Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 28 March 2022

NMB YAZINDUA HUDUMA YA WAKALA KWA SIMU ZA MKONONI

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi (wapili kushoto), kutoka kushoto - Kaimu Mkuu wa Uthibiti Hatari na Utekelezaji, Oscar Nyirenda, Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidigitali, Kwame Makundi na Mkuu wa Idara ya Bidhaa, Aloyse Maro.

Benki ya NMB imezindua huduma maalumu ya kuweka na kutoa pesa kirahisi kupitia wakala watakao tumia simu zao za mkononi tu.

Huduma hiyo ya NMB Pesa Wakala imezinduliwa jijini Dar es Salaam, ikilenga kusogeza ‘Karibu Zaidi’ huduma za kifedha kwa wananchi, pamoja na kutoa fursa za ajira kwa Watanzania, lengo likiwa kuongeza idadi ya mawakala kutoka 11,000 wa sasa, hadi 100,000 miaka mitano ijayo. 



Huu ni muendelezo wa utoaji wa suluhishi za kidijitali zilizo rahisi na salama kwa wateja ili kuwafanya kuendelea kufurahia huduma zao popote walipo.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alivitaja vigezo vya mtu kuomba uwakala wa NMB Pesa Wakala kuwa ni pamoja na Leseni ya Biashara, Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na simu ya mkononi ya aina yoyote (smartphone au kitochi).



Sasa Wakala anaweza kutumia huduma hii kupitia simu yake ya mkononi tu, bila kuhangaika kupata mashine za PoS ambazo zinatumia kadi. Kwa mteja, hakikisha umejiunga na NMB Mkononi kuweza kufurahia huduma hii kiurahisi.

No comments:

Post a Comment