Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 25 January 2025

SWAHIBA (CRDB) AWAKUTANISHA MAAFISA WAKUU WA FEDHA NA KUYAJENGA



Benki ya CRDB, ambayo hivi karibuni imepokea tuzo ya Mwajiri Kinara na kutajwa kama moja ya walipakodi waliofanya vizuri kwa mwaka 2023/2024, inaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya taifa kwa kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali ambapo Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, ameongoza jukwaa maalum lililolenga kupeana uzoefu katika masuala ya fedha, pamoja na kusimamia mipango endelevu.



Kwa ukarimu wa kipekee, viongozi wakuu wa Benki ya CRDB akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na Afisa Mkuu Uendeshaji, Bruce Mwile nao pia walishiriki jukwaa hili ambapo walipata nafasi ya kutoa uzoefu wao, kubadilishana mawazo na kujenga mahusiano. Katika jukwaa hili, waalikwa walipitishwa na kujionea mandhari nzuri ya jengo la Makao Makuu ya Benki ya CRDB na wenyeji wao ambao ni viongozi na wafanyakazi wa Benki. 



#crdbbank
#tunakusikiliza

No comments:

Post a Comment