Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 16 September 2015

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AZINDUA MIRADI YA NYUMBA ZA NHC MKOANI KIGOMA

Picha za matukio mbalimbali wakati Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipofanya uzinduzi wa jengo la Lumumba Complex na nyumba za bei nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC eneo la Mlole mjini Kigoma.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za bei nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC eneo la Mlole mjini Kigoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya (wapili kulia), Mbunge aliyemaliza muda wake wa Kigoma mjini Mh.Peter Serukamba (wanne kjshoto), Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Ndugu Walid Aman Kabouru.
Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Ardhi, Lukuvi, Mkurugenzi Mkuu NHC, Mchechu na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Machibya wakifurahi mara baada ya kukata utepe.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa NHC Lumumba Complex mjini Kigoma. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, (watatu kushoto), Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Lukuvi, (wanne kushoto), Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya, (Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bwana Nehemia Mchechu (kulia), na kushoto ni Mbunge aliyemaliza muda wake wa Jimbo la Kigoma mjini Mh.Peter Serukamba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe katika jiwe kuashiria kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa National Housing Lumumba Business Complex mjini Kigoma. Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na watatu kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu.
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Lumumba Complex Mjini Kigoma.
Rais Jakaya Kikwete alipowasili katika jengo la Lumumba plaza ambapo alifungua rasmi jengo hilo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa mjini Kigoma. Anayesalimiana naye ni Meneja wa NHC Kigoma, Nistas Mvungi na wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa NHC, Hamad Abdallah, Mjumbe wa Bodi ya NHC, Subira Mchumo na kushoto kabisa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki Haikamen Mlekio akitoa maelezo ya mradi wa gharama nafuu NHC Mlole mkoani Kigoma kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete. Mradi huu wa Mlole, ulianza Novemba 2012 na umeshakamilika. Una nyumba za kuishi familia 36 na zina vyumba viwili na vitatu, jiko na sebule. Nyumba zote zinauzwa kwa wananchi watakaohitaji na zimejengwa kwa utaalamu wa kisasa wa kutumia matofali ya yanayotengenezwa na mashine za hydraform.
Rais Jakaya Kikwete akifurahia mara baada ya kufungua Mradi wa nyumba za gharama nafuu Mlole. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Umati wa wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Jengo la Biashara wa Lumumba Complex ambalo ni miongoni mwa majengo machache marefu mkoani Kigoma linavyoonekana kwa mbali mjini Kigoma.

No comments:

Post a Comment