Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_211026

Stanbic Bank Banner_201026

Monday, 26 October 2026

VODACOM YAENDELEA KUKUZA GOLF NCHINI, PAUL CHIDALE AIBUKA KINARA VODACOM TANZANIA OPEN 2026

Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mshindi kutoka Malawi Paul Chidale, tuzo baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom Tanzania Open 2026 jijini Arusha. Chidale alimaliza mashindano hayo kwa mikwaju 289 na kujinyakulia Sh9.35 milioni, akifuatiwa na Mtanzania Nuru Mollel aliyeshika nafasi ya pili kwa mikwaju 293 na Robinson Owiti kutoka Kenya aliyemaliza wa tatu kwa mikwaju 294.
Rais wa chama cha Golf nchini (Tanzania Golf Union - TGU) Gilman Kasiga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa Vodacom Tanzania Open katika kukuza ushindani na kuendeleza mchezo wa golf nchini, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika Kili Golf Course jijini Arusha, Oktoba 22 hadi 25, 2026. Mashindano hayo yaliwakutanisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi mbalimbali wakishindania zawadi za jumla ya Sh40 milioni.
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mchezaji golf kutoka Malawi, Paul Chidale, mfano wa hundi ya Sh9.35 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom Tanzania Open 2026 jijini Arusha. Chidale alimaliza mashindano hayo ya siku nne kwa jumla ya mikwaju 289, akimzidi Mtanzania Nuru Mollel aliyeshika nafasi ya pili kwa mikwaju 293 na Robinson Owiti kutoka Kenya aliyemaliza nafasi ya tatu kwa mikwaju 294.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Tanzania Plc, Joseph Sayi, akishiriki mchezo wa gofu wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye mazoezi wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha katika viwanja vya Kili Golf Club jijini Arusha. Mashindano hayo ya siku nne yaliwakutanisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi nyingine mbalimbali, wakishindania zawadi za jumla ya Sh40 milioni.
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, akishiriki mchezo wa gofu wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika katika viwanja vya Kili Golf Club jijini Arusha, Oktoba 22–25, 2026.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC na wadau mbalimbali, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kilele cha mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha. Mashindano hayo yaliwashirikisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi nyingine, yakiwa sehemu ya mchango wa Vodacom katika kukuza mchezo wa gofu, kuendeleza vipaji na kuimarisha ushindani wa mchezo wa gofu nchini.

No comments:

Post a Comment