakika na zaidi unapata Burudani kali kutoka kwa wasanii kibao kwenye tamasha la Wasafi Tumewasha na Tigo kesho uwanja wa Taifa-Kahama.

Piga *147*00# kujiunga. @wasafitv

#TumewashaNaTigo

#JazaTukujazeTena

AIRLINK YAZINDUA SAFARI MPYA DAR - JOHANNESBURG

Airlink ikiwa imepaki uwanja wa ndege wa O.R Thambo Afrika Kusini.
Muonekano wa ndani wa ndege ya Airlink.
Huduma ya chakula.
Huduma ya vinywaji.

Kampuni ya ndege ya Airlink imezindua safari mpya za ndege kutoka Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini Desemba mosi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Rodger Foster alisema wameanzisha huduma mpya kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini ili kukuza fursa za kiuchumi.

"Airlink ina furaha kuanzisha huduma za moja kwa moja za ndege zetu ili kukuza biashara na utalii kwa kuwa sehemu hizi mbili zinafanana kwa namna moja ama nyingine katika mambo hayo," alisema.

PRESIDENT MWINYI CALLS FOR GOVERNMENT, FINANCIAL INSTITUTIONS PARTNERSHIP

Zanzibar president, Dr. Hussein Ali Mwinyi, exchanges views with CRDB Bank Chief Executive Officer, Abdulmajid Nsekela (right) during a seminar organised by CRDB Bank for government officials and members of the House of Representatives held at Verde Hotel in the Isles on Sunday. Looking on is Zanzibar Second Vice-President, Hemed Suleiman Abdallah. 

 President of Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi, has called on financial institutions and local development partners to work with the government to bring about significant change for the benefit of the people.

President Mwinyi was speaking during a special seminar organised by CRDB Bank to highlight various opportunities offered by the bank and discuss how best to work together between the government and the lender in achieving development projects in the country and move banking services closer to citizens to stimulate economic growth.

Continue Reading > > > 

STANDARD CHARTERED BANK, SANLAM LAUNCH BANCASSURANCE PRODUCTS

Standard Chartered Bank Chief Executive Officer (CEO), Sanjay Rughani (centre) shares thoughts on the importance of insuring property and services in Dar es Salaam over the weekend. Second right is SANLAM Tanzania CEO, Hamis Suleiman and their Chief Operating Officer, Geofrey Masige (right). Second left is the Bank's Head of Retail Banking, Ajmair Riyaz and Head of Corporate Affairs, Brand & Marketing, Juanita Mramba. 
Standard Chartered Bank in partnership with SANLAM Tanzania, has launched a suite of bancassurance products covering property and motor insurance.

The joint business venture aims at serving customers who want to widen the scope of insurance service penetration that ensures the security and safety of their properties and motor vehicles.

Continue Reading > > >  

BENKI YA NMB TAASISI KINARA KUSAIDIA JAMII ELIMU NA AFYA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala - Ng'wilabuzu Ludigija (kulia), akikabidhi cheti cha shukrani kwa Benki ya NMB, Meneja Mwandamizi Idara ya Biashara za Serikali wa NMB - Adelard Mang'ombo (kushoto), kama mmoja wa wadau walipa kodi wakati wa Siku ya Mlipa Kodi katika Manispaa ya Ilala.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala - Ng'wilabuzu Ludigija (kulia), akizungumza na Meneja Mwandamizi Idara ya Biashara za Serikali wa NMB - Adelard Mang'ombo baada ya kukabidhiwa cheti cha shukrani kwa Benki ya NMB kwa mmoja wa wadau walipa kodi wakati wa Siku ya Mlipa Kodi katika Manispaa ya Ilala. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Uhusiano Biashara na Serikali wa NMB - Amanda Feruzi na Meneja Mauzo ya Kidijitali - Hezbon Mpate.

Benki ya NMB imetajwa kuwa taasisi kinara ya kifedha katika Manispaa ya Ilala mkoani Dar es salaam inayotumia kiasi kikubwa cha pato lake kuisaidia jamii katika Nyanja za Elimu na Afya kupitia Mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Kupitia mpango huo Benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kati ya taasisi nyingi za fedha kwenye mkoa huo, ambayo imekuwa ikishirikiana na serikali kuhakikisha huduma bora za kiafya na elimu zinapatika kwa wananchi.

Hatua hiyo ilipelekea Manispaa hiyo kuipatia Benki hiyo cheti cha Pongezi, kwenye hafla ya kufunga kongamano la siku ya mlipakodi lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika hafla hiyo, Manispaa ya Ilala ilikabidhi vyeti kwa taasisi, mashirika, makampuni na wafanyabiashara 100 Bora wa Ulipaji Kodi Bila Shuruti, huku NMB ikipongezwa na kutunukiwa kama Kinara wa matumizi ya pato lake katika kusaidia jamii.

Sunday 29 November 2020

TANZANIA CONSUMER CHOICE AWARDS 2020 EXCLUSIVE VVIP EVENT - SUNDAY, 13 DECEMBER 2020












 

UBALOZI WA TANZANIA AFRIKA KUSINI WAPEWA CHANGAMOTO YA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI, SIASA

Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiwatambulisha baadhi ya wafanyakazi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ibuge wakati alipowasili Ubalozini tarehe 27 Novemba 2020.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisaini kitabu cha wageni katika Ubalozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini tarehe 27 Novemba 2020.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisisitiza jambo kwa watumishi (hawapo pichani) wakati wa mkutano.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akiendesha kikao na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akimuonesha baadhi ya mali Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi wakati alipokuwa anakagua mali za Serikali Ubalozini.

Na Nelson Kessy, Pretoria

Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini wapewa changamoto ya kuhakikisha kuwa unatekeleza Diplomasia ya Uchumi pamoja na Diplomasia ya Siasa iliyopo ndani ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM (2020-2025).

Changamoto hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge wakati alipotembelea Ubalozi huo jijini Pretoria nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujionea utendaji kazi wa Ubalozi na mali za Serikali nchini humo.  

Balozi Ibuge ameutaka Ubalozi huo kuhakikisha kuwa unatekeleza diplomasia ya uchumi pamoja na diplomasia ya siasa kwa weledi ili kuleta manufaa ya Taifa.

"Nawapongeza kwa utendaji kazi wenu na nawasihi muendelee kujituma katika kazi (proactive) katika kuwapata wawekezaji na kutengeneza kuwa ni sehemu ya mfumo wa kuleta mabadiliko ambayo Serikali imeyapanga kupitia Ilani ya CCM ya 2020-2025," Amesema Balozi Ibuge.

Saturday 28 November 2020

SADC-TROIKA, UN KUBORESHA MFUMO WA USALAMA NDANI YA DRC

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa Mataifa kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji uliofanyika Tarehe 27, Novemba 2020, mjini Gaborone Botswana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa Mataifa kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji uliofanyika Tarehe 27, Novemba 2020, mjini Gaborone Botswana
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa Mataifa kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji uliofanyika Tarehe 27, Novemba 2020, mjini Gaborone Botswana.

Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) zimekubaliana kuboresha mfumo utakao weka ulinzi bora na usalama ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akithibitisha kuhusu mashirikiano ya mfumo wa kuimarisha ulinzi na usalama nchini DRC, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amemuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika mkutano huo amesema kuwa kamati ya utatu inayoshughulika na usalama ndani ya jumuiya ya SADC imekutana kwa dharura ili kuweza kuangalia namna ya kukabiliana na matishio ya ugaidi yanayotishia sana hali ya amani na usalama katika nchi zilizopo ukanda wa SADC ikiwemo Msumbiji, Congo DRC na Tanzania.

Friday 27 November 2020

TANZANIA CONSUMER CHOICE AWARDS 2020 EXCLUSIVE VVIP EVENT - SUNDAY, 13 DECEMBER 2020



ASSOCIATION OF TANZANIA EMPLOYERS ORGANISES A MEETING OF FEMALE FUTURE ALUMNI NETWORK MEMBERS

John Ulanga (first right), Trade Mark East Africa's representative in Tanzania, addresses a meeting of Female Future Alumni Network members organised by the Association of Tanzania Employers (ATE) in Dar es Salaam yesterday. With him (from left) are Peter Ulanga, a Consultant on Technology; ICT Entrepreneur Cynthia Bavo and Digital Advisor Kai Mollel. ATE and the Confederation of Norwegian Enterprises launched the network last year as a Professional Networking and Mentorship platform for career women in Tanzania advocating for gender sensitivity in various aspects of business environments which excessively affect the performance and effectiveness of businesses.

7 TRILLION TO LIFT ZANZIBAR BLUE ECONOMY

 

Zanzibar - Zanzibar based Salmin Fisheries Limited has secured 3bn US Dollar (about 7 trillion Shillings) business partnership in the construction of fish processing industries and a fish landing port.

Salmin Fisheries Executive Director, Dr. Salmin Ibrahim said here yesterday that Turkish Northland Capital Investments is willing to invest the amount in the ambitious projects under the Government spearheaded Blue Economy.

The indigenous fishing firm and Equity Bank have teamed up under a strategic programme to support small-scale fisheries through training, financing and marketing.

Continue Reading > > >

KCB GROUP SIGNS DEAL TO BUY TWO BANKS IN RWANDA, TANZANIA

KCB Group CEO Joshua Oigara.

KCB Group has signed a deal with London-listed financial services firm Atlas Mara Limited to buy stakes in it's banking units in Rwanda and Tanzania, its chief executive Joshua Oigara announced on Thursday.

The proposed transaction will see Kenya’s biggest lender by assets acquire Banque Populaire du Rwanda Plc (BPR) and the African Banking Corporation Tanzania (BancABC), strengthening its business in the two countries.

Under the proposed deal KCB will the acquire a 62.06 per cent stake in Banque Populaire du Rwanda Plc and a 100 per cent stake in African Banking Corporation Tanzania.

The transaction is subject to obtaining shareholder and regulatory approvals in Rwanda and Tanzania.

In a statement, Mr Oigara said the transaction is part of KCB’s "ongoing strategy to explore opportunities for new growth while investing in and maximising returns from the Group’s existing businesses."

The acquisition, he added, will buttress the Group’s leadership position and give it a stronger edge to play a bigger role in driving the financial inclusion agenda in the East African region while building a robust and financially sustainable organization.

The East African

KAA MKAO WA PIRA BIRIANI WIKIENDI HII KUTAZAMA MICHUANO YA EPL NDANI YA DStv


 

Kaa mkao wa Pira Biriani Wikiendi hii kutazama michuano ya EPL ndani ya Bomba kwa TShs 19,900 tu.

Man City na Burnley

Arsenal Vs Wolves

Piga sasa *150*53# kulipia kifurushi cha Bomba TShs 19,900 tu utazame michuano hii Live.

Kupitia Vibe La Sikukuu na DStv kama DStv, piga 0659 07 07 07 kujiunga kwa TShs 79,000 tu na upate ofa ya kifurushi cha Family.

MAKATIBU WAKUU SADC - TROIKA WAKUTANA KUJADILI SIASA NA USALAMA

Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA wamekutana na kujadiliana Mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani ya SADC mjini Gaborone, Botswana.

Awali, Mkutano wa Makatibu Wakuu ulifunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Bw. Gaeimelwe Goitsemang ambae pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.

Ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kukutana ana kwa ana tangu ulipotokea ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (Covid-19).

Kwa upande wa Makatibu wakuu waliohudhuria katika Mkutano huo kutoka Tanzania ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.

Mkutano wa Makatibu Wakuu utafuatiwa na Mkutano wa Dharua wa Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama baadae mjini Gaborone.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ukifuatilia Mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA uliofanyika mjini Gaborone, Botswana.
Mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA ukiendelea.
Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ngazi ya Makatibu Wakuu ukifuatilia mkutano.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiwasilisha mada katika Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya ushirikiano katika siasa, ulinzi na Usalama unaondelea Mjini Gaborone, Botswana.

MAWAZIRI SADC - TROIKA WAKUTANA KWA DHARURA BOTSWANA

Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama wakutana katika mkutano wa dharura na kujadili masuala ya siasa, ulinzi na usalama.

Mkutano huo umefanyika jana mjini Gaborone, Botswana ambapo ulitanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ulioanza asubuhi na kumalizika mchana.

Kupitia mkutano huo, mawaziri wameweza kujadili masuala ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC na kupendekeza njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwenye siasa, ulinzi na usalama ndani ya ukanda wa SADC.

Pamoja na mambo mengine, Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama inawajibika kukuza amani na usalama katika eneo la SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo kuhusu mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (mwenye tai nyekundu) akifuatilia mkutano wa dharura wa baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama uliofanyika Mjini Gaborone. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ukiwa ukiimba wimbo wa SADC kabla ya kuanza kwa mkutano wa dharura wa baraza la Mawaziri.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana Dkt. Lemogang Kwape akifungua mkutano wa Dharura wa baraza la mawaziri, kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kumaliza mkutano wao.