Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 5 September 2023

BETPAWA, POLISI WATOA MAFUNZO KWA BODABODA DAR

Meneja Masoko wa kampuni ya betPawa Tanzania, Borah Ndanyungu (kushoto) pamoja na SP Deus Sokoni, Mkuu wa Dawati la Elimu, Kitengo cha Usalama Barabarani kutoka Jeshi la Polisi, wakimkabidhi Boniface Matale mmoja kati ya madereva bodaboda 250 aliyeshiriki katika mafunzo ya usalama barabarani kwa mkoa wa Dar es Salaam cheti cha ushiriki. Mafunzo hayo yalidhaminiwa na betPawa kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani. Anayeshudia kulia ni Koplo Rashid Msuya kutoka dawati la elimu jeshi la Polisi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya kubashiri michezo ya betPawa Tanzania, Borah Ndanyungu akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usalama barabarani kwa bodaboda 250 wa mkoa wa Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na betPawa kwa kushirikiana na Polisi, kitengo cha usalama barabarani na yamefanyika mwishoni mwa wiki.
Sajenti Asha Abdul kutoka makao makuu ya Polisi akiongea wakati wa kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa bodaboda 250 wa mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Mafunzo hayo yalidhaminiwa na kampuni ya betPawa kwa kushirikiana na jeshi la Polisi, kitengo cha usalama barabarani.
Meneja Masoko wa kampuni ya betPawa Tanzania Borah Ndanyungu (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka Jeshi la Polisi, kitengo cha Usalama barabarani pamoja na baadhi ya madereva bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam muda mfupi baada ya kutuoa mafunzo na vifaa vya usalama barabarani kama kofia ngumu na makoti akisi mwanga (reflectors). Mafunzo hayo yaliyofayika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wili yalidhaminiwa na kampuni ya betPawa kwa kushirikiana n a jeshi la Polisi na jumla ya madereva boda boda 250 walinufaika.

Zaidi ya waendesha bodaboda 250 mkoani Dar es Salaam wamenufaika na mafunzo ya usalama barabarani yalioandaliwa na kutolewa na Kampuni ya betPawa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kitengo cha usalama barabarani.

Mafunzo hayo yanayojulikana kama ‘betPawa na elimu ya Usalama Barabarani’ yanalenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kupiga vita ajali za barabarani zinazoweza kuepukika na ambazo husababisha majeraha na vifo haswa kwa waendesha bodaboda ambao wamekuwa ni moja kati ya kundi linaloathirika sana.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja masoko wa betPawa Tanzania, Borah Ndanyungu alisema takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa bodaboda ni kundi ambalo limekuwa likichangia sana katika ajali za barabarani huku akitaja uelewa mdogo wa sheria za usalama barabarani kuwa moja ya chanzo kikuu cha ajali hizo.

“Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 16,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani huku ajali za bodaboda zikichukua nafasi kubwa. Kutokana na ukweli huu, tumeona kuna haja ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kundi hili ambalo limekuwa ni muhanga wa ajali za barabarani,” alisema.

Mwakilishi wa waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam Boniface Mtale alisema ajali za bodaboda zimekuwa zikiongezeka kwa kasi na kufafanua kuwa uelewa mdogo wa sheria na kanuni za usalama barabarani zimekuwa ndiyo chanzo kikuu cha ajali hizo.

“Uelewa mdogo wa sheria na kanuni za usalama barabarabi bado ni changamoto kubwa kwa madereva wengi wa bodaboda. Tunawashukuru sana BetPawa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kutambua tatizo hili na kuamua kutupatia elimu hii muhimu sana kwetu,” alisema.

Kwa upande wake SP Deus Sokoni ambaye ni Mkuu wa Dawati la Elimu, Kitengo cha Usalama Barabarani kutoka Jeshi la Polisi, aliipongeza kampuni ya kubashiri michezo ya BetPawa kwa kudhamini mafunzo hayo muhimu.

“Sisi sote kwa pamoja ikiwa ni Pamoja na jeshi la Polisi, madereva, jamii nzima na wadau wote tuna wajibu wa kufanya barabara zetu ziwe salama. Ninayofuraha kuona BetPawa wamekuwa mstari wa mbele na kuamua kufadhili mafunzo haya ambayo yatasaidia sana kundi hili la bodaboda.

Aliongeza, Ajali za barabarani zinsababisha hasara kubwa kwa taifa, familia na jamii kwa ujumla. Hasara hizi ni Pamoja na kupoteza wapendwa wetu ambao wengine tunawategemea, ulemavu wa kudumu pamoja na gharama kubwa za matibabu kwa wahanga wa ajli. Kwa Pamoja tukiungana tunaweza kupunguza sana kama siyo kumaliza kabisa tatizo hili.”

No comments:

Post a Comment