“Mikopo hiyo ambayo imeanza kutolewa tangu Januari, mwaka huu inahusisha gharama za kununua vifaa vya uchimbaji ikiwemo mitambo na magari ya kubebea mchanga wa madini migodini,” alisema Alex.
Kuhusu madhara ya janga la corona kwa sekta ya biashara, Mgeni alipongeza juhudi za Serikali zilizofanikisha kutokomezwa kwa ugonjwa huo uliosababisha changamoto katika mfumo wa biashara na uwekezaji. Alisema kutokana na mifumo ya biashara kupata changamoto, NMB iliwasaidia wateja wake ambao biashara zao ziliathirika zaidi, hasa wale wa sekta ya utalii.
“Kila mfanyabiashara aliyepata changamoto na kutifikia tulizungumza naye kutafuta namna ya kumsaidia. Wapo waliopunguziwa viwango vya marejesho na wengine marejesho yao yalisimamishwa kwa muda, hasa wale wa sekta ya utalii walioathirika zaidi,” alisema.
Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Baraka Ladislaus, akipata maelezo kutoka kwa msindika mvinyo - Rose Stephen, kwenye kongamano la wafanyabiashara Jijini Mwanza.
|
“Kupitia hoja na mrejesho kutoka kwa wateja wetu wakiwemo wafanyabiashara, NMB tunapata fursa ya kuboresha huduma na bidhaa zetu,” alisema Ladislaus.
Mfanyabiashara, Contilda Magweti wa jijini Mwanza alisema licha ya kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara, kongamano hilo la kila mwaka katika maeneo mbali mbali nchini pia huwapa fursa ya kukutana na kujadiliana uso kwa uso na viongozi na watendaji wa Benki.
“Kwa kukutana pamoja tunapata fursa ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu kibiashara; NMB iangalie uwezekano wa kongamano hili kufanyika angalau mara mbili kwa mwaka,” alisema Magweti
Aliwashauri wafanyabiashara na wajasiriamali wenzake kuendelea kusaidiana maarifa ya kutafuta masoko ya bidhaa zao kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment