Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_170926_270926_101026

Absa Banner_170926_270926_101026

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Tuesday, 13 October 2026

AFRIMMA WAMEMPA TUZO, 1245 WANAMPA JUKWAA! MARIOO NDANI YA 4PLAYS

Mwenye tuzo anakuja, wenye kelele mmejipanga? Marioo ametangazwa kujiunga na line-up ya 4Plays, sherehe za miaka minne ya 1245, zitakazofanyika Oktoba 17, Superdome Arena, Masaki.

Baada ya kutwaa tuzo ya Best Male East Africa kwenye AFRIMMA 2026, Marioo anakuja na sababu nyingine ya mashabiki kusherehekea. Kutoka kumpongeza kwenye comments hadi kuimba naye mbele ya jukwaa, Superdome itachimbika!

Staa huyo anaungana na Young Jonn kutoka Nigeria kwenye line-up inayofanya kauli ya “nitaona kama nitakuja” kuwa ngumu kuitetea. Bongo Flava na Afrobeats zinakutana kwenye usiku mmoja wa kusherehekea miaka minne ya 1245.

Sherehe hizo zinaungwa mkono na Air Tanzania, Clouds Media, Johari Rotana, Heineken na Don Julio, kuongeza nguvu kwenye burudani hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

Birthday ni ya 1245, lakini zawadi ni ya mashabiki! Nunua tiketi kupitia 4plays.1245tz.com au wasiliana kupitia 0748 211 245.

Oktoba 17, Dar es Salaam itasimama. Utakuwepo au itahadithiwa? Hii ni Chess sio Checkers

Monday, 12 October 2026

STANBIC BANK TO FINANCE TANZANIA’S COFFEE VALUE CHAIN AS EXPORT EARNINGS MORE THAN DOUBLE

Stanbic Bank Tanzania’s Head of Agribusiness, Benifrida Tarimo (right), receives a certificate of participation from Moshi District Commissioner, Godfrey Mnzava (second left), in recognition of the Bank’s participation in the Kahawa Festival 2026, held in Moshi, Kilimanjaro Region. Looking on is Tanzania Coffee Board (TCB) Chairperson, Prof. Aurelia Kamuzora (left).

MOSHI, Tanzania - October 8, 2026: Stanbic Bank Tanzania has committed to financing stakeholders across Tanzania’s coffee value chain, from farmers, aggregators and processors to exporters and international buyers, as the country’s coffee export earnings more than double.

According to the Bank of Tanzania’s Monthly Economic Review for July 2026, Tanzania earned USD 391.7 million from coffee exports in the year ending June 2026, up from USD 164.3 million in 2022. The August 2026 review put earnings at USD 396 million for the year ending July 2026.

Stanbic reaffirmed its commitment during the Kahawa Festival, held in Moshi from October 8 to 10, 2026, under the theme “Growing Coffee. Creating Value. Connecting Tanzania to International Markets.”

Speaking about the initiative, Stanbic Bank Tanzania Head of Agribusiness, Benifrida Tarimo, said Tanzanian coffee has significant potential to compete in international markets, with the bank ready to support stakeholders seeking to expand their businesses.

“Tanzania’s coffee is ready for the world. Our role is to be the growth partner behind it, connecting producers, aggregators, processors and commodity traders with the finance they need to invest in production, add value and compete for export markets,” said Tarimo.

Stanbic offers tailored financial solutions to meet the needs of different players across the coffee value chain. These include financing for farm expansion and mechanisation, processing facilities, warehouses, working capital, trade finance and export transactions.

The solutions are designed to help farmers expand production and improve quality, enable cooperatives to pay farmers promptly and store their produce properly, and allow exporters to fulfil larger orders while managing costs between shipment and payment.

MWANGA HAKIKA BANK YATWAA TUZO YA BENKI INAYOWEKA WATEJA MBELE KUPITIA KAMPENI YA BENKI KWA ZERO

Oktoba 12, 2026 - Mwanga Hakika Bank imetunukiwa tuzo ya Customer-Centric Bank of the Year katika tuzo za International Customer Service Week Awards 2026, ikiwa ni utambuzi wa juhudi za benki hiyo katika kuweka mahitaji ya wateja mbele kupitia kampeni yake ya Benki Kwa Zero.

Kupitia kampeni hiyo, Mwanga Hakika Bank inalenga kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha kwa kupunguza gharama zinazohusiana na huduma za kibenki, ikiwemo kuondoa ada za kufungua akaunti, ada za kila mwezi na makato ya miamala kupitia huduma ya PesaHakika.

Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa gharama nafuu, huku ikihamasisha matumizi ya huduma rasmi za kibenki na kuongeza ushiriki wa wananchi katika mfumo wa kifedha.

Tuzo hiyo inaongeza utambuzi wa juhudi za Mwanga Hakika Bank katika kuboresha huduma kwa wateja na kuendeleza suluhisho za kifedha zinazozingatia mahitaji yao.

SERIKALI NA VODACOM TANZANIA FOUNDATION KUIMARISHA MAFUNZO YA KIDIJITALI KWA WALIMU NCHINI

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira (katikati), na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah (wa pili kulia), wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi Naurei, wilayani Arusha. Kituo hicho ni cha kwanza kati ya vituo 50 vinavyotarajiwa kujengwa nchini. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Selemani Msumi (wa kwanza kushoto), na Mkuu wa Shule hiyo, Getrude Tarimo (wa nne kushoto), wakiwa pamoja na wanafunzi. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Arusha, Oktoba 9, 2026 – Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania Foundation, imezindua Kituo cha Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi Naurei, wilayani Arusha, ikiwa ni hatua ya kupanua upatikanaji wa mafunzo ya kidijitali kwa walimu nchini.

Kituo hicho ni cha kwanza kati ya vituo 50 vinavyotarajiwa kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kuwawezesha walimu kupata mafunzo endelevu ya kitaaluma kupitia teknolojia, kuboresha mbinu za ufundishaji na kuongeza fursa za wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira (wa tatu kulia), na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na uongozi wa Shule ya Msingi Naurei katika Kituo cha Rasilimali za Walimu kilichozinduliwa rasmi shuleni hapo.

Ushirikiano huo unatekelezwa kupitia Programu ya Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (TCPD/MEWAKA), inayolenga kuimarisha matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Kujifunza (LMS) pamoja na Vituo vya Rasilimali za Walimu (TRC).

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo hicho, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, alisema uwekezaji katika maendeleo ya walimu ni muhimu katika kuimarisha uwezo wao wa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kuboresha ubora wa elimu nchini.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Rasilimali za Walimu katika Shule ya Msingi Naurei, Arusha, kilichoanzishwa kwa ushirikiano na TIE kuimarisha mafunzo ya kidijitali na maendeleo ya walimu nchini.

Alisema ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuboresha miundombinu, teknolojia na mifumo ya kujifunzia unawawezesha walimu kuendelea kujifunza na kuimarisha ujuzi wao katika kipindi chote cha utumishi wao.

“Mwalimu anayepata maarifa mapya, anayeongeza kiwango cha elimu alichonacho na kutumia teknolojia kwa ufanisi, huongeza nafasi ya wanafunzi kufaulu na kufikia ndoto zao,” alisema Lugangira.

YAS RECOGNISES OUTSTANDING CUSTOMER SERVICE STAFF, CALLS FOR REGULAR TRAINING

Yas Chief Business Officer, Norman Kiondo (third left) congratulates Michenzania Mall Yas Store Supervisor, Ms. Ellen Tumaini Mbwambo on being recognised as one of the company’s outstanding customer service employees for 2026 during a ceremony marking the close of Customer Service Week in Dar es Salaam over the weekend. The event recognised employees’ contributions to assisting customers and resolving service issues.

Dar es Salaam; October 12, 2026 - Telecommunications company Yas has recognised outstanding customer service employees for 2026 and called for regular training to equip staff with the skills needed to address evolving customer needs amid technological advancements and changing services.

The ceremony, held over the weekend in Dar es Salaam, marked the conclusion of Customer Service Week celebrations and recognised employees for their contributions to assisting customers and resolving service-related issues.

Speaking at the event, Yas and Mixx Director for Customer Experience, Mwangaza Matotola, said the rapidly evolving telecommunications sector requires employees to continuously update their skills to deliver better customer experiences.

She noted that customer service had improved over the years, but emphasised the need for continued training to prepare Yas and Mixx customer service teams to address emerging challenges.

TANZANIA KUTUMIA FURSA ZA MIKUTANO YA IMF NA BENKI YA DUNIA, BANGKOK-THAILAND KIMKAKATI

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akiongoza kikao cha ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), inayofanyika jijini Bangkok nchini Thailand, kuanzia tarehe 12 hadi 18 Oktoba 2026.

Bangkok, Thailand; Oktoba 11, 2026 - Tanzania imejipanga kutumia mikutano ya mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group) inayofanyika Bangkok, Thailand, kuanzia Oktoba 12 hadi 18, 2026, kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kuvutia rasilimali za maendeleo na kupanua fursa za uwekezaji nchini.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesisitiza kuwa ushiriki wa Tanzania katika mikutano hiyo ni wa kimkakati, ukilenga kuhakikisha nchi inanufaika na fursa za ufadhili, kuimarisha usimamizi wa fedha za nje na kuendeleza ajenda za maendeleo ya Taifa.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati), akiongoza kikao cha ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), inayofanyika jijini Bangkok nchini Thailand, kuanzia tarehe 12 hadi 18 Oktoba 2026. Wengine katika picha ni Waziri wa Fedha-Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil (Mb) (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa pili kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida (kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto).

Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya ushiriki wa ujumbe wa Tanzania, Waziri Omar alisema mikutano hiyo itatoa fursa ya kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu na viongozi wa taasisi hizo, wakiwemo makamu wa rais anayesimamia Kanda ya Kusini-Mashariki mwa Afrika pamoja na wakurugenzi watendaji, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa maendeleo.

Alieleza kuwa mojawapo ya maeneo muhimu yatakayopatiwa kipaumbele ni utekelezaji wa mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Kimataifa (IDA 21), ambapo Serikali tayari imewasilisha orodha ya awali ya miradi inayotarajiwa kufadhiliwa na Benki ya Dunia.

“Moja ya maeneo muhimu yanayopewa kipaumbele ni utekelezaji wa mzunguko wa 21 wa IDA (IDA 21), ambayo Serikali imewasilisha orodha ya awali ya miradi inayotarajiwa kufadhiliwa na Benki ya Dunia na kuhakikisha kuwa miradi ya kipaumbele ya Taifa inapata ufadhili unaostahili,” alisema Waziri Omar.

Sunday, 11 October 2026

VODACOM TANZANIA YASISITIZA UMUHIMU WA UHUSIANO WA KIBINADAMU KATIKA HUDUMA KWA WATEJA ENZI ZA AI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire (kushoto), akikabidhi tuzo ya pongezi kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika utoaji wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, yaliyolenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka wateja mbele na kuthamini juhudi za wafanyakazi wanaotekeleza dhamira hiyo kila siku. Pembeni ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare.

Oktoba 11, 2026 - Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imesisitiza umuhimu wa kudumisha uhusiano wa kibinadamu katika huduma kwa wateja licha ya kuongezeka kwa matumizi ya akili mnemba (AI), mifumo ya kiotomatiki na roboti zinazolenga kuongeza ufanisi na kuboresha shughuli za biashara.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Bi. Harriet Lwakatare, alisema hayo wakati wa hafla ya kutambua na kutunuku wafanyakazi wa huduma kwa wateja, iliyofanyika kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare, akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026. Katika hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa kuweka mahitaji ya wateja mbele kwa kuwasikiliza, kuwapatia majibu kwa wakati na kuhakikisha wanapata huduma salama na zenye ubora. Maadhimisho hayo yaliwapa wafanyakazi fursa ya kutafakari mchango wao katika kujenga imani ya wateja na kuhakikisha kila mawasiliano na mteja yanawaachia uzoefu mzuri wa huduma.

Kauli hiyo inatolewa wakati ambapo kampuni mbalimbali zinazidi kutumia akili mnemba na mifumo ya kiotomatiki kurahisisha shughuli, kupunguza kazi zinazojirudia na kukidhi mabadiliko ya matarajio ya wateja. Hali hiyo imezifanya kampuni kukabiliwa na changamoto ya kusawazisha ufanisi unaotokana na teknolojia na utoaji wa huduma zinazozingatia mahitaji binafsi ya wateja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bi. Lwakatare alisema maendeleo ya teknolojia yanabadilisha namna kampuni zinavyowahudumia wateja, lakini mchango wa binadamu bado ni muhimu katika kuhakikisha huduma bora.

“Sekta yetu inabadilika. Akili mnemba na mifumo ya kiotomatiki inazidi kuwa sehemu ya shughuli zetu za kila siku, lakini jambo moja linabaki kuwa muhimu, nalo ni uhusiano wa kibinadamu,” alisema.

NBC YADHAMINI KILOMBERO GOLF OPEN 2026 KUKUZA VIPAJI NA KUIMARISHA MCHEZO WA GOFU

Mwenyekiti wa Kilombero Country Club na Mkurugenzi wa Kilimo kwa Wakulima wa Kilombero Sugar, Pierre Redinger (katikati), akiwa na wadau wengine wa mchezo wa gofu, wakiwemo wachezaji na maofisa wa Benki ya NBC, wakionyesha ishara ya mchezo huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mashindano ya siku tatu ya Kilombero Golf Open 2026, yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Kilombero Sugar, mkoani Morogoro, mwishoni mwa wiki. Benki ya NBC ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo.

Kilombero, Morogoro, Oktoba 11, 2026 – Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendelea kuunga mkono maendeleo ya michezo nchini kwa kudhamini mashindano ya Kilombero Golf Open 2026, yaliyofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya gofu vya Kilombero Sugar, mkoani Morogoro, kwa lengo la kukuza vipaji, kuimarisha ushindani na kuongeza ushiriki katika mchezo huo.

Mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki yamewakutanisha wachezaji kutoka vilabu saba vya gofu nchini, ambavyo ni TPDF Lugalo, Dar es Salaam Gymkhana, Kilimanjaro Golf Club, TPC Club, Morogoro Gymkhana, Mufindi Golf Club na Kilombero Golf Club.

Mkuu wa Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC, Jimmy Myalize (kushoto), akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kilombero Country Club na Mkurugenzi wa Kilimo kwa Wakulima wa Kilombero Sugar, Pierre Redinger (kulia), wakati wa mashindano ya Kilombero Golf Open 2026.

Akizungumzia udhamini huo, Mkuu wa Miamala na Amana za Wateja Wakubwa wa NBC, Jimmy Myalize, alisema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa benki kupanua ushiriki wake katika michezo na burudani, sambamba na mchango wake wa muda mrefu katika sekta hiyo kupitia Ligi Kuu ya NBC.

“Tumekuwa wadau wakubwa wa mchezo wa soka kupitia Ligi Kuu ya NBC, na mchezo wa riadha kupitia mbio za NBC Dodoma Marathon. Hata hivyo, tunaendelea kupanua wigo wa ushiriki wetu katika sekta ya michezo na burudani kwa kushiriki katika michezo mingine pia. Tunataka kuwa sehemu ya ukuaji wa mchezo wa gofu nchini Tanzania,” alisema Myalize.

Aliongeza kuwa NBC itaendelea kushirikiana na wadau katika shughuli zinazochochea maendeleo ya jamii, huku ikiendelea kutoa huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya wateja binafsi, makampuni na biashara ndogo na za kati.

NBC YAIPAMBA DABI YA KARIAKOO, YAMKABIDHI ELIE MPANZU TUZO YA MCHEZAJI BORA

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa NBC, Elibariki Masuke (kulia), akimkabidhi tuzo mshambuliaji wa Simba SC, Elie Mpanzu (kushoto), aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyozikutanisha Simba SC na Yanga SC, maarufu kama Dabi ya Kariakoo, iliyochezwa jana katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mchezo huo ulimalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga SC.

Dar es Salaam, Oktoba 11, 2026 – Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC, imeongeza msisimko katika Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC na Yanga SC kwa kuandaa shughuli mbalimbali zilizowakutanisha mashabiki wa soka na wateja wake, huku ikimkabidhi mshambuliaji wa Simba SC, Elie Mpanzu, tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo.

Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, katika mchezo uliovuta hisia za mashabiki na kuendeleza ushindani mkali kati ya miamba hiyo ya soka nchini.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa NBC, Elibariki Masuke (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki NBC, Msafiri Shayo (kushoto) wakifuatilia mchezo huo.

Kupitia shughuli hizo, NBC ilitumia fursa ya dabi hiyo kubwa kuimarisha uhusiano na wateja wake, huku ikiendeleza dhamira yake ya kuunganisha huduma za kibenki na uzoefu wa kipekee kwa wadau wa michezo.

Kabla ya mchezo huo, benki hiyo iliwawezesha baadhi ya wateja wake kusafiri kwa msafara maalumu kuelekea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambako walishuhudia pambano hilo kutoka jukwaa la VIP na kufurahia dabi hiyo katika mazingira ya kipekee.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa NBC, Elibariki Masuke, aliongoza shughuli hizo na kumkabidhi Elie Mpanzu tuzo ya mchezaji bora wa mechi. Tukio hilo lilishuhudiwa na mashabiki waliokuwa uwanjani pamoja na watazamaji waliofuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni.

Sambamba na shughuli za uwanjani, maofisa wa NBC walitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa mashabiki na wadau waliohudhuria mchezo huo, zikiwemo huduma za kufungua akaunti na ushauri wa kifedha. Hatua hiyo iliipa benki fursa ya kuwasogezea wateja huduma zake, huku ikiendeleza ushiriki wake katika kukuza soka nchini.

Akizungumzia ushiriki wa NBC katika dabi hiyo, Masuke alisema benki hiyo inaendelea kutumia michezo mikubwa kuimarisha uhusiano na wateja wake pamoja na wadau wengine wa soka.

“Udhamini wetu hauishii tu katika kuboresha ligi tunazodhamini, bali pia katika kuhakikisha kuwa wadau wetu, wakiwemo wafanyakazi, viongozi na wateja, wanakuwa sehemu ya moja kwa moja ya mchezo huu. Tunataka soka liwe uzoefu wa kipekee, si tukio la dakika 90 pekee,” alisema Masuke.

VODACOM BUSINESS YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WATEJA

Mkuu wa Idara ya Mauzo kwa Biashara Ndogo na za Kati wa Vodacom Tanzania, Jasmine Makori (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Pius Maswaga, zawadi ya shukrani kwa ushirikiano wao wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

October 11, 2026 - Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha Vodacom Business imeendelea kuimarisha uhusiano na wateja wake wa biashara kwa kutembelea taasisi mbalimbali, kutoa zawadi za shukrani na kuendesha mafunzo kwa mawakala, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026.

Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Deogratius Massawe (kulia), akimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Green Telecom, Rahul Sahni, zawadi ya shukrani kwa ushirikiano wao wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Vodacom Business ya kuthamini wateja wake, kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na kuboresha uzoefu wa wateja wanaotumia bidhaa na huduma zake.

Katika ziara hiyo, timu ya Vodacom Business ilitembelea wateja wake, wakiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Green Telecom na Access Bank, ambapo ilikabidhi zawadi kama ishara ya shukrani kwa ushirikiano unaoendelea kati ya taasisi hizo na Vodacom.

Mkuu wa Idara ya Mauzo kwa Biashara Ndogo na za Kati wa Vodacom Tanzania, Jasmine Makori, alimkabidhi Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Pius Maswaga, zawadi ya shukrani kwa ushirikiano wao.

Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia), akimkabidhi mwakilishi wa Access Bank, Roger Lamlembe zawadi ya shukrani kwa ushirikiano wao wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Katika ziara nyingine, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Deogratius Massawe, alimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Green Telecom, Rahul Sahni, zawadi kwa kutambua ushirikiano wao. Aidha, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, alimkabidhi mwakilishi wa Access Bank zawadi kama ishara ya kuthamini uhusiano wa kibiashara kati ya taasisi hizo.

Saturday, 10 October 2026

STANBIC BANK INVESTS TZS 40 MILLION TO STRENGTHEN HEALTHCARE SERVICES IN KIGAMBONI

Omari Mtiga (fourth left), Head of Personal and Private Banking at Stanbic Bank Tanzania, hands over medical equipment to Kigamboni District Commissioner, Hon. Dalmia Mikaya (centre), at Vijibweni Hospital in Kigamboni, Dar es Salaam. The donation is part of the Bank’s efforts to improve healthcare services during Customer Service Week 2026. Looking on are government officials, hospital staff and representatives of Stanbic Bank Tanzania.

Dar es Salaam; October 10, 2026 - Stanbic Bank Tanzania has donated medical equipment and supplies worth TZS 40 million to Vijibweni Hospital in Kigamboni, Dar es Salaam, to strengthen healthcare delivery, improve maternal care and enhance patient monitoring and diagnostic services.

The donation, handed over on Friday, October 9, 2026, is part of the Bank’s continued commitment to supporting community development and improving access to essential services.

The equipment includes five hospital beds, a delivery bed, 15 bedside lockers, a linen hamper, a patient monitor, two oxygen flow meters and 30 digital blood pressure machines. The contribution also covers infection control supplies and computer equipment to support hospital administration and record-keeping.

The donated items are expected to help healthcare professionals improve patient care, particularly in the maternity unit and hospital wards. The additional beds will support mothers and admitted patients, while the patient monitor will strengthen the observation of critical cases. The digital blood pressure machines will also expand access to routine screening across the facility.

Speaking during the handover, Stanbic Bank Tanzania’s Head of Personal and Private Banking, Mr. Omari Mtiga, reaffirmed the Bank’s commitment to improving community well-being through investments in essential services.

“Access to quality healthcare is essential to building healthier, stronger and more productive communities. At Stanbic Bank, we believe our responsibility extends beyond financial services to making a meaningful difference in the lives of the people we serve,” Mr. Mtiga said.

EQUITY BANK CEO APPOINTED TO GLOBAL DEVELOPMENT COMMISSION, AMPLIFYING AFRICA’S VOICE

October 10, 2026 - Equity Group Holdings Managing Director and Chief Executive Officer, Dr. James Mwangi, has been appointed to the South North Commission on Development, a global body established to rethink cooperation between the Global North and Global South in advancing sustainable development.

The appointment places an experienced African private sector leader at the centre of international discussions on development financing, economic partnerships and inclusive growth. It also carries significance for Tanzania, where financial inclusion, access to capital, agricultural development, youth entrepreneurship and digital transformation remain important drivers of economic growth.

The South North Commission is an independent body established by the German government and co-chaired by former German Chancellor Olaf Scholz and former Costa Rican President Laura Chinchilla. Dr. Mwangi is one of two business leaders appointed to the Commission and the only business leader representing Africa.

He joins prominent global figures, including World Bank President Ajay Banga, World Trade Organization Director-General Dr. Ngozi Okonjo-Iweala, United Nations Development Programme Administrator Alexander De Croo and Nobel Peace Prize laureate Dr. Denis Mukwege.

Commenting on his appointment, Dr. Mwangi emphasised the need to reposition Africa's role in global development discussions.

“Africa should no longer be seen through the lens of aid. It is a source of growth, talent, innovation and investment,” said Dr. Mwangi.

Equity Bank Tanzania Highlights Significance for Local Markets

Equity Bank Tanzania Managing Director Isabela Maganga said Dr. Mwangi's appointment was significant for Tanzania because it brings practical African private sector experience into global discussions on development financing and inclusive economic growth.

“Dr. Mwangi’s appointment to the South North Commission on Development is a proud moment for Equity and a significant signal for markets such as Tanzania. It reinforces the importance of development models that move beyond aid and focus on unlocking local enterprise, financing productive sectors and building institutions that can support long-term growth,” said Maganga.

PUMA ENERGY YAWAFIKIA WATEJA KWA HUDUMA ZA PRIS NA ELITE CARD

Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, akiwahudumia wateja na kuwaeleza manufaa ya PRIS na Puma Elite Card katika kituo cha Puma Airport Service Station jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Dar es Salaam, Tanzania – Oktoba 9, 2026: Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeendelea kuimarisha ushirikiano na wateja wake kupitia zoezi maalumu la kuwahamasisha kutumia programu ya uaminifu kwa wateja ya PRIS na kadi ya malipo ya mafuta ya Puma Elite Card katika kituo cha Puma Airport Service Station.

Zoezi hilo linalenga kuongeza uelewa kuhusu huduma hizo na kuwawezesha wateja kufahamu namna zinavyoweza kuwasaidia kupata zawadi, kurahisisha malipo na kusimamia matumizi ya mafuta kwa urahisi zaidi.

Kupitia PRIS, programu ya kidijitali ya Puma Energy, wateja wanaweza kukusanya pointi wanaponunua bidhaa zinazostahili, zikiwemo mafuta, vilainishi vya injini, gesi na bidhaa nyingine katika maduka ya Shop Express. Pointi hizo zinaweza kukombolewa kwa zawadi zinazopatikana kupitia programu hiyo, na hivyo kuwawezesha wateja kupata manufaa zaidi kutokana na manunuzi yao ya kawaida.

Kwa upande mwingine, Puma Elite Card ni kadi ya malipo inayowawezesha watu binafsi, familia na biashara kuweka fedha mapema na kuzitumia kununua bidhaa zinazostahili, zikiwemo mafuta, vilainishi vya injini na gesi. Kadi hiyo inakubalika katika vituo vya Puma Energy na vituo washirika zaidi ya 80 nchini Tanzania.

Akizungumzia zoezi hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, alisema kampuni inaendelea kutafuta njia za kuongeza thamani ya huduma zake na kuboresha uzoefu wa wateja.

“Wateja wetu ni kiini cha biashara yetu, na tunaendelea kutafuta njia za kufanya uzoefu wao wanapopata huduma za Puma uwe bora zaidi, wenye manufaa na unaowapa urahisi. Kupitia PRIS, wateja wanaweza kupata zawadi kutokana na manunuzi yanayostahili, huku Puma Elite Card ikiwawezesha kusimamia matumizi yao ya mafuta kwa urahisi,” alisema Bi. Fatma.

PUMA ENERGY BRINGS PRIS AND ELITE CARD CLOSER TO CUSTOMERS THROUGH AIRPORT SERVICE STATION ACTIVATION

Puma Energy Tanzania Managing Director Fatma Abdallah (right) engages with customers at Puma Airport Service Station, highlighting the benefits of PRIS and Puma Elite Card during Customer Service Week 2026 in Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania, 9 October 2026: Puma Energy Tanzania is stepping up efforts to connect more customers with its PRIS loyalty programme and Puma Elite Card through a customer engagement activation at Puma Airport Service Station, highlighting how customers can earn rewards, simplify fuel payments and gain greater control over their spending.

The activation forms part of the company’s ongoing efforts to raise awareness and encourage participation in its customer-focused solutions, giving motorists and other customers an opportunity to understand the benefits available when purchasing products across Puma Energy’s retail network.

Through PRIS, the digital loyalty programme launched in Tanzania in May 2026, customers can earn points on qualifying purchases, including fuel, lubricants, gas and products purchased at Shop Express outlets. Accumulated points can be redeemed for available rewards, allowing customers to benefit from their everyday purchases.

Alongside PRIS, Puma Energy offers the Puma Elite Card, a prepaid fuel card designed to help individuals, families and businesses manage fuel expenditure more conveniently. Customers can load funds onto the card and use the balance to purchase eligible products, including fuel, lubricants and gas at participating Puma locations. The card is accepted at more than 80 Puma stations and affiliated outlets across Tanzania.

Speaking during the activation, Puma Energy Tanzania Managing Director Fatma Abdallah said the company continues to explore ways to make its products and services more valuable to customers while strengthening their relationship with the brand.

“Our customers are at the heart of our business, and we continuously look for ways to make their experience with Puma more rewarding and convenient. Through PRIS, customers can earn rewards from qualifying purchases, while the Puma Elite Card provides a practical way to manage fuel spending. By bringing these solutions closer to customers, we want more people to understand the benefits available to them and how they can make the most of them,” said Ms Abdallah.

VODACOM TANZANIA FOUNDATION: MADAWATI 1,000 NA MIRADI MBALIMBALI KUBORESHA ELIMU KUPITIA NYERERE CYCLING TOUR 2026

Afisa Miradi ya Jamii wa Vodacom Tanzania Foundation, Deborah Kaluzi (kulia), akikabidhi dawati kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Makumbusho, Yasini Shehaghilo (kushoto), huku Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Archie James Killo (wa pili kushoto), na Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour, Gabriel Landa (wa pili kulia), wakishuhudia. Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia kupitia Nyerere Cycling Tour 2026.

Oktoba 9, 2026 – Vodacom Tanzania Foundation imeendelea kuunga mkono juhudi za kuboresha sekta ya elimu na kuendeleza jamii kupitia Nyerere Cycling Tour 2026, kwa kushirikisha wadau katika miradi inayolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira.

Kupitia mpango huo, madawati yametolewa kwa Shule ya Msingi Makumbusho, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha wanafunzi wanapata vifaa muhimu vya kujifunzia na kusoma katika mazingira bora.

Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour, Gabriel Landa (kushoto), akishiriki zoezi la upandaji miti pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania Foundation za kuhifadhi mazingira kupitia Nyerere Cycling Tour 2026.

Akikabidhi madawati hayo, Afisa Miradi ya Jamii wa Vodacom Tanzania Foundation, Deborah Kaluzi, alisema juhudi hizo zinaakisi dhamira ya taasisi hiyo ya kuchangia upatikanaji wa elimu bora na maendeleo endelevu ya jamii.

Ushirikiano huo unahusisha pia Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour, Gabriel Landa, pamoja na wadau wa elimu wanaoshiriki katika kuhamasisha na kutekeleza miradi ya maendeleo katika jamii zinazopitiwa na msafara huo wa waendesha baiskeli.

Mbali na ugawaji wa madawati, mpango huo unalenga kusaidia shule kupitia ujenzi na ukarabati wa madarasa pamoja na utekelezaji wa miradi mingine ya kijamii inayochangia kuboresha huduma za elimu na mazingira ya kujifunzia.

Friday, 9 October 2026

VODACOM YAONGEZA AKIBA YA DAMU NCHINI KUPITIA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare, akichangia damu jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2026, katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yenye kaulimbiu “Zaidi ya Huduma ni Ukaribu!”, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza akiba ya damu na kuokoa maisha.

Dar es Salaam, Tanzania, 8 Oktoba 2026 — Vodacom Tanzania Plc imeendesha zoezi la uchangiaji damu jijini Dar es Salaam ikiwa sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, katika jitihada za kuongeza akiba ya damu katika Benki ya Damu Taifa na kusaidia kuokoa maisha ya watu wanaohitaji huduma hiyo.

Zoezi hilo lililofanyika Oktoba 7, 2026, liliwakutanisha wafanyakazi wa Vodacom Tanzania pamoja na wateja waliojitolea kuchangia damu, likisisitiza umuhimu wa kuunganisha huduma bora kwa wateja na mchango chanya kwa jamii.

Baadhi ya washiriki waliojitolea kuchangia damu katika zoezi lililoandaliwa na Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2026, wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, kwa lengo la kuongeza akiba ya damu katika Benki ya Damu Taifa na kuokoa maisha.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare, alikuwa miongoni mwa waliojitokeza kuchangia damu katika zoezi hilo, akionesha umuhimu wa kujitolea na kushiriki katika shughuli zinazolenga kuimarisha ustawi wa jamii.

Uchangiaji damu ni mchango muhimu katika sekta ya afya, kwani damu inayokusanywa hutumika kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu wakati wa matibabu, upasuaji na katika kukabiliana na dharura mbalimbali za kiafya.

Mmoja wa wateja wa Vodacom Tanzania akifanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuchangia damu jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2026, katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yenye kaulimbiu “Zaidi ya Huduma ni Ukaribu!”

BANK OF TANZANIA SELLS 5.1 TONNES OF GOLD AS PRICES RISE

Dar es Salaam; October 9, 2026 - The Bank of Tanzania (BoT) sold 5.1 metric tonnes of gold from its reserves last week as prices rose, reflecting its strategy of actively managing bullion holdings to strengthen foreign exchange reserves and support the Tanzanian shilling.

BoT Governor Emmanuel Tutuba disclosed the sale to reporters in Dar es Salaam, saying the central bank held 35.4 tonnes of gold before the transaction.

“We continue to buy and sell depending on when the price is favourable,” Tutuba said, explaining that the bank sells gold when market conditions present an opportunity to realise value and refrains from selling when prices are less favourable.

“If the price is favourable, we sell on any given day. If the price falls, we do not sell,” he added.

BoT Adopts Active Gold Reserve Management Strategy

Tutuba said the central bank treats gold as an actively managed reserve asset rather than simply accumulating bullion over time. The strategy involves purchasing gold to build reserves and selling part of the holdings when favourable market conditions allow the bank to realise gains.

He noted that the bank's relevant departments closely monitor market movements and related calculations to determine appropriate buying and selling decisions.

AKIBA COMMERCIAL BANK REAFFIRMS COMMITMENT TO GOING THE EXTRA MILE FOR CUSTOMERS

Dar es Salaam, Tanzania, 8 October 2026 – Akiba Commercial Bank Plc (ACB) has reaffirmed its commitment to enhancing customer experiences as it celebrates Customer Service Week 2026 under the theme “Going the Extra Mile – Kwenda Hatua ya Ziada kwa Ajili ya Wateja Wetu.”

Speaking during a customer engagement event held at the Bank’s Main Branch in Dar es Salaam, ACB Chief Operating Officer, Ms. Juliana F. Swai, said the Bank’s approach to customer service goes beyond meeting expectations. It involves listening to customers, understanding their needs, addressing their challenges and continuously improving their banking experiences.

Ms. Swai thanked customers for their continued trust in ACB and for choosing the Bank as a partner in their financial and business development journeys.

“Going the Extra Mile is not simply about doing what customers expect us to do. It is about doing more, listening to their needs, understanding their challenges and finding ways to make their banking experience easier, faster and better,” she said.

Twende Kidijitali: Making Banking More Convenient

Ms. Swai highlighted ACB’s continued digital transformation agenda through its Twende Kidijitali initiative, which encourages customers to embrace convenient, accessible and secure digital banking solutions.

Through ACB Mobile, Internet Banking, VISA, ACB LIPA and Akiba Wakala, customers can access a range of banking services and conduct transactions without necessarily visiting a branch.

She emphasized that digital transformation is not just about introducing technology but also about using it to improve the overall customer experience.

“Our objective is to save our customers’ time, provide greater convenience and enable them to access banking services wherever they are,” Ms. Swai said.

NMB YAZINDUA DAWATI MAALUMU LA HUDUMA KWA WATEJA WENYE ULEMAVU

Dar es Salaam - Oktoba 8, 2026: Benki ya NMB imezindua Dawati Maalumu la Huduma kwa Wateja Wenye Ulemavu, likiwa na huduma ya mawasiliano ya video inayosaidiwa na wakalimani wa lugha ya alama, katika hatua inayolenga kuimarisha ujumuishi wa kifedha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki nchini.

Dawati hilo lililoanzishwa katika Kituo cha Mawasiliano cha NMB litahudumia wateja wenye ulemavu wa kusikia, kuona na viungo. Kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kupata msaada kwa kupiga namba ya simu ya bure 0800 002 002, kutumia huduma ya video kupitia WhatsApp inayosaidiwa na wakalimani wa lugha ya alama, au kutembelea matawi ya NMB nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema huduma hiyo inalenga kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata huduma za kibenki kwa heshima na usawa.

Alieleza kuwa dawati hilo pia litasaidia kulinda faragha za wateja na kupunguza utegemezi wao kwa watu wengine wanapohitaji kupata huduma za kifedha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Nemes Temba, aliipongeza NMB kwa kuanzisha huduma hiyo, akisema itasaidia kupunguza vikwazo vya mawasiliano na kuwawezesha watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika matumizi ya huduma za kifedha nchini.

Thursday, 8 October 2026

KOMBE LA EPL KUTUA TANZANIA, GUINNESS KUWAPA MASHABIKI FURSA YA KULISHUHUDIA DAR ES SALAAM

Dar es Salaam - Oktoba 8, 2026: Mashabiki wa Ligi Kuu ya England nchini Tanzania wanajiandaa kushuhudia tukio la kipekee baada ya Kombe la Ligi hiyo kutua rasmi nchini kwa mara ya kwanza kupitia Guinness, Mdhamini Mkuu wa Bia wa Ligi Kuu ya England.

Kombe hilo litawasili nchini Ijumaa, Oktoba 9, 2026, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa tatu asubuhi, kabla ya kuzungushwa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam ili kuwapa mashabiki fursa ya kuliona kwa karibu.

Kwa mashabiki wa EPL ambao wamezoea kuliona Kombe hilo likikabidhiwa baada ya msimu kumalizika kupitia televisheni, safari hii watapata nafasi ya kuliona moja kwa moja katika jiji lao.

Baada ya kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kombe hilo litahamia The Super Dome, Masaki, ambako kutakuwa na hafla maalum itakayowapa wageni na mashabiki fursa ya kuliona kwa karibu zaidi na kupiga picha nalo.

Guinness Kuleta Uzoefu wa EPL Karibu na Mashabiki

Akizungumzia ujio wa Kombe hilo, Mkurugenzi wa Ubunifu na Masoko wa Serengeti Breweries Limited (SBL), Henry Esiaba, alisema Guinness inaleta uzoefu wa EPL karibu zaidi na mashabiki wa soka nchini.

“Mashabiki wa Tanzania wana mapenzi makubwa na Ligi Kuu ya England na kila wiki wanafuatilia mechi, wanajadili timu zao na kusherehekea pamoja. Safari hii tunataka kuwapa nafasi ya kuona Kombe lenyewe kwa karibu na kuwa sehemu ya tukio hili. Ni fursa kwa mashabiki kupata uzoefu tofauti na ule wanaoupata wanapotazama mechi kwenye televisheni,” alisema Esiaba.

 

Burudani ya soka itaendelea Jumamosi, Oktoba 10, ambapo mashabiki watakutana katika Uwanja wa KMC, Mwenge, kwa Guinness Matchday.

Katika tukio hilo, mashabiki watapata fursa ya kushuhudia kwa pamoja mechi za Ligi Kuu ya England kupitia skrini kubwa, ikiwemo mchezo wa Arsenal dhidi ya Leeds pamoja na Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur.