Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 25 July 2022

NMB YAWAGUSA WANAFUNZI WILAYANI TEMEKE

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (wa tatu kushoto), akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa, sehemu ya msaada wa viti 50 na meza 50 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kibasila. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Mbagala, Halima Mcharazo na wa pili kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Kidawa Masoud.
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (wa nne kushoto), akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa, sehemu ya msaada mabati 600 kwa ajili ya shule tatu za msingi zilizopo wilaya ya Temeke.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (katikati), akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa, sehemu ya msaada wa madawati 100 kwa ajili ya Shule ya Msingi Chemchem ya Mbagala katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam.

Benki ya NMB imekabidhi msaada wa mabati 600, madawati 100, pamoja na viti 50 na meza 50, kwa ajili ya shule nne za Msingi na Moja ya Sekondari, zilizopo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh.Mil.39.

Hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Kibasila, huku shule za msingi zilizonufaika na msaada huo zikiwa ni Keko Magulumbasi, Mtoni, Azimio na Chemchem.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard alimkabidhi misaada hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Meya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke.

Donatus alisema wakati wa hafla hio, thamani ya msaada huo ni sehemu tu ya Sh. Bilioni 2, ambazo ni sawa na asilimia 1 ya faida ya NMB kwa mwaka uliopita wa 2021, kwa kupitia Sera ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) katika Sekta za Elimu, Afya na Majanga mbalimbali.

Meneja huyo aibainisha kuwa, Kibasila imepokea viti 50 na meza 50, huku shule za msingi Keko Magulumbasi, Azimio ya Tandika na Mtoni ya Mtoni kijichi kila moja ikipewa mabati 200, wakati Shule ya Chemchem ya Mbagala ikijipatia madawati 100.

Aidha, Rugwa aliipongeza NMB kwa namna inavyoijali jamii kwa kushirikiana bega kwa bega na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali kwa kuboresha mazingira ya kujisomea, kufundishia, na upatikanaji wa huduma za afya ndani ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

"Hakika NMB ni mshirika sahihi sio tu wa harakati za maboresho ya mazingira ya kujisomea na kufundishia, bali na suluhishi mbalimbali za kifedha. Kila yanapotokea mahitaji, NMB haijawahi kusita kuisapoti jamii inayoizunguka,” Rugwa aliongezea.

No comments:

Post a Comment