Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 29 July 2022

NMB YAENDELEA KUWA KINARA WA UFANISI NCHINI TANZANIA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna.

Kwa Ufupi: Benki ya NMB yaendelea kuwa kinara wa ufanisi nchini Tanzania. Faida ya benki kabla ya kodi yafikia TZS bilioni 298, sawa na ongezeko la asilimia 54.
  • Faida baada ya kodi: TZS bilioni 208 - ongezeko la asilimia 53 kwa mwaka
  • Jumla ya Mapato ya benki: TZS bilioni 562- ongezeko la asilimia 21 kwa mwaka 
  • Jumla ya Mali: TZS Trilioni 9 - ongezeko la asilimia 19 kwa mwaka
Dar es Salaam. July 28, 2022 - Benki ya NMB imeendeleza ufanisi wake kiutendaji katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2022. Faida kabla ya kodi imeongezeka kwa asilimia 54 na kufikia Shilingi bilioni 298 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 193 ya kipindi kilichoishia June 2021. Faida baada ya kodi imeongezeka kwa asilimia 53 na kufikia Shilingi bilioni 208 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 135 ya kipindi kilichoishia June 2021. Faida hii inatokana na kuongezeka kwa ufanisi, kukua kwa mizania ya benki, ubora na umakini katika kusimamia mikopo, na kuongezeka kwa miamala ya wateja.

Mapato ya Benki yameongezeka kwa asilimia 21 hadi kufikia shilingi bilioni 562 katika kipindi kilichomalizikia mwezi Juni 2022 ikilinganishwa na shilingi bilioni 463 zilizopatikana kipindi kama hicho mwaka jana. Mapato haya yamechangiwa na ongezeko la mikopo kwa wateja na uwekezaji kwenye hati fungani za Serikali, pamoja na ongezeko la miamala ya kibenki.

Benki imeendelea kuimarisha ufanisi kwenye gharama za uendeshaji, ulioshuhudia uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato ukishuka mpaka asilimia 42 kutoka asilimia 47 katika kipindi kama hichi mwaka uliopita. Benki imeendelea kutilia mkazo uimarishaji wa ufanisi huku ikiboresha uwekezaji katika teknolojia na vipao mbele vya kimkakati vyenye lengo la kuongeza ubora wa huduma za kibenki.

Thursday 28 July 2022

NBC YAZINDUA HUDUMA MPYA YA KADI YA MALIPO YA DOLA

Meneja wa Biashara ya Kadi wa Benki ya NBC, Esnat Hollela akipeana mkono na Abel Kaseko, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mauzo wa NBC wakati wa uzinduzi wa huduma ya kadi ya malipo ya Dola inayowezesha malipo mtandaoni bila makato ya ziada. Kushoto ni Meneja wa Bidhaa na Mauzo wa NBC, Dorothea Mabonye na Ulrik Peter, Kaimu Mkuu wa Huduma za Kidigitali.
  • Kadi hiyo ya USD Visa Debit Card itasaidia ufanyaji wa malipo ya huduma na bidhaa bila malipo ya ziada 
Dar es Salaam, Julai 18, 2022 - Benki ya NBC imezindua kadi inayowezesha malipo mtandaoni kwa njia ya Dola. Kupitia kadi hii wateja wanapata fursa ya kufanya malipo ya bidhaa na huduma kwa dola pasipo makato ya ziada. Ni mapinduzi ya tehama yanayowezesha malipo ya VISA kadi inayohakikishia wateja usalama na urahisi pindi wafanyapo malipo ya mtandao. 

Mkurugenzi msaidizi wa benki ya NBC, Elibariki Masuke, amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha wateja wao wanazifikia fedha zao kiusalama na wanakuwa na uwezo wa kufanya miamala kwa urahisi, kuboresha huduma zao.” Kadi hii ni haraka, rahisi kutumia na salama, njia bora kabisa ya kufanya malipo na miamala ya kimtandao. Kadi hii inaondoa kero ya kubena fedha nyingi kwani hali hiyo huhatarisha usalama wa fedha hizo”. “Tunayofuraha, kuzindua kadi hii ya malipo ya VISA ya fedha za kimarekani, ambapo itaongeza ufanisi kwa wateja wetu na kuwezesha urahisi wa kufanya malipo na miamala ya dola za kimarekani,” aliongeza. 

RC MAKALLA AIPONGEZA NMB KUZINDUA KIFURUSHI CHA MIKOPO KWA WALIMU DAR

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wapili kushoto) akizindua Mpango maalum 'Mwalimu Spesho' na Mhe. Amos Makalla (watatu kulia) Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Meneja Kanda ya Dar es Salaam wa NMB - Donatus Richard.

Watumishi wa Umma wakiwemo Walimu wametakiwa kufanya maandalizi bora ya kustaafu mapema kwa kuchangamkia fursa ya Mkopo kwa kuanzisha miradi ya kujikimu kwa mustakabali ya maisha ya sasa na baadae.



Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla katika kuadhimisha Siku ya walimu Mkoa wa Dar es Salaam na kizindua kifurushi cha NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’ chenye masuluhisho mahususi kwa ajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya Walimu Mkoani Dar es Salaam.



RC Makalla amesema Benki ya NMB ndiyo benki ambayo inatoa huduma bora na kutoa taarifa sahihi kwa wateja wake hivyo kupelekea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita iliyo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.



Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi alisema katika kifurushi cha “Mwalimu Spesho” kimejumuisha huduma zote zinazomuwezesha Mwalimu ikiwemo mikopo mbalimbali yenye riba nafuu ikiwemo ikiwemo ya kujiendeleza kielimu yeye na watoto wake.

ECOBANK GROUP DELIVERS STRONG PERFORMANCE DURING THE FIRST HALF OF 2022 AND INCREASES PROFIT BEFORE TAX BY 24%


  • Profit before Tax increases by 24% to $261 million 
  • Net revenues up 10% to $910 million
  • Record return on tangible equity of 19.5% 
  • Earnings per share increases by 24% year-on-year
Lomé, 25 July 2022 – Ecobank Group today reports strong performance during the first half of 2022, with unaudited Profit before Tax (PBT) increasing by 24% to US$261 million. The Group also announced a record return on tangible equity of 19.5% and increased earnings per share for shareholders by 24% year-on-year. Despite the challenging operating environment of high inflation, weakening African currencies, and slower economic growth, the Group's net revenues increased by 10% to $910 million.

These results demonstrate the sustained success of our revenue expansion goals under our 'Execution Momentum' strategy. They also show the effectiveness of the Bank's diversified operating model, which impacts our customers and clients positively, as we benefit from our ‘Manufacturing centrally, Distributing locally' strategic approach. Our business lines, Corporate and Investment Banking (CIB), Consumer Banking (CSB) and Commercial Banking (CMB), grew their PBT by 33%, 43% and 15%, respectively. The performance of each of our regions also demonstrates the strength of our diversified pan-African presence. Nigeria, French-Speaking West Africa countries (UEMOA), Central, East, Southern African countries (CESA) and Anglophone West Africa markets (AWA) grew their PBT by 74%, 42%, 37% and 8%, respectively.

Wednesday 27 July 2022

WASHINDI WA WIKI YA KWANZA WA PROMOSHENI YA VODACOM M-PESA IMEITIKA WAPATIKANA JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi akimkabidhi funguo mshindi wa Bajaj wa promosheni ya Vodacom "M-Pesa Imeitika" kutoka Morombo jijini Arusha, Mwanaisha Nyonyo Mohamed wakati wa hafla ya wiki ya kwanza iliyofanyika kwenye viwanja vya Soko la Kilombero jijini humo. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini, Abednego Mhagama. Vodacom inatoa zawadi ya bajaj moja na bodaboda nne (zote mpya) kila wiki kwa wiki nane ili kuhamasisha matumizi ya pesa kidijitali. Zawadi kuu itakuwa ni nyumba mpya iliyosheheni samani zote.

 

Washindi waliojishindia bodaboda kwenye promosheni ya Vodacom "M-Pesa Imeitika" wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Vodacom inatoa zawadi ya bajaj moja na bodaboda nne (zote mpya) kila wiki kwa wiki nane ili kuhamasisha matumizi ya pesa kidijitali. Zawadi kuu itakuwa ni nyumba mpya iliyosheheni samani zote.




ALHAMIS HII SAA TATU USIKU DR KUMBUKA NDANI YA DStv



#YAANI wiki hii tunakaa kufichuka na madini mengi kutoka kwa #SalamaNaDrKumbuka matibabu yote yako mezani Alhamis hii saa tatu kamili usiku ndani ya @maishamagicpoa only on @dstvtanzania

Piga *150*53# kulipia kifurushi chako cha Poa TShs. 9,900 tu ufurahie majadiliano haya.
@drkumbuka_majaliwa

#DStvShangweka

Tuesday 26 July 2022

FUATILIA TAMTHILIA KALI NDANI YA MAISHA MAGIC BONGO



Fuatilia tamthilia kali ndani ya chaneli ya Maisha Magic Bongo.
  • Huba; Jumatatu - Ijumaa, saa 3 usiku
  • Kitimtim; Jumatatu - Jumanne, saa 3:30 usiku 
  • Pazia; Jumatatu - Jumatano, saa 1:30 usiku
  • Yalaiti; Jumatatu - Ijumaa, saa 4 usiku 
  • Jua Kali; Jumatano - Jumapili, saa 3:30 usiku 
Yote haya ni ndani ya kifurushi cha Bomba TShs. 21,000/= tu ndani ya @dstvtanzania pekee.

Piga *150*53# kulipia kwa urahisi zaidi.

#DStvShangweka


DTB BANK STAFF IN CLEANING EXERCISE AT MAJENGO MARKET IN DODOMA

Dodoma District Commissioner, Mr. Jabir Shekimweri alongside Diamond Trust Bank staff members in Dodoma take part in Majengo Market cleaning exercise over the weekend.

Diamond Trust Bank Tanzania staff members in Dodoma, joined Dodoma District Commissioner, Mr. Jabir Shekimweri, His Worship Lord Mayor of Dodoma Prof. Davis Mwamfute and traders in cleaning Majengo Market in Dodoma over the weekend. 



The cleaning exercise is part of the banks’ Corporate Social Responsibility [CSR] agenda that promotes good citizenry amongst employees while also giving back to the communities in the fields of Environment, Health, Education and Financial Inclusion.

LETSHEGO BANK SUPPORTS SMALL BUSINESSES AT SABASABA TRADE FAIR


Letshego Bank Tanzania joined more than 3,200 local and international companies to support the 46th Dar es Salaam International Trade Fair held at Sabasaba grounds, Kilwa Road, Dar es Salaam.

In support of this year's Sabasaba theme; Tanzania is the right Destination for trade and investment; Letshego Bank continues to invest and grow its business by diversifying its product offering, digitising channels to increase customer experience as well as facilitating easy access to more affordable financial solutions for more customers.


Speaking to our Correspondent, Mr. Omar Msangi, the CEO of Letshego Bank said; “Letshego Bank recently launched Mkopo Fasta – a tailored product Letshego has created to support small business owners to overcome the challenges of cash flow. Mkopo Fasta increases access to capital, quickly and simply, to enable small businesses to buy stock, meet business expenses or even support any production costs needed to meet current delivery orders on time.” Mr Msangi added, “Once applications are approved, cash is deposited into the small business owners’ account within 72 hours, unlocking income and growth potential.”

In addition to supporting small businesses, Letshego Bank also supports individuals with financial solutions and products for youth, health, wellbeing, savings and retirement.



Public service loans are transferred into customer accounts within 48 hours of approval, with loan values extending up to 60 million shillings for payment within various terms up to and including 84 months.

Monday 25 July 2022

NMB YAWAGUSA WANAFUNZI WILAYANI TEMEKE

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (wa tatu kushoto), akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa, sehemu ya msaada wa viti 50 na meza 50 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kibasila. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Mbagala, Halima Mcharazo na wa pili kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Kidawa Masoud.
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (wa nne kushoto), akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa, sehemu ya msaada mabati 600 kwa ajili ya shule tatu za msingi zilizopo wilaya ya Temeke.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (katikati), akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa, sehemu ya msaada wa madawati 100 kwa ajili ya Shule ya Msingi Chemchem ya Mbagala katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam.

Benki ya NMB imekabidhi msaada wa mabati 600, madawati 100, pamoja na viti 50 na meza 50, kwa ajili ya shule nne za Msingi na Moja ya Sekondari, zilizopo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh.Mil.39.

Hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Kibasila, huku shule za msingi zilizonufaika na msaada huo zikiwa ni Keko Magulumbasi, Mtoni, Azimio na Chemchem.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard alimkabidhi misaada hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Meya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke.

Donatus alisema wakati wa hafla hio, thamani ya msaada huo ni sehemu tu ya Sh. Bilioni 2, ambazo ni sawa na asilimia 1 ya faida ya NMB kwa mwaka uliopita wa 2021, kwa kupitia Sera ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) katika Sekta za Elimu, Afya na Majanga mbalimbali.

GGM KILI CHALLENGE CAMPAIGN RAISES SH1.1 BILLION

The Regional Commissioner of Kilimanjaro, Stephen Kagaigai (right) receiving a flag from one of the participants of the GGM Kili Challenge campaign 2022 who climbed Mount Kilimanjaro with the aim of donating money to continue the fight against HIV/AIDS. Behind them wearing a hat is the Vice President of AngloGold Ashanti- GGML who handles sustainable projects for Ghana and Tanzania, Simon Shayo. The reception was held at the end of the week at Mweka entrance in Moshi.

Geita Gold Mining Limited (GGML) in collaboration with the National AIDS Control Commission (TACAIDS), has continued to set a record for the provision of social services after collecting more than Shs 1.1 billion through the GGM Kili Challenge 2022 campaign that started on June 29 and ended on July 21 this year.



The campaign founded by GGML 20 years ago, is specifically to provide education about HIV/AIDS and also to raise funds for the control of HIV infection with the aim of supporting the Government's efforts to reach three zeros in the sense of zero new infections, zero stigma and zero AIDS deaths



Speaking at the end of the week in Moshi district at a reception event for 52 participants of which 24 climbed Mount Kilimanjaro by walking and 28 by cycling around it through the Machame gate and down to Mweka, the Vice President of AngloGold Ashanti- GGML who handles sustainable projects for in Ghana and Tanzania, Simona Shayo, said this year's campaign has been a unique success.



He said the campaign was officially launched on June 29 in Dodoma and was followed by fundraising held on July 14 and then on July 15, 2022. The participants were allocated for the mountain climbing exercise, which also involved the provision of free HIV and diabetes testing services and the provision of UVIKO-19 vaccination for residents of Moshi Town and the Kilimanjaro region in general.

He said that these services started to be provided in Machame, Kialia, Soko la Kalali and Nshara and now Mweka.

TMSA AWARDS TOP MARKETERS IN TANZANIA FOR 2022

Deputy Minister of Investment, Trade and Investment (centre), Hon. Exaud Kigahe speaking with distinguished guests (not in the picture) during an event to award top marketers for the year 2022, which was hosted by the Tanzania Marketing Science Association (TMSA) on July 22nd in Dar es Salaam, where 14 categorical winners in marketing were awarded.
Managing Partner from HESA Africa, Bruce Mugaisi hands over the rising star marketing award to Shumbana Walwa, Senior Marketing Manager at MultiChoice Tanzania at the TMSA awards.
A group photo of winners of the TMSA awards with the guest of honor, Deputy Minister of Investment, Trade and Investment (centre), Hon. Exaud Kigahe and TMSA board.
Deputy Minister of Investment, Trade and Investment (L), Hon. Exaud Kigahe, presenting a certificate of recognition to Bruce Mugaisi, Managing Partner of HESA Africa (centre) for their exemplary support in sponsoring the TMSA Marketing awards for the year 2022, held on July 22 in Dar es Salaam. On the right is the Chairman of the Board of TMSA, Dr Emmanuel Chao.

Dar es Salaam, 25th July 2022 - The Tanzania Marketing Science Association (TMSA) has awarded top marketers in 14 different marketing categories for 2022 in order to encourage more professionalism in Tanzania's marketing ecosystem.

The 2022 marketing awards were held on the evening of July 22 in Dar es Salaam, and were attended by the country's top marketing brands and professionals, including Kilombero Sugar Company, CocaCola, JCDeaux, Vodacom, HESA Africa, Jackson Group, and Bramex.

Dr. Emmanuel Chao (PhD), Board Chairman of TMSA, addressed the event's guests and emphasized its significance. "This night is a special night not only for marketers, but for the business ecosystem in Tanzania," he said, "because when you have the proper marketing science, you have confidence in where you are going as a business institution."

Dr. Chao went on to say, "These awards are being held for the second time here in Tanzania." We had a long list of top 50 marketing awards in 2021, but this year the category has been reduced to a maximum of ten. The marketing awards in 2022 will include 14 categories ranging from individuals to organizations.

The event was officiated by Hon. Exaud Kigahe, Deputy Minister for Investment, Industries, and Trade, who emphasized how the government is doing everything possible to prioritize and promote a friendly business environment in which marketers can be more creative and innovative.

Sunday 24 July 2022

BENKI YA NBC YAMWAGIWA SIFA KWA KUTOA FIDIA YA BIMA YA MAZAO KWA WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA

  • Benki ya Kwanza nchini kutoa fidia ya Bima ya mazao kufuatia mvua kubwa zilizoharibu zao tumbaku Tabora
  • Zaidi ya Milioni 9 zatolewa kwa vikundi vya AMCOS
  • Mkuu wa Mkoa ashauri Bima hiyo kuhusisha mazao mengi zaidi ya biashara na chakula
 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Batilda Buriani (katikati) akitoa hundi kwa vyama vya Ushirika (AMCOS) mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya fidia ya hasara ya mazao iliyotokana na kuwepo kwa mvua kubwa katika msimu wa 2021/2022. Fedha hizo zimetolewa kupitia huduma ya Bima ya mazao ya Benki ya NBC ambayo inatoa kinga dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ukame, vimbunga, wadudu na mafuriko.

Tabora,  21 Julai 2022: Kwa mara ya kwanza nchini, wakulima wa zao la tumbaku mkoani Tabora wamelipwa fidia na Benki ya NBC kufuatia hasara waliyoipata kutokana na uharibifu wa mazao yao baada ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika msimu uliopita. Fidia hivyo imelipwa kupitia mpango wa Bima za Mazao wa Benki ya NBC. Katika mpango huo, Vyama vinne vya Ushirika (AMCOS) vya Insolelansabo, Muloku, Ngulu Moja na Isenegezya vimepewa zaidi ya shilingi milioni tisa, kufidia hasara iliyosababishwa na kuwepo kwa kiwango cha juu cha mvua na hivyo kuharibu mazao na kusababisha hasara kwa wakulima hao. 

 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Batilda Buriani akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali mara baada ya kutoa hundi kwa wanachama wa vyama vya Ushirika (AMCOS) mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya fidia ya hasara ya mazao iliyotokana na kuwepo kwa mvua kubwa katika msimu wa 2021/2022. Fedha hizo zimetolewa kupitia huduma ya Bima ya mazao ya Benki ya NBC ambayo inatoa kinga dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ukame, vimbunga, wadudu na mafuriko.

Akizungumzwa wakati wa kukabidhi hundi ya fidia kwa vyama hivyo, Mkurugenzi wa Wateja wadogo wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke alisema fidia hiyo imetolewa kupitia mpango wa bima kwa wakulima ambayo inawalinda dhidi ya hasara zinazosababishwa na athari za hali ya hewa kama vile ukame, vimbunga, wadudu,mvua ya mawe na mengineyo. “Kwa msimu wa mwaka huu kupitia vyama ambavyo vilikopeshwa na Benki ya NBC katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga, wakulima waliweza kupata bima ya Kilimo ambayo iliwawezesha kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali,” alisema. Alisema hatua hiyo imetokana na upembuzi wa hali ya hewa uliofanyika na kuonekana kuwa katika vijiji vya Lolangulu, Ishishimulwa, Imalakaseko na Isenegzya kulikuwa na kiwango cha juu cha mvua. Bima hiyo inatolewa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee. Benki ya NBC inaamini kuwa kupitia bima hiyo, vyama vitapunguza kwa kiwango kikubwa hasara zinazoweza kutokea kutokana mabadiliko ya hali ya hewa na majanga mengine yasiyotabirika na yaliyo nje ya uwezo wa mkulima. Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeunda mpango maalum wa kuboresha kilimo ujulikanao kama “ajenda 10/30” ambao unalenga kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kutoka asilia 5 mpaka 10 ifikapo mwaka 2030, kujitosheleza kwa chakula na kuwawezesha wakulima kubadili uzalishaji wa mazao ya chakula kuwa ya biashara.

Friday 22 July 2022

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAKANDARASI NA WAZABUNI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEZESHAJI KUTOKA BENKI YA CRDB


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amewataka wakandarasi na wazabuni nchini kutumia fursa za uwezeshaji zinazotolewa na Benki ya CRDB ili kuongeza ufanisi katika kazi zao, na kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu katika miradi ya kimkakati nchini.

Prof. Mbalawa alisema hayo wakati akifungua Kongamano la Uwezeshaji kwa Wakandarasi na Wazabuni lililoandaliwa na Benki ya CRDB katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Waziri alisema fursa hizo zitasaidia kupunguza changamoto za ucheleweshwaji wa miradi mbalimbali kwasababu ya kukosekana kwa mtaji.


“Benki ya CRDB imewaletea fursa mlangoni, itumieni kupata mitaji nafuu kujijengea uwezo utakaowawezesha kushiriki kikamilifu katika miradi,” alisema Prof. Mbarawa huku akibainisha kuwa uwezeshaji huu unaofanywa na Benki ya CRDB utasidia kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha wakandarasi wazawa wanashiriki katika miradi (local content).

Prof. Mbalawa alipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika miradi ya ujenzi wa miondombinu mbalimbali nchini ambayo itasadia kuchochea ukuaji wa uchumi. “Tunatambua na kuthamini sana ushikiri wa Benki ya CRDB katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini, asanteni na hongereni sana,” alisema.

Prof. Mbalawa aliishauri Benki ya CRDB kupunguza riba katika mikopo ya wakandarasi kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa sekta nyengine ikiwamo ya kilimo ili kuwajengea uwezo wakandarasi na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika miradi inayotekelezwa na Serikali.


“Tunawapongeza kwa mikopo hii isiyo na dhamana na maboresho mengine mliyofanya, lakini niwaombe mpunguze riba ili kutoa unafuu zaidi. Vilevile, nitoe rai kwa Wakandarasi kurejesha mikopo kwa wakati kama ilivyo katika makubaliano,” aliongezea Prof. Mbalawa huku akiishauri Benki ya CRDB kuisaidia Serikali kutoa mafunzo ya usimamizi wa miradi kwa Wakandarasi na Wazabuni.

Aidha, Prof. Mbarawa alipongeza uamuzi wa Benki ya CRDB kufungua kampuni tanzu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) akisema uamuzi huo utasaidia kufungua fursa nyingi kwa wafanyabiashara nchini ikiwamo wakandarasi na wazabuni.

“Congo kuna uhitaji mkubwa wa miundombinu ya barabara na nchi zetu zimekuwa katika mazungumzo ya namna gani tunaweza kusaidia katika kuboresha eneo hili hasa ukizingatia biashara baina ya nchi zetu inaendelea kukua”, alisema Prof. Mbalawa huku akihitimisha kwa kuipongeza Benki hiyo kwa kutunikiwa tuzo ya Benki Bora Tanzania na jarida la Euromoney la nchini Uingereza.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alimhakikishia Prof. Mbalawa kuwa Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya “Tupo Tayari” imejipanga vilivyo katika kuhakikisha inashirikiana na Serikali kuboresha miundombinu nchini ili kufungua fursa za kiuchumi na kuvutia wawekezaji.

Nsekela alisema Benki ya CRDB imefanya maboresho katika huduma zake inazotoa kwa kundi hilo ambapo hivi sasa wakandarasi wakubwa na wadogo watawezeshwa kupata huduma za mikopo bila dhamana yoyote. Alisema baadhi ya huduma zilizofanyiwa maboresho ni pamoja na dhamana ya zabuni “Bid bond”, dhamana za utekelezaji wa miradi “Performance Guarantee”, dhamana za malipo ya awali “Advance Payment Guarantee”, pamoja na huduma za mikopo ya mitambo.


Nsekela aliongezea kuwa Benki hiyo pia imeboresha taratibu zake za utoaji mikopo na hivyo kuwasihi Wakandarasi kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo, kufungua akaunti, pamoja na kujiunga na huduma za bima ili kujikinga na majanga yanayoweza kutokea. “Benki ya CRDB ni Benki yenu, niwahakikishie tu sisi Tupo Tayari kuwahudumia,” alihitimisha Nsekela.

BENKI YA CRDB YAWASHUKURU WATEJA TUZO YA ‘BENKI BORA TANZANIA’ YA EUROMONEY

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori (wakwanza kushoto) akifurahia tuzo ya 'Benki Bora Tanzania' na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, pamoja na Meneja Mipango ya Biashara Benki ya, Masele Msita katika hafla ya kuwashukuru wateja na wadau wa Benki hiyo kwa mafanikio hayo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai 2022. Jarida maarafu la fedha na uchumi la Euromoney liliitaja Benki ya CRDB kama moja ya benki bora duniani katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa benki zilizofanya vizuri iliyofanyika Julai 13 2022 Jijini London nchini Uingereza.


Benki ya CRDB imewashukuru wateja na wadau wake baada ya kutunukiwa tuzo ya “Benki Bora Tanzania” na jarida maarafu la masuala ya fedha na uchumi la nchini uingereza la Euromoney.

Shukrani hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB na kuhudhuriwa na wajumbe wa bodi, wafanyakazi, na wateja, wa Benki hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam, Nsekela alisema wateja wa benki hiyo wamekuwa sehemu ya mafanikio ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya biashara ambao umepelekea kupata tuzo hiyo.


“Niwashukuru wateja, wanahisa, Serikali, Benki Kuu ya Tanzania na washirika wetu wa biashara kwa ushirikiano wanaotupa na kuendelea kutufanya kuwa bora zaidi. Hii sio tuzo ya Benki ya CRDB peke yake, ni tuzo ya Watanzania wote,” alisema Nsekela.

Mwaka 2019, Benki hiyo ilianza ikifanya mageuzi katika biashara yake ambayo yamejikita katika kutengeneza thamani endelevu, kuongeza ujumuishi wa kifedha, na kujenga uchumi jumuishi kupitia bidhaa, huduma, na mifumo bunifu ya utoaji huduma.

“Tuzo ya Euromoney inathibitisha nafasi ya Benki ya CRDB kama ‘Benki Kiongozi’ nchini. Vilevile, inatambua mafanikio ya mageuzi haya ambayo yamepelekea ukuaji endelevu wa Benki yetu na ukinufaisha wateja, wawekezaji na uchumi wa nchi kwa ujumla wake.”


Waandaji wa tuzo hizo pia wametambua mchango wa mageuzi wa kidijitali ambayo yamefanyika ndani ya Benki ya CRDB, ikielezwa kuwa kiasi kikubwa yamesaidia kuchochea ongezeko la ujumuishi wa kifedha nchini.

“Tumekuwa pia tukishiriki kikamilifu katika kusaidia sekta mbalimbali za maendeleo nchini hususani kilimo, na ujusariliamali ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa letu,” aliongezea Nsekela huku akibainisha kuwa Benki hiyo ilitoa ahueni kubwa kwa sekta ya biashara nchini katika kipindi ambacho janga la UVIKO-19 limeikumba dunia.

Aidha, alisema Benki hiyo pia imetambuliwa kwa kuwa na uwezo mkubwa katika uwezeshaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali na sekta binafsi akitolea mfano Mradi wa Umeme wa Maji wa Nyerere na Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR). Nsekela alisema jitihada na mafanikio hayo pia yamekuwa yakijidhihirisha katika matokeo ya kifedha ambayo imekuwa ikiyapata mwaka hadi mwaka.


Benki ya CRDB ndio Benki ya kwanza nchini kutunikiwa tuzo ya ‘Benki Bora Tanzania’ na Euromoney mwaka 2004. Ushindi wa tuzo hiyo mwaka huu unadhihirisha kuimarika kwa utendaji wa Benki siku za hivi karibuni na kutambuliwa kimataifa.

Mwaka jana Benki hiyo ilitajwa kama Benki Bora Tanzania’ na ‘Benki inayoongoza kwa Ubunifu’ na jarida maarufu duniani la masuala ya fedha la ‘Global Finance’, huku Taasisi ya Utafiti wa Ubora barani Ulaya ikiitunikia ‘Tuzo ya Ubora’.






BIG BROTHER NAIJA NDANI YA DStv PEKEE

 

Imebaki siku 1, kuelekea kwenye Msimu wa 7 wa Big Brother Naija.

Kaa tayari kwa msimu huu utakaoanza Jumamosi hii ndani ya chaneli ya BBN 198 kupitia kifurushi cha Bomba Tshs. 21,000/= tu.

Lipia mapema kifurushi chako ili usikose burudani hii.

#DStvEwaaaaah