Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 24 March 2022

FAINALI NMB MASTABATA - MILIONI 90/- KWA WASHINDI 30


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya Nmb, Filbert Mponzi (wa tatu kulia) akibonyeza kitufe kuashiria kuchezesha Droo ya mwisho ya msimu wa tatu wa Kampeni ya NMB MastaBata Kivyako Vyako. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi Benki ya NMB, Aikansia Muro na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga, (kulia) ni Meneja Mwandamizi kitengo cha Kadi, Manfredy Kayala na Balozi wa Kampeni hiyo, Masoud Kipanya.

Miezi mitatu ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ iliyoendeshwa na Benki ya NMB, imefikia tamati leo kwa wateja 30 kujinyakulia kitita cha Sh. Mil. 90 (sawa na Mil. 3 kila mmoja), hivyo kukamilisha kinyang’anyiro kilichobeba zawadi ya pesa taslimu Sh. Mil. 240.



Hitimisho ‘Grand Finale’ la kampeni hiyo, limefanyika NMB Tawi la Sinza jijini Dar es Salaam, kufikia ukomo kwa mchakato uliowanufaisha wateja 1,080, kati yao 1,000 wakijinyakulia Sh. Milioni 100 (sawa na Sh. 100,000 kila mmoja), huku 50 wakitwaa Sh. Mil. 50 (sawa na Mil. 1 kila mmoja) na 30 wa fainali wakishinda Mil. 90 hizo.



Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi, alisema malengo ya kampeni hiyo, ambayo ni kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu, yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kumekuwa na ongezeko la asilimia 10 ya watumiaji wa kadi.



Huu sio mwisho, kampeni hizi zitaendelea na tutaendelea kutoa elimu kwa jamii itambue umuhimu wa kutumia kadi badala ya pesa taslimu, kwa sababu ni rahisi, nafuu na salama zaidi.

No comments:

Post a Comment