- Hatua hiyo imelenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kupunguza hatari ya kusambaa kwa magonjwa.
Matenki hayo yatasiaida kuhakikisha wanfunzi wanapata nafasi ya kunawa mikono yao kwa maji safi na sabuni hivyo kuhakikisha mazingira salama kwa Watoto shuleni. Kampuni hiyo ni kampuni tanzu ya kampuni ya UAP Holdings Plc inayotimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1920.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UAP, Stephen Lokonyo alisema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uwajibikaji kwa jamii na umelenga kuhakikisha wanafunzi wanakuwa kwenye mazingira salama wakati wote wawapo shuleni na kupunguza hatari ya kupata magonjwa.
“Tunafarijika kuunga mkono jitihada za Serikali na wadau wengine katika kuhakikisha kwamba wanafunzi ambao ni taifa la kesho wanapata elimu bora. Msaada huu utahakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu katika mazingira ambayo ni salama kwa afya zao muda wote,” alisema.
Matanki hayo yatasambazwa kwenye shule za Msingi na Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam kulingana na mahitaji kama itakavyoelekezwa na Ofisi ya Elimu mkoa.
Akipokea msaada huo, Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Dar es Salaam,Boniphace Wilson alipongeza hatua hiyo akisema kwamba itasaidia kuongeza kasi ya udhibiti wa milipuko ya magonjwa mashuleni na kufanya mazingira ya kujifunzia kuwa salama zaidi.
“Tunawapongeza UAP Tanzania kwa kuona umuhimu wa kutoa matanki haya kwaajili ya shule zetu za Mkoa wa Dar es Salaam, hii itasaidia kuhakikisha wanafunzi wanapata nafasi ya kuosha mikono yao kwa maji safi na sabuni na kuleta usalama wa mazingira ya kujifunzia,” alisema.
Msaada huo ni utekelezaji wa sera ya uwajibikaji kwa jamii ambayo UAP imekuwa ikiendesha katika maeneo mbalimbali ikiwamo Afya, elimu pamoja na mazinigira tangu ilipoanza kutoa huduma hapa Tanzania.
Kwa sasa kampuni hiyo inatoa huduma katika nchi mbalimbali ikiwamo Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Tanzania.
Kuhusu UAP Insurance Tanzania;
UAP Tanzania ilianza kutoa huduma za bima hapa nchini mwaka 2013 baada ya kununua asilimia 60 ya hisa kwenye kampuni ya Century Insurance Ltd na kuitwa UAP Insurance Tanzania.
UAP imejipambanua katika kuwa mdau mkubwa katika kuchochea ukuaji wa soko la bima Pamoja na huduma za kifedha kwa kutoa huduma za bima ikiwamo usafiri wa majini, anga huku ikilenga kuanzisha huduma kamili za kifedha.
No comments:
Post a Comment