Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Proparco Afrika Mashariki, Jean Bendit-Du Chalard (kulia) wakionyesha mikataba ya makubaliano ya mkopo na dhamana za mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 182 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB. Mkopo na dhama hizo zilizotolewa na Proparco zitaiwezesha Benki ya CRDB kutoa mikopo kwa wajasiriamali wa sekta ya kilimo, wajasiriamali wanawake, pamoja na wajasiriamali walioathirika na janga la UVIKO-19.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Proparco Afrika Mashariki, Jean Bendit-Du Chalard (kulia) wakisaini mikataba wa makubaliano ya mkopo na dhamana za mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 182 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB. Mkopo na dhama hizo zilizotolewa na Proparco zitaiwezesha Benki ya CRDB kutoa mikopo kwa wajasiriamali wa sekta ya kilimo, wajasiriamali wanawake, pamoja na wajasiriamali walioathirika na janga la UVIKO-19.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Proparco Afrika Mashariki, Jean Bendit-Du Chalard (kulia) wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya mkopo na dhamana za mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 182 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Proparco Afrika Mashariki, Jean Bendit-Du Chalard (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Ufaransa Tanzania, Alex David Gullion (wapili kulia), Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya, Mihaela Marcu (wakwanza kushoto), na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB wakati wa hafla ya kusaini mikataba ya makubaliano ya mkopo na dhamana za mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 182 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB.
Benki ya CRDB imeingia makubaliano ya uwezeshaji wajasiriamali wadogo na wakati (MSMEs) wenye thamani ya Shilingi bilioni 182 na shirika la fedha la nchini Ufaransa la Proparco.
Makubaliano hayo ambayo yanajumuisha mkopo na dhamana za mikopo kwa wajasiriamali, itasaidia kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na mpango wa maendeleo wa Taifa, kwa kuzingatia zaidi wajasiriamali wanawake, wajasiriamali katika sekta ya kilimo, pamoja na wajasiriamali ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa na janga la UVIKO-19.
Proparco, ni kampuni tanzu ya shirika la maendeleo la UfaransaAgence Française de Développement Group (AFD Group), ambalo limejikita katika kutoa ufadhili na usaidizi kwa biashara na taasisi za kifedha barani Afrika, Asia, Amerika Kusini na Mashariki ya Kati.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka na utasaidia kwa kiasi kikubwa kufufua sekta ya ujasiriamali nchini na kuchochea ukuaji wa uchumi.
"Nidhahiri kuwa katika kipindi cha mitatu iliyopita wajasiriamali wengi wameathirika na janga la UVIKO-19. Tunatarajia kuwa fedha pamoja na dhamana hizi tunazozipata leo, pamoja na huduma zetu bunifu kwa ajili ya wajasiriamali, zitasaidia kuwainua na kuwawezesha wajasiriamali nchini kuboresha biashara,” amesema Nsekela.