Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Wednesday, 7 December 2022

YAPI MERKEZI JOINS BUSINESS LEADERS ON TPSF AWARDS

Yapi Merkezi Vice Chairman, Erdem Arioglu speaking at the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) Awards and thought leadership session, part of the event held in Dar es Salaam last Friday. The event was attended by business leaders from across different sectors and industries.
Yapi Merkezi Vice Chairman, Erdem Arioglu listening attentively during the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) Awards and thought leadership session, part of the event held in Dar es Salaam last Friday. The event was attended by business leaders from across different sectors and industries.
A panel of speakers made of business leaders engaging during the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) Awards and thought leadership session, part of the event held in Dar es Salaam, last Friday. The event was attended by business leaders from across different sectors and industries.
Yapi Merkezi Vice Chairman, Erdem Arioglu engaging with the audience attending the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) Awards and thought leadership session, part of the event held in Dar es Salaam last Friday. The event was attended by business leaders from across different sectors and industries.

KAMPUNI YA KILOMBERO YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA ATE 2022

Dar es salaam - Kampuni ya Sukari ya Kilombero imefanikiwa kunyakua tuzo katika kipengele cha cha Uanagenzi na Mafunzo (Apprenticeship and Internship) huku ikishika nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) na kupokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla hiyo wakati wa tuzo za zitolewazo na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika Disemba 2, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdory Mpango (kulia) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Cleopatra Nasari, Mkuu wa Rasilimaliwatu Idara ya Kilimo wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero (katikati) kwa kudhamini hafla ya Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Desemba 2, 2022. Kushoto ni Mhe. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.
Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Joyce Ndalichako (kulis) akimkabidhi tuzo Meneja wa Maghala wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero (kushoto), Anthony Rweyemamu baada ya Kampuni kushinda nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City tarehe 2 Desemba 2022 ambapo kampuni hiyo ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa hafla hiyo.
Anthony Rweyemamu, Meneja wa Maghala wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero akipokea tuzo ya mshindi wa katika kipengele cha Uanagenzi na Mafunzo katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika tarehe 2 Desemba 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City ambapo kampuni hiyo pia ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kilombero Sugar Company Limited wakiwa katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika Desemba 2, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City. Kampuni hiyo ilitajwa kuwa mshindi wa kipengele cha Uanagenzi na Mafunzo, na Mshindi wa pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) na kupokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Masuala ya Biashara - Bruno Daniel, Mkuu wa Rasilimaliwatu Idara ya Kilimo - Cleopatra Nasari, Meneja wa Maghala Dar es Salaam/Morogoro - Anthony Rweyemamu na Mtafiti wa Masoko Lenin Rugaimukamu.

POWER LEARN PROJECT EMPOWERING YOUTHS IN TANZANIA THROUGH A FULLY FUNDED SCHOLARSHIP FOR SOFTWARE DEVELOPMENT

Pictured from left; Kaori Mitsuma - PLP Partner Emurgo Africa, Neria Rutashobya - Secretary Ministry of Loans DARUSO, Daud Balele - Minister of Science, Tech and Innovation DARUSO, George Ndekwa - Finance Manager, Adanian Labs Tanzania, Bernadette Massawe - Vice President DARUSO, Minja Spencer - President of DARUSO, Mumbi Ndung’u - Chief Growth Officer PLP, Paul Siniga - PLP Tanzania Ambassador, Baraka Malele - Secretary Ministry of Science, Tech and Innovation.

Power Learn Project launches in Tanzania, setting its sights on training 300,000 youths from Tanzania in its quest to train 1 Million Software developers across Africa by 2027 

Dar es Salaam, 3 December 2022 - Innovation for a resilient and inclusive digital economy is relevant, timely, and aligns well to ensure innovation is at the heart of achieving industrialization and creating jobs. At the University of Dar es Salaam, Power Learn Project (PLP), in partnership with Adanian Labs Tanzania and the Dar es Salaam University Students Organization, has launched the #1MillionDevs4Africa Program in Tanzania in a bid to train 1 Million software developers across the continent by 2027.

In 2016, the government of Tanzania launched the National ICT Policy 2016, an update to an earlier version adopted in 2003, in recognition of the contribution of the ICT sector to promoting socioeconomic development in the country.

Digital technology can help address a range of socioeconomic challenges in any society. This is particularly true in developing countries where large swathes of the population lack access to essential services, mainly due to insufficient resources and weak infrastructure. In many countries, digital technologies, particularly the internet, now serve as a platform for improving healthcare, education, commerce, information sharing, employment, and innovation. In turn, this generates measurable economic, social and cultural value, from improving productivity and efficiency in critical sectors of the economy to enabling access to life-enhancing services for individuals and communities.

Tuesday, 6 December 2022

MOROCCO VS SPAIN RAUNDI YA 16 BORA NDANI YA DStv


Jumanne hii kwenye michuano ya kombe la dunia, raundi ya 16 bora, Morocco kuvaana na Spain! Unadhani Morocco ataweza kuikomboa Africa?

Piga *150*53# kulipia kifurushi cha Bomba TShs. 23,000 tu ufurahie mechi hii kwa picha ang'avu.

#Hiinikwakilashabiki

SERENGETI BREWERIES WINS ATE'S EMPLOYER OF THE YEAR AWARD ON LOCAL CONTENT

Serengeti Breweries Ltd. (SBL) staff (from left) George Masele, Conrad Msoma - SBL’s Human Resource Director and Chris Gitao - SBL’s Sales Director, display the Employer of the Year award win on Local Content Category. The gala dinner was held at Mlimani City Conference Center recently.
Serengeti Breweries Staff (from left), Emmanuel Kirumbuyo, Edith Nasuwa, Janeth Rumanyika and Anna Mary Laurean, enjoying their recent Employer of the year Award for Local Content Category during the event, held at Mlimani City Conference center recently.
SBL staff in a group photo after winning the Employer of the Year Award for Local Content Category in 2022. The event was organized by Association of Tanzania Employers (ATE) and was held at Mlimani City Conference Center in Dar es Salaam recently.
Serengeti Breweries Limited Human Resources Director, Conrad Msoma displays the Employer of the Year Award to invited guests a gesture of joy during the event held at Mlimani City Conference Center organized by Association of Tanzania Employers (ATE).
Vice President of Tanzania, Dr Philip Mpango (centre), Association of Tanzania Employers (ATE) Board Chair, Joyce Nyimbo (right) and far left is Minister of Labour, Youth, Employment and Persons with Disability, Prof. Joyce Ndalichako follow proceedings during the keynote address at the Association of Employers (ATE) Employer of the year Award gala dinner held at Mlimani City Conference Center in Dar es Salaam recently.
Tanzania Vice President, Dr Philip Mpango hands over the Employer of the Year award for Local Content to SBL’s Human Resource Director, Conrad Msoma. Looking on from left is Minister in the Prime Minister’s Office responsible for Labour, Youth, Employment and the Disabled, Prof. Joyce Ndalichako and Association of Tanzania Employers (ATE) Board Chair, Joyce Nyimbo.

NBC YAMWAGA ZAWADI WASHINDI WA ‘VUNA ZAIDI NA NBC SHAMBANI’ MSIMU WA PILI

Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Claudia Kitta (wa tatu kushoto) akikabidhi zawadi ya pikipiki ya mataili matatu (Guta) kwa mmoja wa wakulima wa zao la korosho Mkoa wa Mtwara, Edwin Jackob Amir kutoka CHAMALI Amcos ambae ni mmoja wa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi mbambali kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika wilayani Masasi mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mariamu Chaurembo (kulia) pamoja na maofisa kutoka benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki hiyo, Msafiri Shayo (wa pili kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Claudia Kitta, Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mariamu Chaurembo pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki ya NBC, Msafiri Shayo wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi mbambali kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika wilayani Masasi mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni viongozi waandamizi wa Chama Kikuu Cha Ushirika wa Wakulima Mtwara-Masasi (MAMCU), viongozi wa chama na serikali pamoja na maofisa kutoka benki hiyo.

Mtwara: Disemba 4, 2022 - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendelea kugawa zawadi kwa washindi mbalimbali wa kampeni yake ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ msimu wa pili inayoendeshwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi zikiwemo baiskeli, pikipiki, guta, pampu za kupulizia dawa, huku serikali ikibainisha kuwa zawadi hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochoea kasi ya uzalishaji wa mazao ya korosho na mazao mengine katika mikoa hiyo.



Hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi wa droo ya pili ya kampeni hiyo ilifanyika wilayani Masasi, Mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki ikipambwa na uwepo wa wakuu wa wilaya ya Masadi Bi Bi Claudia Kitta, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi Bi. Mariamu Chaurembo, viongozi waandamizi wa Chama kikuu Cha Ushirika wa wakulima Mtwara-Masasi ( MAMCU) pamoja na wakulima wa zao la korosho wilayani humo.

Monday, 5 December 2022

NMB YAONGOZA TUZO ZA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (kulia) akimkabidhi Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (katikati), Tuzo ya Mwajiri Bora 2022 baada ya NMB kuibuka mshindi wa jumla katika hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango (wa pili kulia), akimkabidhi Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (wa pili kushoto), Tuzo ya Mwajiri Bora 2022 baada ya NMB kuibuka mshindi wa jumla katika hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako na kulia ni mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa ATE, Jayne Nyimbo.

Benki ya NMB imetangazwa kuwa Mwajiri bora wa mwaka 2022 katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.



Benki hiyo mbali na kushinda Tuzo ya mshindi wa jumla kama Mwajiri Bora wa Mwaka pia ilinyakua tuzo nyingine mbili za Mwajiri mkubwa zaidi na tuzo ya Mwajiri Bora wa Jumla kwenye Sekta Binafsi na kufanya jumla ya tuzo ilizoshinda benki hiyo kufikia 21 hadi sasa mwaka huu.



Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay alisema kutajwa kuwa mwajiri namba moja nchini kunatambua weledi wa benki hiyo katika kufata misingi bora ya utumishi huku ikiwajengea wafanyakazi wao mazingira wezeshi ya kiutendaji.

“Tunafurahi kwamba leo tumetunukiwa tuzo ya Mwajiri Bora wa ujumla baada ya kushinda tuzo nyingi mwaka huu. Maono yetu ni kuwa taasisi inayoongoza katika kusaidia kujenga mustakabali mwema kwa Watanzania wote. Kama sehemu ya mkakati wetu wa biashara, tunawekeza pakubwa katika kujenga utamaduni jumuishi ambapo wafanyakazi wetu wanathaminiwa na kushirikishwa katika mambo yanayohusu biashara na maslahi yao” Akonaay alisema.

BENKI YA EXIM YAENDELEA KUNGÁRA TUZO ZA MWAJIRI BORA, YAIBUKA KINARA MWAJIRI BORA NDANI YA NCHI

Mkuu wa Idara ya Rasirimali Watu wa Benki ya Exim Tanzania, Frederick Kanga (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako baada ya benki hiyo kuibuka kinara kwenye tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 (EYA 2022) kipengele cha Mwajiri bora kutoka ndani ya nchi (First Runner Up Local Employer) zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Hafla ya utoaji wa tuzo hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara wa Rasirimali Watu wa Benki ya Exim Tanzania, Frederick Kanga (katikati) akionyesha tuzo aliyokabidhiwa baada ya benki hiyo kuibuka mshindi kwenye tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 (EYA 2022) kipengele cha usimamizi bora wa utendaji kazini (Perfomance Management) zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Hafla ya utoaji wa tuzo hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara wa Rasimali Watu wa Benki ya Exim Tanzania, Frederick Kanga (wa tatu kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo wakifurahia baada ya kutwaa tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 (EYA 2022) kipengele cha Mwajiri bora kutoka ndani ya nchi (First Runner Up Local Employer) na kipengele cha usimamizi bora wa utendaji kazini (Perfomance Management) zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Dar es Salaam, Disemba 4, 2022 - Benki ya Exim Tanzania imeendelea kutamba kwenye tuzo za mwajiri bora mwaka 2022 (EYA 2022) baada ya kuibuka kinara kwenye kipengele cha Mwajiri bora kutoka ndani ya nchi (First Runner – up Local Employer). Zaidi benki hiyo hiyo ilitangazwa kuwa mshindi kwenye kipengele cha usimamizi bora wa utendaji kazini (Perfomance Management).



Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Phillip Isdor Mpango. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako.



Awali akizungumza kwenye hafla ya tuzo hizo Dk Mpango aliwahimiza waajiri wote kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na nafasi zao huku akibainisha kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha sera na sheria za nchi zinakidhi vigezo vya ajira na waajiriwa.



“Natambua pia juhudi za ATE katika kuhakikisha inasimamia vyema majukumu ya pande zote yaani baina ya mwajiri na mwajiriwa katika sehemu za kazi. Hatutaki malalamiko ya wafanyakazi yafike juu kabisa tunataka waajiri mtoe haki na stahiki za wafanyakazi wenu kwa mujibu wa miongozi iliyopo ” alisema.



Saturday, 3 December 2022

RATIBA YA RAUNDI YA 16 BORA WIKIENDI HII NDANI YA DStv


Ratiba ya Round ya 16 wikiendi hii ndani ya @dstvtanzania pekee!

Tuandikie timu zitakazoibuka na ushindi!

Hakikisha unafurahia mechi hizi kwa picha ang'avu bila kukosa.

Kulipia kifurushi chako piga *150*53#

#HiiNiKwaKilaShabiki

Friday, 2 December 2022

TANGA CEMENT YANYAKUA TUZO ZA NBAA MWAKA WA SITA MFULULIZO

Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Pieter de Jager (kulia), akiwa katikapicha ya pamoja na Maofisa wengine wa kampuni hiyo wakiwa wameshika Tuzo walizoshinda katika hafla ya utoaji tuzo wa Uandaaji na Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), ya mwaka 2021 katika hafla iliyofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamal Kassim Ali akikabidhi tuzo ya Mshindi wa kwanza kipengele cha wazalishaji viwandani katika tuzo za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), ya mwaka 2021 kwa Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Pieter de Jager katika hafla iliyofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Wengine kulia ni Maofisa wa Tanga Cement.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamal Kassim Ali akikabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika tuzo za za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), mwaka 2021 kwa kwa Mkuu wa wa Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela.

Baadhi ya Maofisa kutoka Tanga Cement wakiwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamali Kassim Ali (kushoto), akikabidhi Tuzo kwa Meneja Mauzo kitaifa wa Kampuni ya Tanga Cement, Mhandisi Leslie Masawe wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ambapo Tanga Cement ilishiriki kwenye maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam, Novemba 30, 2022.

Washindi wa jumla wa tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Washindi wa Kwanza wa tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Tanga Cement PLC imeshinda tuzo za NBAA kwa mwaka wa sita mfululizo leo imeshinda Mshindi wa kwanza kipengele cha wazalishaji viwandani katika tuzo za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu (NBAA), ya mwaka 2021 kwa kufuata viwanga stahiki.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAAkilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Tanga Cement imeibuka na mshindi wa kwanza wa jumla katika tuzo za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu (NBAA), mwaka 2021.

Thursday, 1 December 2022

MSHINDI WA PROMOSHENI YA NMB MASTABATA KOTEKOTE AKABIDHIWA PIKIPIKI JIJINI MWANZA

Mshindi wa Kampeni ya MastaBata KoteKote, Bernard Matiku (kulia) akipokea funguo ya pikipiki kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Baraka Ladislaus wakati wa hafla ya kukabidhiwa. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya kadi wa NMB - Philbert Casmir.
Mshindi wa Kampeni ya MastaBata KoteKote, Bernard Matiku (wa pili kushoto) akibonyeza kitufe ili kuwapata washindi wengine wa kampeni hiyo. Wakishuhudia; Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kadi wa NMB - Philbert Casmir, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Baraka Ladislaus(wa tatu kushoto) na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha - Erick Mremi (kulia).

Msimu wa nne wa promosheni ya NMB MastaBata kwa ajili ya kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za kidijitali umezidi kunoga baada ya kundi la kwanza la washindi 51 wa kila mwezi kupatikana katika droo iliyofanyika kwenye tawi la NMB Kenyatta mkoani Mwanza wiki hii, ambapo 49 walijishindia pesa taslimu TZS 1,000,000 kila mmoja na wawili wakishinda pikipiki aina ya Boxer.



Lengo la kampeni hii ya MastaBata KoteKote ni kuhamasisha matumizi ya kadi ya NMB Mastercard na Lipa Mkononi (Mastercard QR) kwa wateja wetu wanapofanya malipo kwenye manunuzi yao.

Mkazi wa Bunda jijini Mara, Bernard Lucas Matiku alisema 'Asante sana Benki yangu ya NMB kwa kunizawadia pikipiki, nimeanza vizuri msimu huu wa sikukuu maana sasa sina wasiwasi kuendesha mishe zangu' baada ya kukabidhiwa pikipiki aliyoshinda katika promotion ya NMB MastaBata KoteKote.



Zoezi hilo lililosimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania limepelekea idadi ya washindi wa kampeni ya NMB MastaBata KoteKote kufikia 225 hadi sasa. Zawadi walizoshinda wateja hao kwa siku hii zina thamani ya zaidi ya TZS milioni 55 huku shindano zima likiwa na thamani ya zaidi ya TZS milioni 300.

BENKI YA EXIM YANG’ARA TUZO ZA NBAA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania - Jaffari Matundu (kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya benki hiyo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar - Jamal Kassim baada ya benki hiyo kuwa miongoni mwa benki tatu bora katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA). Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti Bodi ya NBAA - CPA Prof. Sylivia Shayo (kushoto). Tuzo hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mwakilishi kutoka Benki ya Exim Tanzania - Frim Paul (kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya benki hiyo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar - Jamal Kassim ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha maandalizi ya tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2010 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA - CPA Pius Maneno. Tuzo hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Viongozi waandamizi wa Benki ya Exim Tanzania wakiongozwa na Jaffari Matundu (katikati) wakionesha tuzo walizopata kwenye hafla ya tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2010 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).



Muonekano wa tuzo umahiri ambazo benki ya Exim Tanzania ilifanikiwa kuzitwaa kwa wakati wa hafla ya tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2010 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Washindi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

HATS OFF AS GEITA GOLD MINING LTD CONTINUES WITH KILI CHALLENGE AGAINST AIDS

Some participants of the Geita Gold Mining Ltd Kili Challenge 2022 campaign who climbed Mountain Kilimanjaro with the aim of raising funds for the fight against HIV. This year a total of TSh 1.1 billion was collected by GGML through various stakeholders.

As the World AIDS Day is celebrated today, Geita Gold Mining Limited (GGML) in Tanzania has vowed to continue with the fight against HIV/AIDS through its Kili Challenge Campaign initiave.

With support and collaboration from stakeholders, the campaign has made great strides and impact since its inception in 2002 to the extent of becoming an international fund.

Making the revelation in Lindi, Dr. Kiva Mvungi, Senior Manager (Health Safety, Environment and Training) at Geita Gold Mining Limited said the campaign launched 20 years ago was aimed at raising awareness and funds to fight HIV/AIDS in Tanzania.

He remarked, "The Kili Challenge has evolved into an international fund involving Kilimanjaro climbers and cyclists from all seven continents and more than twenty countries." We are glad that this accomplishment allows us to make this fund sustainable so that the government's goals against this epidemic can be met."

Dr. Mvungi elaborated by stating that this year, GGML, in collaboration with the Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS), through the Kili Challenge campaign, was able to raise more than 1.1 billion Tanzanian Shillings (TZS) to be used in the fight against the pandemic.

WADAU KUWEZESHA WANAWAKE KUJIKWAMUA BAADA YA JANGA LA UVIKO-19

Katika picha, kutoka kushoto ni Aziza Ibrahim mwakilishi kutoka Hekima Consultants, katikati ni Marion Elias - Mkurugenzi katika kampuni ya Ekima Consultants na anayefuatia upande wa kulia ni Ernestina Mwenda - Mkurugenzi wa kampuni ya Active Mama wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 30 Novemba 2022 jijini Dar es Salaam kuzungumzia tamasha la Mama’s Day Out linalotarajia kufanyika 9 Disemba 2022 lenye kauli mbiu ya “Anza Upya” likiwa na lengo la kumwezesha mwanamke kujikwamua na changamoto mbali mbali za kiuchumi na kijamii.

30 Novemba 2022, Dar es Salaam - Wakati dunia ikiadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani, kampuni ya Ekima Consultants na wadau wa maendeleo wameandaa tamasha la wanawake lenye lengo la kuwawezesha, na kuwahamasisha wanawake kujikwamua na changamoto baada ya janga la Uviko-19.

Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya ‘Anza Upya’ linalotarajiwa kufanyika tarehe 9 Desemba jijini Dar es Salaam lina lengo la kukuza uwezo wao katika kuchangia maendeleo endelevu. Mada zitakazotolewa kwenye tamasha hilo zitaangazia afya ya akili, ustawi, uwezeshaji wa kifedha na kiuchumi, kujijali, na afya ya wanawake; ambazo zitatolewa na wataalamu kutoka sekta ya afya, taasisi za kifedha, mashirika na makampuni binafsi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, muandaaji wa tamasha hilo, Mkurugenzi wa EKIMA Consultants Marion Elias alisema kuwa tamasha linawalenga wanawake walioajiriwa na waliojiajiri wenye umri kuanzia miaka 25 hadi 65

BANK OF TANZANIA MONETARY POLICY COMMITTEE STATEMENT