- Benki ya Kwanza nchini kutoa fidia ya Bima ya mazao kufuatia mvua kubwa zilizoharibu zao tumbaku Tabora
- Zaidi ya Milioni 9 zatolewa kwa vikundi vya AMCOS
- Mkuu wa Mkoa ashauri Bima hiyo kuhusisha mazao mengi zaidi ya biashara na chakula
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Batilda Buriani (katikati) akitoa hundi kwa vyama vya Ushirika (AMCOS) mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya fidia ya hasara ya mazao iliyotokana na kuwepo kwa mvua kubwa katika msimu wa 2021/2022. Fedha hizo zimetolewa kupitia huduma ya Bima ya mazao ya Benki ya NBC ambayo inatoa kinga dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ukame, vimbunga, wadudu na mafuriko.
Tabora, 21 Julai 2022: Kwa mara ya kwanza nchini, wakulima wa zao la tumbaku mkoani Tabora wamelipwa fidia na Benki ya NBC kufuatia hasara waliyoipata kutokana na uharibifu wa mazao yao baada ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika msimu uliopita. Fidia hivyo imelipwa kupitia mpango wa Bima za Mazao wa Benki ya NBC. Katika mpango huo, Vyama vinne vya Ushirika (AMCOS) vya Insolelansabo, Muloku, Ngulu Moja na Isenegezya vimepewa zaidi ya shilingi milioni tisa, kufidia hasara iliyosababishwa na kuwepo kwa kiwango cha juu cha mvua na hivyo kuharibu mazao na kusababisha hasara kwa wakulima hao.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Batilda Buriani akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali mara baada ya kutoa hundi kwa wanachama wa vyama vya Ushirika (AMCOS) mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya fidia ya hasara ya mazao iliyotokana na kuwepo kwa mvua kubwa katika msimu wa 2021/2022. Fedha hizo zimetolewa kupitia huduma ya Bima ya mazao ya Benki ya NBC ambayo inatoa kinga dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ukame, vimbunga, wadudu na mafuriko.
Mafunzo yakiendelea kwa wanachama na wanachama wa vyama vya Ushirika (AMCOS) mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya fidia ya hasara ya mazao iliyotokana na kuwepo kwa mvua kubwa katika msimu wa 2021/2022.Fedha hizo zimetolewa kupitia huduma ya Bima ya mazao ya Benki ya NBC ambayo inatoa kinga dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ukame, vimbunga, wadudu na mafuriko.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk.Batilda Buriani aliipongeza Benki ya NBC kwa kubuni huduma hiyo ambayo imetoa suluhisho juu ya majanga ambayo yamekuwa yakiwakumba wakulima kwa muda mrefu. “Naipongeza sana Benki ya NBC kwa kuleta sokoni Bima hii ya mazao yenye lengo la kuwalinda wakulima pindi watapatapo majanga yanayoleta uharibifu wa mazao yao na hivyo kuwaletea hasara. Hakika bima hii ya kilimo itakuwa ni chachu kwa wakulima wetu wa zao la Tumbaku na wakulima wote nchini, kuweza kulima bila kuwa na hofu juu ya majanga yeyote, tunawashukuru sana Benki ya NBC kwa kuunga mkono adhma ya serikali yetu kwa kuja na huduma hii muhimu sana kwa wakulima wetu. Nawasihi sasa muongeze bima hii katika mazao mengine ya biashara na chakula ili kutoa ahueni kwa wakulima ambao ndio sekta kubwa na uti wa mgongo wa taifa letu” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Batilda Buriani akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa vyama vya Ushirika (AMCOS) mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya fidia ya hasara ya mazao iliyotokana na kuwepo kwa mvua kubwa katika msimu wa 2021/2022. Fedha hizo zimetolewa kupitia huduma ya Bima ya mazao ya Benki ya NBC ambayo inatoa kinga dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ukame, vimbunga, wadudu na mafuriko.
No comments:
Post a Comment