Singapore; Oktoba 22, 2026 – Kundi la Benki ya CRDB limefanya mazungumzo ya kimkakati nchini Singapore kwa lengo la kufungua fursa mpya za biashara za kimataifa, kuimarisha ufanisi wa shughuli za benki na kuendeleza huduma bunifu za kidijitali kwa wateja wake.
Mazungumzo hayo yameongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bank Group, Prof. Neema Mori, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi hilo, Dkt. Abdulmajid Nsekela, na kuhusisha taasisi za benki, wabunifu wa teknolojia za kifedha na taasisi za elimu.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kutumia teknolojia za kisasa, ikiwemo akili unde (AI), kuboresha utoaji wa huduma za kifedha, kupunguza muda wa kushughulikia maombi ya mikopo, kurahisisha malipo ya kimataifa na kuimarisha usalama wa huduma za kidijitali.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Prof. Mori amesema CRDB Bank Group inalenga kutumia ubunifu wa kiteknolojia kuongeza ufanisi wa shughuli zake, kuimarisha usalama na kuongeza thamani inayotolewa kwa wateja.
Amesisitiza pia umuhimu wa utawala bora na usimamizi wa vihatarishi katika kuhakikisha matumizi ya teknolojia yanaenda sambamba na ulinzi wa maslahi ya wateja, uaminifu na ubora wa huduma za benki.
Kwa upande wake, Dkt. Nsekela amesema ushirikiano huo unalenga kuwezesha utoaji wa huduma za kifedha zilizo za haraka, rahisi na zinazopatikana kwa wateja bila kujali mahali walipo.
Ameeleza kuwa mazungumzo hayo yameweka msingi wa kuanzisha miradi ya majaribio na kubadilishana ujuzi na uzoefu, hatua zinazotarajiwa kusaidia kuendeleza huduma za kidijitali na kupanua wigo wa ujumuishi wa kifedha katika masoko ambayo CRDB Bank Group inahudumia.
Ushirikiano huo unaonesha dhamira ya CRDB Bank Group ya kuendelea kutumia teknolojia na ubunifu kuimarisha ushindani wake, kurahisisha biashara za kimataifa na kuboresha uzoefu wa wateja katika mazingira ya sekta ya fedha yanayoendelea kubadilika.
Kupitia hatua hizo, CRDB inalenga kuimarisha nafasi yake katika utoaji wa huduma za kisasa za kifedha na kuchangia ukuaji wa biashara, uwekezaji na ujumuishi wa kifedha katika masoko yake.
Endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari za hivi karibuni kuhusu benki, biashara, uwekezaji, teknolojia za kifedha na maendeleo ya uchumi.
Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii:
- LinkedIn: https://www.linkedin.com/feed/
- Facebook: https://www.facebook.com
- Instagram: https://www.instagram.com
- X (Twitter): https://x.com/home
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)


No comments:
Post a Comment