Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Chalangwa Selemani (wa pili kushoto), Meneja wa NMB Kanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingu Pugu Station, Valentine Mhagama (katikati) wakipiga makofi baada ya makabidhiano ya viti na meza kwa ajili ya Walimu wa Shule ya Pugu Station. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Ilala, Christine Lifiga na kulia ni Meneja Mwandamizi Mahusiano ya Serikali wa NMB, Mkunde Joseph.
Benki ya NMB, imeendelea kutatua kero katika Sekta za Elimu na Afya, kwa kutoa misaada yenye thamani ya Sh. Milioni 35 katika mikoa mbalimbali nchini, vikiwemo viti 35, meza 35 vyenye thamani ya Sh. Milioni 8 kwa matumizi ya Walimu wa Shule ya Msingi Pugu Station, iliyoko Manispaa ya Ilala.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada wa shule ya Msingi Pugu kwa Katibu Tawala (DAS), Ilala, Charangwa Seleman, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard alisema changamoto katika sekta za elimu, afya na hata majanga ni kipaumbele cha Benki yake, huku akiishukuru Kamati ya Shule hiyo kwa kuwafikiria wao, walipotafuta ufumbuzi wa uhaba wa viti na meza za walimu.
Kwa upande, DAS Charangwa aliipongeza NMB kwa kuwajibika ipasavyo kwa jamii inayofanya nayo biashara.