Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 15 July 2022

KUPITIA JUKWAA LA MKAPA LEGACY 2022, VODACOM TANZANIA PLC YAELEZEA MIKAKATI KUSAIDIA SEKTA YA AFYA

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Vodacom Group, Mwamvita Makamba akizungumza kwenye kongamano la pili la Mkapa Legacy 2022 lililofanyika Visiwani Zanzibar, wakati wa mada ya Mageuzi ya kimkakati ya Afya nchini kupitia muungano wa biashara ya afya (Accelerating strategic health transformation in Tanzania through business coalition for health) ambapo Vodacom Tanzania Foundation wanatoa huduma ya afya kupitia program za m-mama, fistula inatibika, wazazi nipendeni, washable sanitary pads pia wamedhamini kongamano hilo. Kulia ni Sarah Maongezi kutoka Taasisi ya Aga Khan Health Services na muongoza mjadala Dkt. Faustine Ndugulile.
Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud akizungumza kwenye Kongamano la Pili la Benjamin Mkapa Foundation (Mkapa Legacy 2022) lililofanyika Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye Kongamano la Pili la Mkapa Legacy 2022 lililofanyika Visiwani Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Senkoro akizungumza kwenye Kongamano la Pili la Mkapa Legacy 2022.

Mama Anna Mkapa akiwa na Mama Shadya Karume wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa inaendelea kwenye Kongamano la Pili la Mkapa Legacy 2022.



No comments:

Post a Comment