Miaka minne katika tasnia ya nightlife ya Dar es Salaam si jambo dogo, na 1245 Bar, Restaurant & Lounge ina sababu ya kusherehekea hatua hiyo kwa namna ya kipekee.
Kwa kipindi cha miaka minne, 1245 imeendelea kuwa sehemu ya matukio mbalimbali yanayohusisha lifestyle na burudani jijini Dar es Salaam — kuanzia dinner na marafiki, birthday celebrations na muziki, hadi zile plan za “tupitie tu kidogo” ambazo mara nyingi huishia kuwa usiku mzima.
Sasa, katika kusherehekea kutimiza miaka minne, 1245 imeamua kuongeza kiwango cha sherehe hiyo kwa kuandaa 4PLAYS, tukio litakalofanyika Oktoba 17, 2026 katika Superdome Arena, Masaki.
Sherehe hizo zimeanza na shamrashamra za Bongo Flava Night, iliyowakutanisha wasanii Harmonize, Nandy, Abby Chams na Ommy Dimpoz, huku 1245 sasa ikielekeza nguvu zake kwenye 4PLAYS.
Young Jonn Kuongoza Burudani
Katika 4PLAYS, hitmaker kutoka Nigeria, Young Jonn, anatarajiwa kupanda stejini na kutoa burudani kwa mashabiki.
Msanii huyo anafahamika kupitia nyimbo kama “Xtra Cool” na “Big Big Things”, huku Ms DSF pamoja na dance troupe kutoka Afrika Kusini wakitarajiwa kuongeza ladha na upekee katika experience ya usiku huo.
Tukio hilo pia limeungwa mkono na wadau mbalimbali wakubwa, wakiwemo Don Julio, Heineken, Air Tanzania na Clouds Media, ambao ni miongoni mwa partners wanaoshiriki katika anniversary programme ya 1245.
Zaidi ya Sherehe
Zaidi ya kuwa tukio la kusherehekea miaka minne, safari ya 1245 inaonyesha namna hospitality, muziki na nightlife vinavyoendelea kukua na kuwa sehemu muhimu ya lifestyle ya Dar es Salaam.
Kwa 1245, formula inaonekana kuwa rahisi: muziki unaweza kuleta watu, lakini experience nzuri ndiyo inayowafanya warudi.
Na Oktoba 17, 2026, formula hiyo itaingia kwenye test nyingine kubwa kupitia 4PLAYS.
Kama wanavyosema wenyewe: “Hii ni chess, sio checkers!”
Kwa manunuzi ya tiketi, tembelea 4plays.1245tz.com au piga 0748 211 245.
Follow Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari zaidi za biashara, benki, fedha, kampuni, lifestyle na matukio mbalimbali Tanzania.
LinkedIn | https://www.linkedin.com/feed/
Facebook | https://www.facebook.com
Instagram | https://www.instagram.com
X (Twitter) | https://x.com/home


No comments:
Post a Comment