Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Monday, 30 November 2020
BENKI YA NMB TAASISI KINARA KUSAIDIA JAMII ELIMU NA AFYA
Benki ya NMB imetajwa kuwa taasisi kinara ya kifedha katika Manispaa ya Ilala mkoani Dar es salaam inayotumia kiasi kikubwa cha pato lake kuisaidia jamii katika Nyanja za Elimu na Afya kupitia Mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Kupitia mpango huo Benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kati ya taasisi nyingi za fedha kwenye mkoa huo, ambayo imekuwa ikishirikiana na serikali kuhakikisha huduma bora za kiafya na elimu zinapatika kwa wananchi.
Hatua hiyo ilipelekea Manispaa hiyo kuipatia Benki hiyo cheti cha Pongezi, kwenye hafla ya kufunga kongamano la siku ya mlipakodi lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika hafla hiyo, Manispaa ya Ilala ilikabidhi vyeti kwa taasisi, mashirika, makampuni na wafanyabiashara 100 Bora wa Ulipaji Kodi Bila Shuruti, huku NMB ikipongezwa na kutunukiwa kama Kinara wa matumizi ya pato lake katika kusaidia jamii.
Akiongea katika kongamano hilo, Meneja Uwajibikaji Miradi ya Jamii - Lilian Kisamba, alisema kuwa toka mwaka 2020 hadi leo Benki hiyo imetoa shilingi Milioni 218.9 katika mkoa wa Dar es salaam kwenye miradi inayogusa jamii moja kwa moja.
Alisema kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha Shilingi Milioni 153.9 zimetumika katika sekta ya Elimu na Millioni 65 ikienda kwenye Afya, ambapo jumla ya shule 26 zimepokea madawati 300 na kusaidia watoto 3900 ambao walikuwa wanakaa chini kwa kukosa madawati.
Aliongeza kuwa shule sita zilipatikwa msaada wa mabati yenye thamni ya shilingi Milioni 40, ambapo mkuu wa Wilaya hiyo Ng'wilubuzu Ludigija wakati akikabidhi cheti hicho cha pongeza aliishiruku benki hiyo kwa juhudi zake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment