Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Sunday, 17 August 2025

CRDB BANK MARATHON 2025 YAKUSANYA SHILINGI BILIONI 2 KUSAIDIA AFYA YA JAMII

Dar es Salaam, 17 Agosti 2025 – Zaidi ya wakimbiaji na wapenda michezo 16,000 kutoka ndani na nje ya Tanzania walijitokeza leo kushiriki CRDB Bank Marathon 2025 katika viwanja vya The Green, Oysterbay.
Mwaka huu, mbio hizo za hisani zimefanikisha kukusanya Shilingi Bilioni 2 kusaidia:

  • Watoto wenye matatizo ya moyo
  • Wakina mama wenye ujauzito hatarishi
  • Vijana kupitia programu ya iMBEJU


Viongozi Wakuu Wapongeza Hatua Hii

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, aliongoza washiriki na kusisitiza kuwa mbio hizo ni alama ya mshikamano wa jamii na moyo wa huruma.

“Ushiriki wetu katika CRDB Bank Marathon ni ushahidi kwamba tukishirikiana, tunaweza kubadilisha maisha,” alisema Dkt. Tulia.

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, aliongeza kuwa mbio hizo si tu zimeimarisha afya na mshikamano wa kijamii, bali pia zimefungua milango ya ajira na fursa za kiuchumi kwa vijana.


CRDB Yapanua Wigo Hadi Nje ya Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Abdulmajid Nsekela, alieleza kuwa msimu huu wa sita umefanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya Benki ya CRDB, na kwa mara ya pili pia umefanyika nchini Burundi na DRC.

  • DRC (Lubumbashi): Dola za Marekani 70,000 zilikusanywa kuboresha huduma za afya.
  • Burundi (Bujumbura): Faranga milioni 175 zilikusanywa kufanikisha bima ya afya kwa zaidi ya watu 58,000.

VODACOM TANZANIA YASHEREHEKEA MIAKA 25 YA MAFANIKIO NA WANANCHI TEMEKE



Vodacom Tanzania imeadhimisha miaka 25 ya kuwahudumia Watanzania tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika Agosti 15, 2025, ikianzia makao makuu yake jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zilipambwa na ukataji wa keki iliyoashiria robo karne ya ukuaji, ubunifu na uongozi wa sekta ya mawasiliano nchini.





Baada ya hafla hiyo, familia ya Vodacom ilijumuika na wateja wake katika Soko la Stereo lililoko Temeke, ikiwa ni ishara ya kuthibitisha msemo wao wa “Tupo Nawe, Tena na Tena.” Kupitia tukio hilo, Vodacom iliendelea kuonesha dhamira yake ya kusogea karibu zaidi na wananchi, kusherehekea nao mafanikio yaliyopatikana kwa pamoja.

Saturday, 16 August 2025

TBL YAWEZESHA WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI JUU KUONGEZA UZALISHAJI NA UBORA

Monduli Juu, Arusha – 15 Agosti 2025: Tanzania Breweries Plc (TBL) imefanya mafunzo ya vitendo kwa wakulima wa shayiri Monduli Juu, Arusha, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuendeleza kilimo cha shayiri nchini. Zaidi ya wakulima 200 walihudhuria katika Siku ya Wakulima wa Shayiri, tukio lililoambatana na Shamba Darasa na majadiliano ya changamoto za kilimo.

Hafla hiyo iliudhuriwa na viongozi wa serikali akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Monduli, Mheshimiwa Muhsin Kassim, ambaye alisisitiza dhamira ya serikali kuimarisha upatikanaji wa pembejeo bora, huduma za ugani na masoko yenye tija.

“Wakulima ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu. Leo tunathibitisha dhamira yetu ya kuwasaidia kupitia utafiti, huduma bora na masoko salama,” alisema Mheshimiwa Kassim.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Mahusiano wa TBL, Bi. Neema Temba, alisema kampuni itaendelea kuunga mkono wakulima wadogo kwa mikataba ya mauzo na mafunzo ya kitaalamu.

“Matukio kama haya yanatukumbusha nafasi muhimu ya wakulima siyo tu katika usalama wa chakula, bali pia katika kuendeleza viwanda kama chetu,” alisema Bi. Temba.

TBL ni mnunuzi mkubwa wa shayiri nchini na imekuwa ikishirikiana na wakulima wadogo kwa muda mrefu ili kuongeza tija na kuhakikisha malighafi za ndani zinatumika katika viwanda vyake vya bia.

Friday, 15 August 2025

PRIME MINISTER DIRECTS SPEEDY COMPLETION OF BRT PHASE TWO FOR SWIFT SERVICE LAUNCH

Prime Minister, Kassim Majaliwa (centre) inspects the newly acquired articulated buses at Dar es Salaam Port on Wednesday.

DAR ES SALAAM — Prime Minister Kassim Majaliwa has directed operators of the second phase of the Bus Rapid Transit (BRT) project to work around the clock to finalise infrastructure preparations along the remaining sections of the route, paving the way for immediate commencement of services.

Speaking on Wednesday while inspecting the newly acquired 99 buses for the project, Mr Majaliwa toured key facilities including the Mbagala Rangi Tatu BRT Main StationGerezani Bus Stop, and a Compressed Natural Gas (CNG) refuelling station under construction at the Mbagala Rangi Tatu site.

“We want this project to start providing services to Tanzanians, especially Dar es Salaam residents. This project will boost efficiency of public transport by bringing modern, safe, and fast services for the citizens,” he said.

The Prime Minister also instructed Mofat Company Limited’s Executive Director, Mohammad Kassim, to expedite clearance of the buses at Dar es Salaam Port and stressed that ticketing should be issued electronically to improve transparency and revenue monitoring.

He further encouraged Tanzanians to seize job opportunities from the project — particularly driving roles — by upgrading skills at the National Institute of Transport (NIT).

The new 99 articulated buses are part of Mofat Company Limited’s plan to introduce a total of 255 buses valued at approximately TZS 200 billion. Each 18-metre-long unit runs on natural gas, supporting Tanzania’s climate action goals of cutting carbon emissions.

CRDB BANK TOPS DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE AS THE MOST CAPITALISED COMPANY

Dar es Salaam, 15 August 2025 — CRDB Bank PLC has officially become the Most Capitalised Company on the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE), boasting a share price of TZS 1,510 and a market capitalisation of TZS 3.94 trillion.

The announcement was made yesterday by Abdulmajid Nsekela, Group CEO & Managing Director of CRDB Bank PLC, through his LinkedIn account.

“This achievement is more than just numbers. It’s a testament to the trust of our customers, the dedication of our people, and the shared vision of an inclusive and prosperous future for all,” Nsekela stated, adding, “Thank you for walking this journey with us. The best is yet to come.”

#CRDBBank 
#FinancialExcellence 
#TheBankThatListens

Thursday, 14 August 2025

NMB YADHAMINI KONGAMANO LA NGOs, YABAINISHA MCHANGO WA SEKTA YA FEDHA

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Benki ya NMB imedhamini na kushiriki kikamilifu Kongamano la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) 2025, lililofanyika Agosti 13 jijini Dodoma, likiwa na lengo la kutathmini na kuenzi mchango wa mashirika hayo katika maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kongamano hilo limehitimishwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isidory Mpango, ambaye alisisitiza jukumu la Serikali kuboresha mazingira ya utendaji wa NGOs ili ziendelee kushirikiana na Serikali katika sekta muhimu ikiwemo afya, kilimo, elimu, maji, mazingira, utawala bora, mifugo na uvuvi.

Kupitia banda lake, NMB imewasilisha suluhisho za kifedha zinazolenga kuimarisha ushirikiano na NGOs nchini, sambamba na mchango wake katika kukuza sekta ya fedha na kusaidia utekelezaji wa miradi ya kijamii.

Uwakilishi wa benki hiyo umeongozwa na Mkuu wa Idara ya Biashara ya Serikali, Bi. Vicky Bishubo, akiambatana na viongozi wengine wa NMB, ambao walitoa ufafanuzi wa huduma na bidhaa zinazoweza kusaidia NGOs kuongeza ufanisi na uendelevu wa shughuli zao.

GOVERNMENT PLEDGES TO MATCH AIRTEL’S INVESTMENT DRIVE IN SUPPORT OF TANZANIA’S VISION 2050

President of the United Republic of Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan (center), listens to Airtel Founder and Chairman Sunil Mittal (left) during his courtesy visit to State House in Dar es Salaam. Mittal, accompanied by Airtel Africa Group CEO Sunil Taldar (right), was on a two-day working visit to the country.

Dar es Salaam, Tanzania – August 13, 2025 – The Government of Tanzania has reaffirmed its strong commitment to working hand-in-hand with Airtel to accelerate the country’s digital transformation and achieve the Tanzania Development Vision 2050.

Treasury Registrar Nehemiah Mchechu made the pledge following high-level talks with Sunil Bharti Mittal, Airtel Group Chairman & CEO, and Charles Kamoto, Airtel Tanzania Managing Director, at the Treasury Registrar’s Office in Dar es Salaam. The discussions centred on advancing digital connectivity, expanding financial inclusion, and boosting socio-economic growth.

“Today is a very crucial day. We are hosting key executives from Airtel Global, including their Chairman and CEO. Our discussions focused not only on Airtel Tanzania’s operations but also on the broader development of the telecommunications sector and digital systems in general,” Mchechu told journalists.

He further stressed that the government is ready to match Airtel’s commitment by ensuring supportive policies, robust infrastructure, and a favourable investment environment are in place.


Airtel’s Commitment to Deepening Investment

Mr. Mittal underscored Airtel’s determination to expand its footprint in Tanzania, particularly in digital infrastructure, fibre networks, and connectivity services — all vital components of the country’s digital economy agenda.

“The government’s 49% ownership in Airtel Tanzania is a clear testimony that Airtel Tanzania belongs to the people of Tanzania. Today, we have made further commitments to invest more money in our networks and fibre, and more importantly, accelerate digital penetration in Tanzania,” Mittal said.

EQUITY YAIBUA UBUNIFU MPYA: “SHULE MKONONI” KUBADILISHA USIMAMIZI WA ELIMU TANZANIA

Dar es Salaam – Benki ya Equity imezindua rasmi mfumo mpya wa kidijitali uitwao “Shule Mkononi” (School in Your Hand), unaolenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa taasisi za elimu na kuboresha huduma kwa wateja wake.

Kwa mujibu wa benki hiyo, mfumo huo utawezesha shule na vyuo kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi, mahudhurio na mapato ya taasisi kwa wakati wowote, hivyo kuongeza ufanisi wa kiutawala na kifedha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma za Malipo wa Benki ya Equity, Christopher Msangule, alisema mfumo huo utarahisisha ufuatiliaji wa ada, malipo na madeni kwa uwazi, jambo litakalowanufaisha wamiliki wa shule na vyuo.

Aidha, Msangule alibainisha kuwa “Shule Mkononi” itaongeza mawasiliano kati ya wazazi/walezi na taasisi za elimu, kwani itawawezesha kupata taarifa za maendeleo ya watoto wao moja kwa moja kupitia simu za mkononi bila kulazimika kufika shuleni.

CRDB BANK LAUNCHES TANZANIA’S FIRST MULTI-CURRENCY ISLAMIC BOND – AL BARAKAH SUKUK

Dar es Salaam — CRDB Bank has officially launched CRDB Al Barakah Sukuk, a Sharia-compliant, interest-free bond aimed at supporting sustainable investment and businesses in Tanzania and the wider East African region.

The Sukuk aims to raise TZS 30 billion and USD 5 million, with the possibility of increasing to TZS 40 billion and USD 7 million. This makes it the largest bond ever issued by a financial institution in Tanzania, allowing multi-currency investment.


FORMER PRESIDENT KIKWETE: “THIS IS A CAPITAL MARKETS REVOLUTION”

Speaking at the launch over the weekend, former President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, commended CRDB Bank for promoting inclusive economic participation.

“This Sukuk brings a revolution to our capital markets. It creates opportunities for people who were previously excluded from the formal financial system due to religious beliefs, offering an interest-free investment aligned with Sharia principles. It’s a major step towards economic inclusion and moral development,” said Dr. Kikwete.


PART OF A USD 300 MILLION MEDIUM-TERM STRATEGY

CRDB Al Barakah Sukuk is the third bond under the 2023–2027 Medium Term Strategy worth USD 300 million approved by the Capital Markets and Securities Authority (CMSA). It follows the Green Bond and Samia Infrastructure Bond, both of which attracted higher-than-expected investor interest.


INVESTMENT TERMS

CRDB Bank CEO, Abdulmajid Mussa Nsekela, said proceeds will fund Sharia-compliant projects including:

  • Healthcare services
  • Agriculture and livestock
  • Education
  • Environmentally friendly production

Wednesday, 13 August 2025

TBL AND PETPRO LAUNCH TANZANIA’S FIRST-EVER SCALABLE GLASS RECOVERY AND RECYCLING MODEL

DAR ES SALAAM, 13 AUGUST 2025 – Tanzania Breweries Plc (TBL) and PETPRO have signed a historic Memorandum of Understanding (MoU) to launch Tanzania’s first scalable post-consumer glass recovery and recycling model. The signing ceremony was held at TBL Headquarters in Ilala, Dar es Salaam.

This strategic partnership comes at a crucial time when waste management and environmental conservation are rising to the top of national priorities. The initiative seeks to address the growing challenge of post-consumer glass waste, creating a long-term, sustainable solution that promotes environmental protection and economic empowerment.

The model aims to significantly reduce the volume of glass waste ending up in landfills, boost nationwide recycling rates, and develop a more circular glass economy for manufacturers across the country. By turning waste glass into valuable raw materials, the programme will directly contribute to Tanzania’s national sustainability goals and align with TBL’s 2025 Sustainability Roadmap.

Speaking at the event, TBL Managing Director, Ms. Michelle Kilpin, said:

“This partnership with PETPRO is a blueprint for how manufacturers can elevate their role in driving both environmental and economic impact. We are excited at the prospect of transforming waste into opportunity, empowering local communities, and protecting our planet for future generations. Ultimately, we hope this initiative becomes a platform to enhance Producer Responsibility within the industry, fostering collaboration among manufacturers as we harness our collective capabilities to deliver even greater impact.”

PETPRO Managing Director, Mr. Nicholaus Jackson, added:

“Through this collaboration with TBL, we are setting a new standard for glass recycling in Tanzania. Our combined expertise will ensure that we collect, process, and return glass to the production cycle at scale—proving that sustainable practices can deliver both environmental conservation and economic opportunity. Together, we are building a cleaner, more resilient future.”

EXIM BANK YAZINDUA MKOPO ‘KOPA KIBOSS’ – MAREJESHO MPAKA MIAKA 11 KWA WATUMISHI WA UMMA

Mkuu wa Mtandao wa Wateja wa Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Kopa Kiboss na Wafanyakazi Loan’, ambapo Exim inakuwa benki ya kwanza nchini kumwezesha mtumishi wa umma kufanya marejesho kwa muda wa hadi miaka 11, na kuchukua mkopo kuanzia TSh 200,000 hadi TSh milioni 200. Kushoto ni Elihoria Matillya, Meneja Mkuu – Mauzo, na Mtenya Cheya, Mkuu wa Bidhaa na Uhakika wa Mapato, wakiwa katika tukio hilo lililofanyika tarehe 13 Agosti 2025 katika Makao Makuu ya Benki hiyo, Exim Tower, jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Agosti 13, 2025 – Katika hatua kubwa ya kuimarisha ustawi wa kifedha wa watumishi wa umma, Benki ya Exim Tanzania imefanya maboresho makubwa kwenye huduma yake ya Wafanyakazi Loan na kuzindua kampeni ya mikopo maarufu kama ‘Kopa Kiboss’. Hatua hii inaiweka Exim Tanzania kama benki ya kwanza nchini kuruhusu mtumishi wa umma kurejesha mkopo kwa kipindi cha hadi miaka 11, huku kiwango cha mkopo kikianzia TSh 200,000 hadi kufikia TSh milioni 200.

Huduma hii inalenga kuwafikia watumishi wa umma kote nchini kupitia suluhisho za kifedha zenye ubunifu na masharti nafuu. Zaidi ya muda mrefu wa marejesho, maboresho haya pia yanajumuisha huduma ya kuhamisha mikopo (loan takeover) kutoka taasisi nyingine – hatua ambayo Exim Tanzania imeiwezesha kwa mara ya kwanza nchini kupitia mfumo wa kisasa wa mtandaoni wa Employee Self Service (ESS), unaojulikana kama ‘Utumishi Portal’.

Agnes Kaganda, Mkuu wa Mtandao wa Wateja wa Exim Bank Tanzania, alisema:

“Lengo letu kuu ni kuhakikisha watumishi wa umma wananufaika na suluhisho za kifedha zinazoleta mabadiliko chanya na ya kweli katika maisha yao. Kwa kuhamisha mikopo yao iliyopo, tunalenga kuwapunguzia mzigo wa madeni na kuwapatia masharti bora ya ulipaji yaliyoboreshwa kulingana na mahitaji yao binafsi.”

Kwa mujibu wa benki, Wafanyakazi Loan inalenga kumsaidia mtumishi wa umma kutotegemea tu mshahara wake, bali kuweza kugharamia matumizi mbalimbali kama kulipia ada za shule, kuhudumia familia, kulipa madeni, au kuanzisha biashara kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.

Mtenya Cheya, Mkuu wa Bidhaa na Uhakika wa Mapato wa benki hiyo, alieleza kuwa huduma hii imeundwa kwa kuzingatia urahisi, uharaka na unyumbufu:

“Wakopaji watakuwa na nafasi ya kuongeza mikopo yao kulingana na uhitaji, huku ulipaji ukipangwa kwa mafungu sawa kila mwezi (EMI) katika kipindi chote cha mkopo, jambo linalowapa uhakika na amani ya akili.”

Pia, mkopo huu unajumuisha bima ya maisha ya mkopo (credit life insurance), inayohakikisha salio lililosalia litalipwa iwapo mkopaji atafariki dunia au kupata ulemavu wa kudumu.

EQUITY BANK YAWEZESHA WAKANDARASI WANAWAKE KUPITIA UFADHILI WA MKUTANO WA TWCA

Equity Bank Tanzania imeendeleza dhamira yake ya kukuza huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (MSEs na SMEs) kwa kudhamini Mkutano Mkuu wa Chama cha Wakandarasi Wanawake Tanzania (TWCA). Hatua hii inalenga kuchangia moja kwa moja juhudi za kitaifa za kuwawezesha wanawake kiuchumi, hususan katika sekta ya ujenzi inayokua kwa kasi nchini.

Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Kitengo cha Fedha za Biashara na Mtaji wa Uendeshaji wa Equity Bank, Bw. Stephen Matinya, alisema benki imebuni suluhisho maalum za kifedha kwa wakandarasi wanawake, zikiwemo mikopo ya mtaji wa uendeshaji, ushauri wa kifedha na huduma za kidijitali zinazorahisisha miamala. Aliongeza kuwa mipango hii inaendana na mikakati ya maendeleo endelevu kwa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi sawa na wanaume katika zabuni, ufadhili na fursa za biashara.

Kwa upande wake, Bi. Jacqueline Mollel, Meneja Mwandamizi wa Fedha za Biashara na Mtaji wa Uendeshaji kutoka Equity Bank, alibainisha kuwa uwezeshaji wa kifedha unapaswa kuambatana na elimu ya ujasiriamali na usimamizi wa miradi. Alisema benki imekuwa ikiendesha mafunzo ya mara kwa mara kwa wateja wake ili kuongeza uelewa kuhusu usimamizi wa fedha, uboreshaji wa rekodi za biashara, na matumizi ya teknolojia katika kusimamia miradi mikubwa.

TANZANIA’S 25-YEAR TREASURY BOND AUCTION SHATTERS RECORDS WITH NEARLY FIVEFOLD OVERSUBSCRIPTION

DAR ES SALAAM: The Bank of Tanzania’s latest auction of 25-year Treasury Bonds has made history, with investor bids soaring to nearly five times the amount on offer — a landmark moment for the nation’s securities market.

The government had targeted 264.31bn/- through the long-term bond issuance, yet demand surged to 1.23tri/-. Despite the overwhelming response, the Central Bank maintained discipline, accepting exactly 264.31bn/- in successful bids — matching the offer and resisting the temptation to absorb excess liquidity, even at favourable pricing.

Market analysts say the extraordinary oversubscription underscores investor confidence in Tanzania’s economic stability, debt management capability, and government policies.

“As expected in this rate-downcycle, investor sentiment has aligned with the Central Bank’s easing stance — but the demand far exceeded even my most optimistic expectations,” said Mr. Geofrey Kamugisha, Head of Business Development and Customer Service at Alpha Capital. He noted that the auction’s success came despite a coupon cut from 15.75% to 15.00%, reflecting strong trust in the government’s fiscal direction.

The weighted average yield to maturity stood at 14.4239%, down 37.39 basis points from the last 25-year auction on June 4 (14.7978%). Of 939 bids submitted, only 79 succeeded — highlighting intense competition and a scarcity premium for long-duration securities.

Monday, 11 August 2025

NMB YAENDELEZA UKARIBU NA WATEJA ZANZIBAR, YAAHIDI HUDUMA BINAFSI NA MIKOPO MIKUBWA ZAIDI

Zanzibar — Benki ya NMB imeendelea kuimarisha uhusiano wake na wateja wakubwa visiwani Zanzibar kupitia mikutano ya ana kwa ana, sambamba na kutoa elimu kuhusu masuluhisho mbalimbali ya kifedha kwa wafanyabiashara.

Ujumbe wa NMB, ukiongozwa na Meneja Biashara wa NMB Zanzibar, Bi. Naima Said Shaame, uliambatana na Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara, Bw. Dickson Richard, pamoja na viongozi wengine wa benki, katika ziara maalum ya kikazi kwa wateja wakubwa.

Ziara hiyo imelenga kuendeleza ukaribu na kuimarisha uaminifu kati ya NMB na wateja wake, huku ikihakikisha kuwa huduma na bidhaa zinazotolewa zinaendana na mahitaji halisi ya wafanyabiashara.

Kwa miaka mitatu mfululizo, NMB imetambuliwa na jarida la Global Banking & Finance Magazine kama Benki Salama Zaidi Tanzania (Safest Bank in Tanzania) — ikithibitisha ubora wake na kutambulika kimataifa katika nyanja mbalimbali za huduma za kifedha.

Akizungumza katika kikao hicho, Bi. Shaame aliwashukuru wateja wote waliohudhuria na kuwasihi waendelee kuwa mabalozi wa NMB kwa kuwaleta wateja wapya. Aidha, aliwahimiza kuhakikisha mauzo na malipo yote ya biashara zao yanapitishwa kupitia akaunti zao za NMB ili kuongeza nafasi ya kupata mikopo mikubwa zaidi.

Friday, 8 August 2025

NANE NANE 2025: BENKI YA NBC YATANGAZA FURSA MPYA ZA KIFEDHA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakulima wa Benki ya NBC, Bw. Raymond Urassa (kulia), akikabidhi mfano wa kadi ya bima ya mifugo kwa Bw. Maiya Saitia Maumbi (kushoto), mfugaji kutoka Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nane Nane) yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo. Bw. Maiya ni mnufaika wa bima ya mifugo ya NBC, mahsusi kwa wafugaji, inayotolewa na benki hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, Bw. Godwin Semunyu (kushoto), akimpongeza Bw. Maiya Saitia Maumbi (kulia), mfugaji kutoka Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, kwa kupata bima ya mifugo kutoka Benki ya NBC, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nane Nane) yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo.

DODOMA, AGOSTI 8, 2025 — Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imepongeza hatua ya Serikali ya kuboresha mfumo wa mauzo ya mazao ya wakulima, hususan kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani, ambao umeziwezesha taasisi za kifedha, ikiwemo NBC, kuwafikia wakulima kwa urahisi zaidi.
Hatua hiyo imeboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kama mikopo na elimu ya fedha, na kuongeza uaminifu kati ya wakulima na taasisi za kifedha.

Akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nane Nane) kitaifa jijini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakulima wa NBC, Bw. Raymond Urassa, alisema maboresho hayo yamerahisisha mchakato wa kuwatambua wakulima kama wateja wanaoweza kukopesheka kupitia dhamana za malipo ya mazao yao.

"Kupitia dhamana hii ya msingi, sasa tumekaribiana zaidi na wakulima," alisema Bw. Urassa.
"Kupitia akaunti ya NBC Shambani, wakulima wanaweza kupata mikopo ya nyumba bora, pembejeo na zana za kisasa za kilimo, ikiwemo matrekta, ‘power tiller’, na ‘combine harvester’. Pia wanapata mikopo ya malipo ya awali wakiwa wanasubiri malipo yao, hivyo kuepuka mikopo umiza ya mitaani. NBC tumeenda mbali zaidi kwa kuwasaidia kujenga maghala ya kuhifadhia mazao yao."

Aidha, NBC imebuni huduma za bima mahsusi kwa wakulima na wafugaji, ikiwemo bima ya afya, bima ya mifugo, na bima ya kilimo. Benki hiyo pia inashirikiana na kampuni mbalimbali ili kuwapatia wafugaji mbegu bora za mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku, kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa nyama, maziwa na mayai.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU), Bw. Karimu Chipola, alisema ushirikiano kati ya NBC na vyama vya ushirika umeleta manufaa makubwa, hasa kwa wakulima wa korosho na ufuta wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kupitia mikopo ya zana za kilimo na elimu ya fedha.

"Sasa ni rahisi zaidi kwa vyama vya ushirika kufanikisha miamala ya wanachama kupitia akaunti zao NBC. Kupitia ushirikiano huu, tunajiandaa kujenga maghala makuu ya kuhifadhia mazao na kiwanda cha kubangua korosho," alisema Bw. Chipola.

ZANZIBAR YAIDHINISHA RASMI HUDUMA ZA USAFIRI WA MTANDAONI, BOLT YAINGIA SOKONI

Zanzibar, 6 Agosti 2025 — Katika hatua ya kihistoria ya kisera, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeidhinisha rasmi uzinduzi wa huduma za usafiri wa mtandaoni visiwani humo, hatua iliyowezesha kampuni ya Bolt kuanza shughuli zake wiki hii. Uamuzi huu umefungua ukurasa mpya wa usafiri wa kisasa unaoendeshwa kwa teknolojia katika visiwa vya Zanzibar.

Kwa mujibu wa Bolt, ambayo inatoa huduma katika zaidi ya nchi 50 na miji 600 duniani, uwepo wake Zanzibar unamaanisha kuwapatia wasafiri chapa ya usafiri ambayo wageni kutoka mataifa mbalimbali tayari wanaifahamu na kuizoea kutumia wakiwa nyumbani kwao.


Kuchochea Uchumi na Fursa za Ajira

Serikali inatarajia hatua hii itachochea shughuli za kiuchumi kwa kuongeza upatikanaji wa usafiri wa bei nafuu na unaopatikana kwa urahisi. Hatua hiyo pia inalenga kuwahamasisha watalii, wafanyakazi wa kigeni, na wakazi kutoka Tanzania Bara kutumia zaidi huduma na bidhaa za ndani.

Ujio wa Bolt unatarajiwa kuleta faida kubwa za kijamii na kiuchumi — kuanzia ajira kwa vijana, ujasiriamali wa kidijitali, hadi kuongeza usalama na ufanisi wa usafiri kwa wakazi na wageni.

Kama jukwaa linaloaminika kimataifa, Bolt pia itaimarisha uthabiti wa huduma za usafiri hasa wakati wa msimu wa juu wa utalii, jambo litakalonufaisha biashara ndogo ndogo na sekta ya huduma Zanzibar.


Kauli ya Bolt Tanzania

“Tunapongeza uamuzi wa kishujaa na wa kisasa wa Serikali kuikubali huduma ya ride-hailing kama chombo cha kuchochea uchumi na kukuza maendeleo jumuishi,” alisema Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania.

Thursday, 7 August 2025

AIRTEL AFRICA FOUNDATION LAUNCHES ‘TECH FOR HER’ PROGRAM TO EMPOWER YOUNG WOMEN IN TECH

Dr. Segun Ogunsanya, Chair of the Airtel Africa Foundation.

Africa, 7 August 2025 — In a strategic move to foster digital inclusion and gender equity, the Airtel Africa Foundation has launched the ‘Tech For Her’ Program, an intensive five-week online training initiative aimed at upskilling young women in Kenya, Uganda, and Zambia.

In collaboration with Tertiary DNS, the initiative seeks to equip participants with in-demand digital skills including Linux AdministrationCybersecurity, and Data Analytics — with the broader goal of connecting them to global tech opportunities.

The program is part of Airtel Africa Foundation’s broader commitment to empower Africa through Digital Inclusion and addresses the glaring gender gap in tech employment across the continent.

“Africa’s digital revolution cannot reach its full potential without gender equity,” said Dr. Segun Ogunsanya, Chair of the Airtel Africa Foundation.
“The Tech For Her program helps to level the playing field by providing women with industry-relevant skills, mentorship, and pathways to high-growth tech roles around the world. By investing in Africa’s women, we are investing in sustainable economic transformation.”

Flexible Learning, Real Impact

Participants will engage in over 100 hours of intensive training, delivered through a flexible learning model that accommodates both working professionals and full-time learners. Weekend classes are designed for employed participants, while weekday sessions cater to those who are not currently working.

Eligible applicants must have basic digital literacy, and hold at least a national diploma in Science and Technology or equivalent.

DAR RAPID TRANSIT SET FOR MAJOR TRANSFORMATION AS NEW CNG BUSES ARRIVE

Dar es Salaam, Tanzania – Dar es Salaam’s public transport system is on the verge of a significant upgrade, following the arrival of 99 brand-new compressed natural gas (CNG)-powered rapid buses at the city’s port. These eco-friendly buses are expected to start operations within the next two weeks, marking a bold step in the city’s journey toward sustainable urban mobility.

This development is part of a broader investment led by local firm Mofat Company Limited, which plans to deploy a total of 255 articulated buses valued at approximately TSh 200 billion under the Bus Rapid Transit (BRT) Phase II project. The initiative is expected to ease congestion and improve commuter services across key routes in Tanzania’s commercial capital.

The 18-metre-long CNG buses will operate along a 20.3-kilometre corridor stretching from Mbagala to Gerezani via Kilwa Road, with extensions to Magomeni and Chang’ombe. This aligns with the government’s climate action efforts to cut down emissions from the transport sector.

According to Dar es Salaam Rapid Transit Agency (DART) Executive Director, Dr Athuman Kihamia, the buses arrived on Tuesday night and are undergoing final clearance procedures before hitting the roads by August 30, 2025.

“For the first time in the history of our country, articulated buses will be powered by natural gas,” he told the Daily News.

Wednesday, 6 August 2025

BOLT LAUNCHES OPERATIONS IN ZANZIBAR AFTER GOVERNMENT APPROVES RIDE-HAILING SERVICES

Tanzania, 6 August 2025 — In a landmark move toward a modern transport ecosystem, the Revolutionary Government of Zanzibar has officially approved the operation of ride-hailing services on the islands. This regulatory shift has paved the way for Bolt, a leading global ride-hailing platform, to begin operations in Unguja, marking a new era of tech-driven urban mobility in the archipelago.

The approval not only reflects the government’s progressive stance on innovation but also signals a deliberate push to boost economic activity and increase access to safe, affordable transportation in Zanzibar communities.

A Welcome Brand for Locals and Tourists

Bolt, which operates in over 50 countries and 600 cities globally, sees Zanzibar as a strategic market — particularly due to the island’s status as a globally renowned tourist destination.

“Being present in Zanzibar means offering a mobility brand that many foreigners already know and trust from their home countries,” said the company in a statement.

The availability of a globally recognized ride-hailing platform is expected to provide both residents and visitors with greater convenience, enhanced safety, and digital access to mobility — all essential elements in a rapidly evolving tourism economy.

STANBIC YAKAMILISHA KAMPENI YA SALARY SWITCH KWA KUZAWADIA WATEJA 90 KWA JUMLA

Sarah Odunga (kulia), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Stanbic Bank Tanzania, akiwa pamoja na Judith Wililo (kushoto) kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, wakati wa droo ya tatu na ya mwisho ya kampeni ya Salary Switch iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, 4 Agosti 2025 – Benki ya Stanbic Tanzania imehitimisha rasmi Kampeni ya Salary Switch kwa kufanya droo ya tatu na ya mwisho katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limeashiria mafanikio ya kampeni iliyolenga kuwathamini na kuwazawadia wateja waliamua kuhamishia mishahara yao Stanbic.

Katika droo hiyo ya mwisho, wateja 30 walishinda zawadi za pesa taslimu, huku tukio likishuhudiwa na Bi. Judith Wililo, mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, pamoja na waandishi wa habari ili kuhakikisha uwazi na uaminifu wa mchakato mzima wa uchaguzi wa washindi.

Kuimarisha Uhusiano na Wateja

Kampeni ya Salary Switch ilizinduliwa ili kuwahamasisha wafanyakazi walio kwenye ajira rasmi kuhamishia mishahara yao kupitia akaunti za Stanbic. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, kampeni hiyo imefanikiwa kutoa zawadi kwa jumla ya washindi 90, ambapo kila mshindi alipokea hadi TZS 500,000 kupitia droo za kila mwezi.

“Tunajivunia kufanikisha hitimisho la kampeni ya Salary Switch. Kampeni hii haikuwa tu kuhusu zawadi, bali ilikuwa ni fursa ya kuimarisha uhusiano wetu na wateja na kuonyesha thamani halisi ya huduma za kibenki tunazotoa,” alisema Sarah Odunga, Meneja wa Thamani kwa Wateja – Stanbic Bank Tanzania.

BENKI YA EXIM NA JKCI WAUNGANISHA NGUVU KUKUZA HUDUMA ZA MOYO NA USTAWI WA JAMII


Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu (kushoto), Afisa Masoko wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Irene Mbonde, na Mkurugenzi wa Hospitali ya JKCI–Dar Group, Dkt. Tulizo Shem, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa zoezi la upimaji wa moyo na utoaji wa elimu ya afya kwa wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania. Zoezi hilo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya JKCI, limefanyika katika Makao Makuu ya benki hiyo – Exim Tower, jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania – Agosti 5, 2025: Benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wametangaza mpango mpya wa afya unaolenga kuimarisha ushirikiano wao wa muda mrefu katika kuchochea afya ya jamii na kukuza huduma za moyo nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika kuadhimisha miaka 10 ya mafanikio ya JKCI, taasisi hiyo imeendesha zoezi la upimaji wa magonjwa ya moyo na kutoa elimu ya afya kwa wafanyakazi wa Exim Bank Tanzania, lililofanyika katika Makao Makuu ya benki hiyo – Exim Tower, jijini Dar es Salaam.

Ushirikiano wa Kuokoa Maisha Ndani na Nje ya Mipaka

Exim Bank Tanzania imekuwa mmoja wa waungaji mkono wa mwanzo na muhimu wa JKCI, ikionesha dhamira thabiti ya kuwekeza katika sekta ya afya. Ushirikiano huu umekuwa kichocheo kikubwa katika kukuza utalii wa matibabu, hasa kwa nchi jirani kama Comoros, ambako benki hiyo ina matawi na imewezesha kambi za matibabu kufanyika – kama ile ya mwezi Novemba 2024 ambayo iliokoa maisha ya watu wengi.

“Exim Bank tunajivunia kuwa mshirika wa muda mrefu wa JKCI katika safari yao ya kuokoa maisha ya Watanzania. Uwekezaji wetu katika afya ya wafanyakazi na jamii kwa ujumla ni sehemu ya msingi ya dhamira yetu ya kijamii,” alisema Stanley Kafu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Exim Bank.

NBC NAMED TANZANIA’S BEST DIGITAL BANK FOR CONSUMERS 2025 AT EUROMONEY AWARDS

Director of Retail Banking at NBC Bank, Mr. Elibariki Masuke (center), proudly holds the Tanzania’s Best Digital Bank for Consumers 2025 award, recently presented by Euromoney in recognition of the bank’s excellence in digital innovation, security, and financial inclusion. He is joined by Mr. Ulrik Peter, Head of Digital Alternative Channels and Transformations (left); Ms. Zubeider Haroun, Coastal Zone Manager (second left); Mr. David Raymond, Head of Marketing (second right); and Mr. Abel Kaseko, Head of Products and Sales (right).

Dar es Salaam, August 6, 2025 – The National Bank of Commerce (NBC) has been named Tanzania’s Best Digital Bank for Consumers 2025 by Euromoney during a prestigious award ceremony held in London, United Kingdom. This recognition reflects NBC’s commitment to innovation, financial inclusion, and digital excellence in the banking sector.

Pioneering Financial Inclusion through Technology

Addressing journalists in Dar es Salaam, Mr. Elibariki Masuke, Director of Retail Banking at NBC—on behalf of the bank’s Managing Director, Mr. Theobald Sabi—emphasized that the award is a result of the bank’s focused strategy to promote inclusive banking services through its digital platform, NBC Kiganjani.

“Through NBC Kiganjani, we have opened the doors of financial services to all Tanzanians – urban and rural, large and small businesses, smartphone users and those with basic phones. Our USSD and App services ensure that every Tanzanian has the opportunity to participate in the formal economy,” said Mr. Masuke.

He added that the platform's success is rooted in its ability to meet everyday financial needs such as bill payments, money transfers, instant microloans, transport ticket purchases, and more—offering convenience and accessibility to millions.

Innovation, Security, and Local Collaboration

Mr. Masuke also highlighted NBC’s strong digital infrastructure, which leverages technologies like NIDA verification, fingerprint authentication, and two-step verification, enabling seamless customer onboarding and enhanced security.

“Our efforts also support the UN’s Sustainable Development Goals, particularly SDG 9, which focuses on building resilient infrastructure and fostering innovation,” he noted.

AIRTEL AFRICA SIGNS STRATEGIC MULTI-YEAR PARTNERSHIP WITH XTELIFY TO ACCELERATE DIGITAL TRANSFORMATION

Africa, August 4, 2025 – Airtel Africa, a leading provider of telecommunications and mobile money services across 14 African countries, has entered into a multi-year, multi-million-dollar strategic partnership with Xtelify, the digital arm of Bharti Airtel India.

Under this landmark agreement, Airtel Africa will adopt Xtelify’s cutting-edge AI-powered software platforms to drive large-scale digital transformation, boost customer experience, and improve operational efficiency across its markets.

Transforming the Telco Landscape in Africa

Xtelify, a wholly owned subsidiary of Bharti Airtel, unveiled a future-ready software platform designed to simplify telecom operations worldwide. The platform combines:

  • Converged Data Engine for AI-driven insights and intelligence at scale,
  • A Workforce Platform to streamline tasks in real time, and
  • An Experience Platform to manage the full customer journey seamlessly.

By deploying Xtelify's Data Engine, Work, and IQ platforms, Airtel Africa’s 150,000-strong field workforce will be empowered with advanced market insights and tools to execute hyper-local strategies. The solution also includes critical use cases such as spam and fraud protection—key concerns in today’s telecom environment.

The Xtelify IQ solution will provide secure, real-time, omnichannel customer engagement, greatly enhancing service delivery and customer satisfaction across the continent.

“This partnership marks a transformative leap in our mission to build Africa’s digital future. By harnessing Airtel’s AI platforms that have proven scale in India, we are simplifying operations and accelerating hyper-personalized experiences for our customers,” said Jacques Barkhuizen, Group Chief Information Officer, Airtel Africa. “This is Airtel leveraging Airtel—a powerful synergy for sustainable growth, innovation, and unmatched value across our 14 African markets.”

Tuesday, 5 August 2025

AIRTEL MONEY NA BENKI YA I&M WAZINDUA MPANGO MAALUM KUWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Charles Kamoto (kulia), akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa I&M Bank Tanzania, Bw. Zahid Mustafa, wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango unaolenga kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini kupitia elimu ya kifedha na nyenzo nyingine muhimu za kukuza biashara zao. Katikati ni mmoja wa wanawake wajasiriamali walioudhuria semina iliyofanyika sambamba na uzinduzi huo, Bi. Virginia Gift.

DAR ES SALAAM – Airtel Money kwa kushirikiana na Benki ya I&M wamezindua rasmi mpango maalum unaolenga kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini kupitia elimu ya kifedha na nyenzo muhimu za kukuza biashara, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha maisha ya wanawake na kuchochea usawa wa kijinsia.

Mpango huu ni sehemu ya Mkakati wa Uendelevu wa Benki ya I&M Tanzania unaojikita kwenye nguzo kuu tatu: ujumuishaji wa kifedhaelimu ya kifedha, na uwajibikaji wa mazingira. Mkakati huu unaendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), hasa SDG 5 (Usawa wa Kijinsia) na SDG 13 (Hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi).

Kupitia huduma ya Kamilisha, iliyoundwa kwa pamoja na Airtel Money na Benki ya I&M, wateja hupata mikopo midogo kupitia simu zao za mkononi, hata wanapokosa salio kwenye akaunti zao za Airtel Money, ili waweze kutuma pesa au kulipa bili muhimu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Charles Kamoto, alisema:

"Kuna matumizi makubwa ya Airtel Money nchini, na tunalenga kujenga uwezo wa kifedha hasa kwa wanawake, kwa kuwawezesha kutumia huduma za kifedha za kidijitali kwa ufanisi. Tunataka kuhakikisha kuwa wateja wetu wana ujasiri na ujuzi wa kutumia teknolojia hii kwa maendeleo yao."

BANK OF AFRICA CELEBRATES 26TH ANNIVERSARY OF KING MOHAMMED VI'S ASCENSION TO THE THRONE

Pictured from left: Mr. Hamza Cherkaoui, Deputy Managing Director – Commercial; H.E. Zakaria El Goumiri, Ambassador of the Kingdom of Morocco to Tanzania; and Mr. Taha Bezzaz, Chief Financial Officer, Bank of Africa Group.

DAR ES SALAAM, TANZANIA – Bank of Africa Tanzania proudly participated in the 26th anniversary celebration of His Majesty King Mohammed VI’s accession to the throne of the Kingdom of Morocco. The prestigious event took place in Dar es Salaam, bringing together diplomatic corps, business leaders, and cultural representatives to honour the milestone.

Bank of Africa Tanzania is a subsidiary of the BANK OF AFRICA Group — a leading pan-African banking network headquartered in Morocco, with operations in 17 African countries and a strategic presence in France. The Group is majority-owned by BANK OF AFRICA – BMCE, Morocco’s second-largest private bank.

During the celebration, Bank of Africa Tanzania reaffirmed its commitment to strengthening bilateral ties between Tanzania and Morocco through financial collaboration, trade support, and cultural engagement. The event highlighted the growing economic and diplomatic relationship between the two countries, with the bank playing a pivotal role in connecting East and North Africa.

NMB YALETA MAPINDUZI SEKTA YA KILIMO NA UFUGAJI KUPITIA BIMA NA MIKOPO NAFUU

Dodoma, Tanzania – Benki ya NMB imeonesha dhamira ya dhati ya kuiwezesha sekta ya kilimo na ufugaji kwa kuzindua huduma ya bima ya mazao na mifugo, ikiwa ni hatua kubwa ya kulinda maisha na mali za wakulima na wafugaji nchini.

Wakati wa maonesho ya wakulima ya Nane Nane yanayoendelea jijini Dodoma, Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Bi. Janeth Shongo, alieleza mafanikio ya benki hiyo katika kufanikisha huduma hizo mpya na mpango mpana wa kutoa elimu ya fedha vijijini.


Ng’ombe 2,000 Wamekatiwa Bima – Thamani Yafikia Bilioni 1.5

Kupitia mpango wa bima ya mifugo, Bi. Shongo alibainisha kuwa hadi sasa takribani ng’ombe 2,000 wamekatiwa bima na wafugaji, huku kiwango cha chini cha gharama za bima kikiwa ni Shilingi 20,000. Thamani ya jumla ya bima hizo imefikia Shilingi bilioni 1.5.

"Mfugaji hana sababu ya kuwa na hofu tena. Iwapo mifugo yake itakumbwa na majanga, bima itamsaidia kurudia tena katika uzalishaji," alisema Shongo.


Wakulima 300,000 Wanufaika na Bima ya Mazao

Kwa upande wa kilimo, NMB imetoa bima ya mazao kwa zaidi ya wakulima 300,000. Jumla ya bima zilizotolewa zina thamani ya takribani Shilingi bilioni 659, huku bilioni 658 zikitolewa moja kwa moja kwa wakulima waliojiunga na mpango huo.

Shongo alisisitiza umuhimu wa wakulima kukata bima kwa ajili ya kulinda mazao yao dhidi ya changamoto kama ukame, mafuriko, na magonjwa ya mimea.


Mikopo Nafuu Ya Shilingi Bilioni 100 kwa Wafugaji

Katika juhudi za kufanikisha maendeleo ya sekta ya ufugaji, NMB imekopesha zaidi ya Shilingi bilioni 100 kwa wafugaji kote nchini. Mikopo hiyo inatolewa kwa masharti rafiki na riba nafuu, ikilenga kuwainua wafugaji wadogo na wa kati.

NMB YAIMARISHA USHIRIKIANO NA WAFANYABIASHARA MWANZA KUPITIA HAFLA YA CHAKULA CHA USIKU

Mwanza, 1 Agosti 2025 – Benki ya NMB imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwa mshirika imara wa wafanyabiashara nchini, baada ya kukutana na zaidi ya wafanyabiashara wakubwa 120 wa Mkoa wa Mwanza katika hafla maalum ya chakula cha usiku iliyofanyika jijini Mwanza.

Mkutano huo, uliolenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya NMB na wateja wake wakubwa, uliwakutanisha viongozi waandamizi wa benki hiyowawakilishi wa serikali, pamoja na viongozi wa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza. Katika hafla hiyo, maoni na matarajio ya pande zote yalitolewa kwa uwazi, kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kimkakati.

NMB: Benki Yenye Uwezo Halisi wa Kifedha

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMBFilbert Mponzi, alieleza kuwa benki hiyo ina uwezo mkubwa wa kuhudumia wateja wakubwa, akifichua kuwa NMB inaweza kutoa mkopo wa hadi zaidi ya shilingi bilioni 550 kwa mteja mmoja.

“Hii ni ishara tosha ya uimara wa NMB katika masuala ya kifedha na uwezo wa kweli wa kuwahudumia wafanyabiashara wakubwa,” alisema Mponzi.

Aidha, alisifu juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuweka mazingira bora ya kufanya biashara, hatua ambayo imesaidia ukuaji wa sekta binafsi na kuongeza mahitaji ya huduma za kifedha nchini.

Monday, 4 August 2025

NMB BANK DEEPENS BUSINESS RELATIONS IN MWANZA WITH HIGH-LEVEL DINNER EVENT

Mwanza, 1 August 2025 – In a move to reaffirm its strong partnership with the private sector, NMB Bank hosted a high-profile dinner event for 120 prominent businesspeople from the Mwanza region. The exclusive gathering, held in Mwanza city, brought together senior NMB executives, key government officials, and influential entrepreneurs to strengthen ties and share strategic insights.

The event served as a platform for open dialogue, where both the bank and its clients exchanged views and expectations to enhance mutual growth and collaboration.

“We have all the essential solutions for businesses. From large loans to modern payment innovations and insurance, we are well-positioned to serve you,” said Filbert Mponzi, NMB’s Chief Retail Banking Officer.

Mponzi emphasized the bank's financial strength and capacity, revealing that NMB can offer loans of over TZS 550 billion to a single client. He praised the government for fostering a business-friendly environment that has boosted private sector growth and increased demand for financial services.

He also highlighted the bank's accolades, including:

  • Being named Safest Bank in Tanzania for three consecutive years by Global Banking & Finance
  • Winning the Best Bank in Tanzania award 11 times in the past 13 years by Euromoney

A Trusted Partner Through Good Times and Tough Challenges

Representing the local business community, Gabriel Mgini, Mwanza Region Business Chairperson, expressed heartfelt appreciation to NMB Bank for its unwavering support.

“You have been with us in all stages of business—through both success and challenges. It’s clear that to grow, a business must partner with a strong financial institution. And NMB has proven to be just that,” said Mgini.