Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 15 December 2025

VODACOM YAENDELEA KUSHEREHEKEA MSIMU WA SIKUKUU, YAGAWA MAKAPU YA VODA ARUSHA

Arusha, Tanzania – Vodacom Tanzania Plc imeendelea kuonyesha shukrani kwa wateja wake kupitia zoezi la ugawaji wa Makapu ya Voda, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya msimu wa sikukuu unaoendelea kote nchini.

Katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Soko Kuu jijini Arusha, Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania Plc, George Venanty, alikabidhi Kapu la Voda kwa mmoja wa wateja wa kampuni hiyo, Bi. Regina Julius. Tukio hilo ni sehemu ya kampeni ya Vodacom inayolenga kusherehekea pamoja na wateja wake na kuimarisha uhusiano wa karibu kati ya kampuni na jamii inayohudumiwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, alieleza kuwa zoezi la kugawa makapu ni ishara ya kuthamini uaminifu wa wateja wake, sambamba na kushiriki furaha ya msimu wa sikukuu. Kampuni hiyo imekuwa ikiendesha zoezi hili katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwafikia wateja wa makundi tofauti na kuwapa zawadi kama njia ya kusema asante.

Wateja waliopokea makapu hayo walionesha furaha na shukrani zao kwa Vodacom, wakieleza kuwa hatua hiyo inaongeza ukaribu na kuifanya kampuni ionekane kuwa sehemu ya familia zao, hasa katika kipindi hiki cha sikukuu.

Kupitia kampeni hii, Vodacom Tanzania inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuwa karibu na wateja wake, si tu kwa kutoa huduma bora za mawasiliano, bali pia kwa kushiriki katika matukio yanayoleta furaha na mshikamano katika jamii.

No comments:

Post a Comment