Benki ya Exim Tanzania imefanikiwa kuendesha droo ya kwanza ya kampeni yake ya Chanja Kijanja, Dili Ndio Hili, ambapo washindi watano waliibuka na zawadi ya Sh. 100,000 kila mmoja, ikiwa ni mwanzo wa msimu wa ushindi kwa wateja wa benki hiyo.
Akizungumza wakati wa droo hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim, Bw. Silas Matoi, alieleza kuwa kampeni hiyo inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia kadi za Exim kufanya malipo ya bidhaa na huduma, huku akisisitiza kuwa fursa za ushindi ni nyingi zaidi zinazoendelea.
“Hii ni mwanzo tu wa kampeni. Kila wiki tutakuwa tunatangaza washindi, na kila mwezi washindi 10 watajishindia Sh. 200,000 kila mmoja. Aidha, katika droo kuu, washindi watapata zawadi nono za Sh. milioni 5, Sh. milioni 10, na mshindi mkuu atajishindia Sh. milioni 15,” alisema Bw. Matoi.
Droo hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki ilisimamiwa kwa uwazi na uwajibikaji, ikihusisha Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya Kidijitali wa Benki ya Exim, Bw. Benedict Mwinula, pamoja na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Rodgers Biteko.
Kupitia kampeni ya Chanja Kijanja, Benki ya Exim inalenga kuhamasisha matumizi ya malipo yasiyotumia fedha taslimu, huku ikiwapa wateja wake nafasi ya kushinda zawadi kila wanapotumia kadi za Exim kulipia bidhaa au huduma mbalimbali.
Kwa wateja wa Exim na Watanzania kwa ujumla, huu ni wakati sahihi wa kuchanja kijanja — kwani kila muamala unaweza kukuweka hatua moja karibu na ushindi wa zawadi kubwa hadi kufikia Sh. milioni 15.


.jpeg)
No comments:
Post a Comment