Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 31 August 2021

KAMPUNI YA BIA YA AFRIKA MASHARIKI (EABL) KUPITIA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI (SBL) YAZINDUA REPOTI YA UWEKEZAJI WAKE KWA JAMII 2020

Uongozi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ukiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Balozi wa Uingereza hapa nchini Rick Shearn (wa tatu kulia) muda mfupi baada ya uzinduzi wa ripori ya uwekezaji kwa jamii wa kampuni hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya uwekezaji kwa jamii wa kampuni hiyo uliyofanyika wajijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya SBL John Ulanga (wa pili kulia), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga (wa tatu kulia) muda mfupi baada ya uzinduzi wa ripoti ya uwekezaji kwa jamii ya SBL (Sustainability Report). Kulia ni Deputy British High Commissioner to Tanzania Rick Shearn na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti, Mark Ocitti.

Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) leo imezindua ripoti inayoelezea uwekezaji wake kwa jamii. Ripoti hiyo ya mwaka 2020, inaelezea kwa undani uwekezaji ambao kampuni hiyo imeufanya kwa jamii katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania ambako inafanya biashara zake.

Kwa Tanzania miradi ya uwekezaji kwa jamii inatekelezwa na kampuni tanzu ya EABL, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL). Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, programu ya kilimo biashara inayowasaidia wakulima wazawa, unywaji wa kistarabu, programu za ujumuifu pamoja na utunzaji wa mazingira kupitia kupanda miti. Miradi hiyo inatekelezwa chini ya mpango wa kusaidia jamii unakwenda mpaka 2030.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti alielezea baadhi ya miradi inayotekelezwa na kampuni hiyo akianza na miradi ya kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama ambapo alisema SBL imeweza kuwafikishia huduma hiyo muhimu Watanzania milioni mbili ikilenga kurudisha kila tone inalotumia katika uzalishaji wa bidhaa zake. SBL imetekeleza miradi 21 ya maji hapa nchini tangu mwaka 2010.

Monday 30 August 2021

KAA MKAO WA KULA KUPITIA DStv #ZiGo

 

Kaa mkao wa kula kupitia @dstvtanzania pekee...

#ZiGo

RAIS SAMIA APONGEZA JITIHADA ZA BENKI YA CRDB KUCHANGIA MAENDELEO KATIKA JAMII

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akikata utepe kuzindua Afisi ya Maendeleo kata ya Kizimkazi Dimbani na nyumba mbili za madaktari zilizonjengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB na kugharimu shilingi milioni 300. Wengine pichani ni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Haroun Ali Suleiman (watatu kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid (wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kulia) na Mwenyekiti wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (wakwanza kulia).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (watatu kulia) akikata utepe kuzindua Afisi ya Maendeleo kata ya Kizimkazi Dimbani na nyumba mbili za madaktari zilizonjengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB na kugharimu shilingi milioni 300. Wengine pichani ni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Haroun Ali Suleiman (wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid (wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay (watatu kushoto), Mwenyekiti wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (watatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wanne kushoto).

Zanzibar, 28 Agosti 2021 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kuchangia maendeleo katika jamii. Rais Samia ametoa pongezi hizo wakati wa kilele cha Tamasha la Kizimkazi alipokuwa akikabidhiwa miradi ya nyumba za madaktari na ofisi za shehia Kizimkazi Dimbani zilizojengwa kwa udhamini wa Benki hiyo.

Akipokea miradi hiyo iliyo gharimu kiasi cha shilingi milioni 300, Rais Samia alisema Serikali inajivunia ushirikiano wa kimaendeleo baina yake na Benki ya CRDB. Aliongezea kuwa Benki hiyo imekuwa mfano mzuri wa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma (PPP) katika kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Maendeleo ya 2025.


“Suala la kuijenga nchi yetu ni wajibu wa kila mmoja wetu na si la Serikali peke yake, niwapongeze Benki ya CRDB kwa kujitoa kwenu kutatua changamoto zilizopo katika jamii. Leo hii mmetutoa kimasomaso kwa kutusaidia kuimarisha sekta ya afya na kuhakikisha wananchi wa Kizimkazi Dimbani wanapata huduma bora za kijamii, ama hakika hii ni Benki ya kizalendo,” alisema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia alisifu mafanikio ya Tamasha la Kizimkazi kwa mwaka huu 2021 ambalo lililenga katika kuhamasisha jamii kudumisha utamaduni na kuongeza ujumuishaji wa kiuchumi kwa wananchi kwa kuonyesha fursa mbalimbali zitokanazo na tamaduni za Kitanzania. Tamasha hilo lilihusisha mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 500 juu ya ubunifu wa bidhaa za asili, elimu ya fedha na uendeshaji biashara, pamoja na michezo mbalimbali ya asili.


Pia alieleza kwamba wakati umewadia kwa Watanzania kuacha utamaduni wa kigeni na kujivunia utamaduni wetu. Alitoa rai kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa na mikakati mbalimbali itakayosaidia kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania. Rais Samia alisema jamii pia ina wajibu wa kushiriki kikamilifu katika matamasha ya utamaduni ili kusaidia ukuzaji na uendelezaji wa mfumo wa utamaduni na sanaa katika jamii ya Kitanzania.

“Benki ya CRDB imetuonyesha kwa mfano kuwa tukiwekeza katika utamaduni wetu tutafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa kutengeneza soko kwa bidhaa zetu za asili na Sanaa yetu. Kupitia Tamasha hili la Kizimkazi niiombe Wizara iweke mikakati ya kuanzisha matamasha ya utamaduni katika kila kanda hii itasaidia kukuza tamaduni za maeneo mbalimbali na kuchochea utalii,” alisisitiza Rais Samia.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamjaid Nsekela alisema utekelezaji wa miradi hiyo na uandaaji wa Tamasha hilo la Kizimkazi ambalo zamani lilikuwa likijulikana kama “Kizimkazi Day,” ni muendelezo wa utekelezaji wa Sera ya Benki hiyo ya uwekezaji katika jamii ambayo inaelekeza asilimia 1 ya faida ya Benki kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii kupitia program bunifu za uwezeshaji.

Nsekela alisema Benki hiyo imedhamiria kwa dhati kusaidiana na Serikali kujenga uchumi jumuishi na kuwa utamaduni ni moja ya eneo ambalo Taifa likiwekeza vizuri linaweza kusaidia kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Pato la Taifa kwa ujumla. “Pamoja na vijielezi vingi vya neno utamaduni, sisi Kama Benki ya kizalendo tunaamini kuwa; utamaduni ni ujasiriamali, utamaduni ni utalii, utamaduni ni ajira, utamaduni ni uchumi.”


Aidha Nsekela alibainisha kuwa Benki hiyo imedhamiria kuweka mchango wake katika pande zote za Muungano na hivyo kuchochea maendeleo ya Taifa. Akielezea mchango wa Benki hiyo katika kukuza uchumi wa visiwa vya Zanzibar, Nsekela alisema katika nusu mwaka 2021 pekee Benki ya CRDB imetoa zaidi ya shilingi bilioni 150 kuwezesha sekta mbalimbali za maendeleo ili kuwezesha ajenda ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Buluu.

Alimwambia Mheshimiwa Rais, Benki hiyo pia inajivunia zaidi kuleta mapinduzi makubwa katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mwaka 2014 Benki ya CRDB iliunganisha mfumo wake wa kielekroniki wa ukusanyaji mapato na mfumo wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, ambapo ndani ya mwaka mmoja tu makusanyo yaliongezeka kwa zaidi 600%,” aliongezea.


Nsekela alimuahidi Mheshimiwa Rais kuwa Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya “Tupo Tayari” itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendelo nchini ili kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.

Pamoja na mafunzo ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na Benki ya CRDB, Tamasha la Kizimkazi pia lilijumuisha usafi wa mazingira, mashindano ya michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na pete, kufua na kukuna nazi, nage, karata , bao, kuvuta kamba, resi za baskeli, resi za ngalawa, shomooo , na mashindano ya kuhifadhi Qurani.

Wananchi pia walipata fursa ya kupata chanjo ya UVIKO 19 ambayo itatolewa katika viwaja vya Kizimkazi Dimbani Mji Mpya, zoezi ambalo liliongozwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Ahmed Nassor Mazrui.

Kilele cha Tamasha la Kizimkazi kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiwa kwenye sherehe hizo.
 

Friday 27 August 2021

FULL TANK INAKUHUSU - LIPA KWA NMB MASTERCARD / QR UPATE PUNGUZO LA 15% KWENYE MAFUTA

TAZAMA MECHI YA ATLETICO MADRID DHIDI YA VILLARREAL NDANI YA DStv JUMAPILI HII



Biriani la Kandanda ndani ya Bomba, Jumapili hii ungana na @georgeambangile kutazama mechi ya Atletico Madrid dhidi ya Villarreal kupitia SuperSport 224 ndani ya @dstvtanzania pekee.

Lipia mapema kifurushi chako TShs 19,900 tu kwa kupiga *150*53#

#Birianiiendelee

THERE IS NEVER GOING TO BE ENOUGH MONEY TO SAVE


By Godwin Semunyu
  • Need to inculcate savings culture
I just finished reading a memoir by former President Ally Hassan Mwinyi, "Mzee Ruksa, Safari ya Maisha Yangu." Probably the best narrated Swahili biography of all time. In the book, Mzee Mwinyi discloses how he learned the saving culture from an early age through his late grandfather, Nzasa.

He says, during harvest season, when everyone was busy partying and plummeting the harvests, Nzasa would carefully stock the family harvest, ready to sell at higher prices during drought or in exchange for labor. That mentality, he says, has guided him through his entire life (he just turned 96 years), so much so that he has never borrowed money from anyone, thanks to self-discipline in savings and avoiding unnecessary expenditures.

In Tanzania, we are slowly becoming a nation of spenders rather than savers. The savings to income ratio is lower as the social norm is spending to achieve a particular lifestyle or status, regardless of income. The price tags and brands are essentials, irrespective of income.

JENGA HUB TEAMS UP WITH 'KIDS FINANCE WITH TRACY' TO LAUNCH DIGITAL AND ENTREPRENEURSHIP BOOTCAMP FOR CHILDREN

Nancy Sumari, CEO of Jenga Hub signs a memorandum of understanding with Kids Finance with Tracy, Tracy Rabi, (2nd to the right). Gertrude Mligo, Founder of Natokaje kidigitali (3rd to the right) and Lilian Makoi, CEO of Mipango App.

Dar es Salaam, 25.08.2021 – Kids Finance with Tracy a business founded by an 11 year old girl, Tracy Rabi has today signed a Memorandum of Understanding with Ms Nancy Sumari, former Miss Tanzania and Founder of Jenga Hub to empower Tanzanian children with Digital, Entrepreneurship and Finance education.

The partnership also includes, Natokaje Kidigitali, founded by Getrude Mligo. Natokaje kidigitali has linked children of age 8-17 with successful local businessman, Mohammed Dewji and digital legends like Gillsant Mlaseko. Giving children the opportunity to learn from the finest talent in the country.

Ms Sumari has been running a successful hub that has for over 3 years now has helped children experiment with technology through coding classes, animation classes and more.

A 11year old, Tracy Rabi not only writes financial and entrepreneurship books for children, but also founded The Tanzania Youth Entrepreneurship Experience Fair that brings together children with entrepreneurship projects to showcase and sell their products to other children, as an avenue for children to experiment and practically learn entrepreneurship skills from a young age.

SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 118 KUNUSURU KAYA MASIKINI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg wakisaini Hati ya makuliano ya msaada wa SEK milioni 450 sawa na sh. bilioni 118 za Tanzania zilizotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia Mfuko wa TASAF, katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg wakiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) Hati ya makuliano ya msaada wa SEK milioni 450 sawa na sh. bilioni 118 za Tanzania zilizotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya kusaidia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia Mfuko wa TASAF, katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg wakipongezana baada ya kusaini Hati ya makuliano ya msaada wa SEK milioni 450 sawa na sh. bilioni 118 za Tanzania zilizotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya kusaidia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia Mfuko wa TASAF, katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Serikali ya Sweden imeipatia Tanzania msaada wa sarafu ya nchi hiyo (SEK) milioni 450 sawa na shilingi bilioni 118 za kitanzania kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

Hati za makubaliano ya msaada huo zimetiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mheshimiwa Anders Sjöberg.

“Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili ulianza kutekelezwa mwaka 2020 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2023, umepangiwa kutekelezwa kwa gharama ya dola za Marekani milioni 883.3 sawa na shilingi trilioni 2.02 na Sweden imesaidia jumla ya dola na Marekani milioni 237 sawa na shilingi bilioni 542.2” alisema Bw. Tutuba.

Alisema kuwa mradi huo umelenga kuongeza fursa za kiuchumi na kijamii kwa kaya za walengwa pamoja na kulinda na kuimarisha rasilimali watu kwa kutoa ruzuku kwa kaya zilizoko kwenye mpango huo.

“Hadi kufikia Desemba 2020 zaidi ya kaya milioni 1 zilihakikiwa Tanzania Bara na Zanzibar na kuingizwa katika mpango huo huku kaya 56,800 kazi ya kuzihakiki inaendelea ili nazo ziweze kuingizwa kwenye mpango huo ulioonesha mafanikio makubwa” alisema Bw. Tutuba

NMB YATOA MSAADA WA MILIONI 54 ZANZIBAR NA KUDHAMINI KIKAO KAZI CHA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja - Hadidi Rashid Hadidi, msaada wa vitanda vya hospitali vilivyotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya hospitali za Mkoa Kusini Unguja huko Binguni.
Watendaji wa Benki ya NMB, wakiwa katika picha wa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Binguni baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa vifaa vya kuezekea shule hiyo huko Binguni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Aikansia Muro (mwenye koti ya bluu) mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Jeshi la Polisi cha Mwaka, kilichofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB ilikua mdhamini Mkuu wa kikao hicho.

Katika kuhakikisha shamra shamra za Siku ya Kizimkazi visiwani Zanzibar zinafana, Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya hospitali na shule vyenye thamani ya Shilingi Milioni 54 ili kuwapa tabasamu wakazi wa Kizimkazi katika kipindi hiki.

NMB imetoa jumla ya vitanda 42 ambapo kati ya hivyo vipo vya kujifungulia, vya kufanyia uchunguzi na vya kulalia wagonjwa wodini; vilivyoenda katika Vituo vya Afya saba ikiwemo Bumbwini, Walezo Jeshini, Kizimbani, Chuini, Mwera, Chwaka na Unguja Ukuu pamoja na mabati yaliopelekwa kukamilisha ujenzi wa madarasa ya shule za Kizimkazi, Makunduchi na Binguni zilizopo mkoa wa Kusini na Shule za Mbuzini na Mtoni Kigomeni za Mjini Magharibi.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara za Kati wa NMB, Filbert Mponzi alisema kuwa NMB imekuwa ikitenga sehemu ya faida na kuirudisha kwa jamii huku akibainisha kuwa mbali na misaada hiyo NMB wamekua wakitoa elimu ya kutunza fedha kwa wanafunzi wa shule mbali mbali, ambayo inawafahamisha namna ya kutumia na kutunza fedha kwa maisha ya baadae.

Thursday 26 August 2021

MUONEKANO WA MRADI WA SGR, MOROGORO - MAKUTUPORA

 

IMPACT BUSINESS BREAKFAST; THEME - FINANCIAL OPTIONS FOR POST-COVID 19 BUSINESS CONTINUITY

 

We are happy to announce the new date for #IBB6. Have you registered? 

Hurry now to reserve your slot by registering today.

CLICK HERE FOR MORE DETAILS > > >

Or call: +255 762 234 005

TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS UPCOMING TRAINING

 

NOTICE TO TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS MEMBERS

 

SITHOLIZWE MDLALOSE APPOINTED AS MANAGING DIRECTOR OF VODACOM TANZANIA PLC


Vodacom Tanzania Plc Chairman of the Board of Directors, Judge (Rtd) Thomas B. Mihayo is pleased to announce the appointment of Sitholizwe Mdlalose as the new Managing Director.

Sitholizwe joins the company from Vodacom South Africa (VSA) where he was the Finance Director since 2017. Sitholizwe has previously held various roles in the Vodacom Group including that of Interim Chief Finance Officer as well as Chief Finance Officer of Vodacom Group’s International Business. 

Prior to joining Vodacom Group, he worked with Vodafone Group for more than 6 years holding senior roles within the Group. He has more than 19 years of finance, management, and consulting experience, of which 13 have been in telecommunications across both emerging and developed markets. 

He holds a Bachelors of Accounting Science (BCompt) degree from the University of South Africa. Sitholizwe is a qualified accountant (ACCA) and has completed a Senior Executive Programme Africa at Harvard Business School.

LIPA KWA NMB MASTERCARD / QR UPATE PUNGUZO LA 15% BATANI


ZIGO LINAKUJA SOON NDANI YA DStv...

 

Je ni ZIGO gani analosubiri dogo?🤔🤔

Tukutane tarehe 1.9.2021 ndani ya @dstvtanzania

Wednesday 25 August 2021

COMING SOON FROM DStv TANZANIA.... STAY TUNED!!!

 

LIPA KWA NMB MASTERCARD / QR UPATE PUNGUZO LA 15% KWENYE MAFUTA

 

ZANZIBAR TO BUILD AFRICA’S 2ND TALLEST SKYSCRAPER AND LARGEST HOTEL IN EAST AND CENTRAL AFRICA


Zanzibar/Dar es Salaam - Zanzibar will in the next few years be home to a $1.3 billion (about Sh3 trillion) commercial tower that could change the face of the semi-autonomous Indian Ocean archipelago.

A joint venture of Tanzania’s AICL Group and Edinburgh Crowland Management Ltd yesterday signed a contract with New York and Dubai-based architect xCassia that will see the latter come up with architectural designs for what will be the tallest building in eastern, central and southern Africa.

When completed, the 70-storey building will be the second tallest in Africa behind Iconic Tower in Egypt, which covers a total area of 65,000 square metres, with two underground floors and 78 floors above the ground.

Speaking during the signing ceremony, Zanzibar’s Minister of State in the President’s Office (Economy and Investment), Mr Mudrik Ramadhan Soraga, said the project was a big step towards building the isles’ blue economy.

“Its implementation supports the government’s efforts in inviting more local and foreign investors to the isles,” he said.

Crowland Management Ltd CEO Emmanuel Umoh said the building, to be known as Zanzibar Domino Commercial Tower, is expected to be an iconic feature that will facilitate tourism and culture and offer business opportunities.

“The Zanzibar Domino is a unique project which is exceptionally well-suited to our investment philosophy of providing our investors with superior returns through exceptional schemes as well as strategic socioeconomic projects that leverage prosperity, people and the planet,” he said.

According to the founder and design director of xCassia, Mr Jean-Paul Cassia, the idea to construct the building on a man-made island was a decade-long dream, and became a reality after a site and investors were found.

FACEBOOK MARKETPLACE ROLLS OUT TO 37 COUNTRIES & TERRITORIES ACROSS SUB-SAHARAN AFRICA


August, 24 2021 - Facebook today announced the launch of Marketplace to 37 countries and territories in Sub-Saharan Africa, including: Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Cape Verde, Central African Republic, Comoros, Democratic Republic of the Congo, Djibouti, Eritrea, Eswatini, Equatorial Guinea, Guinea, Guinea-Bissau, Gabon, Gambia, Ghana, Liberia, Lesotho, Malawi, Mali, Mauritania, Mauritius, Namibia, Niger, Republic of the Congo, Rwanda, Sao Tome and Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, South Sudan, Tanzania, Togo, Uganda, Western Sahara and Zimbabwe.

Currently available in South Africa, Ethiopia, Kenya and Nigeria, Marketplace is a convenient destination where people can discover, buy and sell items from others in their local communities, simply by tapping on the Marketplace icon or visiting www.facebook.com/marketplace to browse and search for items, or filter by distance or category.

Commenting on the launch, Facebook Director of Public Policy Africa Kojo Boakye said, “Increasing the availability of Marketplace to 37 more countries and territories in Sub-Saharan Africa reinforces our ongoing commitment to helping connect communities and support buying and selling through one simple online destination. As the effects of the COVID-19 pandemic continue to impact people and businesses, the expansion of Marketplace will provide more people with a convenient destination where they can discover new products, shop for things they want, or find buyers for the things they want to sell.”

Friday 20 August 2021

LALIGA INAZIDI KUBAMBA NDANI YA CHANELI ZA MICHEZO

 


LaLiga inazidi kubamba ndani ya chaneli za michezo SuperSport!

Jumapili hii, ⚽ Levante vs Real Madrid, ðŸ“º SS Football 224, ðŸ•°️ Saa 05:00 Usiku

Je ni timu gani itaibuka na ushindi wa pointi 3?

Hakikisha mtanange huu haukupiti kwa kulipia kifurushi chako cha Bomba TShs 19,900 tu kwa kupiga *150*53#.

#Birianiiendelee

BODI YA MAZAO MCHANGANYIKO (CPB) YAASWA KUYAONGEZEA THAMANI MAZAO NCHINI

Waziri wa Kilimo nchini, Mhe. Profesa Adolf Mkenda (wapili kushoto) akishirikiana na Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde, Mkurugenzi wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko (CPB), Dkt. Anselm Moshi na viongozi wengineo kuzindua viwanda vya uchakataji mazao jijini Dodoma Jumatano iliyopita.
Waziri wa Kilimo nchini, Mhe. Profesa Adolf Mkenda akipokea maelezo ya bidhaa itokanayo na zao la alizeti wakati wa sherehe ya kuzindua viwanda vya uchakataji mazao jijini Dodoma Jumatano iliyopita.

Waziri wa Kilimo nchini, Mhe. Profesa Adolf Mkenda akipokea maelezo juu ya mafuta yatokanayo na zao la alizeti wakati wa sherehe ya kuzindua viwanda vya uchakataji mazao jijini Dodoma Jumatano iliyopita.

Bodi ya Mazao Mchanganyiko (CPB) nchini imeaswa kufanya jitihada za ziada katika kuyaongezea thamani mazao ili kuweza kushindana na soko la nchi za nje.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Profesa Adolf Mkenda wakati akizindua viwanda vya bodi hiyo ya mazao mchanganyiko vilivyozinduliwa mnamo Jumatano iliyopita katika makao makuu ya Tanzania jijini Dodoma.

Profesa Mkenda aliitaka bodi hiyo na sekta binafsi zinazojihusisha na uchakataji wa mazao nchini kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao ili kuweza kuyapeleka kuuza nchi za nje.

Alisema kuwa ni vyema bodi hiyo ikaangalia ni namna inaweza kushirikiana na wakulima katika kuyaongezea thamani mazao.

“Nyie bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko mkisaidia na sekta binafsi mnaweza kutusaidia kuhakikisha mazao yetu yanaongezewa thamani,” alisema Profesa Mkenda.

Pia alitoa wito kwa bodi hiyo kuhakikisha inaingia mikataba na wakulima wenye mashamba makubwa nchini ili waweze kulima alizeti ya kutosha.

KLABU YA BIASHARA YA NBC YAINGIA MKOANI RUVUMA

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando (wa nne kushoto), pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC,  Elibariki Masuke (wa tatu kulia), akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,  Theobald Sabi wakifungua bango kuashiria uzinduzi rasmi wa ufunguzi wa Klabu ya Bishara Mkoani Songea wenye lengo la kuwakutanisha wateja wake wafanyabiashara na wenye viwanda na wadau wengine. Kutoka kushoto ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Simon Ntwale,
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando pamoja na maofisa wa Benki ya NBC na wateja wake wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara iliyozinduliwa na Benki ya NBC Mkoani Songea.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando pamoja na maofisa wa Benki ya NBC na wateja wake wakiserebuka mara baada ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara iliyozinduliwa na Benki ya NBC Mkoani Songea.

Benki ya Taifa ya Biashara imezindua NBC Biashara Club, Mkoa wa Ruvuma katika hafla ya uzinduzi ilifanyika katika hoteli ya Heritage Cottage Wilaya ya Songea na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Songea, DC Pololet Komando ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, RC John Ibuge.

NBC Biashara Club ni sehemu ya mkakati mpana wa benki hiyo wa kuwainua wajasiriamali kwa kuwajengea uwezo wa kibiashara kupitia semina za mafunzo, kuwasogezea huduma za kibenki, kuwajengea mitandao ya kibiashara pamoja na kuwapa mbinu za kurasimisha biashara zao ili waweze kukopesheka. Jitihada hizi za Benki ya NBC zinaonekana kuzaa matunda kwani benki hiyo ilifanikiwa kuzindua klabu ya biashara kwa Mkoa wa Kigoma miezi michache iliyopita.

Zaidi ya kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara, NBC Biashara Club pia inatoa fursa ya kuwakutanisha wanachama wake na watoa huduma mbali mbali katika sekta ya biashara zikiwemo taasisi za serikali kama TRA ili kujadili na kutatua changamoto na kupata mafunzo zaidi kwenye masuala ya kodi, uagizaji malighafi na bidhaa kwenda na kutoka nje.

Uzinduzi wa NBC Biashara Club mkoani Ruvuma unakuja siku chache baada ya benki hiyo kuanzisha huduma ya NBC Wakala Plus wilayani Mbinga. Benki hiyo pia iliendesha semina za mafunzo kwa makundi mbali mbali ya wajasiriamali wilayani humo kwa dhumuni la kuwajengea uwezo katika kuendesha biashara. Pamoja na semina kwa wajasiriamali benki ya NBC kupitia huduma ya NBC Shambani, ilikutana na viongozi na wanachama wa vyama vya ushirika (AMCOS) Mkoani Ruvuma ili kujadili fursa zinazotokana na kushirikiana kwa sekta za kilimo ya kibenki.

AKIBA COMMECIAL BANK YAZINDUA "AKIBA WAKALA"

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Akiba Commercial Bank,  Webster Kaunga (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za Akiba Wakala katika Tawi la Makao Makuu Barabara ya Ohio jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine pichani ni  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki, Dora Saria na Mkuu wa Kitengo cha mikopo wa Benki hiyo, Charles Kamoto.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Akiba Commercial Bank, Webster Kaunga na Mkuu wa Kitengo cha mikopo wa Benki hiyo, Charles Kamoto na Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wakifunua kitambaa mara baada ya uzinduzi huo.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Akiba Commercial Bank Dora Saria amesema benki hiyo imeanzisha huduma ya Wakala ijulikanayo kwa jina la "Akiba Wakala".

Huduma hii itawasaidia wateja wa benki hiyo kupata huduma kwa urahisi zaidi popote pale walipo kupitia mtandao mpana wa huduma za Wakala unaopatikana nchi nzima.

Dora Saria ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo kwenye tawi la benki hiyo ililopo baeabaea ya Ohio mkabala nahoteli ya Serena jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Amesema Mteja anaweza kupata huduma ya kutoa na kuweka fedha mahali popote penye tangazo la Akiba Wakala Kupitia huduma hii tutawafikia Watanzania wengi popote pale walipo na wataweza kunufaika na huduma zetu.

Pia ameongeza kuwa kwamba, kupitia huduma hii ya Akiba Wakala Benki watakuwa washiriki wazuri katika kuunga mkono harakati za Serikali za kuhakikisha uwepo wa huduma jumuishi za kifedha yaani (Financial inclusion) kwa Watanzania wote.

WAZIRI WA TEKNOLOJIA AZINDUA HUDUMA YA NMB MKONONI PLUS *150*68#

Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dk. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kulia), wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa huduma ya NMB Mkononi Plus uliofanyika Makao Makuu ya NMB - jijini Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Neema Lutula. Wapili kulia ni Kaimu Afisa Mkuu Teknolojia na Mabadiliko ya Digitali wa NMB Kwame Makundi na Mkuu wa kitengo cha Bima NMB Martine Massawe.

Benki ya NMB imezindua huduma mpya ya NMB Mkononi Plus, ambayo Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Faustine Ndugulile, ameitaja kama muarobaini wa upotevu wa pesa na kichocheo cha kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za Bima na za kibenki kwa njia ya mtandao.

Uzinduzi NMB Mkononi Plus 'Ya Wote,' huduma inayotolewa kwa wateja na wasio wateja wa NMB, umefanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Ndugulile na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Neema Lutula.

Akizungumza kabla ya kuzindua huduma hiyo, Waziri Ndugulile alisema NMB Mkononi Plus ni huduma inayoakisi jitihada za benki hiyo katika kwenda na kasi ya Serikali, ambayo imejikita katika kutokomeza foleni za kihuduma maofisini, sambamba na kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za Bima na fedha kwa njia za mtandao.

"Ubunifu uendelee zaidi na NMB msiishie hapa, kwa sababu uzinduzi huu unaakisi utayari wenu katika kwenda na kasi ya Serikali, ambayo furaha yake ni kuona inaongeza idadibya watumiaji wa Bima na kutokomeza upotevu wa fedha, foleni za huduma maofisini, ambalo kwetu sisi sio jambo la sifa kamwe.

Thursday 19 August 2021

UNGANA NASI NDANI YA MAISHA MAGIC BONGO 160

 

Tunamtambulisha kwenu rasmi Bi. Zainab Saidi @zaiylissa anaungana rasmi na familia ya #MMBJUAKALI. Je atakuja kama nani? 

Ungana nasi kila Jumatano - Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya @maishamagicbongo 160 pekee!

Piga *150*53# kulipia kifurushi chako cha Bomba TShs 19,900 tu.

#vyanyumbanihuanziadstv

FIRST ISLAMIC BOND IN TANZANA IS OVERSUBSCRIBED

  • The maiden Sukuk bond to have been issued in Tanzania was oversubscribed last week as investors’ appetite for assorted investment avenues remains high.
Dar es Salaam - The maiden Sukuk bond to have been issued in Tanzania was oversubscribed last week as investors’ appetite for assorted investment avenues remains high.

Sukuk is the Arabic name for financial certificates, also commonly referred to as sharia compliant bonds.
They are simply securities of equal denomination representing individual ownership interests in a portfolio of eligible existing or future assets.

The bond, issued by Imaan Finance Limited, was oversubscribed by 36 percent last week, market data shows.

The company sought to collect Sh2 billion, but ended up receiving a total of Sh2.72 billion in bids. With a greenshoe option of Sh1 billion, the company will take all the amount as per the agreement.

The company issued the bond to grow its loan portfolio under sharia principles.
“Though the oversubscription was not too big, it shows that there is huge demand for such investment avenues in the country,” said Fimco Limited chief executive Ivan Tarimo.

Both institutional and individual investors took part in the exercise.
According Mr Tarimo, the performance of the maiden Sukuk bond shows that there was big demand that would capture people who previously avoided investing their money in avenues that attract interest.

“It’s important that this Sikuk should not be the last in order to continue capturing people who are still interested in participation in such financial assets. It will help sharia-compliant institutions to grow their investor bases, and thus contribute immensely to inclusion endeavours,” he said.

Wednesday 18 August 2021

PRESIDENT SAMIA SULUHU HASSAN CALLS FOR DEBT RELIEF

President Samia Suluhu Hassan addresses the SADC 41st Ordinary Summit of Heads of State and Government in Lilongwe, Malawi yesterday.

President Samia Suluhu Hassan has called for Southern African Development Community (SADC) member states to speak with one voice in asking for debt relief or extension of repayment time for developing countries which are struggling with the impacts of Covid-19.

The Tanzanian leader said the move would help SADC member countries recover from shocks of the global pandemic, in particular to effectively re-build their devastated economies.

President Samia made the remarks yesterday as she was making her maiden speech at the 41st Ordinary Summit of SADC Heads of State and Government held in Lilongwe, Malawi.

Continue Reading > > >

ENDELEA KUFURAHIA LIGI MBALIMBALI KUPITIA DStv



Endelea kufurahia michuano ya ligi mbalimbali ikiwemo ya #SeriaA, #LaLiga, #EPL kupitia @dstvtanzania pekee!

Unachotakiwa kufanya ni kulipia kifurushi chako mapema na kwa urahisi kwa kupiga *150*53#.

#Birianiiendelee