Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 5 May 2023

BENKI YA MWANGA HAKIKA YAZINDUA TAWI JIPYA LA KISASA JIJINI ARUSHA

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba (wa tatu kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika Bank, Eng. Ridhiwan Mringo (wa pili kushoto) wakifungua Kitambaa cha jiwe la Msingi kuashiria Ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha. Wanaoshuhudia pembeni kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe. Hafla ya uzinduzi ilifanyika hivi karibuni. 

Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Benki ya Mwanga Hakika wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba (kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha. Wanaoshuhudia pembeni ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika Bank, Eng. Ridhiwan Mringo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika Bank Eng. Ridhiwan Mringo akitoa hotuba katika hafla ya ufunguzi wa tawi jipya Jijini Arusha.  

Arusha. Aprili 28, 2023: Benki ya Mwanga Hakika (MHB) imezindua tawi jipya na la kisasa jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutanua mtandao wake wa huduma za kifedha nchi nzima. Tawi hilo jipya lililopo katika jenga la Central Plaza, barabara ya Sokoine jirani na Clock tower jijini Arusha, linafanya idadi ya matawi ya benki hiyo kufikia saba. Matawi mengine yapo Dar es Salaam, Moshi, Dodoma, Mwanga na Same. 


Akiongea wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Jagjit Singh alisema tawi hilo litaweza kurahisisha huduma kwa wateja wake na wakazi wa Arusha kwa ujumla. “Tawi hili la hapa Arusha litarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa kuwa lipo kati kati ya jiji. 

Tawi ni la kisasa na lina sehemu maalum kwa ajili ya wateja wakubwa, vifaa vya kisasa, huduma ya kubadilisha fedha nakadhalika. Hii yote ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma bora za kisasa na kwa urahisi,” alisema Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa tawi hilo limefunguliwa mahsusi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa fursa za kiuchumi zilizopo jijini Arusha zinaweza kuwafaidisha wakazi wa jiji hilo. 

“Tawi linalozinduliwa leo ni sehemu ya mkakati wetu wa kujitanua na kuwafikia wateja wengi zaidi. Lengo letu ni kuwafikia wateja popote pale walipo lakini pia tukizingatia utoaji wa huduma bora za kifedha zinazoendana na mahitaji yao,” alifafanua.

  

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba aliipongeza benki hiyo kwa kujikita katika kutoa huduma kwenye miradi ya miundo mbinu na kufanya kazi na wajasiriamali wadogo na wakati. 

“Napenda kuipongeza benki ya Mwanga Hakika kwa jitihada zake za kujitanua na hivyo kutoa fursa za wananchi wa kada mbali mbali kufikiwa na huduma za kifedha pamoja na kusaidia swekta mbali mbali ikiwamo ujenzi wa miundo mbinu,” alsema 



No comments:

Post a Comment