Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Tuesday, 28 July 2026

SELCOM MICROFINANCE BANK YAZINDUA SELCOM BUSINESS KUPUNGUZA GHARAMA ZA MIAMALA KWA WAFANYABIASHARA

Julai 28, 2026 | Dar es Salaam

Katika hatua inayotarajiwa kuongeza kasi ya matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali nchini, Selcom Microfinance Bank imezindua Selcom Business, akaunti mpya ya benki ya kidijitali inayolenga kuwapa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), kampuni na watengenezaji wa mifumo (developers) huduma za benki zenye gharama nafuu, uunganishaji wa mifumo kwa haraka na usimamizi bora wa fedha za biashara.

Uzinduzi huo unakuja wakati ambapo biashara nyingi nchini zinaendelea kutafuta njia za kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi kupitia teknolojia. Selcom Microfinance Bank inaeleza kuwa huduma hiyo imebuniwa kushughulikia changamoto mbili zinazowakabili wafanyabiashara wengi—gharama kubwa za kufanya miamala na muda mrefu unaochukuliwa kuunganisha mifumo yao na taasisi za kifedha.

Kupitia Selcom Business, biashara zinaweza kufanya uhamisho wa fedha kwenda benki zote za ndani, mitandao ya simu na wafanyabiashara wanaotumia TanQR kwa gharama ya kuanzia TZS 100 kwa kila muamala. Vilevile, biashara zinaweza kujisajili na kupata REST APIs moja kwa moja kupitia dashboard ndani ya saa chache, bila kulazimika kupitia taratibu ndefu za makubaliano au kulipa ada za uunganishaji wa mifumo.

Mabando Matatu kwa Mahitaji Tofauti ya Biashara

Ili kukidhi mahitaji ya makundi mbalimbali ya biashara, Selcom Business imeanzisha mabando matatu ya kila mwezi yenye viwango tofauti vya gharama za miamala.

BandoAda ya Mwezi (Siku 30)Miamala hadi TZS 20 Milioni (Benki, Mitandao ya Simu na TanQR)TZS 20–50 Milioni(Benki za Ndani)Zaidi ya TZS 50 Milioni(Benki za Ndani)
Bando PoaTZS 49,999TZS 250TZS 4,000TZS 8,000
Bando BombaTZS 99,999TZS 150TZS 2,500TZS 5,000
Bando MaxTZS 199,999TZS 100TZS 1,500TZS 3,000

Benki hiyo imeeleza kuwa hakuna kikomo cha idadi ya miamala inayoweza kufanywa ndani ya mwezi. Kadri biashara inavyochagua bando kubwa zaidi, ndivyo gharama ya kila muamala inavyopungua. Viwango vyote vinajumuisha VAT na ushuru wa bidhaa.

Ubunifu Unaolenga Kuongeza Ufanisi wa Biashara

Mbali na gharama nafuu za miamala, Selcom Business imejengwa juu ya huduma tatu kuu ambazo benki inaamini zitabadilisha namna biashara zinavyofanya shughuli zao za kifedha.

Kwanza ni bei nafuu za miamala, ambapo biashara zinaweza kufanya uhamisho wa fedha kwa gharama ya kuanzia TZS 100 kwa kila muamala kupitia Bando Max bila kikomo cha idadi ya miamala ndani ya mwezi.

Pili ni API za kujihudumia, zinazowawezesha wafanyabiashara kupata API credentials, kuweka IP whitelist, callback URLs na kusimamia ukwasi (liquidity) kupitia dashboard bila kusubiri taratibu za muda mrefu za uidhinishaji. Mfumo huo unapatikana kupitia REST APIs kwa huduma za usimamizi wa akaunti, malipo, uhamisho wa fedha na makusanyo kupitia Lipa Number.

Tatu ni udhibiti wa matumizi ya fedha za biashara, ambapo waajiri wanaweza kufanya malipo ya mishahara, malipo ya makundi na matumizi ya petty cash kwa hatua tatu tu. Mfumo pia una ufuatiliaji wa matumizi kwa wakati halisi, stakabadhi za kidijitali na viwango tofauti vya ruhusa kwa watumiaji kulingana na majukumu yao.

Maro: Tunarahisisha Biashara Kufanya Miamala na Kuunganisha Mifumo

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Selcom Microfinance BankAloyse Maro, alisema muda na gharama za kufanya miamala vina mchango mkubwa katika ufanisi wa biashara.

"Kupitia Selcom Business, wateja wanaweza kujisajili kwenye bando la kila mwezi na kufanya miamala kwa gharama ya kuanzia TZS 100 kwa muamala, bila kikomo cha idadi ya miamala. Pia tumerahisisha uunganishaji wa API kwa mfumo wa kujihudumia, unaowezesha biashara kuunganisha mifumo yao na Benki kwa haraka, kwa urahisi na bila vikwazo," amesema Maro.

Selcom Microfinance Bank, ambayo inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inaamini kuwa uzinduzi wa Selcom Business utawezesha biashara nyingi zaidi kutumia huduma za benki za kidijitali kwa gharama nafuu na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa fedha zao.


Endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari za uhakika kuhusu sekta ya benki, fedha, biashara na maendeleo ya uchumi Tanzania na Afrika.

No comments:

Post a Comment