Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 7 December 2022

KAMPUNI YA KILOMBERO YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA ATE 2022

Dar es salaam - Kampuni ya Sukari ya Kilombero imefanikiwa kunyakua tuzo katika kipengele cha cha Uanagenzi na Mafunzo (Apprenticeship and Internship) huku ikishika nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) na kupokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla hiyo wakati wa tuzo za zitolewazo na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika Disemba 2, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdory Mpango (kulia) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Cleopatra Nasari, Mkuu wa Rasilimaliwatu Idara ya Kilimo wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero (katikati) kwa kudhamini hafla ya Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Desemba 2, 2022. Kushoto ni Mhe. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.
Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Joyce Ndalichako (kulis) akimkabidhi tuzo Meneja wa Maghala wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero (kushoto), Anthony Rweyemamu baada ya Kampuni kushinda nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City tarehe 2 Desemba 2022 ambapo kampuni hiyo ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa hafla hiyo.
Anthony Rweyemamu, Meneja wa Maghala wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero akipokea tuzo ya mshindi wa katika kipengele cha Uanagenzi na Mafunzo katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika tarehe 2 Desemba 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City ambapo kampuni hiyo pia ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kilombero Sugar Company Limited wakiwa katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika Desemba 2, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City. Kampuni hiyo ilitajwa kuwa mshindi wa kipengele cha Uanagenzi na Mafunzo, na Mshindi wa pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) na kupokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Masuala ya Biashara - Bruno Daniel, Mkuu wa Rasilimaliwatu Idara ya Kilimo - Cleopatra Nasari, Meneja wa Maghala Dar es Salaam/Morogoro - Anthony Rweyemamu na Mtafiti wa Masoko Lenin Rugaimukamu.

No comments:

Post a Comment