Kukuza udadisi na kushirikishana maarifa miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu, Vodacom kwa kushirikiana na Infinix wataendesha ‘Chemsha Bongo’ kwa vyuo vinne vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Bw. Lugata ameonesha kujivunia ukurasa mpya wa upatikanaji wa simu nafuu ambazo wamezindua kwa wateja na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi kupitia Mtandao Supa ambapo kwa sasa unaendesha kampeni ya ‘Zaidi ya Mtandao’ iliyojikita katika kudhihirisha utoaji wa huduma na bidhaa zenye manufaa kwa Watanzania wote nchini.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Infinix, Eric Mkomoya amesema kuwa, “Infinix ni kampuni yenye mafanikio inayojulikana kimataifa. Leo tunayo furaha kubwa kuwatangazia ujio mpya wa Infinix HOT 30 yenye maboresho ya hali ya juu kwa wapenzi wa michezo na burudani za kwenye simu ikiwa imekuja na ‘8-core Helio G88 chip’ ikiwa na ‘ARM Cortex-A75 cores’ mbili zenye nguvu kufanya kazi kwa kasi ya juu mpaka kufikia 2.0GHz. Pia ina teknolojia bunifu ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi vitu, kutoka 8GB iliyonayo mpaka kufikia 16 GB. Matokeo yake inawezesha kuwaka kwa haraka na uwezo wa kuruhusu applikesheni zingine kufanya kazi, kuwapatia watumiaji urahisi wa kutumia kwa ufanisi bila kuathiri matumizi mengine."
Mkomoya alifafanua kuwa Infinix HOT 30 imekuja na teknolojia ya kuchaji ya 33W yenye betri yenye uwezo wa 5000mAh hivyo kufanya kikomo cha matumizi ya betri kuendelea kudumu kwa muda mrefu. Imekwishafanyiwa majaribio kuona betri ya simu itadumu kwa muda gani kupitia programu tofauti maarufu kama vile za filamu, michezo na burudani, na video fupi. Na kwa ufanisi kwenye picha angavu, simu hii ina 90Hz ambayo huboresha matumizi mara kwa mara ili mtumiaji aendelee kufurahia.
‘Chemsha Bongo’ kwa wanafunzi wa vyuo vikuu itaendeshwa kwa muda wa wiki nne ambapo washindi wataondoka na simu za Infinix HOT 30. Kwa kuongezea, wataweza kununua simu hizi mpya kwa punguzo la bei ndani ya kipindi ambacho ya zoezi hili kwenye maeneo yao ya vyuo.
No comments:
Post a Comment