Watendaji wa Benki ya NMB, wakiwa katika picha wa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Binguni baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa vifaa vya kuezekea shule hiyo huko Binguni. |
NMB imetoa jumla ya vitanda 42 ambapo kati ya hivyo vipo vya kujifungulia, vya kufanyia uchunguzi na vya kulalia wagonjwa wodini; vilivyoenda katika Vituo vya Afya saba ikiwemo Bumbwini, Walezo Jeshini, Kizimbani, Chuini, Mwera, Chwaka na Unguja Ukuu pamoja na mabati yaliopelekwa kukamilisha ujenzi wa madarasa ya shule za Kizimkazi, Makunduchi na Binguni zilizopo mkoa wa Kusini na Shule za Mbuzini na Mtoni Kigomeni za Mjini Magharibi.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara za Kati wa NMB, Filbert Mponzi alisema kuwa NMB imekuwa ikitenga sehemu ya faida na kuirudisha kwa jamii huku akibainisha kuwa mbali na misaada hiyo NMB wamekua wakitoa elimu ya kutunza fedha kwa wanafunzi wa shule mbali mbali, ambayo inawafahamisha namna ya kutumia na kutunza fedha kwa maisha ya baadae.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid, ameipongeza Benki ya NMB kwa misaada mbalimbali wanayoendelea kutoa kwa jamii ya wananchi wa Zanzibar na kuwaomba kutochoka kutoa misaada visiwani Zanzibar.
Aidha, Benki ya NMB imekuwa mdhamini mkuu wa kikao kazi cha mwaka cha Jeshi la Polisi kilichofanyika katika bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbey jijini Dar es salaam ambapo kikao hicho kilifunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Wakuu wengine wa Majeshi mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment