Dar es Salaam - Oktoba 8, 2026: Benki ya NMB imezindua Dawati Maalumu la Huduma kwa Wateja Wenye Ulemavu, likiwa na huduma ya mawasiliano ya video inayosaidiwa na wakalimani wa lugha ya alama, katika hatua inayolenga kuimarisha ujumuishi wa kifedha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki nchini.
Dawati hilo lililoanzishwa katika Kituo cha Mawasiliano cha NMB litahudumia wateja wenye ulemavu wa kusikia, kuona na viungo. Kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kupata msaada kwa kupiga namba ya simu ya bure 0800 002 002, kutumia huduma ya video kupitia WhatsApp inayosaidiwa na wakalimani wa lugha ya alama, au kutembelea matawi ya NMB nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema huduma hiyo inalenga kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata huduma za kibenki kwa heshima na usawa.
Alieleza kuwa dawati hilo pia litasaidia kulinda faragha za wateja na kupunguza utegemezi wao kwa watu wengine wanapohitaji kupata huduma za kifedha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Nemes Temba, aliipongeza NMB kwa kuanzisha huduma hiyo, akisema itasaidia kupunguza vikwazo vya mawasiliano na kuwawezesha watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika matumizi ya huduma za kifedha nchini.
Uzinduzi wa dawati hilo unaonesha hatua ya NMB katika kupanua upatikanaji wa huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali ya jamii, kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na kuweka mazingira yanayowawezesha watu wenye ulemavu kupata huduma kwa urahisi na kwa uhuru zaidi.
Endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari za hivi punde kuhusu sekta ya benki, fedha, biashara na maendeleo ya uchumi nchini Tanzania.
Mitandao ya Kijamii ya Kitomari Banking & Finance Blog
- LinkedIn: https://www.linkedin.com/feed/
- Facebook: https://www.facebook.com
- Instagram: https://www.instagram.com
- X (Twitter): https://x.com/home
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

No comments:
Post a Comment