Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_301026

Stanbic Bank Banner_201026

Thursday, 20 August 2020

VODACOM NA SMART CODES WATANGAZA WASHINDI WA SHINDANO LA ‘VODACOM DIGITAL ACCELERATOR PROGRAM 2020’

Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za ziada kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutangaza washindi wa mchakato wa shindano la “Vodacom Digital Accelerator.” Shindano hili lilihusisha vijana wabunifu chipukizi nchini na kudhaminiwa na Vodacom, ambapo Harrieth Peter na Adam Duma kutoka Smart Class (wawili kulia) walishinda shindano hilo. Wengine ni Mkurugenzi wa uendeshaji kutoka mfuko wa Kuendeleza Huduma za Fedha (FSDT) Irene Madeje (wa pili kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Code, Edwin Bruno.
Timu ya majaji wa shindano la “Vodacom Digital Accelerator” ikiongozwa na Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za ziada kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Tehama kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Connie Francis, Mkurugenzi Mkazi wa HDIF, Joseph E. Manirakiza, na Edwin Bruno Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Code.
  • Mchakato mrefu wa uchunguzi uliodumu kwa miezi kumi na moja umeibua kampuni tatu chipukizi za Kitanzania, ambapo wamechaguliwa kutimiza ndoto zao za kibiashara.
Tarehe 18 Agosti 2020 - Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania Plc na Kampuni ya Smart Codes wanayofuraha ya kutangaza washindi wa tatu wa mchakato wa shindano la “Vodacom Digital Accelerator.”

Mchakato huu ambao ulizinduliwa mwaka jana ukiwa na lengo la kusaidia vijana chipukizi na wanaoanzisha biashara katika sekta ya teknolojia kuweza kufikia mafanikio na kuwa na biashara zenye kuleta faida. Mchakato huu ulipokea zaidi ya maombi 600 ya vijana chipukizi wenye mawazo yao ya kibunifu katika nyanja za kilimo, teknolojia ya huduma za kifedha (Fintech), habari, Afya, elimu na biashara ya mtandao (E-commerce) ilipoanza. Kwa mwaka mzima uliopita wamepitia mafunzo, semina na kupata misaada mbalimbali.

Wakati akitoa tangazo hili, Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za ziada kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Bwana Nguvu Kamando amesema maono ya Kampuni ya Vodacom ni kuifikisha Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, na yataweza kufikiwa kwa kuhamasisha mawazo ya kibiashara yenye msukumo wa kiteknolojia ambayo yataleta mabadiliko endelevu.

BENKI YA NCBA YAAPA KUSAIDIA UKUAJI WA BIASHARA ZA VIWANDA VIDOGO NA VYA KATI NCHINI TANZANIA

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dokta Ashatu Kijaji (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi benki mpya ya NCBA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume na Mwenyekiti wa bodi ya NCBA, Sharmapal Aggarwal.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dokta Ashatu Kijaji akizungumza na wafanyakazi wa Benki mpya ya NCBA na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume akizungumza na wafanyakazi wa Benki mpya ya NCBA na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya NCBA wakiongozwa na bendi ya polisi kwenye maandamano ya sherehe za uzinduzi wa benki ya NCBA jijini Dar es Salaam.
  • Benki yaelezea namna itakavyokuwa mstari wa mbele kuleta uwezeshaji wa kiuchumi kupitia ujumusishwaji wa kifedha huku ikiwahamasisha wanaojituma kufikia malengo yao ya ukuaji 
Agosit 19, 2020 - Benki ya NCBA yaapa kusaidia biashara za viwanda vidogo na vya kati ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi.

Haya yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya NCBA Margaret Karume kwenye kusheherekea ujio wa Benki hio nchini, tukio likiambatana na uzinduzi wa Makao Makuu ya Ofisi ya NCBA na Tawi lao Kuu mtaa wa Ohio, Amani House jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Margaret Karume alisema kuwa, malengo ya Benki ni kuhamasisha wanaojituma kwenye safari yao ya mafanikio na kuchochea ukuaji wa kiuchumi nchini na zaidi. ‘Kupitia uvumbuzi wetu unaomzingatia mteja na uwekezaji kwenye bidhaa za kidijitali za benki, tuko tayari kuharakisha ukuaji na maendeleo katika sekta muhimu za kiuchumi kama vile biashara za viwanda vidogo, vya kati, mashirika, miradi mikubwa ya miundombinu na sekta ya kilimo’.

APPOINTMENT OF MS. RUTH H. ZAIPUNA AS CHIEF EXECUTIVE OFFICER OF NMB BANK PLC


Wednesday, 19 August 2020

BENKI YA NMB YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 15.2

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 15.2 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (wa pili kutoka kushoto) ikiwa ni gawio kwa Serikali wakati wa hafla iliyofanyika jana Wizara ya Fedha jijini Dodoma. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Mary Maganga na wa kwanza kutoka kulia ni Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 16 Afisa wa Ubalozi wa Uholanzi nchini, Mathis van Eeuwen (kushoto) iliyotolewa na Benki ya NMB kwa Rabo Bank Group. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Ruth Zaipuna.
Benki ya NMB imetoa shilingi 15. 2 bilioni kama gawio kwa serikali ambayo inamiliki asilimia 31.8 ya hisa zote ndani ya Benki hiyo.Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 45 ya gawio lililotolewa mwaka uliopita ambazo serikali ilipata Sh10.48 bilioni zilizotokana na faida ya mwaka 2018.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema kuwa, fedha zilizokabidhiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana katika mwaka wa fedha 2019 baada ya kuondoa gharama na kodi ambayo ilikiwa shilingi 45 bilioni.

Zaipuna amesema mbia mwingine ni Benki ya Rabo ya nchini Uholanzi ambayo imepata gawio la shilingi 16. 8 bilioni huku shilingi 16 bilioni zikienda kwa wawekezaji wengine ikiwemo taasisi za serikali. Alisema kwa mwaka 2019 licha ya benki kuwa chini ya uongozi wa mpito, lakini iliendelea kufanya vizuri na hata kipindi cha corona bado waliendelea kufanya vizuri kwani katika nusu ya mwaka wa fedha 2020 NMB wameshasajili faida ya shilingi 93 bilioni.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo, wameshaanza mkakati wa kuinua kilimo nchini na tayari wamekopesha wakulima shilingi 800 bilioni huku wafanyabiashara wakikopa shilingi 2.2 trilioni. Nyingine ni ununuzi wa madawati 40,000 na kompyuta 1000 zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia shule mbalimbali na kuwa wameendelea kuwa benki bora kwenye tuzo za jarida la kimataifa la Euro Money kwa miaka 8 mfululizo.

Akipokea mfano wa hundi hiyo, Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango alisema kiwango kilichotolewa ni kizuri na kuna matumaini makubwa ya gawio kupanda kwa mwaka huu. Dk. Mpango aliitaja Benki ya NMB kuwa miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri zaidi.

Awali Mwenyekiti wa bodi ya NMB Dk Edwin Mhede aliahidi Benki hiyo itafanya vizuri zaidi mwaka ujao baada ya kupata Afisa Mtendaji Mkuu kwani alipokuwa akikaimu hakuwa na nguvu zaidi katika maamuzi, Hivyo, wanaamini benki hiyo itaendelea kuwa imara zaidi na kuwa mfano kwa mabenki mengine nchini.

KAMPUNI YA UAP INSURANCE TANZANIA YACHANGIA MATANKI KWAAJILI YA SHULE ZA UMMA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima ya UAP, Stephen Lokonyo akionyesha mfano jinsi ya kuosha mikono kwa maji na sabuni kutumia matanki maalumu ya kuoshea mikono yaliyotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya Shule za Sekondari na Msingi za Mkoa wa Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika jana katika Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa. Kulia ni Afisa Elimu Taaluma Mkoa, Boniphace Wilson na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, Eunice Mganga.
Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Stephen Lokonyo akikabidhi matenki maalumu kwaajili ya kuoshea mikono kwa Afisa elimu taaluma Mkoa wa Dar es Salaam, Boniphace Wilson katika hafla iliyofanyika jana katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Shule ya Minazi Mirefu, Aveline Chugulu. Msaada huo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 100 ya utoaji wa huduma za bima Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Stephen Lokonyo akipeana mkono na Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Benjamini Mkapa, Maliki Salum wakati Kampuni hiyo ilipokabidhi matanki 40 ya kuoshea mikono kwaajili ya shule za Mkoa wa Dar es Salaam. Kulia (mwenye miwani) ni Mkuu wa Shule ya Minazi Mirefu, Aveline Chugulu.
  • Hatua hiyo imelenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kupunguza hatari ya kusambaa kwa magonjwa.
Dar es Salaam - Katika kuadhimisha miaka 100 ya utoaji huduma kwenye soko la bima, Kampuni ya UAP Insurance Tanzania imetoa msaada wa matanki 40 ya kuoshea mikono kwaajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Matenki hayo yatasiaida kuhakikisha wanfunzi wanapata nafasi ya kunawa mikono yao kwa maji safi na sabuni hivyo kuhakikisha mazingira salama kwa Watoto shuleni. Kampuni hiyo ni kampuni tanzu ya kampuni ya UAP Holdings Plc inayotimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1920.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Stephen Lokonyo alisema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uwajibikaji kwa jamii na umelenga kuhakikisha wanafunzi wanakuwa kwenye mazingira salama wakati wote wawapo shuleni na kupunguza hatari ya kupata magonjwa.

ABSA BANK TANZANIA LAUNCHES A NEW BRANCH IN DODOMA

Dodoma Regional Commissioner, Dr. Binilith Mahenge (second right), cuts a ribbon to officially open a new Absa Bank Tanzania branch in the Tanzanian Capital, Dodoma, located at PSSSF House. Witnessing the event held recently are from right; Absa Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi, ABT Chief Finance Officer, Obedi Laiser and other bank officials.
Dodoma Regional Commissioner, Dr. Binilith Mahenge (centre), leads Absa Bank Tanzania senior officials to celebrate inauguration of the bank's new branch located at PSSSF House in the Tanzanian Capital Dodoma on Monday. Others in the picture from right (partly hidden) are; Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi, Chief Finance Officer, Obedi Laiser, Head of Branch Network, John Beja and other bank officials and customers.
Dodoma Regional Commissioner, Dr. Binilith Mahenge (second left), exchanges views with Absa Bank Tanzania Chief Finance Officer, Obedi Laiser (second right), during the official launching ceremony of Absa’s new Dodoma branch at PSSSF House, in the Tanzanian Capital Dodoma. Looking on from the left are; Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi and Head of Branch Network, John Beja.
Absa Bank Tanzania Chief Finance Officer, Obedi Laiser (centre), together with some of the bank's customers cut a cake during the official launch ceremony of Absa’s new Dodoma branch in the Tanzanian Capital Dodoma.
Dodoma Regional Commissioner, Dr. Binilith Mahenge (Centre, seated), Absa Tanzania CFO, Obedi Laiser (right, seated), ABT’s Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi (left), with some of the bank's officials, pose for a memento photograph during the official launch ceremony of Absa’s new Dodoma branch in Dodoma on Monday.

JE, LYON AU BAYERN NANI KUFUZU FAINALI ZA UEFA LEO?

Baada ya ushindi wa PSG wa bao 3-0 jana, Je Lyon au Bayern nani kufuzu fainali za UEFA leo?

Kama kawaida sehemu pekee utakapoweza kuona mechi hii ni ndani ya @dstvtanzania kupitia ulimwengu wa kimichezo SuperSport.


Piga *150*53# kulipia kifurushi chako sasa au 0659 07 07 07 kujiunga na DStv kwa gharama nafuu zaidi.


#UCLOnDStv

RUTH ZAIPUNA ATEULIWA KUWA AFISA MTENDAJI MKUU MPYA WA BENKI YA NMB

Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna.
Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB imemtangaza Ruth Zaipuna kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Benki hiyo uteuzi ulioanza jana Agost 18,2020.

Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede alimtangaza Zaipuna huku akikiri kuwa mchakato wa kumpata haukuwa mwepesi lakini hakukuwa na upendeleo isipokuwa walitazama wasifu, utendaji na maslahi ya Benki na Tanzania.


Dk. Mhede alisema katika kipindi kirefu Benki hiyo ilikosa mtu baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake kuondoka na hivyo walibaki na mtu aliyekuwa anakaimu kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu lakini takwa la kisheria lilikuwa linawabana kuwa ni lazima wapate mtu.

Zaipuna anakuwa Mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu Benki hiyo ilipobinafsishwa ambapo kwa nyakati zote nafasi za juu zilishikwa na wageni wakiwemo Ineke Bussemaker aliyekuwa Mkurugenzi tangu 2014 – 2018 kisha nafasi hiyo ikachukuliwa na Albert Jonkergow ambaye alishikiria kwa kipindi cha mpito cha miezi sita kabla ya Zaipuna kupewa nafasi ya kukaimu.

Mwenyekiti alisema mchakato wa kumpata Mtendaji Mkuu ulikamilika Juni 30,2020 na jana ilikuwa ni siku ya kumtangaza huku akibainisha kuwa sifa zote zilizotakiwa katika nafasi hiyo, walijiridhisha kuwa Zaipuna anazo hivyo hakuna shaka kuhusu utumishi wake katika nafasi hiyo.


"Katika kipindi chote tulihangaika kumpata mtu mwenye kufikia vigezo vinavyotakiwa, lakini wakati mwanamama huyu alipokuwa anakaimu, Benki imeendelea kufanya vizuri zaidi na kukuza mtaji wake, hakuna mahali paliyumba chini ya usimamizi wake,hivi kwa hali hiyo mnadhani tungefanyaje," alisema Dk. Mhede.

Tuesday, 18 August 2020

BENKI YA NMB YATANGAZA NEEMA KWA WACHIMBAJI WADOGO

Benki ya NMB imetenga shilingi bilioni 32 kwa ajili ya mikopo kwa wachimbaji wadogo nchini. Akizungumza jijini Mwanza wakati wa kongamano la wafanyabiashara ‘NMB Business Club’, Mkuu wa idara ya Biashara wa Benki hiyo - Alex Mgeni alisema kutolewa kwa mikopo hiyo ni matokeo ya maboresho ya sheria na sera kwenye sekta ya madini yanayofanywa na serikali kwa lengo la kuongeza tija.

“Mikopo hiyo ambayo imeanza kutolewa tangu Januari, mwaka huu inahusisha gharama za kununua vifaa vya uchimbaji ikiwemo mitambo na magari ya kubebea mchanga wa madini migodini,” alisema Alex.


Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB - Alex Mgeni, akizungumza kwenye kongamano la biashara (NMB Business Club) Jijini Mwanza lililoratibiwa kwa ajili ya kuwafunda wafanyabiashara zaidi ya 200 kuhusu huduma za kifedha na faida za kutumia huduma za benki hiyo.
Kuhusu madhara ya janga la corona kwa sekta ya biashara, Mgeni alipongeza juhudi za Serikali zilizofanikisha kutokomezwa kwa ugonjwa huo uliosababisha changamoto katika mfumo wa biashara na uwekezaji. Alisema kutokana na mifumo ya biashara kupata changamoto, NMB iliwasaidia wateja wake ambao biashara zao ziliathirika zaidi, hasa wale wa sekta ya utalii.

“Kila mfanyabiashara aliyepata changamoto na kutifikia tulizungumza naye kutafuta namna ya kumsaidia. Wapo waliopunguziwa viwango vya marejesho na wengine marejesho yao yalisimamishwa kwa muda, hasa wale wa sekta ya utalii walioathirika zaidi,” alisema.


Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Baraka Ladislaus, akipata maelezo kutoka kwa msindika mvinyo - Rose Stephen, kwenye kongamano la wafanyabiashara Jijini Mwanza. 
Akizungumzia NMB Business Club, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Baraka Ladislaus alisema kongamano hilo linatoa fursa kwa benki kusikiliza, kupokea na kufanyia kazi hoja za wateja.

“Kupitia hoja na mrejesho kutoka kwa wateja wetu wakiwemo wafanyabiashara, NMB tunapata fursa ya kuboresha huduma na bidhaa zetu,” alisema Ladislaus.


TANZANIA REVENUE AUTHORITY NOTICE TO THE PUBLIC - INTRODUCTION OF ELECTRONIC FILING SYSTEM (E-FILING SYSTEM)


TANZANIA REVENUE AUTHORITY NOTICE TO THE PUBLIC - SUBMISSION OF TAX RETURNS IS NOW ELECTRONIC


NATIONAL BANK OF COMMERCE TENDER NOTICE - REQUEST FOR PROPOSAL FOR THE PROVISION OF VARIOUS SERVICES


VODACOM TANZANIA YAPONGEZWA KWA UWEKEZAJI MKUBWA WALIOUFANYA NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angela Kairuki (katikati) akizungumza na waandishi wa habari alipoitembelea kampuni ya Vodacom Tanzania PLC hivi karibuni na kuipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji mkubwa waliofanya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia na Mkurugenzi wa kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC, Dkt. Maduhu Isaack Kazi. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angela Kairuki akizungumza na Menejimenti ya Vodacom Tanzania PLC.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angela Kairuki akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Vodacom Tanzania PLC na maofisa aliofuatana nao.

Monday, 17 August 2020

TIGO - ZANTEL MERGER SET TO BOOST INNOVATION AND BENEFIT CUSTOMERS

It is well known that the African telecoms market has emerged as one of the fastest-growing telecoms markets in the world.

Boosted by the continent’s young and growing population, Africa has become a leader in the adoption of mobile technology and internet apps.

The growth of this sector is also apparent in Tanzania. For some time now, the country’s telecoms industry has proven to be a leader in the field of innovation. Today, mobile internet penetration has reached over 40 percent of the population.

Meanwhile, mobile-based applications – such as mobile money – have become an invaluable service for countless people.

The growth of this area is, in part, the result of mobile operators investing in next-generation infrastructure and developing a network which connects population centres across the country.

ABSA BANK TANZANIA SPONSORS SPECIAL TRAINING AT VETA UNDER COORDINATION OF PACT TANZANIA AND WAMATA

Absa Tanzania Citizenship Manager, Helen Siria (left) along with PACT Tanzania Corporate Engagements Manager, Beatrice Kamugisha handing over saloon equipment to Neema Bakari who has graduated at VETA. Neema is one of  the students who attended special training sponsored by Absa Tanzania under coordination of PACT Tanzania and WAMATA. The event was held at WAMATA offices in Dar es Salaam last week.
Absa Bank Tanzania has said it would keep on supporting the community, mentioning it as the bank’s priority along with providing quality services.

Speaking during the handing over ceremony of various equipment to girls who have recently graduated from VETA, Absa Bank Tanzania Citizenship Manager, Hellen Siria, said the vow was publicly given for Absa Bank is part of the community.

“We came from the community so we must be supportive to each other. Instead of waiting for customers to visit our branches, we support them at their specific surroundings,” said Hellen.


At least six selected youths from difficult surroundings attended special training at VETA sponsored by Absa Tanzania under coordination of PACT Tanzania and WAMATA.

MBIO ZA HISANI ZA BENKI YA CRDB ZAKUSANYA SHILINGI MILIONI 200 KUSAIDIA UPASUAJI WA WATOTO WENYE MAGONJWA YA MOYO KATIKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE


Mbio za hisani za Benki ya CRDB zimekuwa na mafanikio makubwa kwa kukusanya shilingi milioni 200 kusaidia watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo zaidi ya watu 4,000 walishiriki.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa mbio hizo za hisani zenye lengo la kusaidia jitihada za Serikali katika kutoa huduma bora za afya kwa watoto na kuongeza uelewa kwa jamii kuhusiana na magonjwa wa moyo kwa watoto.

“Kupata huduma bora za afya ni haki ya kila binadamu, haki ambayo ni muhimu katika maendeleo ya kila binadamu, hususan watoto wetu na vijana katika kukua vizuri na kuwa na afya njema,” alisema Mama Samia.



Makamu wa Rais pia aliwapongeza washiriki na makampuni yaliyoshiriki kuandaa CRDB Bank Marathon kwa kuungana kwa pamoja kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia upasuaji wa watoto, huku akiwataka watu wote kuendeleza jitihada hizo. “Upo usemi usemao ukiokoa maisha ya mtu umeikokoa dunia, jitihada hizi zisiishie hapa, tuendelee kushirikiana na Taasisi yetu ya Moyo katika kurejesha tabasamu kwa Watoto wetu,” alisisitiza.

Akitoa hotuba yake, katikati ya shangwe na nderemo za mziki, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema mbio hizo za hisani zimefanikiwa kuvuka lengo la kiwango kilicho wekwa cha shilingi milioni 200. Nsekela alisema mbio hizo za hisani zilizokuwa na kauli mbiu ya Kasi Isambazayo Tabasamu zimeweza kuwaunganisha washiriki kwa pamoja kuchangia fedha hizo zinazoelekezwa kwenye upasuaji wa moyo kwa watoto.

Nsekela alisema kwa muda mrefu Benki ya CRDB kupitia sera yake ya kusaidia jamii (CSR Policy) imekuwa ikiisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kufanya upasuaji kwa watoto. Ili kuongeza ushiriki wa jamii kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwamo changamoto ya upatikanaji wa huduma bora afya kwa watoto, Benki ya CRDB imeanzisha mbio hizo za hisani ambazo zitakuwa zikifanyika kila mwaka.



“Michezo ina nguvu ya kuwahamasisha watu kushiriki katika mabadiliko chanya. Nifuraha kubwa sana kwetu kuona mbio hizi za hisani za CRDB Bank Marathon zinachochea mabadiliko chanya katika jamii na kuongeza ushiriki wa watu katika kutatua changamoto na kuleta maendeleo.

“….nimefarijika kuona watu wengi wemaungana nasi katika jitihada za kusambaza tabasamu kwa watoto wetu. Mafanikio haya tusingeyafikia isipokuwa kwa kujitoa kwao. Tunawashukuru washiriki wote na makampuni yaliyoshirikiana nasi kuwezesha kufikia lengo,” aliongezea Nsekela.

Naye Waziri wa Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni Dkt. Harison Mwakyembe aliipongeza Benki ya CRDB na wadau walioshiriki katika mbio hizo za hisani kwa mchango wao walioutoa kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto.

“Benki ya CRDB imeonyesha sio tu ni bora kwa kutoa huduma bora kwa wateja, lakini pia ipo mstari wa mbele katika kusaidia jamii kwasababu uongozi wa benki hii unaelewa taifa lolote lenye mafanikio ni lazima kuwekeza katika afya ya watoto,” alisema Dkt. Mwakyembe.

 

Dkt. Mwakyembe alisema Benki ya CRDB imedhihirisha kuwa wapo Watanzania ambao wanauwezo wa kuongoza taasisi kubwa nchini na kwa mafanikio makubwa huku akibainisha kuwa miaka ya nyuma mabenki mengi yalikuwa yakiendeshwa na watu kutoka nje.

WAFANYABIASHARA WAHIMIZWA KUJIUNGA MTANDAO WA WATEJA WAKUBWA WA BENKI YA NMB

Benki ya NMB imewahimiza wafanyabiashara nchini kujiunga na Mtandao wa wateja wakubwa (NMB Business Executive Network) kujua na kunufaika na fursa za elimu juu ya mpangilio na uendeshaji biashara, kodi na taratibu za Serikali kuhusu biashara.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akisalimiana na Afisa Mkuuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Severine Lalika.
Akizungumza jijini Mwanza juzi katika wa mkutano wa mtandao huo wa Kanda ya Ziwa, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Filbert Mponzi alisema wafanyabiashara wanaojiunga na mtandao huo pia hupata fursa kukutana na kujadiliana ana kwa ana na uongozi wa juu wa benki hiyo.

 “Kupitia vikao vya kila mwaka vya NMB Business Executive Network wafanyabishara hupata elimu kutoka kwa wataalam wa fani mbalimbali kuhusu namna bora ya kufanya biashara kirahisi, kwa tija na gharama nafuu kupitia teknolojia,” alisema Mponzi.

Sehemu ya wageni waalikwa.
Mtandao huo ulioanza mwaka 2014, tayari unajumuisha wafanyabiashara zaidi ya 760 kutoka miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Mtwara na Morogoro.

“Hata wafanyabiashara wasiyo wateja wa NMB wanaweza kujiunga na mtandao huu kuona fursa, bidhaa na huduma zinazotolewa na benki yetu inayoongoza kwa faida baada ya kodi na ubora kwa miaka 11 mfululizo,” aliongezea Mponzi

VODACOM M-KULIMA INAVYOWEZESHA WAKULIMA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI

Mrajisi wa vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, akizungumza kwenye banda la Vodacom katika viwanja vya Nyakabindi kwenye maonesho ya nanenane, wakati wa uzinduzi wa mfumo wa M-Kulima unaowawezesaha wakulima kuwasiliana na kufanya miamala kwa kutumia mtandao wa Vodacom. Pembeni ni naibu Mrajisi, Charles Malunde na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania PLC Kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya (kulia).
Mkuu wa Mauzo Vodacom Tanzania PLC Kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa M-Kulima unaowawezesha wakulima kuwasiliana na kufanya miamala, mfumo huo umezinduliwa kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu kwenye maonesho ya nane nane. Mrajisi wa vyama vya Ushirika Dk Benson Ndiege (kushoto) Naibu Mrajisi Charles Malunde.
Wakulima wakifuatilia hotuba za uzinduzi wa mfumo wa Vodacom M-Kulima unaowawezesha kufanya miamala na kuwasiliana kwa urahisi, mfumo huo umezinduliwa kwenye viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa katika picha ya pamoja na Mrajisi baada ya uzinduzi wa M-Kulima. 

VODACOM YAZINDUA DUKA KUBWA LA KISASA MJINI LINDI

Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga (katikati) akikata utepe kuzindua duka la kisasa la Vodacom mjini Lindi mwishoni mwa wiki ili kuwafikishia wananchi huduma karibu yao. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo wa Vodacom kanda ya Pwani na Dar Es Salaam, Brigita Stephen na Meneja wa Vodacom Lindi, Omary Kilumanga.
Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga amepongeza kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC kwa kuwasogezea huduma mkoani humo na hivyo kuwaondolea adha ya kwenda Mtwara kufuata huduma.

Alisema kwa muda mrefu wakazi wa Lindi walipokuwa wakihitaji huduma za Vodacom walikuwa walilazimika kwenda Mtwara kupata huduma.

Mkuu huyo wa wilaya alisema hayo wakati wa uzinduzi wa duka kubwa la kisasa la kampuni hiyo ya simu mkoani Lindi, lililopo mtaa wa soko kuu mjini Lindi.


MWANGA HAKIKA MICROFINANCE BANK, BENKI MPYA BAADA YA KUUNGANA KWA BENKI TATU (MWNAGA BANK, HAKIKA NA EFC BANK)

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya (katikati) wakifuatilia zoezi la uzinduzi wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd. Benki hiyo ni muunganiko wa benki tatu (Mwanga Community bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd.
Naibu Gavana wa BOT, Dk. Bernard Kibesse (kulia), Naibu Mwekezaji, Raymond Tarimo pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Mhandishi Ridhuan Mringo wakifurahi baada ya kuzindua benki mpya iitwayo Mwanga Hakika Microfiance Bank baada ya muunganiko wa benki tatu tatu (Mwanga Community bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank).Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Jagjit Singh.
Naibu Gavana wa BOT, Dk.Bernard Kibesse akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi benki ya Mwanga Hakika Microfinance Bank iliyotokana na muunganiko wa benki tatu ikiwamo Mwanga community Bank, Hakika Microfinance Bank Pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi, Eng. Ridhuan Mringo.

Dk. Gabriel Ndunga, mteja wa kwanza kupata huduma kutoka benki mpya ya Mwanga Hakika Microfinance Bank iliyozinduliwa jana baada ya kuungana kwa benki tatu ikiwamo Mwanga Community Bank, Hakika Microfinance Bank Pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank.
  • Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza uimara wa benki katika utoaji wa huduma pamoja na ubunifu.
Dar es Salaam. Agosti 14, 2020. Mwanga Community Bank Ltd, Hakika Microfinance bank Ltd na EFC Tanzania Microfinance zimefanikiwa kuungana na kuwa benki moja ijulikanayo kama ‘Mwanga Hakika Microfiance Bank Ltd’, hatua inayoashiria ukuaji wa sekta ya kibenki nchini.

Muunganiko huo umefanikiwa kufuatia uthibitisho kutoka benki ya Tanzania (BoT) pamoja na Tume ya ushindani (FCC) na kupelekea kuundwa kwa Benki moja yenye thamani ya 40.5 bilioni ya mali.Pia, benki hiyo inatarajia kuongeza nguvu ya ushindani katika soko nchini.

Muungano huo ulizinduliwa rasmi katika hafla iliyohudhuriwa na Naibu Gavana wa BoT, Dk.Bernard Kibesse na kushuhudiwa na wadau mbalimbali kutoka sekta ya fedha.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Eng. Ridhuan Mringo alisema muungano huo ni muhimu katika kuunda benki imara inayoweza kutoa huduma zenye viwango kwa wateja zenye kuzingatia unafuu na teknolojia za kisasa.

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAUNGANISHA WANAFUNZI MAENEO YA PEMBEZONI KUPITIA PROGRAM YA INSTANT SCHOOL

Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald akizungumzia namna mradi wa Vodacom Instant Schools unavyounganisha intaneti na kusaidia wanafunzi katika maeneo ya pembezoni kujisomea wakiwa nje ya shule lakini pia jinsi ambavyo program hii inaunganisha shule zilizoko vijijini (School Connectivity). Wengine pichani ni Mhandisi kutoka UCSAF Ritha Kimolo (kushoto) na Msaidizi wa Mradi kutoka ISOC Peter Mmbando.

Friday, 14 August 2020

PKF TANZANIA HOSTS SECOND TAX WEBINAR IN COLLABORATION WITH TANZANIA REVENUE AUTHORITY AND CONFEDERATION OF TANZANIA INDUSTRIES

How well prepared are you for tax audits? How well are you able to assess the related risks and what solutions are available at your disposal?

PKF Tanzania in collaboration with the Tanzania Revenue Authority (TRA) and the Confederation of Tanzania Industries; invites you to a FREE Zoom webinar on Friday, August 14th 2020 from 1500hrs. The webinar will focus on managing tax audits and related risks.

This comes one month after the first live event that focused on key tax changes over the last five years, successfully impacted approximately 600 participants last July.

Join us, have your questions answered, share experiences and receive your participation certification from the comfort of your own device.