Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_170926_270926

Absa Banner_170926_270926

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Tuesday, 12 September 2023

FURSA ZA IMBEJU WAJASIRIAMALI WANAWAKE NA VIJANA


Dar es Salaam. Tarehe 11 Septemba 2023: Akizindua Maonesho ya Imbeju ya Wajasiriamali Ilala 2023, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima amewahimiza wafanyabiashara wadogo nchini hasa wanawake na vijana kuchangamkia fursa ya mafunzo, ushauri, na mitaji wezeshi inayotolewa na CRDB Bank Foundation kupitia program ya IMBEJU.

Waziri Gwajima amesema wanawake na vijana ndio injini ya uchumi wa taifa kwani ni kundi lenye uwezo mkubwa wa kuchangia mafanikio ya kijamii na kiuchumi. Hata ripoti ya Sensa na Makazi ya mwaka 2022, amesema inadhihirisha hilo ikibainisha kuwa asilimia 51 ya watu wote nchini ni wanawake na asilimia 75 ni vijana hivyo makundi haya mawili kuwa sehemu muhimu ya nguvukazi ya taifa.


“Hata hivyo, wanawake na vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwamo mila na desturi kandamizi, elimu duni, ukosefu wa mitaji na stadi za ujasiriamali. Serikali imechukua hatua mbalimbali zinazolenga kujenga uchumi jumuishi na shirikishi ili kuwakomboa kiuchumi, ni wakati sasa wa kila mjasiriamali mdogo kuzitumia fursa zinazotolewa na CRDB Bank Foundation na Benki ya CRDB kwani mkizitumia vizuri, itakuwa rahisi kukabiliana na changamoto hizi na kukuza biashara zenu,” amesema Waziri Gwajima.

Vilevile, Waziri amesema Serikali inafanya kazi usiku na mchana kuwawezesha wanawake kiuchumi hivyo inaendelea kutekeleza mkakati wa kutimiza malengo ya Jukwaa la Kimataifa ya Kukuza usawa wa Kijinsia hususan katika Haki na Usawa wa Kiuchumi.

Uwezeshaji wa wanawake na vijana, amesema ni suala linalotiliwa mkazo katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2050, na Sera ya Maendeleo na Jinsia ya Mwaka 2000.


Maonesho hayo ya wajasiriamali yanayofanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Septemba 11 mpaka 13 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yameandaliwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Wilaya ya Ilala yakiwakusanya zaidi ya wajasiriamali 3,000 wa halmashauri hiyo, Jiji la Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema benki inathamini shughuli za kijasiriamali kwa kutambua kuwa zimekuwa msaada mkubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa.


“Tunaamini ili sekta hii itoe mchango wake kikamilifu katika kukuza uchumi wa Taifa, kunahitajika huduma na mifumo shirikishi itakayowawezesha wajasiriamali kutimiza malengo yao. Imani hii ndio iliyoishawishi Benki yetu ya CRDB kuanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja wa kundi hili tangu mwaka 2005,” amesema Nsekela.

DStv WAZIDI KUNOGESHA BURUDANI NDANI YA BOMBA!


DStv wazidi kunogesha burudani!

Sasa unaweza kufurahia tamthilia za kihindi, kituruki na nyingine nyingi ndani ya chaneli ya Mambo Moto ambayo @dstvtanzania wameishusha kutoka kifurushi cha Shangwe mpaka kifurushi cha Bomba cha 24,000/= tu.

Pata ladha ya tamthilia uzipendazo zilizotafsiriwa kwa Kiswahili kupitia Chaneli ya Mambo Moto 140 inayopatikana ndani ya DStv pekee!

Piga *150*53# kulipia kwa urahisi zaidi kifurushi chako.

#UtamuNiBomba
#Unakosaje

NMB BENKI YA TATU KWA FAIDA AFRIKA MASHARIKI

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna.
Benki ya NMB imeshika nafasi ya tatu kwa ukubwa wa faida katika ukanda wa Afrika Mashariki, hii ni kutokana na mafanikio yake kiutendaji hasa ufanisi katika uendeshaji na utoaji wa huduma bora za kibenki nchini.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu benki hiyo imeweza kutengeneza faida baada ya kodi ya Shilingi Bilioni 262 ikiwa ni ongezeko la asilimia 27 ukilinganisha na nusu ya kwanza ya mwaka 2022.

Kutokana na kutengeneza kiasi hicho cha faida, NMB imeweza kushika nafasi ya tatu kwa ukubwa wa faida kati ya mabenki yote ndani ya ukanda huu wa Afrika Mashariki, ikitanguliwa na Benki ya Equity pamoja na Benki ya KCB zote kutoka nchini Kenya ambazo zimepata faida ya TZS bilioni 430 na TZS bilion 264 mtawalia. NMB imepanda kutoka nafasi ya 10 mwaka 2018 hadi kufikia nafasi ya tatu sasa.

Takwimu na uchambuzi wa hivi karibuni wa masoko ya hisa katika ukanda huu unaonyesha kuwa taasisi hiyo kubwa ya fedha nchini yenye mali zenye thamani ya zaidi ya Tsh Trilioni 11 imekua sana kiushindani na kuimarika sokoni katika miaka ya hivi karibuni, huku bei ya hisa zake sokoni ikiongezeka kwa takribani asilimia 28% tangu kutangazwa kwa matokeo yake ya kifedha ya nusu mwaka 2023 hadi kufikia shilingi 4,440 kwa kila hisa Septemba 8 2023.

Kutokana na kufanya vizuri kifedha, mtaji wa Benki ya NMB katika soko la hisa umekua kutoka Tsh 1.38 trilioni mwaka 2018 hadi kufikia mtaji wa kiasi cha Tsh 2.22 trillion Tarehe 8 Septemba 2023, hivyo kuifanya NMB kuwa kampuni ya pili kwa ukubwa katika soko la Tanzania ikitanguliwa na kampuni ya TBL na pia kampuni ya sita kwa ukubwa ndani ya kanda ya Afrika Mashariki, Shelisheli na Mauritus, ikitokea nafasi ya 14 mwaka 2019. Kampuni ya Safaricom Kenya ndiyo inayo ongoza katika ukanda huu ikiwa na mtaji wa zaidi ya shilingi trilioni nne.

Monday, 11 September 2023

EXIM BANK, ZANZIBAR eGOVT. AGENCY SIGN MoU

Exim Bank Chief Finance Officer (CFO), Shani Kinswaga (left) and Zanzibar eGovernment Agency (eGaz) Managing Director, Said Seif Said (right) sign a Memorandum of Understanding (MoU) that seeks to support Zanzibar Digital Government Strategy for 2023-2027.
Exim Bank Chief Finance Officer (CFO), Shani Kinswaga (second left) and Zanzibar eGovernment Agency (eGaz) Managing Director Said Seif Said (center) display copies of a signed Memorandum of Understanding (MoU) that seeks to support Zanzibar Digital Government Strategy for 2023-2027. Looking on from left are Exim Bank Head of Retail Banking, Andrew Lyimo and eGaz Legal Department Head, Haji Saleh (second right).

Exim Bank Tanzania has signed a Memorandum of Understanding (MoU) with the Zanzibar eGovernment Agency (eGaz) geared towards accelerating Zanzibar’s digital transformation journey.

The MoU has been signed after the recent launch of the Zanzibar Digital Government Strategy for 2023-2027 that was graced by Dr. Hussein Ali Mwinyi, President of the Revolutionary Government of Zanzibar.

Speaking before the signing ceremony held in Zanzibar over the weekend, the Exim Bank Chief Finance Officer (CFO) Shani Kinswaga said the signing of the new MoU aligns with Zanzibar’s digital transformation goals laid out in the Isle nation’s Digital Economy Blueprint and Roadmap.

Kinswaga said the bank will leverage technology as a tool to provide an exceptional digital experience by collaborating with eGaz to digitize payments which will ultimately increase Zanzibar Government’s revenues and improve efficiency.

“This new partnership reiterates Exim bank’s commitment to support sustainable economic development in Zanzibar. As a bank, we believe that the MoU signed today will not only significantly contribute to robust economic growth but help to accelerate Zanzibar’s transformation into a strong digital economy,” Kinswaga said.

VODACOM KUPUNGUZA PENGO LA ELIMU YA KIDIGITALI


Kwa mara ya kwanza nchini, wanafunzi wa kike wasiosikia (viziwi) 22 wa shule za sekondari ambao ni sehemu ya wanafunzi wa kike zaidi ya 150 wa shule za sekondari mkoani Arusha wamepatiwa mafunzo ya kutengeneza tovuti na ‘coding’.


Ikijulikana kama ‘Code Like a Girl’, jitihada hizi zinachangia kutengeneza mustakabali endelevu zaidi jumuishi na wa kidigitali barani Afrika huku ikianisha changamoto ya uwakilishi mdogo wa wanawake katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM) kupitia mpangilio wa programu maalaum ya kielimu inayowalenga wasichana wasio na uwezo.


Ikiwa ni programu ilianzishwa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC, Meneja Maendeleo ya Rasilimali Watu wa kampuni hiyo ya mawasiliano na teknolojia, Bw. Naiman Moshi amewaambia waandishi wa Habari mwishoni mwa wiki ambapo mafunzo hayo yamefanyika kuwa programu inalenga kutengeneza na kuleta shauku kuhusu masomo yanayohusiana na sayansi (STEM) kwa wasichana.


Amebainisha kuwa kupitia mpango huu, ambao ulianzishwa mwaka 2018, wanafunzi wa kike wanapatiwa fursa ya kufahamu hatua za awali na msingi za ‘coding’ na njia za kufuata kwa taaluma zinazohusiana na ujuzi wa sasa na ujao huku wakitengeneza vipaji ambavyo vinaainisha mahitaji ya maarifa yanayohitajika sasa na baadae.


“Kama kampuni ya teknolojia na mawasiliano, tumeamua kufanya jitihada hizi kwa lengo la kupunguza pengo lililopo kwenye maarifa ya kidigitali miongoni mwa wanafunzi wa kike,” alielezea Bw. Moshi, wakati akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kumalizika kwa mafunzo yaliyofanyika kwa siku nne katika Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC).

Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) linakadiria kwamba ni 35% pekee ya wanafunzi wote wanaojiunga na masomo yanayohusiana na Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM) ni wanawake.

UBORA WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE NDANI YA DStv


Friday, 8 September 2023

GOVT. DENIES ALLEGATIONS OF GGML BLACKLISTING YOUTH


The government has denied rumors that Geita Gold Mining Limited (GGML) has blacklisted youth whose employment has been terminated for various reasons, as claimed by some individuals.

In its investigation, it has been found that GGML has established a system to keep records of the performance and conduct of its employees, including actions and incidents of violation of rules and regulations committed during their employment.


This was revealed today, September 8, 2023, in the Parliament in Dodoma by the Deputy Minister, Office of the Prime Minister (Labor, Youth, Employment, and Persons with Disabilities), Patrobas Katambi, while responding to a question from the Member of Parliament for Geita Town, Constatine Kanyasu (CCM).
Kanyasu asked whether the government is aware of GGML's practice of blacklisting youth in the country and how many youth are currently blacklisted.

Continuing to respond to the question, Katambi said that in the hiring process, almost all companies and employers follow up on the performance information of job applicants with their previous employers.
"Therefore, GGML provides performance information and conduct of employees who have worked with them when requested to do so. Additionally, despite providing that information, GGML does not prohibit the specific mine from hiring applicants in any way.

TMSA KUTOA TUZO BORA ZA MASOKO 2023

Mkurugenzi wa Chama cha wataalamu wa Masoko Tanzania, Dkt. Emmanuel Chao (PhD) (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akitangaza tuzo za masoko na kongamano la 2023 litakalofanyika tarehe 27 Oktoba kwenye ukumbi wa Blue Saphire jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni mwakilishi na mdhamini kutoka kampuni ya Bramex, Sylvia Joseph. Wa kwanza kulia ni Gloria Malikita kutoka kampuni ya Smartcodes (mdhamini) na wa pili kushoto ni Iche Omari kutoka Smartcodes (mdhamini).

Dar es Salaam, 7 Septemba 2023 - Katika nia ya kuhamasisha weledi zaidi katika sekta ya masoko nchini Tanzania, Chama cha wataalamu wa Masoko Tanzania (TMSA) kinatarajiwa kufungua kongamano la masoko kwa mara ya nne na kutoa tuzo za masoko kwa mara ya tatu mfululizo katika vipengele 20 tofauti kwa mwaka huu.

Tuzo hizi za masoko 2023 zitafanyika tarehe 27 Oktoba jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Blue Saphire pembezoni mwa hoteli ya Ramada. Tukio hili litafunguliwa na kongamano saa tatu asubuhi, na majira ya saa kumi na mbili jioni ugawaji wa tuzo hizo zitafanyika.

Tangu mwaka wa 2021, TMSA imetumia tuzo hizo ili kuakisi juhudi na mafanikio ya watu binafsi, mashirika, na wasomi ambao wanaleta mabadiliko katika nyanja ya masoko.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa TMSA, Dkt. Emmanuel Chao (PhD), alieleza jinsi masoko kuwa nguzo muhimu ili kuhakikisha ukuaji wa kampuni na kuleta faida. Alisema, "Katika biashara yoyote, idara ya masoko ni ya kipekee, kwani inajumuisha kati ya asilimia 30 na 40 ya bajeti ya biashara, na ndio kati ya msingi wa kudumisha biashara yoyote".

EUROPEAN QUALIFIERS IJUMAA HII NDANI YA DStv


Thursday, 7 September 2023

BENKI YA EXIM KUENDELEA KUTOA HUDUMA ZA KIBENKI KWA UFANISI MKUBWA

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim, Shani Kinswaga (kushoto) akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumanne jioni uliongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura. Benki hiyo iliwataka maafisa wakuu wa polisi kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumanne jioni uliongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim, Shani Kinswaga (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Pilisi, ACP Anthony Ruta (wa tatu kushoto) mara baada ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumanne jioni uliongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya Exim Andrew Lyimo.

Benki ya Exim imetangaza kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma za kibenki kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuimarisha ushirikishwaji wa kifedha nchini.

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumanne jioni, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Shani Kinswaga alisema benki hiyo imejizatiti kutekeleza kikamilifu mikakati wake wa kupunguza pengo la watu ambao bado halijafikiwa na benki.

Kinswaga alisema benki yake itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza ukuaji wa sekta ya benki hapa nchini huku akisisitiza malengo ya benki hiyo ya kuinua maisha ya wateja wake kupitia upatikanaji wa huduma za kifedha bila vikwazo, kupitia matumizi ya suluhu za kidijitali na huduma zinazotengenezwa mahususi.

“Tunashukuru sana kwa nafasi hii ya kipekee ya kuonyesha huduma zetu mbalimbali za kibenki kwa Jeshi la Polisi. Kama benki, tutaendelea kuwa mstari wa mbele kusogeza huduma za benki karibu na watu hasa katika ngazi za chini,” Kinswaga.

Wednesday, 6 September 2023

NMB SOLUTIONS TO EMPOWERING LOCAL FARMERS

NMB Bank Chief Executive Officer, Ruth zaipuna (right) speaks at the Africa Food Systems Summit 2023, as one of the presenters in the first session of the conference yesterday, which involved various stakeholders from the food sector within and outside Africa. On the left is the Head of Strategy Alliance and Transition Finance, Rabobank - Ben Valk and Vice-President of Farmer Solutions, OCP Africa - Mehdi Filali.

Smallholder farmers have a critical role to play in ensuring food security in the country which NMB Bank has said is ready to finance and continues to support in partnership with local and international partners.


Speaking yesterday in Dar es Salaam at the ongoing AGRF 2023 Summit, Chief Executive Officer Ruth Zaipuna outlined the bank’s backing of the farmers and the solutions it offers them, noting that financial institutions are obliged to empower them economically.


According to her, digitalization of financial services has greatly helped to surmount barriers hindering the small-scale farming fraternity from accessing formal funding sources and other banking solutions that are crucial in their operations.


“Financial institutions still have a significant role to play in driving economic empowerment of smallholder farmers, majority of whom are subsistence based, with low productivity, and living in extreme poverty,” she noted during the panel discussion on how the private sector can support smallholder farmers to increase food and nutrition security in Africa.


The side event at the Africa Food Systems Forum 2023, whose theme is “Recover, Regenerate, Act: Africa’s Solutions to Food Systems”, was organised by OCP Africa in conjunction with Fertilizer Canada and the World Business Council for Sustainable Development (WBCSD).


Commenting on the role of top lenders like NMB in empowering African peasants economically, Ms Zaipuna said they deserve and require financial support due to their economic relevance and importance in the growth and development of the agricultural sector.


Peasants not only make up 90 per cent of farmers in sub-Saharan Africa (SSA) and produce 80 per cent of the continent’s food but also constitute a major chunk of the population in the region.


The NMB leader said access to financial services has been a critical barrier for smallholder farmers in achieving their full economic potential, a challenge the bank has been addressing through innovative digital financial solutions and capacity building programmes as well as awareness campaigns such as Teleza Kidijitali.

“At NMB we firmly believe that for all smallholder farmers in our communities, financial inclusion is a pathway from poverty to prosperity,” Ms Zaipuna told the panel.

MECHI YA KUFUZU AFCON - ALGERIA vs TANZANIA @DStv


WATEJA WA PRECISION AIR KUKATA TIKETI M-PESA APP

  • Ushirikiano huu ambao umepewa nguvu na TripSiri unaendeleza dhamira ya Vodacom ya kuekelea dunia ya kidigitali
Vodacom M-Pesa na Precision Air waemingia ushirikiano ambao utawawezesha wateja kukata tiketi ya ndege kupitia applikesheni ya M-Pesa Super App na kufurahia punguzo la bei mpaka 20% kwa bei ya tiketi ya kawaida. Ushirikiano huo umepewa nguvu na TripSiri, kampuni ya usafiri na teknolojia ya Tanzania ambayo inalenga kurahisisha huduma ya ukataji wa tiketi kupitia M-Pesa Super App.


Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni amesisitiza suhirikiano huu unaonyesha kujizatiti kwao kuifanya M-Pesa kuwa sehemu ya Maisha ya kidigitiali ya kila mtu ikiwezesha manunuzi na malipo ya bidhaa na huduma muhimu zinazotumiwa na Watanzania katika maisha yao ya kila siku zinapatikana kwenye simu zao za mkononi.


“Tunayo furaha kuwakaribisha Precision Air kujiunga na familia ya watoa huduma wanaokaribia 20 katika mtandao wetu mpana wa M-Pesa. Kupitia ushirikiano huu, wateja hawatohitajika tena kutembelea ofisi au tovuti zao kwa ajili ya kukata tiketi za ndege. Tumewarahisishia zoezi hilo na sasa wanaweza kufanya hivyo kwa kupitia aplikesheni ya M-Pesa inayopatikana katika simu zao za mkononi. 


Kwa kuongezea, watanufaika na punguzo la 20% kwa kukata tiketi ikiwa ni faida ya kutumia mtandao wetu. Malengo yetu ni kuwajengea wateja na Watanzania utamaduni wa kufanya malipo na manunuzi yao kwa usalama na uharaka pamoja na kuwarahisishia kutunza kumbukumbu zao za kifedha kwasababu kupitia M-Pesa unaweza kuzipata taarifa zote za manunuzi unayoyafanya,” alielezea Bw. Mbeteni.


M-Pesa imeleta mapinduzi katika manunuzi na malipo ya huduma na bidhaa kutoka kwa mamia ya wafanyabiashara mbalimbali Tanzania kupitia simu za mkononi. Tangu kuanza kuwahudumia Watanzania kwa miaka 15 sasa, imekuwa ni chachu katika maendeleo ya shughuli za kibenki na kifedha na kupunguza pengo kwa watu ambao bado hawajaunganishwa na mifumo hiyo.

Bw. Mbeteni aliongezea kuwa, “mbali na kuwezesha malipo, pia tunalenga kuwarahisishia wafanyabiashara shughuli zao kwa kuwaleta karibu zaidi na wateja. Jukwaa la M-Pesa limekuwa kama soko ambalo mteja akiingia ana uwezo wa kuchagua mahitaji yake ya siku, akalipia, akatoka na kuendelea na shughuli zake zingine. 

Tuesday, 5 September 2023

BETPAWA, POLISI WATOA MAFUNZO KWA BODABODA DAR

Meneja Masoko wa kampuni ya betPawa Tanzania, Borah Ndanyungu (kushoto) pamoja na SP Deus Sokoni, Mkuu wa Dawati la Elimu, Kitengo cha Usalama Barabarani kutoka Jeshi la Polisi, wakimkabidhi Boniface Matale mmoja kati ya madereva bodaboda 250 aliyeshiriki katika mafunzo ya usalama barabarani kwa mkoa wa Dar es Salaam cheti cha ushiriki. Mafunzo hayo yalidhaminiwa na betPawa kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani. Anayeshudia kulia ni Koplo Rashid Msuya kutoka dawati la elimu jeshi la Polisi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya kubashiri michezo ya betPawa Tanzania, Borah Ndanyungu akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usalama barabarani kwa bodaboda 250 wa mkoa wa Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na betPawa kwa kushirikiana na Polisi, kitengo cha usalama barabarani na yamefanyika mwishoni mwa wiki.
Sajenti Asha Abdul kutoka makao makuu ya Polisi akiongea wakati wa kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa bodaboda 250 wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Mafunzo hayo yalidhaminiwa na kampuni ya betPawa kwa kushirikiana na jeshi la Polisi, kitengo cha usalama barabarani.
Meneja Masoko wa kampuni ya betPawa Tanzania Borah Ndanyungu (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka Jeshi la Polisi, kitengo cha Usalama barabarani pamoja na baadhi ya madereva bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam muda mfupi baada ya kutuoa mafunzo na vifaa vya usalama barabarani kama kofia ngumu na makoti akisi mwanga (reflectors). Mafunzo hayo yaliyofayika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wili yalidhaminiwa na kampuni ya betPawa kwa kushirikiana n a jeshi la Polisi na jumla ya madereva boda boda 250 walinufaika.

Zaidi ya waendesha bodaboda 250 mkoani Dar es Salaam wamenufaika na mafunzo ya usalama barabarani yalioandaliwa na kutolewa na Kampuni ya betPawa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kitengo cha usalama barabarani.

Mafunzo hayo yanayojulikana kama ‘betPawa na elimu ya Usalama Barabarani’ yanalenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kupiga vita ajali za barabarani zinazoweza kuepukika na ambazo husababisha majeraha na vifo haswa kwa waendesha bodaboda ambao wamekuwa ni moja kati ya kundi linaloathirika sana.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja masoko wa betPawa Tanzania, Borah Ndanyungu alisema takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa bodaboda ni kundi ambalo limekuwa likichangia sana katika ajali za barabarani huku akitaja uelewa mdogo wa sheria za usalama barabarani kuwa moja ya chanzo kikuu cha ajali hizo.

VODACOM YATAMBULISHA eSIM, KADI YA KIELEKTRONIKI


Kampuni ya teknolojia na mawasiliano inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania PLC imewataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kuwa sasa wanaweza kuhamia kwenye kadi za kielektroniki yaani eSIM zinazopatikana kwenye mtandao supa wa Vodacom. Laini hii ambayo inafanya kazi sawa na kadi za sasa ni rafiki kwa mazingira kwani huunganishwa moja kwa moja kielektroniki kwenye vifaa vinavyokubali matumizi yake, hivyo havitegemei kuzalishwa kwa kutumia plastiki.


Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho huo, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Vodacom Tanzania, Bi. Linda Riwa amebainisha kuwa kuletwa kwa kadi hizi mpya kunaenda sambamba na ari ya kampuni hiyo, ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ulimwenguni, kukidhi mahitaji ya wateja wake na kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira.


“Kuongezeka kwa matumizi ya simujanja kunapelekea uhitaji wa teknolojia zilizoendelea zaidi na ndio maana leo tunatambulisha kwenu huduma hii. Najua wengi wenu mtakuwa mnajiuliza kwanini mbadilishe kadi mlizonazo endapo eSIM tunayoitambulisha leo inafanya kazi sawa na kadi za sasa. Jibu ni rahisi, eSIM inakuwezesha kuwa na namba zaidi ya moja kwenye simu yako hivyo utaweza kubadilisha mitandao pasipo kuhitajika kutoa kadi ya simu. Vile vile, kwa kuwa eSIM inaunganishwa moja kwa moja kwenye simu yako basi si rahisi kupotea au kuharibika na ni chaguo lilio rafiki kwa mazingira,” alielezea Bi. Riwa.


Mkurugenzi huyo wa Biashara aliongeza kuwa mteja yeyote wa Vodacom mwenye simujanja yenye uwezo wa kutumia eSIM anaweza kutembelea maduka ya Vodacom ili kubadilishiwa laini yake.


“Kuna njia mbili za kutambua kama simu yako ina uwezo wa kutumia eSIM; ya kwanza ni kwa mteja kupiga namba *#06# na kisha utaona namba nyingi zenye lebo za IMEI, ICCID na EID. EID ni kitambulisho kuwa simu ina uwezo wa matumizi ya eSIM. Njia ya pili ni kupitia menu ya simu kwenye Settings ambapo kwa watumiaji wa Android wataipata kwa kwenda kwenye Settings > Connections > SIM Manager > hapa itaonyesha eSIM. Kwa upande wa watumiaji wa iPhone, wataenda kwenye Settings > Mobile Data > Hapa itaonyeha Add eSIM” alimalizia Bi. Riwa.

EUROPEAN QUALIFIERS NDANI YA DStv WIKI HII