Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 11 August 2025

NMB YAENDELEZA UKARIBU NA WATEJA ZANZIBAR, YAAHIDI HUDUMA BINAFSI NA MIKOPO MIKUBWA ZAIDI

Zanzibar — Benki ya NMB imeendelea kuimarisha uhusiano wake na wateja wakubwa visiwani Zanzibar kupitia mikutano ya ana kwa ana, sambamba na kutoa elimu kuhusu masuluhisho mbalimbali ya kifedha kwa wafanyabiashara.

Ujumbe wa NMB, ukiongozwa na Meneja Biashara wa NMB Zanzibar, Bi. Naima Said Shaame, uliambatana na Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara, Bw. Dickson Richard, pamoja na viongozi wengine wa benki, katika ziara maalum ya kikazi kwa wateja wakubwa.

Ziara hiyo imelenga kuendeleza ukaribu na kuimarisha uaminifu kati ya NMB na wateja wake, huku ikihakikisha kuwa huduma na bidhaa zinazotolewa zinaendana na mahitaji halisi ya wafanyabiashara.

Kwa miaka mitatu mfululizo, NMB imetambuliwa na jarida la Global Banking & Finance Magazine kama Benki Salama Zaidi Tanzania (Safest Bank in Tanzania) — ikithibitisha ubora wake na kutambulika kimataifa katika nyanja mbalimbali za huduma za kifedha.

Akizungumza katika kikao hicho, Bi. Shaame aliwashukuru wateja wote waliohudhuria na kuwasihi waendelee kuwa mabalozi wa NMB kwa kuwaleta wateja wapya. Aidha, aliwahimiza kuhakikisha mauzo na malipo yote ya biashara zao yanapitishwa kupitia akaunti zao za NMB ili kuongeza nafasi ya kupata mikopo mikubwa zaidi.

Bi. Shaame alisisitiza kuwa ubunifu unabaki kuwa nguzo kuu ya benki hiyo, na NMB itaendelea kuibua suluhisho bora zitakazoongeza tija kwa wateja na kuchochea ukuaji wa biashara zao.







No comments:

Post a Comment