Sehemu ya Walimu walioyohudhuria hafla ya uzinduzi wa NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’ katika ukumbi wa ELCT – Kayanga, Karagwe. |
Haya yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mhe. Innocent Bashungwa wakati akizindua kifurushi cha NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’ chenye masuluhisho mahususi kwa ajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya Walimu Mkoani Kagera.
Kifurushi cha ‘Mwalimu Spesho’ kimejumuisha huduma zote zinazomuwezesha Mwalimu: Kupata Mikopo yenye riba nafuu - ikiwemo ya kujiendeleza kielimu yeye na watoto wake, mikopo ya biashara ndogo ndogo, ujenzi, vyombo vya moto kama Boda boda na Pikipiki za miguu mitatu. Kupata mkopo wa Bima yaani Insurance Premium Finance (IPF), ambayo inawezesha Walimu kulipa bima na kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali. Lakini pia, Walimu watapata mikopo ya pembejeo na Mashine za kilimo pamoja na kupata elimu ya masuala ya kifedha.
Mhe. Bashungwa aliwaasa Walimu kutumia fursa hii kuelewa kwa kina na upana huduma mbalimbali zinazotolewa na NMB na ni jinsi gani wanaweza kunufaika nazo kwa unafuu, uharaka na ufanisi kwa wakati wote ili wazidi kuboresha hali zao za kiuchumi.
Nae, Mkuu wa Idara ya huduma za Serikali wa NMB – Bi Vicky Bushubo alisema, NMB itaendelea kuja na masuluhisho bora na nafuu kwa watanzania na uwajibikaji wake kwa jamii ukibaki kuwa katika viwango vya juu huku wakiendela kushirikiana na Serikali kuhakikisha kwa pamoja, wanasukuma mbele maendeleo ya kiuchumi ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.
Benki ya NMB kila inapokutana na Walimu, hutumia fursa hiyo kuwahabarisha juu ya maendeleo yake pamoja na huduma mbalimbali zinazo wahusu na kupata mrejesho na mawazo yatakayo wasaidia kuendelea kuboresha huduma zao.
Mpaka sasa, NMB kupitia Mwalimu Spesho, imewafikia Walimu wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza na Kagera na bado wanaendelea kufikia Mikoa mingine.
No comments:
Post a Comment