Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Thursday, 14 August 2025

EQUITY YAIBUA UBUNIFU MPYA: “SHULE MKONONI” KUBADILISHA USIMAMIZI WA ELIMU TANZANIA

Dar es Salaam – Benki ya Equity imezindua rasmi mfumo mpya wa kidijitali uitwao “Shule Mkononi” (School in Your Hand), unaolenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa taasisi za elimu na kuboresha huduma kwa wateja wake.

Kwa mujibu wa benki hiyo, mfumo huo utawezesha shule na vyuo kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi, mahudhurio na mapato ya taasisi kwa wakati wowote, hivyo kuongeza ufanisi wa kiutawala na kifedha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma za Malipo wa Benki ya Equity, Christopher Msangule, alisema mfumo huo utarahisisha ufuatiliaji wa ada, malipo na madeni kwa uwazi, jambo litakalowanufaisha wamiliki wa shule na vyuo.

Aidha, Msangule alibainisha kuwa “Shule Mkononi” itaongeza mawasiliano kati ya wazazi/walezi na taasisi za elimu, kwani itawawezesha kupata taarifa za maendeleo ya watoto wao moja kwa moja kupitia simu za mkononi bila kulazimika kufika shuleni.

Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Moga, Henry Mungoli, aliipongeza Benki ya Equity kwa ubunifu huo, akisisitiza kuwa mfumo huo utarahisisha kazi za kiutawala na kuongeza usalama wa wanafunzi kwa kufuatilia muda wa kuwasili shuleni.

Hadi sasa, shule 10 tayari zimejiunga na huduma hiyo, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi na uwazi katika usimamizi wa elimu nchini.


ENDELEA KUFUATILIA
Kwa habari zaidi za kina kuhusu sekta ya benki, masoko ya mitaji, na maendeleo ya kidijitali katika huduma za kifedha, endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog – chanzo chako namba moja cha taarifa sahihi na za kuaminika.

No comments:

Post a Comment