Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Tuesday, 28 July 2026

NMB YAONGEZA NGUVU KWA SEKTA BINAFSI KUPITIA MASULUHISHO MAALUM YA KIFEDHA

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kulia), Mkuu wa Idara ya Biashara NMB, Deogratias Shirima (kushoto) wakifurahia tuzo za Benki Bora ya Huduma kwa Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (SMEs), zilizotolewa na Euromoney na Global Finance wakati wa hafla iliyowakutanisha NMB na Mtandao wa Wafanyabiashara Wakubwa Wanaohudumiwa na benki hiyo ‘NMB Business Executive Network’ iliyofanyika Ijumaa jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TTI, Leonard Shayo na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya High Quality, Selina Letara.

Dar es Salaam – Benki ya NMB imeendelea kuimarisha ushirikiano wake na sekta binafsi kwa kuahidi kuendelea kutoa masuluhisho ya kifedha yanayolengwa kukidhi mahitaji maalum ya sekta mbalimbali za uchumi, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa biashara na maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Ahadi hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki wakati wa Jukwaa la NMB Business Executive Network 2026, lililowakutanisha zaidi ya wafanyabiashara 300 kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa lengo la kujadili fursa za biashara, changamoto za kifedha na njia za kuimarisha ushirikiano kati ya benki na sekta binafsi.

Akizungumza katika jukwaa hilo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, alisema benki hiyo imeanzisha Madawati ya Kisekta (Sector Desks) yanayotoa huduma na ushauri wa kifedha unaoendana na mahitaji ya sekta mbalimbali ikiwemo madini, ujenzi, utalii, kilimo, afya na elimu.

Alieleza kuwa kupitia mkakati huo, NMB imeboresha upatikanaji wa bidhaa na huduma za kifedha zinazosaidia wafanyabiashara kuendesha na kupanua shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Miongoni mwa masuluhisho yanayotolewa kupitia madawati hayo ni pamoja na Asset FinancingBid BondAdvance Payment Guarantee na Performance Guarantee, huduma zinazowawezesha wafanyabiashara kupata mtaji, kushiriki katika zabuni na kutekeleza miradi kwa ufanisi huku wakijenga imani kwa washirika wao wa biashara.

NMB Yajivunia Tuzo Mbili za Kimataifa

Katika jukwaa hilo, NMB pia ilitambulisha mafanikio yake ya kimataifa baada ya kutunukiwa tuzo mbili muhimu mwaka huu.

Benki hiyo ilitangazwa kuwa Benki Bora kwa Wafanyabiashara Tanzania 2026 na jarida la Euromoney, pamoja na kutwaa tuzo ya Benki Bora kwa Wafanyabiashara Tanzania 2026 kutoka jarida la Global Finance.

Tuzo hizo zinathibitisha kutambuliwa kwa NMB katika kiwango cha kimataifa kutokana na ubora wa huduma zake, ubunifu wa bidhaa za kifedha na mchango wake katika kusaidia ukuaji wa biashara nchini.

Kuimarisha Ushirikiano na Sekta Binafsi

Mbali na kuonesha bidhaa na huduma zake, Jukwaa la NMB Business Executive Network 2026 lilitoa fursa kwa wafanyabiashara na viongozi wa benki kujadiliana kuhusu changamoto na mahitaji ya sekta binafsi pamoja na mikakati ya kuendelea kuimarisha ushirikiano unaochochea uwekezaji, ukuaji wa biashara na maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Kwa kuendelea kubuni masuluhisho yanayolenga mahitaji halisi ya sekta mbalimbali, NMB inaimarisha nafasi yake kama mshirika muhimu wa maendeleo ya biashara nchini na benki inayowezesha wafanyabiashara kufikia malengo yao ya ukuaji.


Endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari za uhakika kuhusu sekta ya benki, fedha, biashara na uchumi nchini Tanzania na Afrika Mashariki.





No comments:

Post a Comment