Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_301026

Stanbic Bank Banner_201026

Tuesday, 14 July 2020

VODACOM TANZANIA WAIPONGEZA SIMBA KUTWAA UBINGWA VODACOM PREMIER LEAGUE

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Linda Riwa (mwenye fulana nyeusi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa mabingwa wa ligi ya Tanzania VPL Simba SC mara baada kutawazwa kuwa mabingwa wa msimu wa 2019/2020 kwenye uwanja wa Majaliwa Ruangwa Lindi jumatano iliyopita. Vodacom Tanzania ndio mdhamini mkuu wa Ligi hiyo.




Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania PLC, ambaye ni mdhamini mkuu wa ligi kuu ya Vodacom Premier League (VPL) wameipongeza timu ya Simba Sports Club kwa kutwaa ushindi wa VPL 2019/2020. Pia kampuni hiyo imezipongeza timu zote zilizoshiriki VPL msimu huu.

"Tunajivunia sana kuwa sehemu ya ligi kuu ya Tanzania bara kwani inaendelea kukua na kuboreshwa mwaka hadi mwaka. Pongezi zetu pia ziwaendee viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), bodi ya ligi, vilabu vyote shiriki, waandishi wa habari, wadhamini wenza pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu katika ligi kuu mwaka huu," Linda Riwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom alisema.

Monday, 13 July 2020

SASA UNAWEZA KUPATA HUDUMA YA VISA KUPITIA ATM ZETU ZA UMOJA


VODACOM TANZANIA FOUNDATION YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU (MAKISATU 2020)


Baadhi ya wawakilishi kutoka Wizara Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni tano kutoka kwa Grace Chambua Meneja Mauzo Vodacom Kanda ya Kati iliyotolewa kwa mmoja wa shindano la Kitaifa wa shindano la Teknolojia ya ubunifu (makisatu 2020) lililofanyika Jijiji Dodoma mwezi machi mwaka huu uwanja wa Jamhuri.Vodacom walitoa sh milioni 20 kwa washindi wa ubunifu kwa shule za Msingi na Seondari.
Meneja Mauzo Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha (kushoto) wakati wa hafala fupi ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la teknolojia na ubunifu iliyofanyika jana Jijini Dodoma. Vodacom ilitoa sh milioni 20 kwa washindi wa shindano hilo.
Meneja Mauzo Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua akizungumza kwenye hafala fupi ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la teknolojia na ubunifu lililofanyika machi mwaka huu na zawadi zake kukabidhiwa jana Jijini Dodoma. Vodacom ilitoa sh milioni 20 kwa washindi wa shindano hilo uapnde wa wabunifu wa Shule za Msingi na Sekondari.
Meneja Mauzo Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua (kulia) akiwa na Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Profesa James Mdoe walipokuwa kwenye hafala fupi ya kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la teknolojia na ubunifu lililofanyika machi mwaka huu na zawadi zake kukabidhiwa Jijini Dodoma.

MULTICHOICE YAUNGANA NA UN KWENYE KAMPENI MAALUM YA COVID-19

Mwenyekiti Mtendaji wa kundi
la makampuni ya MultiChoice,
Imtiaz Patel.
Julai, 2020: Kundi la makampuni ya MultiChoice limetangaza mkakati wao mpya wa kusaidia katika kupambana na janga la COVID19 kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) ambapo wamezindua kampeni maalum ya kukabiliana na usambazaji wa taarifa zisizo sahihi kwa umma.

Kampeni hiyo imezinduliwa kwa kuzingatia ukweli kuwa kumekuwa na taarifa zisizo sahihi na ambazo hazitoki katika vyanzo na mamlaka husika na mara nyingi taarifa hizo huleta taharuki, woga na hofu kwa umma na hivyo kuathiri jitihada za kupambana na janga a COVID-19 kote duniani.

Tangu kulipuka kwa ugonjwa huo, MultiChoice imekuwa mstari wa mbele katika kupambana nao ambapo ilianza kutumia vyombo vyake kutoa matangazo ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya vifaa muhimu vya kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika muendelezo huo, sasa MultiChoice imeungana na umoja wa mataifa kwenye kampeni mahsusi ijulikanayo kama ‘Pause’ ambayo inawaasa watu kuacha kutunga au kusambaza habari zisizothibitiswa na mamlaka stahiki kuhusu COVID-19 kwakuwa habari hizo zinaleta madhara kwa umma.

BENKI YA NMB YASISITIZA UWEZESHAJI NA USHIRIKISHAJI WAZAWA

Mkuu wa Idara ya Huduma za Kifedha kwa Biashara za Kimataifa wa Benki ya NMB, Linda Teggisa, akizungumza wakati mabalozi wa nchi nane (Misri, Pakistani, Uturuki Kenya, Uganda, Falme za Nchi za Kiarabu na Sweden) wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini walipotembelea Banda la Benki ya NMB kwenye maonyesho ya Saba saba.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Urusi, Rifat Pateev akizungumza na Ofisa wa Benki ya NMB, BatuIi Sunna wakati mabalozi wa nchi kumi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini walipotembelea Banda la Benki ya NMB kwenye maonyesho ya Saba saba.
Benki ya NMB inaupa uwezeshaji na ushirikishaji wazawa kipaumbele katika kuchangia kwake utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo humu nchini, hasa ile endelevu ya kimkakati iliyoanzishwa na Serikali.

Sera hii ya benki hiyo ambayo pia inatumika kwenye kufadhili uwekezaji, ni mpango wake wa makusudi kusaidia uendelezaji na ushiriki wa Watanzania na biashara zao katika ujenzi wa taifa na maendeleo yake kwa ujumla.

Hiyo ni kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Huduma za Kifedha kwa Biashara za Kimataifa wa Benki hiyo - Bi. Linda Teggisa, aliyetoa ufafanuzi huo baada ya kuupokea ujumbe wa Mabalozi nane walioambatana na uongozi wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) walipotembelea banda la Benki ya NMB kwenye Maonyesho ya Saba Saba ambayo yanafungwa rasmi leo.

Saturday, 11 July 2020

EMPLOYMENT OPPORTUNITY AT TANZANIA AGRICULTURAL DEVELOPMENT BANK - MANAGER, PUBLIC RELATIONS, EVENTS AND STAKEHOLDERS MANAGEMENT

The jobholder reports to the Managing Director. He / She will be responsible for management of bank’s public relations, protocol services and all TADB’s events. He / She will also manage engagements with stakeholders across Local Authorities, Central Government, Statutory and Non-statutory bodies and other parties to establish strong working relationships.

EMPLOYMENT OPPORTUNITY AT TANZANIA AGRICULTURAL DEVELOPMENT BANK - SENIOR PUBLIC RELATIONS AND MARKETING OFFICER

The jobholder reports to the Manager, Public Relations, Events and Stakeholders Management. He / She is responsible for provision of publicity services, maintenance of bank’s relationship with stakeholders and maintenance of local media services for public relations and marketing.

EMPLOYMENT OPPORTUNITY AT TANZANIA AGRICULTURAL DEVELOPMENT BANK - PUBLIC RELATIONS AND MARKETING OFFICER - 2 VACANCIES

The jobholder reports to the Manager, Public Relations, Events and Stakeholders Management. He / She is responsible for supporting the provision of publicity services, maintenance of bank’s relationship with stakeholders and maintenance of local media services for good public relations and positive corporate image as well as marketing.

TCRA CALL FOR SUBMISSIONS - THE EQUALS IN TECH AWARDS

GROWTH IN DIGITAL LANDSCAPE IS IMPORTANT FOR TANZANIA’S ECONOMIC GROWTH

Across the world, the digital landscape is developing at a significant pace, driven in part by people’s use of mobile data.

According to the United Nations Conference on Trade and Development (CTAD), global data traffic is set to increase and reach 150,700 GB per second in 2022. This is a notable increase from just a few years ago in 2017 when there was only 46,600 GB per second.

Part of this growth can be attributed to an increase in data consumption in Africa. For example, across one network the usage of data rose by 52 per cent in 2019.

These recent figures represent positive news for the Tanzanian economy.

Indeed, according to a report by the World Bank, Tanzania’s digital landscape represents an important driver for the future growth of the economy. In addition, the convergence of increasing mobile internet penetration and innovative technologies also serves as one of the best ways of helping to drive Tanzania’s social development forward in years to come.

Friday, 10 July 2020

TAZAMA MECHI MBALIMBALI ZA PREMIER LEAGUE KUPITIA CHANELI ZA SUPERSPORT NDANI YA DStv PEKEE



Jumamosi hii #EPL ni 🔥🔥🔥 wa kuotea mbali.

Tazama mechi ⚽️⚽️⚽️ mbalimbali za Premier League kupitia chaneli za SuperSport.

Piga *150*53# kulipia kifurushi chako cha Compact TShs. 44,000 tu kutazama mitanange hii kabambe.

#EPL
#LiveSportsReturns

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA MILIONI 36 KWA SHULE ZA SEKONDARI TANGA

Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Benedicto Baragomwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakiwa wameshika madawati yaliyokabidhiwa na benki ya NMB kwa ajili ya shule saba za jijini Tanga kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga. Kutoka kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro, katikati mwenye miwani ni Meneja wa NMB Madaraka, Elizabeth Chawinga na mwisho kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga, David Mayeji.
Benki ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya shilingi Milioni 36 kwa shule Saba za Sekondari; Kirare, Japan, Chongoleani, Nguvumali, Pongwe na Galanos za Jijini Tanga, kwa kuzipatia madawati 250 pamoja na mabati 352 ili kutatua changamoto za kielimu.

Akikabidhi msaada huo katika Shule ya Sekondari ya Pongwe kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki hiyo, Benedicto Baragomwa alisema, wamekuwa mstari wa mbele kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Alisema kwa upande wa sekta ya elimu, kipaumbele wamekiweka kwenye madawati, vifaa vya kuezekea huku kwenye afya wakitoa vifaa vya tiba kama vitanda vya kujifungulia wakina mama na vitanda vya wagonjwa na magodoro yake vilevile na kusaidia majanga yanayoipata nchi.


Thursday, 9 July 2020

ACCESS TO MOBILE INTERNET IS AN IMPORTANT TOOL FOR ACHIEVING INCLUSIVE ECONOMIC GROWTH

Nearly 20 years ago, the Tanzanian Government launched an ambitious programme to help the nation reach the status of a middle-income economy by 2025.

Last week, the World Bank announced that Tanzania had finally reached the middle-income category; five years ahead of the initial timeline proposed by the government.

Tanzania has been able to reach this category due to a period of strong economic progress. Last year, for example, Tanzania recorded economic growth figures of 7 per cent, helping it maintain its position as one of Africa’s fastest growing economies.

The country’s achievement of becoming a middle-income economy is an important milestone. It is equally important, however, that the country continues to make every effort to ensure that the benefits of the country’s development are shared by all Tanzanians.

A recent study by academics in the United States found that digital technology is becoming an increasingly important tool for helping African countries achieve inclusive economic growth. Their study indicates that access to mobile internet – through smart phones – helps enhance consumer information, employment networking, job opportunities and financial inclusion.

NCBA BANK TANZANIA LIMITED YAONYESHA NEMBO YAO MPYA

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Bernard Kibesse (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu Mteule wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume (wapili kulia), Mkurugenzi Mteule wa Wateja Wakubwa, Binafsi na Wafanyabiashara wadogo na wa kati wa NCBA Bank Limited, Gift Shoko na Mwenyekiti Mteule wa Bodi wa Benki hiyo, Sharmapal Aggarwal mara baada ya uzinduzi wa Benki mpya ya NCBA uliofanyika jijini Dar Es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu Mteule wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa logo mpya kuashiria kuanzishwa kwa Benki mpya ya NCBA itakayoanza kutoa huduma rasmi kuanzia tarehe 8 ya mwezi huu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar Es Salaam jana.
Mkurugenzi Mteule wa Wateja Wakubwa, Binafsi na Wafanyabiashara wadogo na wa kati wa NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa logo mpya kuashiria kuanzishwa kwa Benki mpya ya NCBA itakayoanza kutoa huduma rasmi kuanzia tarehe 8 ya mwezi huu.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Bernard Kibesse (wapili kulia) akiwa ameshika nembo ya Benki mpya ya NBCA Bank Tanzania Limited pamoja na Mkurugenzi Mkuu Mteule wa NCBA Bank Limited, Margaret Karume (kulia), Mkurugenzi Mteule wa Wateja Wakubwa, Binafsi na Wafanyabiashara wadogo na wa kati wa NCBA Bank Limited, Gift Shoko (kushoto) na Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya NCBA Bank Limited, Sharmapal Aggarwal kwenye hafla ya uzinduzi wa Benki hiyo uliofanyika jijini Dar Es Salaam jana.
NCBA Bank Tanzania Limited (NCBA) imeonyesha nembo yao mpya na kauli mbiu wakati ilipozindua huduma zao rasmi baada ya kuungana kwa NIC Bank Tanzania Limited (NIC Bank) na Commercial Bank of Africa Tanzania Limited (CBA).

Hii ni kufuatia idhini iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kuunganisha benki hizi mbili na kuzipatia kibali cha biashara kuanzisha huduma zao rasmi tarehe 8 Julai 2020 kama NCBA Bank Tanzania Limited.

Idhini ya mdhibiti na utolewaji wa leseni na Benki Kuu ya Tanzania imetoa njia kwa NCBA Bank Tanzania Limited kuanzisha huduma zake rasmi.

Mwenyekiti mteule wa Benki ya NCBA Tanzania Bw Sharmapal Aggarwal alisema, ‘Benki ya NCBA ni benki imara na kubwa yenye nguvu ya kifedha, utaalamu na muunganiko wa kikanda inayowapatia wateja wake bidhaa na huduma mbalimbali’’.

Alielezea kuwa Benki ya NCBA inahamasisha ukuaji kupitia uvumbuzi wa kidijitali ili kuwapa watu msukumo wa kufanya mambo pasipo kurudi nyuma. Benki inathamini mahusiano binafsi na wateja ili kuleta mafanikio, inatoa huduma na bidhaa kwa upana zenye daraja la kwanza kwa wateja wa aina tofauti; binafsi, biashara na mashirika.

NCBA BANK TANZANIA LIMITED UNVEILS NEW LOGO




NCBA Bank Tanzania Limited (NCBA) has unveiled a new logo and tagline as it officially commences its banking operations as a merged entity.

This follows final approval for the merger between NIC Bank Tanzania Limited (NIC Bank) and Commercial Bank of Africa Tanzania Limited (CBA) effective Wednesday, 8th July 2020 and the issuance of a commercial banking licence for NCBA Bank Tanzania Limited from the Bank of Tanzania.

The approval by the regulator and the issuance of the licence by the Bank of Tanzania has paved the way for NCBA Bank Tanzania Limited to officially start operations.

NCBA’s Tanzania designate Chairperson, Mr Sharmapal Aggarwal said ‘‘NCBA Bank is a stronger and larger universal bank, with the financial strength, expertise and regional connectivity to put our customers first through an expanded range of products and services’’.

He noted that NCBA Bank inspires greatness through digital innovation and a can-do attitude that empowers customers to Go For It. The bank fosters successful personal relationships with customers, offering depth and breadth of best-in-class products and services for all segments of customers, be they Personal, Business or Corporate.

DStv INAKULETEA ASTON VILLA VS MAN UNITED LEO ALHAMISI JULAI 9, 2020 SAA 4:15 USIKU



Wednesday, 8 July 2020

UBA BANK TANZANIA JOINS GOVERNMENT ELECTRONIC PAYMENT GATEWAY (GePG) SYSTEM

Dar es Salaam. You can now make payments to over 600 government agencies through UBA Bank Tanzania, thanks to the lender’s integration into the Government e-Payment Gateway (GePG).

UBA Bank said recently that its system has been successfully integrated into the GePG, allowing Tanzanians to effectively make all government payments - tax and non-tax revenue - at any of UBA Tanzania’s branches.

Specifically, UBA Tanzania was one of the eight banks in the country that were certified by Tanzania Revenue Authority (TRA) to start collecting government tax revenue through the GePG Platform from July 1, 2020 as the Authority transits from the use of Taxbank to GePG.

The UBA Tanzania’s Head of Public Sector, Mr Dominick Timothy, said the integration of the bank’s system into the GePG was one of the ways that the pan-African lender was supporting the government’s development initiatives.

Mr. Timothy noted that following the successful completion of the GePG integration for tax and non tax government revenue payment at all our branches, the bank will also be integrating the platform into its multiple digital banking channels like mobile app, internet banking, Leo chatbot, USSD Magic Banking and Webcollect with a view to improving the ease with which members of the public can pay their tax and non-tax bills through UBA from the convenience of their homes and offices.

“It has always been our aspiration to support government initiatives of which efficient means of revenue collection through the unique digital expertise of the bank is a key component. We are glad and grateful to TRA and Ministry of Finance for providing us this opportunity to be of service to the nation” he said.


BENKI YA UBA YAJIUNGA NA MFUMO WA MALIPO WA SERIKALI WA KIELEKTRONIKI (GePG)

Dar es Salaam. Watanzania sasa wanaweza kufanya malipo ya kodi na yasiyo ya kodi kwenda kwa taasisi zaidi ya 600 za serikali wakiwa ndani ya matawi yote ya Benki ya UBA kwa haraka zaidi, imeelezwa.

Hili imetokana na uamuzi wa Serikali kuiunganisha Benki ya UBA na mfumo wa malipo wa Serikali wa kielektroniki (GePG).

UBA ilitangaza jijini Dar es Salaam hivi karibuni kuwa imepata kibali cha kuwa moja kati ya benki nane nchini zinazotumika katika kufanya malipo ya kodi na yasiyo ya kodi kwenda kwa taasisi za serikali kupitia mfumo wa GePG.

Mkuu wa kitengo cha sekta ya umma wa Benki ya UBA, Bw. Dominick Timothy alisema kuwa kuunganishwa kwa benki yake katika mfumo wa GePG ni moja wapo ya njia za taasisi hiyo ya fedha kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Tanzania, chini ya Rais John Magufuli.

Alisema kutokana na kuunganishwa kwa UBA na mfumo wa GePG, Benki hiyo sasa itaoanisha mfumo huo na njia zake za kidijitali zakibenki.

Njia hizo ni pamoja na kupata huduma za benki kwa njia ya simu (Mobile App), huduma za benki kwa njia ya mtandao (internet banking) pamoja na njia zijulikanazo kama Leo chatbot, USSD Magic Banking na Webcollect.

NCBA BANK TANZANIA ANNOUNCES NEW DESIGNATE MANAGING DIRECTOR AND CEO

Ms Margaret Karume.
Ms Margaret Karume brings 27 years of experience to the banking industry

Dar es Salaam. NIC BANK Tanzania Ltd and CBA Tanzania Ltd are in the final stages of concluding the merger that will see the two institutions operate as NCBA Bank Tanzania Ltd. The Board members have appointed Ms Margaret Karume as the Managing Director & Chief Executive Officer –designate of NCBA Bank (T) from 8th July 2020 when the Bank officially starts operations.

Ms Karume is the current Managing Director of NIC Bank Tanzania and brings 27 years of renowned banking experience.

“This is a new chapter for the two banks. I am looking forward to work with like-minded teams to create a strong financial institution in Tanzania. The new institution will reflect both banks’ values and mission, borrowing from the best of both and building a bigger and better new organisation to deliver more value for our customers and stakeholders,” said Ms Karume.

Previously, Ms Karume, a seasoned banker and an exemplary leader who has risen through the corporate ranks, worked at NIC Bank Group in Kenya as Executive Director of Credit Risk. Ms Karume, brings with her strong experience and knowledge in finance and business development. Besides her credit risk management experience, she has a wealth of experience in corporate banking having built her career at both NIC Group plc and previously Barclays Bank Kenya(now ABSA Bank).

She holds a Global Executive MBA and BSc. She attained her International Business Administration mark from the United States International University (USIU) - Africa and holds a Diploma in Customer Relationship Management from the Institute of Financial Services (U.K). She is also an Associate of the Kenya Institute of Bankers.

Confirming the appointment, the NCBA Board Chairperson – designate, Mr Sharmapal Aggarwal congratulated Ms Karume on her appointment.


MKURUNGEZI MTENDAJI WA TIGO SIMON KARIKARI ATEMBELEA BANDA TIGO SABASABA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo, Bw. Simon Karikari akipimwa joto la mwili kabla ya kuingia katika banda la Tigo jana ikiwa ni moja ya tahadhari ya Tigo kwa wateja wake.Tigo inaendelea kutoa ofa kabambe za simu na vifurushi kwa wateja katika msimu huu wa Sabasaba.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mawasiliano Tigo,  Bw. Simon Karikari akipokea maelezo kutoka kwa mtoa huduma jana alipotembelea banda la Tigo katika maonesho ya Sabasaba . Tigo inaendelea kutoa ofa kabambe za simu na vifurushi kwa wateja katika msimu huu wa Sabasaba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo, Bw. Simon Karikari akipata maelezo kutoka kwa watoa huduma kuhusu huduma ya Tigo pesa jana. Tigo inaendelea kutoa ofa kabambe za simu na vifurushi kwa wateja katika msimu huu wa Sabasaba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo, Bw. Simon Karikari akipokea maelezo Kutoka kwa mtoa huduma jana alipotembelea banda la Tigo katika maonesho ya Sabasaba.

WACHEZAJI WA TAIFA STARS WAKUNWA NA UDHAMINI WA SERENGETI PREMIUM LAGER


Wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, wameelezea kufurahishwa na udhamini wa Bia ya Serengeti Premium Lager na kusema kuwa udhamini huo umekuwa chachu kubwa kwa mafanikio ya timu.

John Bocco, mshambuliaji wa Taifa Stars, aliliambia gazeti hili kuwa, udhamini wa Bia ya Serengeti umeiwezesha timu kupiga hatua kubwa ikiwa ni pamoja na kufuzu kucheza Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka jana, baada ya miaka 39 tangu ifuzu mara ya mwisho.

“Mpira unahitaji uwekezaji ili kupata mafanikio. Kampuni ya bia ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti imeweza kutoa udhamini ambao umekuwa chachu kubwa katika kuiimarisha timu yetu ya taifa. Pengine kama siyo udhamini huu tusingeweza kufika hapa tulipofika leo,” anasema mshambuliaji huyo

Kampuni ya SBL kupitia Bia ya Serengeti ilikuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa kuanzia mwaka 2017 baada kusaini mkataba wa miaka 3 na Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa nchini (TFF)

MIPIRA INAENDELEA KUBAMBA NDANI YA DStv



Mipira ⚽️⚽️ inaendelea kubamba ndani ya DStv. Alhamisi hii ni 🔥🔥 na nyasi zitaomba poo.

Mbwana Samatta kukipiga na Red Devils. Nani kuibuka kidedea?

Tazama mechi hii kupitia DStv Now mahali popote http://bit.ly/GetDStvNow

Piga *150*53# kulipia kifurushi chako cha Compact sh 44,000 tu kushuhudia mtanange huu.

#EPL
#LiveSportsReturns

Tuesday, 7 July 2020

VODACOM YATOA PUNGUZO LA BEI YA SIMU JANJA ZA SMART KITOCHI KWENYE MAONESHO YA 44 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA

Meneja wa maduka ya Rejareja Vodacom Tanzania PlC, Vanessa Mlawi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba kuhusu punguzo la bei kwa simu za Smart Kitochi zinazopatikana kwa shilingi 45,000/- na bidhaa mbalimbali zinazopatikana bandani hapo hivi karibuni.
Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (wa pili kushoto ) pamoja na Msaidizi wa Mipango Vodacom Tanzania Foundation, Kelvin Boya wakiwaelezea wateja kuhusu huduma ya Instant School walipotembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba hivi karibuni.
Mtoa huduma kwa wateja Vodacom, Oliver Nyasa (kulia) akimsikiliza mteja aliyetembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba hivi karibuni.
Mtoa huduma kwa wateja Vodacom, Faraja Mwaseke (kulia) akiwasikiliza wateja waliotembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba hivi karibuni.

Monday, 6 July 2020

DIAMOND TRUST BANK (DTB BANK) FOOTBALL CLUB VISITS NURU ORPHANS CENTRE IN UYOLE, MBEYA

Diamond Trust Bank FC (DTB FC) recently visited Nuru Orphans Centre in Uyole, Mbeya to spend time with the Orphans and also present some essentials for the well-being of the Children at the Centre. The centre is located on the outskirts of Uyole in Mbeya and a home to more than 30 Orphans.

DTB FC was in Mbeya for the Second Division League Final match in Group C against Tukuyu Stars and seized the opportunity for the Corporate Social Responsibility event. The team presented the Centre with Blankets, Rice, Beans and Cooking Oil all worth TShs 3 Million.


Osward Batman Poyo, Project Manager (second right) and Mary Kassim Hamiri (left) the Centre Manager in a group photograph with DTB FC players, Diamond Trust Bank Mbeya Staff Team and Children from Nuru Orphans Centre.

DStv INAKUSOGEZEA BURUDANI ZA MICHEZO POPOTE ULIPO



Burudani za michezo ⚽⚽⚽ zinaendelea kupitia king'amuzi chako pendwa cha DStv.

Sasa tumekusogezea burudani zetu popote ulipo, kiganjani mwako kupitia DStv NOW🔥🔥🔥

TELCOS HAVE REVOLUTIONIZED TANZANIAN'S ACCESS TO THE INTERNET

In recent years, the world has witnessed a growth in technology, particularly when it comes to mobile internet.

In many ways, it can be argued that mobile internet has become an indispensable force which has had several significant benefits.

In the world of business, for example, mobile internet has enabled people to work collaboratively and creatively, even when colleagues are separated from one another.

Similarly, mobile internet has created a way of staying connected to friends and family. Many of us now keep in touch with loved ones via our mobile or computer screen in ways that were simply not as easy, even a few years ago.

It is little surprise, therefore, that in a number of countries people are now spending more time online than ever before.

Tanzania is, of course, no exception. Between 2013 and 2019 internet penetration across the country doubled, reaching 46 per cent in 2019.

Part of this growth can be attributed to the country’s telecom operators, such as Tigo Tanzania.

UK GOVERNMENT CONSORTIUM LED BY BHARTI ENTERPRISES WINS BID FOR ONEWEB

Sunil Bharti Mittal, Chairman Bharti Enterprises.
  • OneWeb to provide high speed, low latency wireless broadband connectivity to billions in rural areas across the globe
  • Offers strategic opportunities across a wide range of other applications and working with a broad range of international partners
Friday, July 3, 2020, New Delhi / London: Bharti Enterprises (“Bharti”), one of India’s leading business groups, today announced that a UK Government consortium led by Bharti has won the bid for OneWeb. The deal will enable OneWeb to complete the construction of a global satellite constellation that will provide enhanced broadband and other services to mobile and fixed terminals in countries around the world. OneWeb was formed with a mission to offer high speed, low latency wireless broadband access to billions of people across the globe, especially in rural areas through a constellation of satellites in low earth orbit. Bharti was one of the founding members of OneWeb and had a strategic stake in the company.

Commenting on the development, Sunil Bharti Mittal, Chairman Bharti Enterprises said: “I am delighted that Bharti will be leading the effort to deliver the promise of universal broadband connectivity through OneWeb, with the active support and participation of the British Government.”

“In addition to the strategic opportunities across a wide range of other applications and working with a broad range of international partners, this business has substantial commercial use cases across the telecoms, enterprise, aviation and maritime sectors. With strong operational execution, we will be able to generate an attractive return for investors, while ensuring that Britain plays a leading role in space and next generation communications.”

DKT. TULIA AIPONGEZA BENKI YA CRDB KUPUNGUZA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE KUTOKA ASILIMIA 24 HADI ASILIMIA 14


Dar Es Salaam Tanzania, Julai 2, 2020 – Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameipongeza Benki ya CRDB kwa kupunguza riba kwa mikopo ya wanawake wajasiriamali inayopatikana kupitia huduma ya “CRDB Malkia” hadi kufikia asilimia 14 kwa mwaka. Akitoa hotuba yake katika hafla ya uzinduzi wa “CRDB Malkia” iliyokuwa na kauli mbiu ya “Fanikisha Zaidi na CRDB Malkia”, Dkt. Tulia alisema hatua ya Benki ya CRDB kupunguza riba kwa asilimia 10 kutoka asilimia 24 iliyokuwa ikitozwa mwanzo itasaidia wanawake wengi zaidi kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo.

“Kupungua kwa riba ina maana inapunguza mzigo mkubwa wa marejesho kwa wanawake na kuwafanya kuwa na fedha nyingi kwa ajili ya uwekezaji katika biashara zao na hivyo kupelekea kufanikisha zaidi,” alisema Dkt. Tulia.

Dkt. Tulia alisema pamoja na tafiti kuonyesha wanawake wamekuwa na ushiriki mkubwa katika shughuli za uchumi nchini, kwa asilimia 54, ni asilimia 60% tu ya wanawake ndio wenye kufikiwa na huduma rasmi za kifedha.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akihutubia katika uzinduzi wa huduma ya CRDB Malkia ya Benki ya CRDB inayolenga katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini. Katika uzinduzi huo Benki ya CRDB imetangaza kupunguza riba ya mikopo kwa wajasiriamali kutoka asilimia 24 hadi asilimia 14, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt, jijini Dar es salaam.
“Niwapongeze pia kwa kuboresha masharti ya dhamana ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kuweza mikopo,” aliongezea Dkt. Tulia huku akiwataka wanawake pia wajitokeze kwa wingi kufungua akaunti ya Malkia itakayosaidia kufanikisha malengo yao kwa kujiwekea akiba kidogokidogo jambo litakalosaidia kujenga imani kwa taasisi za fedha. “Mimi ni mmoja wa wanawake waliofungua akaunti ya Malkia wakati ikianzishwa mwaka 2009, nimefurahi kuona leo hii Benki yetu ya CRDB ikifanya maboresho yatakayoweza kumkomboa mwanamke,” aliongezea Dkt. Tulia.

Dkt. Tulia alisema jitihada hizi zinazofanywa na Benki ya CRDB katika uwezeshaji wa makundi mbalimbali ya wananchi zimekuwa na msaada mkubwa katika kuisaidia Tanzania kufikia lengo la kuwa nchi yenye uchumi wa kati.

“Nimefurahi kuona leo hii tukiwa tunajivunia kuwa nchi ya uchumi wa kati, Benki yetu ya CRDB inaendelea kutubeba wanawake na kuwezesha kufikia malengo yetu ya nchi na dunia katika kuwa na usawa katika ushiriki katika shughuli za Maendeleo kama ilivyoainishwa katika mpango wa Maendeleo Endelevu 2030 wa umoja wa mataifa,” alisema Dkt. Tulia

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akihutubia katika uzinduzi wa huduma ya CRDB Malkia ya Benki ya CRDB inayolenga katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini. Katika uzinduzi huo Benki ya CRDB imetangaza kupunguza riba ya mikopo kwa wajasiriamali kutoka asilimia 24 hadi asilimia 14.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema huduma ya CRDB Malkia imelenga katika kumtambua, kumpa nafasi na kumuwezesha mwanamke wa Kitanzania kufikia malengo yake kupitia mikopo ya biashara na ujasiriamali, kujiwekea akiba kwa akaunti ya Malkia na mafunzo ya uendeshaji biashara.

“Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, Benki yetu tayari ilikuwa imekwisha toa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 600 kwa wanawake zaidi ya elfu 55,” alisema Nsekela huku akibainisha kuwa zaidi ya wanawake 30,000 tayari wameshajiunga na akaunti ya Malkia.

Nsekela alisema pamoja na mafanikio ambayo Benki ya CRDB imeyapata katika kumuwezesha mwanamke, bado idadi ndogo ya wanawake wamekuwa wakijitokeza kupata huduma kutokana na changamoto ya riba, masharti magumu ya dhamana na kukosa uelewa wa huduma za kifedha. “Tukiwa Benki ya kizalendo inayothamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa letu, tukasema ni vyema tukatafuta suluhisho la changamoto hizi ili kuweza kumsaidia mwanamke kufankisha malengo yake zaidi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akifafanua jambo katika uzinduzi wa huduma ya CRDB Malkia ya Benki ya CRDB inayolenga katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini. Katika uzinduzi huo Benki ya CRDB imetangaza kupunguza riba ya mikopo kwa wajasiriamali kutoka asilimia 24 hadi asilimia 14.
Nsekela alisema wanawake sasa hivi wataweza kupata mikopo kwa riba ndogo ya asilimia 14 kulinganisha na asilimia 24 iliyokuwa ikitozwa mwanzo huku masharti ya upatikanaji wa mikopo yakirahisishwa kwa kiasi kikubwa. “Kupungua kwa riba kuna maana wanawake sasa wanaweza kukopa zaidi na kwa gharama nafuu kulinganisha na mwanzo hivyo kusaidia kufanikisha malengo yao kwa uharaka zaidi,” alisema Nsekela.

Nsekela alisema katika kuhakikisha wanawake wanapata elimu na usaidizi wa kutosha katika huduma ya CRDB Malkia, Benki ya CRDB imeweka wataalamu wa uwezeshaji wanawake wajulikanao kama “Malkia Rafiki” katika mtandao wa matawi yake yote nchi nzima.

Akihitimisha kongamano hilo, Nsekela alisema kuwa kupitia kauli mbiu ya “Fanikisha Zaidi na CRDB Malkia”, Benki ya CRDB imejipanga vilivyo kushiriki katika safari ya mafanikio ya wanawake wote wa Tanzania na kuwaomba wanawake wajitokeze kwa wingi katika matawi ya Benki ya CRDB ili kuanza kufurahia huduma hiyo mpya ya CRDB Malkia. “Ukifika tawini ulizia Malkia Rafiki naye atakusaidia kuanza safari yako ya mafanikio,” alihitimisha Nsekela.


Kwa mwaka huu hii ni mara ya pili kwa Benki ya CRDB kufanya maboresho katika huduma zake hususani upande wa mikopo, ambapo mwanzoni mwa mwezi Juni, Benki ilizindua kampeni ya mikopo ya wafanyakazi iitwayo “Jiachie Utakavyo” ambapo mteja anapewa uhuru wa kuchagua riba atakayo na muda wa kulipa atakao. Maboresho haya yanakuja wakati muafaka ikiwa wafanyabiashara wengi wakipambana kurudi katika hali ya kawaida baada ya kuathirika na janga la COVID-19.