Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mfumo wa mauzo kiganjani wa Diageo One, Mchongo Kiganjani. |
Dar es Salaam. Ijumaa Mei 19, 2023 - Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua mfumo wa aina yake wa kufanya mauzo wenye lengo la kurahisisha na kuongeza ufanisi wa mauzo yake kwa kuwapa wasambazaji wao (Stockists, Wholesalers & Bars) taarifa za kisasa kwa kutumia simu. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za SBL kukumbatia maendeleo katika uendeshaji wake na mtindo wa biashara.
Programu iliyopewa jina la DIAGEO ONE itakuwa suluhu moja kwa wateja wa SBL na kuwezesha mageuzi ya kiwango cha kimataifa jinsi SBL inavyofanya biashara na wateja wao. SBL ilizindua mfumo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa wateja wake muhimu baada ya awamu ya majaribio iliyoanza Februari mwaka huu kumalizika kwa ufanisi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisema, “SBL tumedhamiria kufanya mageuzi katika shughuli zetu za biashara, hii ni pamoja na kutumia teknolojia na ubunifu ili kuhakikisha kuwa kuna ufanisi katika namna tunavyofanya biashara. SBL ina nafasi kubwa katika sekta hii, na ndio maana tunasimamia ubunifu wa programu kama hizi."
Aliongeza, "kiwango cha kazi iliyohusika katika kufanikisha jambo hili imekuwa muhimu kwa timu mbali mbali za SBL, EABL, na usaidizi mpana wa kampuni mama ya SBL ili kuhakikisha tunatekeleza kwa ufanisi programu hii mpya ambayo itabadilisha njia za kufanya kazi kwa wateja wetu"
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko ya Kidijitali wa SBL Chelu Mapolu alisema uzinduzi wa DIAGEO ONE kwa mkoa wa Dar es Salaam unafuatia mafanikio ya awamu ya majaribio ya mfumo huo, ambapo SBL imepima utendaji kazi na ufanisi wa mfumo huo kwawasambazaji na wateja mbalimbali jijini Dar es Salaam,” tumeifanyia majaribio na tunafurahia kuwaambia wasambazaji na wateja wetu kwamba mfumo huu utaleta mapinduzi makubwa kwa namna SBL inavyofanya mauzo. Kwa mfumo huu wa mauzo, wateja wetu watakuwa na taarifa muhimu zote kiganjani. Mfumo wa Diageo One ni rafiki kwa watumiaji na unafanya mchakato wetu wa uuzaji kuwa rahisi, mzuri na wa kufurahisha zaidi.”
Alibainisha kuwa, baada ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, matumizi ya mfumo wa DIAGEO ONE mchongo kiganjani utaanza kutumika kwa awamu nchini kote kwa wasambazaji wote wa bidhaa za SBL kuanzia mwezi Juni ambapo wateja wetu wote watapatiwa mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumohuo na njia bora wanayoweza kuutumia ili kurahisisha mchakato wao wa kuagiza na kufanya manunuzi
Kuhusu SBL
Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zilichukua nafasi ya zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo.
SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji Dar es Salaam, Mwanza, na Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka wa 2002, biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za kazi kwa watu wa Tanzania.
Kampuni za SBL Brands zimekuwa zikipokea tuzo nyingi za kimataifa na ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Guinness stout, na Guinness smooth. Kampuni hiyo pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon's Gin, Captain Morgan Rum, Baileys Irish Cream, na chapa zinazozalishwa nchini kama vile Bongo Don - SBL's maiden local spirit brand na Smirnoff orange.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na;
Rispa Hatibu
Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL
Simu: 0685260901
Barua pepe: Rispa.Hatibu@diageo.com
No comments:
Post a Comment