Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Phillip Isdor Mpango. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako.
Awali akizungumza kwenye hafla ya tuzo hizo Dk Mpango aliwahimiza waajiri wote kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na nafasi zao huku akibainisha kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha sera na sheria za nchi zinakidhi vigezo vya ajira na waajiriwa.
“Natambua pia juhudi za ATE katika kuhakikisha inasimamia vyema majukumu ya pande zote yaani baina ya mwajiri na mwajiriwa katika sehemu za kazi. Hatutaki malalamiko ya wafanyakazi yafike juu kabisa tunataka waajiri mtoe haki na stahiki za wafanyakazi wenu kwa mujibu wa miongozi iliyopo ” alisema.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Mkuu wa Idara wa Rasimali watu wa benki ya Exim, Bw Frederick Kanga alisema mfululizo wa tuzo hizo kutoka ATE ni kiashiria tosha mbele ya jamii kuhusiana na namna ambavyo benki hiyo imewekeza kwenye rasilimali watu, hatua ambayo ina umuhimu mkubwa katika kufanikisha malengo ya benki hiyo.
“Tuzo hizi kwetu ni mwendelezo wa sherehe zetu katika kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki yetu. Katika maadhimisho hayo agenda ya rasilimali watu ilikuwa ni moja vya vipaumbele vyetu na leo hii tunakamilisha rasmi sherehe hizo kwa tuzo hizi muhimu zinazothibitisha dhamira yetu ya uwekezaji kwa wafanyakazi wetu,’’ alisema Bw Kanga.
Alibainisha kuwa moja ya vipaumbele vya benki hiyo ni pamoja na kuwaandaa watendaji wake kwa kuwaongezea ujuzi unaowawezesha kuwa mbele ya wakati katika utendaji wao ili kuleta matokeo bora na yenye ubunifu mpya kwa wateja.
“Lengo ni kuifanya taasisi yetu iwe sehemu ambayo mfanyakazi anakuwa bora zaidi, mwenye mabadiliko na mwenye utofauti,’’ alisisitiza.
Kwa mujibu wa Bw Kanga benki hiyo imedhamiria kuandaa wafanyakazi wenye ushirikiano katika kuunda timu imara ya pamoja kwa kuandaa mazingira ambayo wafanyakazi hao watajihisi kuwa wanathaminiwa, wanashirikishwa sambamba na kupewa fursa ya kukua na kujiendeleza kitaaluma.

No comments:
Post a Comment