Ikijulikana kama ‘Code Like a Girl’, jitihada hizi zinachangia kutengeneza mustakabali endelevu zaidi jumuishi na wa kidigitali barani Afrika huku ikianisha changamoto ya uwakilishi mdogo wa wanawake katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM) kupitia mpangilio wa programu maalaum ya kielimu inayowalenga wasichana wasio na uwezo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) linakadiria kwamba ni 35% pekee ya wanafunzi wote wanaojiunga na masomo yanayohusiana na Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM) ni wanawake.
Kupunguza pengo la kijinsia lililopo katika sayansi pia ni muhimu kwa mafanikio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Shirika la Umoja wa Mataifa na kufanikisha ajenda ya kufikia mwaka 2030 ya “kutomwacha mtu yoyote nyuma”.
Programu hii, ambayo pia inatekelezwa kwa kushirikiana na Tanzania Data Lab (dlab), imefanikisha kuona zaidi ya wanafunzi wa kike 1900 ambapo wengine ni walemavu wakijiunga na mafunzo haya, kwa dhamira ya kufanikisha dhana ya ujumuishi.
Mratibu wa Programu kutoka dlab, Bi. Somoe Mkwachu, ameelezea kuwa bado kuna jitihada za kimakusudi zinahitajika kufanyika katika kuainisha dhana potofu ya kwamba “masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wavulana” na kusaidia kupunguza pengo la kijinsia lililopo katika masomo ya sayansi.
“Jitihada hizi ni sawa na tone la maji kwenye bahari, inahitajika kuongeza kiwango cha maarifa ya kidigitali ambapo kwa sasa ni suala linalogusa kila Nyanja,” aliongezea.
Mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya sekondari ya Ngarenaro, Dorcas Prima ameelezea kufurahishwa kwake kushiriki katika mafunzo haya, akisema kwamba yatasaidia kuongeza uelewa wake, hususani katika masomo yanayohusiana na sayansi.
Kupitia programu hii, wanafunzi wanajifunza maarifa yanayohusu ‘coding’ na kupata fursa ya kukutana na marafiki wapya pamoja na washauri wa kitaaluma.
No comments:
Post a Comment