Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bulandya Elikana (wa pili kulia) akimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha m-mama katika Hospitali ya Sekou-Toure Mwanza, Pascal John (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa m-mama unaotoa huduma ya usafiri wa dharura kwa wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga ili kuokoa vifo vya mama na mtoto kwa mkoa wa Mwanza. Wakimsikiliza wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania PLC, Athuman Mlinga, na Afisa Mwandamizi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya, Jackson Shayo (wa pili kushoto). Sasa m-mama inapatikana kupitia kupiga namba ya bure (115) katika mikoa 13 ya Tanzania bara na yote mitano ya Visiwani Zanzibar. Na mpaka sasa zaidi ya akina mama 21,800 na Watoto wachanga wamesafirishwa kupitia mfumo huu, ambapo takribani Maisha 806 yameokolewa. |
No comments:
Post a Comment