Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Tuesday, 23 May 2023

TMRC BOND ATTRACTS MORE LOCAL INVESTORS

TMRC Chief Executive Officer, Oscar Mgaya speaks at the event.

The Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) has listed on the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) the 4th tranche bond of which all of its investors are locals.

Commissioner for Debt Management at the Ministry of Finance and Planning, Japhet Justine (3rd left), rings a bell to signal the listing on the Dar es Salaam Stock Exchange, the 4th tranche of the TMRC bond. From his left is TMRC CEO, Oscar Mgaya and DSE Acting CEO, Mary Mniwasa. Second left is CMSA CEO, Nicodemus Mkama.

Compared to the previous tranches, luring more Tanzanian investors brings more hope for increasing the liquidity in the capital market.

Moreover, retail investors scoped a big chunk with 69 per cent against 31 per cent of corporate investors during the public offering.



During the public offering which was opened on April 3, until April 24, the TMRC targeted to collect 10bn/- but it successfully oversubscribed by collecting 11.28bn/-, equivalent to 112.8 oversubscriptions.

Speaking at an event to grace the listing of the bond over the weekend, Commissioner for Debt at the Ministry of Finance and Planning, Japhet Justin, pointed out that the move would give more opportunities to people to invest and list their shares on the DSE.

CRDB BANK APPROVES ALL-TIME HIGH DIVIDENDS

CRDB Bank Group Chairman, Dr. Ally Laay speaks during the 28th Annual General Meeting held in Arusha over the weekend.

CRDB Bank shareholders will be laughing all the way to the bank after the approval of the historical highest dividend of 45/- per share for last year.

The shareholders unanimously approved the proposed dividends at the just-ended annual general meeting over the weekend which is 25 per cent higher than the 36/- of 2021.

CRDB, the largest lender in the country, approved dividend per share bringing the total value for last year to 117.5bn/-.

CRDB Group Chairman Dr Ally Laay said the approved dividend signalling “a strong and progressive growth” in earnings per share to reach 134/50 last year.

“Our experience over the last five years has enlightened us on the value of adopting a resilient business model to navigate the ever-evolving challenges and the continuously shifting business landscape,” Dr Laay said told the AGM.

Last year the bank completed its 2018-2022 five-year medium strategy successfully.

As a result of these achievements, the Group achieved yet another major milestone by crossing the 10tri/- balance sheet threshold, being the first bank in the country to cross the mark,” Dr Laay said.

WANAHISA WA BENKI YA CRDB WAIDHINISHA GAWIO LA TZS 117.5 BILIONI KWA MWAKA WA FEDHA 2022


Arusha, 20 Mei 2023: Kwenye mkutano wao mkuu wa 28 wa mwaka, wanahisa wa Benki ya CRDB wameidhinisha mapendekezo ya Bodi ya Wakurugenzi ya kulipa gawio la Shilingi 45 kwa kila hisa hivyo kufanya jumla ya gawio kwa mwaka wa fedha 2022 kuwa Shilingi 117.5 bilioni.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika katika Kituo cha Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) huku wengine wakifuatilia ajenda zilizojadiliwa kwa njia ya mtandao, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt Ally Laay amesema gawio lililopitishwa ni sawa na ongezeko la 25% likilinganishwa na gawio la Shilingi 36 kwa hisa lililolipwa mwaka jana hali inayodhihirisha kuendelea kuimarika kwa pato kwa hisa ambalo mwaka 2022 limefika TZS 134.5.


“Kwa mara nyingine tena, tunafurahi kupata matokeo mazuri kwa mwaka 2022 yaliyochangia kuongeza thamani kwa wanahisa wetu. Faida tuliyoipata mwaka 2022 ni uthibitisho wa utekelezaji makini wa mpango mkakati wetu wa miaka mitano wa 2018 – 2022. Benki ilipata faida ya baada ya kodi ya Shilingi 351.4 bilioni sawa na ongezeko la 31% ikilinganishwa na Shilingi 268.2 bilioni za mwaka 2021,” amesema Dkt Laay.

Vilevile, Dkt. Laay amesema kampuni tanzu ya Burundi nayo inazidi kuimarika hivyo kuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye faida ya kampuni mama. Kwa mwaka 2022, amesema Benki ya CRDB Burundi imepata faida kubwa zaidi tangu lilipoanzishwa mwaka 2012. Kampuni hiyo tanzu ilipata faida ya Shilingi 23 bilioni mwaka 2022 ambayo ni sawa na ongezeko la 79.7% kutoka Shilingi 12.8 bilioni iliyopatikana mwaka 2021. Kwa faida hiyo, kampuni tanzu hiyo ilichangia 7.0% kwenye faida ya kampuni nzima.



“Nina furaha kuwataarifu kwamba hivi karibuni tumepata leseni ya kuanza kutoa huduma za fedha kutoka Benki Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (BCC). Vilevile, Benki yetu imeanzisha kampuni tanzu mbili mwaka huu ambazo ni CRDB Bank Foundation na CRDB Insurance Company ikiwa ni benki ya kwanza kuanzisha kampuni tanzu kamili a bima,” amesema Dk Laay.

Akizungumzia utendaji wa Benki, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema katika mwaka wa fedha 2022, waliendeleza juhudi za kukuza mapato na wakafanikiwa kwa kiasi kizuri kwani mapato ya uendeshaji yaliongezeka kwa 28% na kufika Shilingi 745.8 bilioni yakichangiwa na kuongezeka kwa mikopo iliyotolewa. Kwa mwaka 2022, uwiano wa mikopo chechefu ulishuka mpaka 2.8% hivyo kuwa ndani ya ukomo uliowekwa kikanuni wa kutozidi 5%.


Mizania ya Benki pia, amesema ilikua kwa 32% kutoka Shilingi 8.8 trilioni mwaka 2021 mpaka Shilingi 11.6 trilioni hivyo kuwa taasisiya kwanza ya fedha nchini kuvuka Shilingi 10 trilioni. Ongezeko hilo, amesema limechangiwa na kuimarika kwa amana za wateja zilizoongezeka kwa 26.4% na kufika TZS 8.2 trilioni kutoka TZS 6.5 trilioni za mwaka 2021.

Monday, 22 May 2023

BENKI YA NBC YAZINDUA HUDUMA YA NBC CONNECT KANDA YA ZIWA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bulandya Elikana, akizungumza na wateja wa benki ya NBC wakati wa kuzindua huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Mkuu wa kwa Kitengo cha Wateja wa Kimataifa wa NBC Wilson Nkuzi, akizungumza na wateja wakati wa uzinduzi wa huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Mkuu wa Kitengo cha Kidigitali na Miamala wa benki ya NBC Jimmy Myalize, akiwasilisha mada ya namna ya kufanya miamala kwa njia nafuu na rahisi wakati wa uzinduzi huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Baadhi ya wateja wa benki ya NBC na wadau wa sekta ya fedha wakipiga makofi kuipongeza benki hiyo, wakati wa kuzindua huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bulandya Elikana (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kimataifa wa benki ya NBC Wilson Nkuzi wakati wa kuzindua huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

MWANZA WAZINDUA RASMI MFUMO WA M-MAMA KURAHISISHA USAFIRI WA DHARURA KWA WAJAWAZITO, WALIOJIFUNGUA NA WATOTO WACHANGA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bulandya Elikana (wa pili kulia) akimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha m-mama katika Hospitali ya Sekou-Toure Mwanza, Pascal John (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa m-mama unaotoa huduma ya usafiri wa dharura kwa wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga ili kuokoa vifo vya mama na mtoto kwa mkoa wa Mwanza. Wakimsikiliza wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania PLC, Athuman Mlinga, na Afisa Mwandamizi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya, Jackson Shayo (wa pili kushoto). Sasa m-mama inapatikana kupitia kupiga namba ya bure (115) katika mikoa 13 ya Tanzania bara na yote mitano ya Visiwani Zanzibar. Na mpaka sasa zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani Maisha 806 yameokolewa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bulandya Elikana (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Athuman Mlinga (kushoto) akielezea namna kampuni hiyo inavyounga mkono juhudi za serikali kuhusu usambazaji wa mfumo wa m-mama unaosaidia kusafirisha akina mama wajawazito, waliojifungua na Watoto wachanga kwa dharura ili kuokoa vifo vya Mama na Mtoto kwa mkoa wa Mwanza. Uzinduzi wa mfumo huo umefanyika katika Hospitali ya Sekou-Toure Mwanza mwishoni mwa wiki, katikati ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Dkt. Bahati Msaki. Sasa m-mama inapatikana kupitia kupiga namba ya bure (115) katika mikoa 13 ya Tanzania bara na yote mitano ya Visiwani Zanzibar. Na mpaka sasa zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani Maisha 806 yameokolewa.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bulandya Elikana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya m-mama inayolenga kuwasafirisha wajawazito, waliojifungua na watoto kwa dharura ili kuokoa vifo vya mama na mtoto. Wakifuatilia wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Hospitali ya Sekou-Toure jijini Mwanza, kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania PLC, Athuman Mlinga na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Claudia Kaluli (katikati). Sasa m-mama inapatikana kupitia kupiga namba ya bure (115) katika mikoa 13 ya Tanzania bara na yote mitano ya Visiwani Zanzibar. Na mpaka sasa zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani Maisha 806 yameokolewa.

Baadhi ya wadau wa Sekta ya afya wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma ya m-mama inayolenga kuwasafirisha wajawazito, waliojifungua na watoto kwa dharura ili kuokoa vifo vya mama na mtoto uliofanyika katika Hospitali ya Sekou-Toure jijini Mwanza. Sasa m-mama inapatikana kupitia kupiga namba ya bure (115) katika mikoa 13 ya Tanzania bara na yote mitano ya Visiwani Zanzibar. Na mpaka sasa zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani Maisha 806 yameokolewa.

SERENGETI BREWERIES YAZINDUA MFUMO WA KUFANYA MAUZO KIGANJANI KWA WASAMBAZAJI WAKE

Mkurugenzi wa Mauzo wa kampuni ya bia ya Serengeti, Christppher Gitau akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa mauzo kiganjani ujulikanao kama Diageo One. Mfumo huo ni maalumu kwa wasambazaji wa bidhaa za kampuni ya bia ya Serengeti. Uzinduzi huo wenye kauli mbiu “Mchongo Kiganjani” ulizinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mfumo wa mauzo kiganjani wa Diageo One, Mchongo Kiganjani.

 

Dar es Salaam. Ijumaa Mei 19, 2023 - Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua mfumo wa aina yake wa kufanya mauzo wenye lengo la kurahisisha na kuongeza ufanisi wa mauzo yake kwa kuwapa wasambazaji wao (Stockists, Wholesalers & Bars) taarifa za kisasa kwa kutumia simu. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za SBL kukumbatia maendeleo katika uendeshaji wake na mtindo wa biashara.

Programu iliyopewa jina la DIAGEO ONE itakuwa suluhu moja kwa wateja wa SBL na kuwezesha mageuzi ya kiwango cha kimataifa jinsi SBL inavyofanya biashara na wateja wao. SBL ilizindua mfumo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa wateja wake muhimu baada ya awamu ya majaribio iliyoanza Februari mwaka huu kumalizika kwa ufanisi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisema, “SBL tumedhamiria kufanya mageuzi katika shughuli zetu za biashara, hii ni pamoja na kutumia teknolojia na ubunifu ili kuhakikisha kuwa kuna ufanisi katika namna tunavyofanya biashara. SBL ina nafasi kubwa katika sekta hii, na ndio maana tunasimamia ubunifu wa programu kama hizi."

JUMAPILI HII DStv INAKULETEA YANGA VS USM ULGER NDANI YA SUPERSPORT


Jumapili hii hapatoshi kwa Mkapa ambapo kikosi kinachowakilisha nchi Yanga watakipiga dhidi ya USM Ulger.

Na @dstvtanzania pekee kupitia Supersport inakupa kutazama Live mtanange huu, tena kwa kifurushi cha Poa TShs 10,000/= tu.

Piga *150*53# kulipia kwa urahisi kifurushi chako ili usikose burudani hii.

#TVNiDStv
#Unakosaje

Friday, 19 May 2023

USAID YASAINI MKATABA WA TZS BILIONI 11.8 KUIUNGA MKONO SERIKALI UTEKELEZAJI WA MFUMO WA M-MAMA NCHINI KOTE

Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Nassor Ahmed Mazrui (katikati) akishuhudia makabidhiano ya mkataba kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Philip Besiimire (kulia) na kiongozi wa Ujumbe wa serikali ya Marekani kutoka USAID, Kate Somvongsiri (kushoto), uliosainiwa baina ya Vodacom Tanzania Foundation na USAID wenye thamani ya dola za kimarekani 5m (Zaidi ya TZS bilioni 11.8) kuiunga mkono serikali katika utekelezaji wa mfumo wa m-mama nchini. Hafla hii imefanyika leo jijini Dar es Salaam. m-mama inapatikana kupitia namba ya bure (115) mitandao yote kwenye mikoa 13 ya Tanzania bara na mitano ya Visiwani Zanzibar, ambapo zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa, na takribani Maisha 722 yameokolewa.

Waziri wa Afya wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Mh. Nassor Ahmed Mazrui (katikati) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Philip Besiimire (kulia), na kiongozi wa Ujumbe wa serikali ya Marekani kutoka USAID, Kate Somvongsiri (kushoto), baada ya utiaji saini wa mkataba kati ya Vodacom Tanzania Foundation na USAID wenye thamani ya dola za kimarekani 5m (Zaidi ya TZS bilioni 11.8) ili kuiunga mkono serikali katika utekelezaji wa mfumo wa m-mama nchini. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. m-mama inapatikana kupitia namba ya bure (115) mitandao yote kwenye mikoa 13 ya Tanzania bara na mitano ya Visiwani Zanzibar, ambapo zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa, na takribani Maisha 722 yameokolewa.

Waziri wa Afya wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Mh. Nassor Ahmed Mazrui (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania PLC, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (wa kwanza kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Philip Besiimire (wa pili kulia) na Kiongozi wa Ujumbe waserikali ya Marekani kutoka USAID, Kate Somvongsiri (wa kwanza kushoto), baada ya utiaji saini wa mkataba kati ya Vodacom Tanzania Foundation na USAID wenye thamani ya dola za kimarekani 5m (zaidi ya TZS bilioni 11.8) ili kuiunga mkono serikali katika utekelezaji wa mfumo wa m-mama nchini. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. m-mama inapatikana kupitia namba ya bure (115) mitandao yote kwenye mikoa 13 ya Tanzania bara na mitano ya Visiwani Zanzibar, ambapo zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa, na takribani Maisha 722 yameokolewa.

Dar es Salaam – May 18, 2023 - Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na USAID zimesaini mkataba wa makubaliano ili kuunga mkono utekelezaji wa afya ya uzazi na mfumo wa usafiri wa dharura Tanzania kupitia mpango wa serikali wa m-mama.

Hatua hii inakuja baada ya serikali ya Tanzania kupitia Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango kutoa wito wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana wa kushirikiana ili kupanua mpango wa m-mama nchini kote. USAID iliahidi kuchangia dola za Marekani 5 milioni (takribani TZS 12 bilioni) ambazo zitajumuishwa na fedha ambazo Vodacom iliahidi kutoa awali, kiasi cha dola za Marekani 10 milioni (takribani TZS 23.5 bilioni) kwa serikali.

Kwa upande wa serikali, mbali na kuendesha na kumiliki kikamilifu mfumo mzima, pia imejidhatiti kugharamia gharama zote za usafiri na rasilimali watu kwenye vituo vya mawasiliano tangu kuanza kwa mfumo huu. Jitihada hizi za pamoja zitasaidia upatikanaji wa mfumo wa m-mama nchini kote na hivyo kuwafikia Watanzania zaidi ya milioni 60.

“Tunashukuru ushirikiano wa USAID na Vodacom Tanzania Foundation wa kuimarisha utekelezaji wa m-mama nchini kote. Ushirikiano baina ya sekta za umma na binafsi una umuhimu mkubwa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya huduma ya afya, kwa hakika tunaamini kuunganisha rasilimali na utaalamu wetu, tutaongeza kasi kuelekea ufanikishaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDG) hususani kwenye afya, tukihakikisha hakuna mama anayeachwa nyuma,” alisema Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mh. Nassor Ahmed Mazrui.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini, Kate Somvongsiri, Mkurugenzi wa Ujumbe wa Marekani kutoka USAID amesema, “ushirikiano huu, na mpango wa m-mama unawawezeshawa wanawake kuwa na maisha yenye afya bora, manufaa yake yatakuwa makubwa na kuongezeka zaidi, kama akina mama, wasichana, na Watoto wachanga watanufaika na ufumbuzi wa kipekee kwa changamoto iliyokuwa inawakabili.”

TSH1.6BN RAISED IN GEITA GOLD MINING KILI CHALLENGE

Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko (kushoto kwake) wakimkabidhi hundi ya Sh milioni 100 Mwenyekiti wa Mfuko wa Udhamini wa kudhibiti UKIMWI -ATF, Caroline Mdundo (wa tatu kushoto) zilizotolewa na Kampuni ya GGML kupitia Kampeni ya GGM Kili Challenge. Wengine wanaoshuhudia kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti - GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo na Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong. Hafla ya uzinduzi wa harambee ya kampeni hiyo imefanyika jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Hamis Nderiananga (kulia) akimkabidhi zawadi maalumu Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake muhimu katika kampeni ya GGML Kili Challenge ambayo ilianzishwa na Kampuni ya GGML mwaka 2002 kwa kushirikiana na TACAIDS kwa lengo la kutokomeza VVU/ UKIMWI.


On Thursday 18 May, a total of $700,000 (about Sh 1.6 billion) was raised at the launch gala in Dar es Salaam to support the government's efforts in the fight against HIV/AIDS.

The campaign is called the GGML Kili Challenge and is coordinated by Geita Gold Mining Limited (GGML) in collaboration with the Tanzania AIDS Control Commission (TACAIDS).

This year, the campaign, which involves climbing Mount Kilimanjaro, starts on 14th July and is scheduled to end on 20th July. The goal is to raise 2.3 billion shillings.

Sh1.6 billion was raised at the launch gala led by former President Jakaya Kikwete on Thursday.

Speaking during the fundraising event held in Dar es Salaam on 18th May 2023, His Excellency Jakaya Kikwete commended GGML and TACAIDS for collaborating on such a campaign which supports the government fight the spread of HIV/AIDS in the country.

"Keep up promoting the GGM Kili Challenge through various ambassadors and celebrities to raise its profile around the world," he said.

STANDARD CHARTERED UNVEILS STRAIGHT2BANK, NEXT GEN

Herman Kasekende, CEO of Standard Chartered Bank Tanzania, speaking to invited guests and journalists during the launch of Straight2Bank Next Gen in Tanzania.

The official Launch of Standard Chartered Bank Tanzania Straight2Bank Next Gen, the latest version of its digital banking platform.

Ms. Efeh Amoah, Head of Transaction Banking for Standard Chartered Bank Tanzania handing over a gift to Dr. Nkundwe Moses, Director General of ICT commission Tanzania during the unveiling ceremony of Straight2Bank Next Gen by Standard chartered earlier today at hyatt hotel dar es salaam.

A group photo of Standard Chartered Bank Tanzania employees and invited guests who attended the launch of Straight2Bank Next Gen in Tanzania.

Panel discussion.

Dar es Salaam, Tanzania - Standard Chartered Tanzania has launched Straight2Bank Next Gen, the latest version of its digital banking platform designed to meet the evolving needs of corporate clients in Tanzania. The new platform promises a more efficient, secure, and seamless banking experience, enabling businesses to easily manage their finances, streamline transactions, and access a range of digital solutions.

The launching event was graced by Dr. Nkundwe Moses, Director General of ICT commission, and attended by Makabelo Malumane, Managing Director of Transaction Banking for Standard Chartered Bank East Africa, Herman Kasekende, CEO of Standard Chartered Tanzania, clients, and other key stakeholders in the banking sector.

In addition to the launch of Straight2Bank Next Gen, Standard Chartered Tanzania also hosted a panel discussion on "The Importance of User Experience in Alternative Banking Channels." The panel featured industry experts and thought leaders.

Speaking during his opening remarks, Herman Kasekende, the CEO of Standard Chartered Bank Tanzania, said, "We are excited to launch Straight2Bank Next Gen in Tanzania, which represents a significant milestone in our ongoing digital transformation journey. As a bank, we are committed to delivering innovative, technology-driven solutions that meet the evolving needs of our clients. With Straight2Bank Next Gen, we are providing a platform that is designed to help our clients thrive in today's digital economy."

Thursday, 18 May 2023

BENKI YA NBC YAKABIDHI GAWIO LA TSH BILIONI 20 KWA WANA HISA WAKE, YAJIVUNIA MAFANIKIO

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu (wa tatu kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh 6 Bilion kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto) ikiwa gawio la mwaka 2022 kwa Serikali ambayo inamiliki asilimia 30 ya hisa za benki hiyo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NBC, Dk. Elirehema Doriye (wa pili kushoto) pamoja na maofisa waandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Dar es Salaam, Mei 17, 2023 – Serikali imepokea kiasi cha TZS 6 bilioni kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ikiwa ni sehemu ya gawio la kiasi cha Tsh bilioni 20 ambayo benki hiyo imetenga kwa ajili ya wanahisa wake kufuatia faida iliyopata katika kipindi cha mwaka 2022. Serikali inamiliki asilimia 30 ya hisa za benki hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi alikabidhi gawio hilo kwa Msajili wa Hazina Bw Nehemiah Mchechu aliewakilisha serikali wakati hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam ikihudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka serikali na maofisa waandamizi wa benki hiyo.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo Bw Mchechu pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika kipindi cha mwaka 2022, aliwasilisha salamu za Rais Samia Suluhu ambae pia aliipongeza benki hiyo huku akitoa wito kwa taasisi na mashirika yenye umiliki wa umma kuhakikisha yanatimiza wajibu wao wa kuwasilisha gawio litokano na faida za uendeshaji wa shughuli zao kwa serikali.

BENKI YA I&M YAZINDUA ‘WAKALA’ KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZA KIFEDHA

Mkurugenzi wa Benki ya I&M, Zahid Mustafa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya wakala mtaani, ambao wateja wa benki hiyo watakuwa wakipata huduma hiyo popote. Kushoto ni Emmanuel Mnema na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja, Deepali Ramayaiya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja, Zainab Maalim.

Dar es Salaam, Tanzania, Mei 17, 2023 – Benki ya I&M Tanzania imezindua huduma yake mpya ya kibenki inayojulikana kama ‘Wakala’ (Agency Banking) ili kukuza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Wateja wao. Huduma hiyo inayolenga kukuza wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha nchini imezinduliwa tarehe 17 Mei katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Huduma ya Wakala itawawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi kupitia mtandao mkubwa wa mawakala walioko kote nchini. Wateja wataweza kufanya aina mbalimbali za miamala ikiwemo kuweka na kutoa pesa, kuangalia salio, kutuma pesa, na kupata taarifa za miamala.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M Tanzania, Bw. Zahid Mustafa, alisema, "Huduma yetu mpya ya ‘Wakala’ au Agency Banking ni hatua muhimu katika jitihada zetu za kukuza upatikanaji wa huduma za kibenki kwa Watanzania. Kupitia huduma hii, wateja wetu hawatalazimika kusafiri umbali mrefu ili kupata huduma za kibenki. Benki imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wetu, na huduma hii mpya ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yetu."

Friday, 5 May 2023

JUMAMOSI HII MAN. CITY WATAVAANA NA LEEDS NDANI YA DStv

Vita ya Manchester City na Arsenal bado inaendelea na Jumamosi ya kesho Manchester City watavaana na Leeds. Je hii mechi itaishaje? Kumbuka Soka ni @dstvtanzania pekee

Lipia mapema kifurushi chako cha Compact ili kutazama Live mechi hii.

Piga *150*53# kulipia kwa urahisi zaidi.

#TVNiDStv
#Unakosaje

POLICE VISIT VODACOM TO OBSERVE HEALTH AND SAFETY AT WORK

Managing Director at Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire (left) receivs a certificate from the Police during a brief visit at the company’s headquarters in Dar es Salaam to learn how it observes health and safety practices at work. The visit is part of the commemoration of the World Day for Safety and Health at Work celebrated on April 28 of every year.
A Member of the Police together with Managing Director at Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire, make a quick inspection of the company’s vehicles during a brief visit at its headquarters in Dar es Salaam to learn how it observes health and safety practices at work. The visit is part of the commemoration of the World Day for Safety and Health at Work celebrated on April 28 of every year.


BENKI YA MWANGA HAKIKA YAZINDUA TAWI JIPYA LA KISASA JIJINI ARUSHA

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba (wa tatu kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika Bank, Eng. Ridhiwan Mringo (wa pili kushoto) wakifungua Kitambaa cha jiwe la Msingi kuashiria Ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha. Wanaoshuhudia pembeni kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe. Hafla ya uzinduzi ilifanyika hivi karibuni. 

Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Benki ya Mwanga Hakika wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba (kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha. Wanaoshuhudia pembeni ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika Bank, Eng. Ridhiwan Mringo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika Bank Eng. Ridhiwan Mringo akitoa hotuba katika hafla ya ufunguzi wa tawi jipya Jijini Arusha.  

Arusha. Aprili 28, 2023: Benki ya Mwanga Hakika (MHB) imezindua tawi jipya na la kisasa jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutanua mtandao wake wa huduma za kifedha nchi nzima. Tawi hilo jipya lililopo katika jenga la Central Plaza, barabara ya Sokoine jirani na Clock tower jijini Arusha, linafanya idadi ya matawi ya benki hiyo kufikia saba. Matawi mengine yapo Dar es Salaam, Moshi, Dodoma, Mwanga na Same. 

SHIRIKA LA KAZI DUNIANI WATUNUKIWA TUZO NA OSHA

Mwakilishi wa Shilika la Kazi Duniani nchini (ILO), Getrude Sima akionyesha tuzo waliyotunukiwa na OSHA kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro hivi karibuni. ILO ilitunukiwa tuzo hiyo kwa kuwa taasisi iliyomstari wa mbele katika kubadilishana taarifa za masuala ya usalama na afya nchini, kikanda na kimataifa.

Mwakilishi wa Shilika la Kazi Duniani nchini (ILO), Getrude Sima akihutubia kwa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro hivi karibuni, ambapo mwakililishi huyo amebainisha sheria ambazo nchi wanachama wa shirika la kazi duniani inabidi kuzitekeleza ili kuweka mazingira salama kwa wafanyakazi.

INFINIX YASHIRIKIANA NA VODACOM KUWANUFAISHA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUPITIA UZINDUZI WA HOT 30

Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc, Bw. George Lugata (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu ya Infinix HOT 30 kwa kushirikiana na Infinix Tanzania uliofanyika kwenye duka la Voda Shop lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki iliyopita. Wakimsikiliza kwa makini, kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Infinix Tanzania, Bw. Eric Mkomoya na kulia ni mzungumza wa lugha za alama, Bi. Fatna Salim Kaeza.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Infinix Tanzania, Bw. Eric Mkomoya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu ya Infinix HOT 30 kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania uliofanyika kwenye duka la Voda Shop lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki iliyopita. Katikati ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc, Bw. George Lugata, na kulia ni mzungumza wa lugha za alama, Bi. Fatna Salim Kaeza.

Dar es Salaam - May 1, 2023: Katika jitihada za kuongeza matumizi ya simu za mkononi nchini, kampuni ya teknolojia na mawasiliano, Vodacom Tanzania PLC imeshirikiana na Infinix kuzindua toleo jipya la simu aina ya Infinix HOT 30 ambayo itaambatana na kampeni maalum kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu.


Kuongeza matumizi ya simu janja ni moja ya chachu kwa Vodacom kufikia mafanikio ya adhma yake ya kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali, ambapo kampuni inalenga kutoa simujanja zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu. Na hii ndiyo sababu mojawapo ya kushirikiana na Infinix kuhakikisha kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu wanashiriki kikamilifu katika jamii ya kidijitali ambayo taifa linafanya jitihada kubwa kuijenga.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, George Lugata amesema, “Vodacom ina historia kubwa katika uendelezaji na uongezaji wa upatikanaji wa huduma za kiteknolojia kupitia simu. Tunaishi katika ulimwengu unaotaka kutuunganisha pamoja ambapo simu za kisasa sio anasa tena; bali ni hitaji muhimu la kiuchumi. Simujanja huwawezesha watu kuwasiliana, kujenga urafiki na pia kunufaika na fursa kadha wa kadha zinazotuzunguka ukilinganisha na kipindi cha nyuma.”