Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 30 March 2022

BENKI KUU YA ETHIOPIA NA SAFARICOM WAJIFUNZA HUDUMA ZA KIFEDHA ZA M-PESA VODACOM ZINAVYOFANYA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Sitholizwe Mdlalose akizungumza na maofisa kutoka Benki Kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Safaricom Ethiopia namna huduma za kifedha kwa njia ya mtandao zinavyoleta tija kwa jamii na kuongeza pato la taifa kwa kufuata sheria na mamlaka husika za nchi. Ujumbe huo umekuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza huduma jumuishi za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi.
Mkurugenzi wa Vodacom M-Pesa, Epimack Mbeteni akiwaelimisha maofisa kutoka Benki Kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Safaricom Ethiopia namna huduma za kifedha kwa njia ya mtandao zinavyoleta tija kwa jamii na kuongeza pato la taifa kwa kufuata sheria na mamlaka husika za nchi. Ujumbe huo umekuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza huduma jumuishi za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi.
Meneja Uendeshaji Kituo cha Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Deogratius Massawe akiwaelezea maofisa kutoka Benki Kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Safaricom Ethiopia namna kituo hicho kinavyofanya kazi za kuweka usalama na kutunza taarifa za wateja wao.
Mkuu wa Mauzo Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Shirima akiwa kwenye kituo cha mafuta kwa ajili ya kuwaonesha maofisa kutoka Benki Kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Safaricom Ethiopia namna ambavyo wateja wanaweza kulipia kwa kutumia huduma ya "Lipa kwa simu" ikiwa ni sehemu ya kuwaonesha namna huduma ya kulipa kidijitali kupitia M-Pesa inavyofanya kazi.

No comments:

Post a Comment