Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Friday, 8 September 2023
TMSA KUTOA TUZO BORA ZA MASOKO 2023
Dar es Salaam, 7 Septemba 2023 - Katika nia ya kuhamasisha weledi zaidi katika sekta ya masoko nchini Tanzania, Chama cha wataalamu wa Masoko Tanzania (TMSA) kinatarajiwa kufungua kongamano la masoko kwa mara ya nne na kutoa tuzo za masoko kwa mara ya tatu mfululizo katika vipengele 20 tofauti kwa mwaka huu.
Tuzo hizi za masoko 2023 zitafanyika tarehe 27 Oktoba jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Blue Saphire pembezoni mwa hoteli ya Ramada. Tukio hili litafunguliwa na kongamano saa tatu asubuhi, na majira ya saa kumi na mbili jioni ugawaji wa tuzo hizo zitafanyika.
Tangu mwaka wa 2021, TMSA imetumia tuzo hizo ili kuakisi juhudi na mafanikio ya watu binafsi, mashirika, na wasomi ambao wanaleta mabadiliko katika nyanja ya masoko.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa TMSA, Dkt. Emmanuel Chao (PhD), alieleza jinsi masoko kuwa nguzo muhimu ili kuhakikisha ukuaji wa kampuni na kuleta faida. Alisema, "Katika biashara yoyote, idara ya masoko ni ya kipekee, kwani inajumuisha kati ya asilimia 30 na 40 ya bajeti ya biashara, na ndio kati ya msingi wa kudumisha biashara yoyote".
Aliendelea, ‘kwahiyo, kama TMSA, tutatumia fursa hii kuhimiza makampuni na watendaji kuwa na weledi zaidi katika hii idara. Na kwa bahati nzuri, katika TMSA, tayari tunatoa programu za masoko. Pia tuko kwenye mazungumzo na Taasisi ya Chartered Marketing Institute ya nchini Uingereza UK kushirikiana kwenye uandaaji wa programu mbalimbali za masoko. Nia yetu ni kuhakikisha soko la ndani linafaidika zaidi kwa kuzalisha wataalamu waliohitimu na wenye uelewa zaidi wa soko la Afrika kuliko soko la nje’’.
‘Aidha, tungependa kuwashukuru wadhamini wetu ambao wametoa usaidizi muhimu katika kufanikisha tukio hili. Hizi ni: Smart Codes, Hessa Africa, Imperial Marketing and Communication, Bremex Marketing and Communication, Integrated Marketing Communication, Kango, 360, Attwood Marketing and Communication na nyinginezo’.
Mmoja wa wadhamini wakuu kutoka kampuni ya SmartCodes, Iche Omari ambae aliiwakilisha kampuni hio alisema kuwa tuzo hizo zitakuwa chachu katika kuchochea ukuaji wa sekta ya masoko. Alinukuliwa, "Tuko pamoja na TMSA katika utoaji wa tuzo za TMSA, na tuna matumaini yetu ni kuwa huu ni mwelekeo sahihi wa kuhamasisha ubunifu na weledi miongoni mwa wafanyabiashara wa Tanzania’.
Mchakato wa kuchagua na kuteua washindi wa tuzo uliendeshwa mtandaoni kupitia tovuti ya www.tma.tmsa.or.tz/nomination, ambapo watu binafsi na mashirika yaliteuliwa. Baada ya mchakato wa uteuzi huo, timu ya majaji wenye uzoefu ilipitia uteuzi uliopendekezwa na washindi waliochaguliwa.
About TMSA
Tanzania marketing science association is driven by an informed community of experts from both the industry and academic. We provide variety of solutions and services. Services include professional training programs ranging from certified to professional marketers. The trainings are also designed to suit specific organizational needs. With a dedicated professional team, the association is generating a big force in creating next generation of marketers in Tanzania and beyond.
Tanzania Marketing Excellence Awards 2022 identify and celebrate outstanding marketing by organizations, teams and individuals.
These awards recognize that high standards of quality and integrity are vital to the success of marketing, as well as rewarding the innovation delivered by marketers who are at the cutting-edge of their profession. Any organization within Tanzania, regardless of size, sector or industry, as well as individuals, teams and agencies can enter these awards.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment