Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Saturday, 20 December 2025

VODACOM YAGUSA MIOYO YA WATEJA NJOMBE KUPITIA KAMPENI YA “TUPO NAWE TENA NA TENA”

Njombe, Tanzania – Katika kuendeleza ukaribu wake na wateja pamoja na kusherehekea msimu wa sikukuu, Vodacom Tanzania imeendelea kuwagusa wateja wake kupitia kampeni maalum ya “Tupo Nawe Tena na Tena”, inayolenga kugawa makapu ya sikukuu kwa wateja katika mikoa mbalimbali nchini.

Hivi karibuni, kampeni hiyo ilifika mkoani Njombe ambapo Meneja Mauzo wa Vodacom Njombe, Malika Malika, alimkabidhi kapu la sikukuu mmoja wa wateja waaminifu wa Vodacom, Dickson Mhapu, kama ishara ya kuthamini mchango na uaminifu wao kwa kampuni hiyo ya mawasiliano.

Tukio hilo lilishuhudiwa na Msimamizi wa Mauzo wa Vodacom eneo la Ilembula, Anania Kiwanga, pamoja na wateja na wadau mbalimbali wa Vodacom, na kufanyika mwishoni mwa wiki katika mji wa Njombe.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Malika Malika alisema kampeni ya “Tupo Nawe Tena na Tena” ni sehemu ya dhamira ya Vodacom ya kuwa karibu na wateja wake, hasa katika kipindi cha sikukuu ambapo mshikamano na kushirikiana ni muhimu zaidi.

Tunathamini sana mchango wa wateja wetu katika safari ya Vodacom. Kupitia kampeni hii, tunasherehekea pamoja nao na kuwashukuru kwa kutuamini kwa miaka mingi,” alisema Malika.

Mbali na kusherehekea msimu wa sikukuu, kampeni hiyo pia inaashiria hitimisho la maadhimisho ya miaka 25 ya Vodacom Tanzania tangu kuanza kutoa huduma zake nchini, kipindi ambacho kampuni hiyo imeendelea kuwekeza katika ubunifu wa kiteknolojia, upanuzi wa mtandao na huduma jumuishi za kidijitali.

Vodacom imesisitiza kuwa kampeni ya “Tupo Nawe Tena na Tena” itaendelea kutekelezwa katika mikoa mingine nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuimarisha mahusiano na wateja na kuthibitisha kauli mbiu yake ya kuwa karibu na Watanzania wakati wote.



No comments:

Post a Comment