Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_211026

Stanbic Bank Banner_201026

Thursday, 21 July 2022

AIRTEL YAWAZAWADIA WASHINDI WA TESA KIMILIONEA ZAIDI GARI MPYA TOYOTA RAV4 PAMOJA NA TSHS 10 MILIONI

Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda (kulia) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa gari aina ya Toyota RAV4 mshindi wa droo kubwa ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA, John Mathayo ambaye ni mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam. Promosheni ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA ilikuwa inawapa fursa wateja na mawakala wa Airtel Money ya kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au gari mpya aina ya Toyota RAV4 pamoja na pesa taslimu Tshs 10 milioni kwenye droo kubwa ya mwisho kila wana wanavyofanya muamala wowote kwa kutumia huduma ya Airtel Money.
  • TESA KIMILIONEA ilikuwa ni wateja na mawakala wa Airtel Money kote nchini.
Dar es Salaam, Jumanne 20 Julai 2022: Airtel Tanzania leo imekabididhi zawadi kwa washindi wawili wa droo kubwa ya promosheni ya TESA KIMILIONEA INAEDELEA, mshindi mmoja amekabidhiwa gari mpya aina ya Toyota RAV4 na wa pili pesa taslimu Tshs 10 milioni.

Washindi hao ni John Mathayo, mkazi wa Bunju na mfanya biashara wa nyanya na Ibrahim Dyamwala ambaye ni mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam.
Wateja na Mawakala walikuwa na nafasi ya kuingia kwenye droo ya kwa kutumia moja ya huduma za kuweka pesa, kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa pesa, kulipia bili kwa kutumia huduma ya Airtel Money ya promosheni ya TESA ZAIDI KIMILIONEA na kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au gari mpya aina ya Toyota RAV4 na pesa taslimu Tshs 10 milioni kwenye droo kubwa.

Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tshs 10 milioni, Ibrahim Dyamwala ambaye ni mshindi wa droo kubwa ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA jijini Dar es Salaam. Promosheni ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA ilikuwa inawapa fursa wateja na mawakala wa Airtel Money ya kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au gari mpya aina ya Toyota RAV4 pamoja na pesa taslimu Tshs 10 milioni kwenye droo kubwa ya mwisho kila wana wanavyofanya muamala wowote kwa kutumia huduma ya Airtel Money. Kulia ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando na wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Airtel Money Maria Mwamyalla.

Kwa upande wake, mshindi wa zawadi ya Tshs 10 milioni Ibrahim Dyamwala alisema ‘Nilikuwa siamini kama ni kweli Naweza kuwa nimeshinda hii zawadi ya Tshs 10 milioni. Kwa leo nimeamini na nawashukuru Airtel kwani kwa sasa nitaweza kukamilisha ujenzi wa nyumba yangu pamoja na kuongeza uwekezaji kwenye kilimo. Naomba kuwahidi kuwa nitaendelea kutumia bidhaa za Airtel pamoja na kuwahimiza ndugu, jamaa na marafiki juu ya umuhimu wa kutumia Airtel Money.

WAZIRI WA KILIMO AKUTANA NA WAKULIMA WA NJE WA MIWA KILOMBERO

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (katikati) akizungumza na viongozi kutoka Kampuni ya Sukari ya Kilombero, Ephraim Mafuru - Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano (kulia) na Guy Williams - Mkurugenzi Mtendaji (kushoto) katika mkutano na wakulima wa miwa wa Kilombero uliofanyika tarehe 17 Julai huko Kilombero mkoani Morogoro.

Morogoro - Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe alifanya mkutano wa hadhara na wakulima wa nje wa miwa Kilombero ili kusikiliza changamoto zao katika azma ya kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo cha miwa. Mkutano huo wa hadhara ulifanyika Julai 17 katika kijiji cha Ruaha, Kilombero na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa maendeleo na maofisa wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero (KSCL) ambao ni wabia wakuu wa wakulima wa miwa Kilombero.

Baada ya kusikiliza changamoto mbalimbali, waziri huyo alikuja na maazimio na maelekezo kama ifuatavyo;

Miundombinu ya Umwagiliaji:
Waziri baada ya kusikiliza kero za wananchi juu ya changamoto zinazowakabili wakulima hao, aliwaeleza kuwa serikali itatengeneza miundombinu ya umwagiliaji na kuunda tume maalum ya kusimamia kilimo cha umwagiliaji nchini ambapo ofisi za umwagiliaji za halmashauri zitasimamia uendelevu wa miundombinu hiyo. Tume ya Umwagiliaji itafanya kazi na KSCL katika kuandaa mpango mkuu wa umwagiliaji kwa ajili ya KSCL na Wakulima kabla ya kuwakilisha mpango huo katika Wizara ya Kilimo.

Mbolea:
Kufuatia changamoto za upatikanaji wa mbolea uliopelekea kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo, Waziri aliwaeleza wakulima kuwa serikali inaendelea na mpango wa kuanzisha ruzuku ya mbolea kwa wakulima wote nchini ambayo itawanufaisha wakulima hao na kupunguza changamoto iliyopo ya ongezeko la bei.

Mbegu Bora:
Wakulima waliwasilisha changamoto zao za upatikanaji wa mbegu bora, tatizo linalochangiwa na ukosefu wa mitaji na utaalamu wa kuzalisha mbegu bora, hivyo kuathiri ubora wa mavuno yao. Baada ya mazungumzo mafupi na uongozi wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero, Waziri aliahidi kwa serikali itaendesha kitalu cha kuzalishia mbegu ambapo wakulima watapata mbegu bora kutoka serikalini. Kampuni ya Sukari ya Kilombero ilikubali kutoa ardhi ya hekari 400 kuiwezesha serikali kuendesha mradi huo wa uzalishaji mbegu.

"Ubora wa muwa ni mchakato kuanzia mbegu iliyopandwa, namna ulivyolima, namna ulivyovuna na namna unavyopeleka kiwandani. Nimesikia kilio cha upatikanaji wa mbegu, tunaanzisha kitalu cha hekta 400 cha serikali cha uzalishaji wa mbegu hapa kwenu." - Mhe. Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

TANZANIA TO RECEIVE SH2.4 TRILLION IMF LOAN


Dar es Salaam - Tanzania will receive a total of $1.046 billion (Sh2.4 trillion) from the International Monetary Fund (IMF) over 40 months in an effort to help the country’s economy to cope with consequences of war in Ukraine as it recovers from the effects of the global Covid-19 pandemic.

“Spillovers from the war in Ukraine are stalling the Tanzanian economy’s gradual recovery from the Covid-19 pandemic, exacerbating the country’s development and reform challenges to unleash its economic potential,” the IMF said in a statement that was availed to The Citizen yesterday.

During the past few months, Tanzania, just like many other countries in the world, has seen a rise in prices of a number of products, including fuel, wheat, fertilizer and cooking oil among others, primarily due to a rise in demand as the global economy recovers from the Covid-19 pandemic and a disruption of commodity delivery channels due to the war in Ukraine.

This has forced President Samia Suluhu Hassan’s administration to come up with a raft of measures in an effort to strike a balance between bringing down the spiralling cost of living and maintaining its tempo of investing in mega infrastructure projects while simultaneously creating an enabling environment for the private sector to thrive.

Though there was no immediate reaction from the government, it is common knowledge that the President Samia’s administration was subsidizing fuel prices to make it affordable to motorists and manufacturers.

In light of the developments, the IMF exuded its support to Tanzania’s economic stimulation plan, with its [IMF’s] experts saying the country will need help to carry out reforms and unleash its economic potential.

Wednesday, 20 July 2022

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YATUZWA NA HOSPITALI YA CCBRT KWA MCHANGO WA KUJENGA WODI YA KINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO

  • Ilichangia shillingi 8 bilioni kukamilisha wodi hiyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi tuzo kutoka Hospitali ya CCBRT Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa aliyepokea kwa niaba ya Asasi ya Vodacom Tanzania Foundation ikiwa ni shukrani ya mchango wa shilingi 8 bilioni waliotoa wakati wa ujenzi wa wodi ya kina mama wajawazito na watoto wachanga hospitalini hapo. Hafla ya ufunguzi wa jengo hilo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc kupitia asasi yake ya Vodacom Tanzania Foundation imepokea tuzo kutoka hospitali ya CCBRT ambapo wamekabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu ikiwa ni shukrani kwa mchango wake wa kuwezesha kujenga wodi ya kina mama wajawazito na watoto wachanga kwa hospitalini hapo. Kampuni hiyo iliwezesha ujenzi wa wodi kwa kutoa msaada wa shilingi 8 bilioni.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Rais Samia aliwapongeza Vodacom kwa kuwezesha suala hili na kwa namna gani wanajitoa kurudisha tabasamu kwa jamiii, huku akiongeza kwamba pamoja na hilo kampuni hiyo ina mradi wa m-mama ambao pia unalenga kuwasaidia wanawake wajawazito na watoto, hii inadhihirisha namna kampuni ya Vodacom iko karibu na jamii kupitia huduma za afya.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania Plc (aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya asasi ya Vodacom Tanzania Foundation) Linda Riwa alisema “sisi kama kampuni ya mawasiliano tunajua wajibu wetu kwa jamiii na malengo yetu makubwa ni kurudisha kwa jamiii kwa kile tunachokipata, ndio maana kupitia sekta ya afya tumekuwa mstari wa mbele mno.”

Asasi ya Vodacom Tanzania Foundation inasaidia maeneo mbalimbali ya kusaidia jamii hususan kwenye afya ambapo inaweza kusaidia wagonjwa wa fistula na watoto njiti.

TMSA KUTOA TUZO BORA ZA MASOKO TANZANIA

Mwenyekiti wa Bodi ya TMSA, Dkt. Emmanuel Chao (PhD) (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la ugawaji tuzo za masoko kwenye vipengele 14. Tukio hilo litafanyika Ijumaa tarehe 22 Julai 2022 katika jengo la PSSSF. Mwanzoni kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Josephine Msalilwa kutoka Coca-Cola ambao ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa tuzo hizo.

Dar es Salaam, 20 Julai 2022 - Katika nia ya kuhamasisha weledi zaidi katika sekta ya masoko nchini Tanzania, Chama cha Sayansi ya Masoko Tanzania (TMSA) kinatarajiwa kutoa tuzo katika vipengele 14 tofauti vya masoko kwa mwaka 2022.

Tuzo hizi za masoko 2022 zitafanyika Julai 22 2022 jijini Dar es Salaam, na tuzo hizi zimevutia kampuni kubwa kudhamini na kushiriki kwenye tukio hili.

Tangu mwaka wa 2021, TMSA imetumia tuzo hizo ili kuakisi juhudi na mafanikio ya watu binafsi, mashirika, na wasomi ambao wanaleta mabadiliko katika nyanja ya masoko.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Bodi ya TMSA, Dkt. Emmanuel Chao (PhD), alieleza jinsi masoko kuwa nguzo muhimu ili kuhakikisha ukuaji wa kampuni na kuleta faida. Alisema, "Katika biashara yoyote, idara ya masoko ni ya kipekee, kwani inajumuisha kati ya asilimia 30 na 40 ya bajeti ya biashara, na ndio kati ya msingi wa kudumisha biashara yoyote".

MITANANGE YA PRE-SEASON NDANI YA DStv


Endelea kutazama michuano ya Pre-Season ndani ya @dstvtanzania kupitia chaneli za SuperSport!

Alhamisi hii Man City atakipiga dhidi ya Club Americas kupitia SS EPL, 223!

Utabiri wako ni upi?

Lipia mapema kifurushi chako cha Compact TShs 51,000 tu kwa kupiga *150*53#

#DStvShangweka

ECOBANK WINS THE COVETED AFRICA'S BEST BANK, AFRICA'S BEST BANK FOR SMES, AND AFRICA'S BEST DIGITAL BANK AWARDS AT THE PRESTIGIOUS EUROMONEY AWARDS.

Ecobank Group Special Executive Advisor to the Group CEO, Cecilia Akintomide (centre) receives the Euromoney awards on behalf of Ecobank Group during the Euromoney Awards for Excellence in London.

LomĂ©, Togo, 18 July 2022 – During the prestigious Euromoney Awards, Ecobank won the coveted titles of 'Africa's Best Bank,' 'Africa's Best Bank for SMEs,' and 'Africa's Best Digital Bank.' The Euromoney Awards for Excellence, which have been running for 30 years, are highly regarded by the global banking industry.

Ade Ayeyemi, Chief Executive Officer of Ecobank Group, said: " I am very honoured by this recognition as the Pan African Bank that Africa and friends of Africa trust. Being responsive in real time to our clients has been an essential part of earning that trust. We have embraced technology to drive operational efficiency and enhance our offerings, service, and customer experience. We have prioritised our clients, placing their needs and experience at the heart of our decision-making and operations. Our unparalleled African presence and operations have also earned us an enviable place as a true Pan African Bank with a depth of knowledge that distinguishes our products and delivery. It is a great honour for all Ecobankers to be recognised for these sustained efforts."

UNITED BANK FOR AFRICA (UBA) GROUP EXPANDS TO EMEA, LAUNCHES BANKING OPERATIONS IN DUBAI INTERNATIONAL FINANCIAL CENTRE, DUBAI

Executive Director, Treasury and International Banking, United Bank for Africa (UBA), Mr. Ndubisi Chiugo; Chief Executive Officer, Dubai International Financial Centre (DIFC) Authority, Prince Arif Amiri; Group Chairman, United Bank for Africa (UBA), Mr. Tony O. Elumelu; Governor, Dubai International Financial Centre (DIFC), His Excellency Essa Kazim; Group Managing Director/CEO, United Bank for Africa (UBA) , Mr. Kennedy Uzoka; and Managing Director, UBA (DIFC), Mr. Vikrant Bhansali, at the official launch of UBA (DIFC), in Dubai, United Arab Emirates (UAE), on Thursday.
Chief Executive Officer, Dubai International Financial Centre (DIFC) Authority, Prince Arif Amiri; Group Chairman, United Bank for Africa (UBA), Mr. Tony O. Elumelu; Governor, Dubai International Financial Centre (DIFC), His Excellency Essa Kazim; Group Managing Director/CEO, United Bank for Africa (UBA) , Mr. Kennedy Uzoka; and Managing Director, UBA (DIFC Branch), Mr. Vikrant Bhansali, at the official launch of UBA (DIFC Branch), in Dubai, United Arab Emirates (UAE), on Thursday.

The UBA branch in the DIFC will service corporate & financial Institutions and customers across the Middle East with a core focus on correspondent banking, relationship management and advisory services

Access Multimedia Content

LAGOS, Nigeria, July 18, 2022/ -- The United Bank for Africa (UBA) (www.UBAGroup.com), Africa’s global bank has been in operation for over seven decades. Today, the group is present in 20 African countries, the United Kingdom, the United States of America and France. The bank has extended its operations to the United Arab Emirates with the official launch of its new branch at the Dubai International Financial Centre (DIFC).

United Bank for Africa Plc (DIFC Branch) will operate under the Category 4 license and will be regulated by the Dubai Financial Services Authority (DFSA), the financial regulatory agency of the special economic zone, the Dubai International Financial Centre.

The UBA branch in the DIFC will service corporate & financial Institutions and customers across the Middle East with a core focus on correspondent banking, relationship management and advisory services.

Through this new expansion, the UBA Group will be able to harness opportunities in the Middle East, Africa and South Asia (MEASA), which comprise of 72 countries with an approximate population of 3 billion and a nominal GDP of US$7.7 trillion and thereby, reinforce its strong franchise as Africa’s Global Bank, facilitating trade and capital flows between Africa and the rest of the world.

Speaking during the launch of the new subsidiary in Dubai on Thursday, the Chairman, UBA Group, Mr. Tony O. Elumelu, explained that with the Group’s foray into the Gulf Region, UBA continues to focus on its strategic intent to lead the way when it comes to doing business in Africa. He said “Collaborating with our franchises in 20 African countries and the major financial centres of London, New York and Paris, UBA (DIFC Branch) will facilitate the financing of trade transactions between the Middle East and Africa, enabling trade finance and investments,” Elumelu said.

FITCH RATINGS AFFIRMS AFRICAN DEVELOPMENT BANK AT 'AAA' - OUTLOOK STABLE


On July 13, the global credit rating agency Fitch Ratings affirmed the African Development Bank’s long-term credit rating: AAA with a Stable Outlook. This is a very strong endorsement of the African Development Bank’s financial strength and profile, as well as the extraordinary support of its shareholders. The importance of the Bank’s public mandate, its governance, and the excellent quality of its risk management was highlighted by Fitch.

The Bank’s Acting Vice President for Finance and CFO, Hassatou N’Sele noted: “this stellar credit rating allows the African Development Bank to provide financial resources to African countries at favorable levels to develop their economies. This is extremely important in the current environment of rising interest rates and issues around debt sustainability.”

Additional recognition

The Bank’s role in shaping the global development landscape received additional recognition this week. Publish What You Fund, the global campaign for aid and development transparency, has ranked the African Development Bank’s Sovereign Portfolio first out of 50 global development institutions in its 2022 Aid Transparency Index.

Based on its strong financial position, the Bank has launched game-changing initiatives for Africa, from helping African countries build back from Covid-19 recovery, to tackling the global food insecurity crisis sparked by the Russia-Ukraine conflict.

TANZANIA KUTUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI KUTOKA BENKI YA AFREXIM

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah, baada ya kukamilika kwa mkutano kati yao, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiahidi kutumia fursa zilizopo katika Benki ya Afrexim alipokutana na Rais wa Benki hiyo, Prof. Benedict Oramah, jijini Dodoma.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah (hayupo pichani), jijini Dodoma.
Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah, akieleza fursa za kiuchumi zilizopo katika Benki yake wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah, uikiendelea jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa sita kushoto) na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah (wa tano kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania na Benki ya Afrexim, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba amemuahidi Rais wa Benki ya Afrexim kuongeza mtaji wa ziada katika Benki hiyo ambayo Tanzania inamiliki hisa ili iwe na wigo mpana wa kuendelea kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Afrexim, Prof. Benedict Oramah, ambapo walijadili masuala kadhaa likiwemo fursa zinazotolewa na Benki hiyo.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali itashirikiana na Benki hiyo ambayo kuanzishwa kwake kulikuwa na lengo la kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika nchi za Afrika.

“Tunatekeleza dira ya Mhe. Rais ya kuweza kuvutia uwekezaji, kuendeleza maeneo mahususi ya uwekezaji (EPZ) pamoja na upande wa Zanzibar ambayo inakusudiwa kutengeneza ajira nyingi kwa vijana ili pato la mtanzania mmojammoja liongezeke na kuweza kupunguza umasikini”, alieleza Dkt. Nchemba.

MHE. INNOCENT BASHUNGWA AZINDUA KIFURUSHI CHA NMB "MWALIMU SPESHO - UMETUFUNZA TUNAKUTUNZA"

Sehemu ya Walimu walioyohudhuria hafla ya uzinduzi wa NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’ katika ukumbi wa ELCT – Kayanga, Karagwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Mkuu wa Idara ya huduma za Serikali wa NMB – Bi Vicky Bushubo (kushoto) wakifunua pazia kama ishara ya kuzindua rasmi kifurushi cha NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’ Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Akishuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe – Mhe. Julieth Nkembanyi Binyura (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mhe. Innocent Bashungwa akionyeshwa na Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa NMB – Bi. Vicky Bushubo chombo cha usafiri aina ya Boda boda ambayo inaweza kupatikana kupitia mkopo wa chombo cha usafiri ambao ni moja ya masuluhisho ya kifurushi cha Mwalimu Spesho. Wakishuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB – Bi. Aikansia Muro, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Bw. Ladislaus Baraka na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe – Mhe. Julieth Nkembanyi Binyura (kulia).

Benki ya NMB imepongezwa kwa kuwajali Walimu kupitia huduma zake mbalimbali zinazotoa masuluhisho ya kifedha kukidhi mahitaji ya kundi hilo.

Haya yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mhe. Innocent Bashungwa wakati akizindua kifurushi cha NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’ chenye masuluhisho mahususi kwa ajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya Walimu Mkoani Kagera.

Kifurushi cha ‘Mwalimu Spesho’ kimejumuisha huduma zote zinazomuwezesha Mwalimu: Kupata Mikopo yenye riba nafuu - ikiwemo ya kujiendeleza kielimu yeye na watoto wake, mikopo ya biashara ndogo ndogo, ujenzi, vyombo vya moto kama Boda boda na Pikipiki za miguu mitatu. Kupata mkopo wa Bima yaani Insurance Premium Finance (IPF), ambayo inawezesha Walimu kulipa bima na kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali. Lakini pia, Walimu watapata mikopo ya pembejeo na Mashine za kilimo pamoja na kupata elimu ya masuala ya kifedha.

Mhe. Bashungwa aliwaasa Walimu kutumia fursa hii kuelewa kwa kina na upana huduma mbalimbali zinazotolewa na NMB na ni jinsi gani wanaweza kunufaika nazo kwa unafuu, uharaka na ufanisi kwa wakati wote ili wazidi kuboresha hali zao za kiuchumi.

Tuesday, 19 July 2022

NMB NA NEEMA MPYA KWA WAKULIMA, WAVUVI NA WAFUGAJI

Kaimu Afisa Mkuu wa Udhibiti na Utekelezaji wa NMB - Ndg. Oscar Nyirenda akiongea kwenye warsha ya wafanyabiashara wa mkoa wa Lindi (NMB Business Club Lindi). Benki ya NMB iliwafunda zaidi ya wafanyabiashara 700 kutoka Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kuhusu Elimu ya biashara na fedha.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa katika hafla ya ufunguzi wa NMB Business Club iliyofanyika Katika ukumbi wa Sea View Beach Resort iliyopo Mkoani Lindi.

Kwa mara ya kwanza wakulima, wavuvi na wafugaji nchini wataweza kupata mikopo kutoka Benki ya NMB kwa riba nafuu kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao, baada ya taasisi hiyo kupunguza riba hadi asilimia tisa.

Hatua ya benki hiyo kupunguza riba ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyotoa mwaka huu kwa taasisi za kifedha kupunguza riba hadi kufikia namba moja (Single Digit).

Kaimu Afisa Mkuu wa Udhibiti na Utekelezaji wa Benki ya NMB, Ndg. Oscar Nyirenda alisema kuwa NMB imepunguza riba ya mikopo kwa sekta mama za kilimo, uvuvi na ufugaji hadi kufikia asilimia tisa mwaka 2022.

Alisema kuanzia Julai, 2021 hadi Juni 2022 jumla ya mikopo 37,500 yenye thamani ya Sh bilioni 752.7 imetolewa kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za biashara.

Aliongezea kuwa kushuka kwa riba kumesababisha idadi ya wafanyabiashara wanaokopa katika benki hiyo kuongezeka kulinganisha na miaka ya nyuma kabla ya NMB kupunguza kwa kiwango hicho cha riba ya mikopo yake.

Meneja wa NMB Kanda ya kusini, Janeth Shango alisema benki hiyo iko tayari kuwahudumia wafanyabiashara katika mitaji na elimu ili huduma zao ziwe na ufanisi na faida kwao pia.

Monday, 18 July 2022

SIMBACHAWENE: STEPS TAKEN BY GGM KILI CHALLENGE IN CONTROLLING AIDS

Minister of State Prime Minister's Office - Policy, Parliament and Coordination, George Simbachawene (second right) handing over a flag to one of the participants climbing Mount Kilimanjaro with the aim of raising funds for the fight against HIV through the GGM Kili Challenge 2022 campaign. On the right is the Director of TACAIDS, Dr. Leonard Maboko.

The Minister of State, Prime Minister's Office - Policy, Parliament and Coordination, George Simbachawene has said that the efforts of the GGM Kili Challenge Campaign, together with various stakeholders in collaboration with the Government, have helped reduce deaths from HIV/AIDS by 50 percent from 64,000 deaths in 2010 to 32,000 in 2020.

He also said that new HIV infections in adults (15 years and older) have dropped from 110,000 in 2010 to 68,000 in 2020 while new infections from mother to child have dropped from 18 percent in 2010 to 7 percent in 2020.



Simbachawene made the statement at the end of the week when wishing a farewell to 52 Kilimanjaro climbers, of whom 28 are going around the mountain by bicycle and 24 by walking.

The challenge, which started on July 15, 2022, is coordinated by Geita Gold Mine Limited (GGML) in collaboration with the Tanzania National AIDS Control Commission (TACAIDS) with the aim of donating funds for AIDS control activities. The climbers will descend on July 21 this year.



Along with other things, Simbachawene said the government will continue to be at the forefront to ensure that the implemented interventions to respond to HIV and AIDS are productive for various groups in society.

He said that in order to achieve these goals as well as others in winning this war against HIV and AIDS, a joint effort is needed between the government and other stakeholders, especially the private sector to obtain sufficient financial resources.



"The Kili Challenge aims to reduce the effects of the decrease in philanthropic aid and enable the country to strengthen its internal capacity to control AIDS," Simbachawene Said.

MSIMU WA SOKA LA KIBABE! WAPI TENA KAMA SIO DStv?

 

Ni kweli tumelimisi Soka, na kama kawaida sehemu pekee palipo na uhakika wa Soka la Kibabe ni ndani ya @dstvtanzania pekee.

Kaa tayari kutazama ligi zako pendwa ulimwenguni kupitia msimu mpya wa soka utakao kujia hivi karibuni na kuruka LIVE kutoka @dstvtanzania pekee.

Jiunge mapema kwa ofa ya TShs 69,000/= tu ili kufaidi soka hili la Kibabe.

Piga 0659 07 07 07 kujiunga.

#MsimuWaSokaLaKibabe
 
#WapiKamaSioDStv

STANBIC BANK REAFFIRMS ITS COMMITMENT TO SUPPORTING THE EDUCATION SECTOR

Stanbic Bank Head of Consumer and High Net Worth Clients, Omari Mtiga (left), handing over one of 50 desks donated by the bank to Ubungo District Commissioner, Hon. Heri James (center) and Kimara Secondary School Headteacher, Elizabeth Bonzo (right). This is a continuation of the bank's campaign dubbed "Stanbic Madawati Initiative" which aims to provide 1,000 desks to various schools in the country. The event was followed by tree planting, which is part of a campaign that aims to restore the ecosystem by planting a tree for every desk donated.

Dar es Salaam, 17th July 2022: Stanbic Bank Tanzania has reiterated its commitment to continue supporting government efforts of improving the quality of education by improving the learning environment for all students in government schools.

The bank made the commitment during a brief ceremony held at Kimara Secondary School to hand over 50 desks valued at TZS 4,500,000 million, which they donated to the learning institution.

The donation is part of the bank's ongoing campaign dubbed Stanbic Madawati Initiative, which seeks to sustainably reduce the shortage of desks in schools by donating desks across the country and planting one tree for every desk donated to ensure a balance in the environmental ecosystem.



The desks were handed over by the bank’s Head of Consumer and High Net Worth Clients, Mr. Omari Mtiga to the Ubungo District Commissioner - Mr Heri James at an event held at the school at the end of the week.

Speaking during the ceremony Mtiga said, ‘’we recognise the efforts made by the government in improving the education sector, and we are committed to being at the forefront of supporting these efforts as we believe that quality education is crucial in creating a learned society and enlightened human capital, which are important for the development of the various sectors of the national economy.’’

Friday, 15 July 2022

MITANANGE YA PRE-SEASON DANI YA DStv

 

#DStvOyoooo ndani ya @dstvtanzania pekee!

Furahia mechi ya Pre Season ndani ya channel za SuperSport

Jumamosi hii

⚽ FC Koln vs Ac Milan

Utabiri wako ni upi?

Lipia kifurushi chako kwa kupiga *150*53#

#DStvShangweka

TOURIST ARRIVALS SOAR AS ROYAL TOUR FILM PAYS OFF


Tanzania registered a phenomenal growth in tourism in May 2022, a month after President Samia Suluhu Hassan launched the Royal Tour documentary that promotes the country as a top tourist and investment destination.

The National Bureau of Statistics (NBS), Director for Economic Statistics, Daniel Msolwa said in Dar es Salaam yesterday that  tourist arrivals in May 2022 more than doubled to 89,271 up from 42,173 in April 2022, equivalent to a 117.7 per cent increase.

"The increase in tourists is attributed to President Samia's efforts to promote the country's attractions through the Royal Tour film that was launched in April 2022", he said noting that this is a wakeup call for service providers to prepare for the booming business.

KUPITIA JUKWAA LA MKAPA LEGACY 2022, VODACOM TANZANIA PLC YAELEZEA MIKAKATI KUSAIDIA SEKTA YA AFYA

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Vodacom Group, Mwamvita Makamba akizungumza kwenye kongamano la pili la Mkapa Legacy 2022 lililofanyika Visiwani Zanzibar, wakati wa mada ya Mageuzi ya kimkakati ya Afya nchini kupitia muungano wa biashara ya afya (Accelerating strategic health transformation in Tanzania through business coalition for health) ambapo Vodacom Tanzania Foundation wanatoa huduma ya afya kupitia program za m-mama, fistula inatibika, wazazi nipendeni, washable sanitary pads pia wamedhamini kongamano hilo. Kulia ni Sarah Maongezi kutoka Taasisi ya Aga Khan Health Services na muongoza mjadala Dkt. Faustine Ndugulile.
Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud akizungumza kwenye Kongamano la Pili la Benjamin Mkapa Foundation (Mkapa Legacy 2022) lililofanyika Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye Kongamano la Pili la Mkapa Legacy 2022 lililofanyika Visiwani Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Senkoro akizungumza kwenye Kongamano la Pili la Mkapa Legacy 2022.

Mama Anna Mkapa akiwa na Mama Shadya Karume wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa inaendelea kwenye Kongamano la Pili la Mkapa Legacy 2022.



MAANDALIZI YA NBC DODOMA INTERNATIONAL MARATHON YAPAMBA MOTO


Ikiwa ni takribani wiki tatu zimesalia kuelekea NBC Dodoma International Marathon itakayofanyika siku ya jumapili Julai 31, wanariadha wameendelea kujifua ili kushiriki mbio hizo za kimataifa. Leo tumeshuhudia klabu za wanariadha ya Kigamboni runners ikishirikiana na klabu ya wanariadha ya NBC Jogging club ambao wamefanya mazoezi ya pamoja kwa kukimbia kilomita 10 na kilomita 5 ikiwa sehemu ya maandalizi ya kuelekea mkoani Dodoma. Akizungumzia maandalizi kwa ujumla, Msemaji wa NBC Jogging Club, Johnson Ngakiziba alisema lengo ni kuhakikisha wanariadha wanapata muda wa kutosha kujiandaa vizuri kuelekea kwenye mbio hizo ambazo pia zitashirikisha wanariadha kutoka nje ya nchi.

“Tumeungana na wenzetu wa Kigamboni Runners ili kufanya maandalizi ya pamoja kwaajili ya NBC Dodoma International Marathon. Lakini pia, wenzetu hawa walikuwa wanaadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa klabu hii kwahiyo tukaona tuungane kwa pamoja,” alisema. Mbio za NBC Dodoma International Marathon zitahusisha wakimbiaji wa Kilomita 42, 21 na kilomita 10 ambapo benki hiyo imetenga jumla ya Sh65 milioni kama zawadi kwa vinara huku watanzania wakipewa kipaumbele zaidi kupitia nyongeza (Bonus). Hadi kufikia leo Julai 7, mauzo ya tiketi za kilomita 10 yalikuwa yamefikia asilimia 80 ikiwa ni siku chache tu tangu kutangazwa kwa mbio hizo.
  

“Nawakumbusha watu waendelee kujisajili mapema ili kuepuka changamoto na kujisajili ni rahisi sana, tembelea tovuti ya www.events.nbc.co.tz na utalipia tiketi kwa njia mbalimbali ikiwamo NBC Kiganjani,” alisema. Kwa upande wake, Katibu wa Kigamboni Runners, Edgar Konyani alisema mapokeo yamekuwa mazuri kwa wakimbiaji wa klabu hiyo ambapo wamekuwa wakishiriki kwa mara ya tatu mfululizo. Mbio za Dodoma International Marathon zimelenga katika kuchangia mapambano dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi (cervical cancer) kwa kushirikiana na taasisi ya Ocean Road ambapo fedha zitakazokusanywa zitapelekwa kwenye taasisi hiyo.

CLYDE & CO UPDATER - UNDERSTANDING THE KEY CHANGES MADE BY THE FINANCE ACT OF 2022

Thursday, 14 July 2022

NMB YATOA VIFAA VYA AFYA NA ELIMU WILAYA YA LUSHOTO

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini (wa nne kulia), Dismas Prosper akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalist Lazaro (kulia) mabati 200 yatakayokwenda kutumika katika Zahanati ya Kwemakame iliyopo Wilayani humo.
Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper akimkabidhi madawati 50 Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Kalist Lazaro kwa ajili ya shule ya Msingi Mbula B iliyopo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.

Benki ya NMB imetoa msaada wa mabati 200 kwa Zahanati ya Kwemakame iliyopo wilayani Lushoto mkoani Tanga yenye thamani ya Sh. milioni 7.1 na madawati 50 katika Shule ya Msingi Mbula B iliyopo wilayani humo yenye thamani ya Sh.milioni 3.9 ambapo jumla ya msaada huo ni Sh. milioni 11.

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper alisema kuwa benki hiyo inatambua juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan za kusimamia huduma za afya na elimu kwa nguvu zote kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hizo mjini na vijijini.

Meneja huyo wa kanda alisema walipopata maombi ya kuchangia katika maendeleo ya elimu kwa Wilaya ya Lushoto walifarijika na kushirikiana nao ili ikawe chachu ya maendeleo ya sekta ya afya na elimu kwa jamii yao hasa katika zahanati ya Kwemakame na kwa Shule ya Msingi Mbula B.

BENKI YA NMB KURAHISISHA UDHIBITI MAKUSANYO YA MAPATO SEKTA YA UTALII ZANZIBAR

Mkuu wa Biashara ya Kadi Benki ya NMB - Philbert Casmir (katikati), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar - Dk. Amina Ameir Issa, mfano wa mashine ya kupokea malipo kwa ajili ya wizara hiyo. NMB imekabidhi mashine 50 ambazo zitasaidia kuimarisha na kukuza ukusanyaji wa mapato kwenye Sekta ya Utalii. Kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi NMB - David Ngusa na Meneja Biashara NMB Zanzibar - Naima Said Shame.

Benki ya NMB katika kuhakikisha Sekta ya utalii visiwani Zanzibar inaimarika, imekabidhi Mashine za malipo (POS) 50 pamoja na Lipa Mkononi (QR) kusaidia kudhibiti na kukuza ukusanyaji mapato katika Sekta ya Utalii visiwani Zanzibar.

Akizungumza katika hafla ya makabidhino, Mkuu wa Idara ya Biashara za Kadi NMB - Philbert Casmir alisema “huu ni utekelezaji wa makubaliano tuliofanya miezi sita iliyopita kati ya Benki ya NMB pamoja na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar - Tulisaini makubaliano ya kuimarisha uchumi wa bluu kwa kutoa elimu na kuhamasisha watu kutembelea vivutio vya kitalii".

Mkuu wa Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Philbert Casmir (katikati), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dk. Amina Ameir Issa, mfumo wa malipo wa Lipa Mkononi (QR) kwa ajili ya wizara hiyo. Kushoto ni Meneja Biashara NMB Zanzibar - Naima Said Shame.

Akipokea mashine hizo pomoja na Lipa Mkononi (QR) Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dk. Amina Ameir Issa alisema kuwa Benki ya NMB imerahisisha malipo, sasa unamiza malipo kidijitali kwani ukienda kwenye vituo vya utalii huna haja ya kubeba fedha taslimu. Uwe Mtanzania au mgeni, unalipia kwa mashine hizi kwa kutumia kadi yako ya benki, ambayo ina pokea mifumo ya MasterCard, VISA na UnionPay au simu za mkononi kutumia mfumo wa Ku-scan au Lipa Namba kufanya malipo.

Aidha, alieleza kuwa sasa Serikali itaweza kujua kiwango cha fedha kinachoingia kwa siku, wiki, mwezi au mwaka hivyo kuwawezesha kufikia malengo ya mwaka huu wa fedha ya kukusanya Sh. Bilioni Moja katika sekta ya utalii. Maeneo yatakayotumia mfumo huu ni pamoja na Mvuleni, Kizimkazi, Mapango ya watumwa Manga Pwani, Bi Khole, Mtoni, Rasi ya Kibweni na Maruhubi.

Wednesday, 13 July 2022

LIPIA KIFURUSHI CHA DStv BOMBA KWA 21,000/= TU



DC wa Instagram anakukumbusha kuwa tamthilia mpya ya YALAITI inaendelea....

Pata kutazama tamthilia hii kai yenye mastaa kama Irene Paul, Uchebe, Chris Mziwanda na wengine kibao kila siku za Jumatatu - Ijumaa saa 4 usiku kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo 160 inayopatikana kuanzia kifurushi cha Bomba kwa 21,000/= tu ndani ya @dstvtanzania pekee.

Piga *150*53# kulipia kwa urahisi zaidi.

#DStvEwaaaaah

BENKI YA CRDB NA IFC KUONGEZA UPATIKANAJI WA MITAJI KWA WAJASIRIAMALI NCHINI TANZANIA NA BURUNDI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Makamu wa Rais wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Afrika, Sergio Pimenta (kulia) wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 105 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es Salaam.

Benki ya CRDB na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) leo wameingia mkataba wa uwezeshaji utakaongeza upatikanaji wa fedha kwa wajasiriamali wadogo na wakati nchini Tanzania na Burundi, na kusaidia kuimarisha uchumi wa nchi zote mbili kutokana na athari za janga la UVIKO-19. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Johari Rotana iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi waaandamizi wa taasisi hizo.

Chini ya ushirikiano huo, IFC inatoa mkopo wa dola milioni 100 kwa Benki ya CRDB Tanzania, nusu ya fedha hizo zitakuwa kwa shilingi ya kitanzania, na mkopo wa dola milioni 5 kwa Benki ya CRDB Burundi kusaidia mikopo kwa wafanyabiashara wadogo katika nchi zote mbili, hasa kwa wafanyabiashara wanaomilikiwa na wanawake.

Katika mkataba huo, asilimia 25 ya mkopo unaoelekezwa nchini Tanzania utatolewa kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake. Imebainishwa kuwa fedha hizo zitaongeza upatikanaji wa mikopo ya muda mrefu, ambayo imekuwa adimu kupatikana tangu kuzuka kwa janga la COVID-19.


Mikopo hiyo ni sehemu ya mpango wa IFC wa uwezeshaji wa tabaka la chini katika uchumi, ambao unalenga kusaidia taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wajasiriamali na wafanyabisahara wadogo ambao wameathiriwa zaidi na janga la UVIKO-19. Ufadhili wa IFC pia unasaidiwa na Dirisha la Sekta ya Binafsi la Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa.

Wajasiriamali ni kundi muhimu kwa uchumi wa Tanzania na Burundi. Nchini Tanzania, wastani wa biashara ndogo ndogo na za kati ni milioni 3.2, huchangia asilimia 27 ya Pato la Taifa, na kuajiri zaidi ya watu milioni 5. Hata hivyo, takriban asilimia 81 ya biashara hizi hazina uwezo wa kupata fedha. Biashara nchini Burundi pia zinachangamoto kubwa katika kupata fedha.

"Fedha hizi zimekuja wakati muafaka na zitaongeza uwezo wetu wa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati huku tukisaidia kuongeza usawa wa kijinsia katika mnyororo wa thamani. Benki ya CRDB tunaamini kuwa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake ni msingi wa maendeleo. Wanawake wameathirika kwa kiasi kikubwa sana janga la UVIKO-19, ambalo limepelekea changamoto nyingi za kiuchumina kuathiri moja kwa moja maisha ya familia na jamii zao,” alisema Abdulmajid Nsekela Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB wakati wa hafla ya utiaji sahihi.

Nsekela aliongezea kuwa ufadhili wa IFC utasaidia maendeleo ya sekta mbalimbali za maendeleo nchini, ikiwamo biashara, kilimo, afya, elimu, makazi, na miundombinu. Maeneo mengine ni pamoja na miradi inayozingatia mabadiliko ya tabianchi, wajasiriamali, pamoja na biashara zinazomilikiwa na wanawake kama ambavyo imesisitizwa katika mkataba huo wa ushirikiano baina ya Benki ya CRDB na IFC.


“Ushirikiano kati ya IFC na Benki ya CRDB utasaidia ukuaji wa sekta ya ujasiriamali katika nchi hizi ambapo mchango wao katika ajira na shughuli za kiuchumi ni mkubwa. Ushirikiano huu pia unajumuisha jitihada maalum katika kusaidia biashara zinazomilikiwa na wanawake na kuendeleza ushirikishwaji wa kijinsia, ikiwa ni sehemu muhimu ya mkakati wa IFC nchini Tanzania na Afrika," alibainisha SĂ©rgio Pimenta, Makamu wa Rais wa IFC Afrika.