Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 2 December 2022

TANGA CEMENT YANYAKUA TUZO ZA NBAA MWAKA WA SITA MFULULIZO

Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Pieter de Jager (kulia), akiwa katikapicha ya pamoja na Maofisa wengine wa kampuni hiyo wakiwa wameshika Tuzo walizoshinda katika hafla ya utoaji tuzo wa Uandaaji na Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), ya mwaka 2021 katika hafla iliyofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamal Kassim Ali akikabidhi tuzo ya Mshindi wa kwanza kipengele cha wazalishaji viwandani katika tuzo za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), ya mwaka 2021 kwa Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Pieter de Jager katika hafla iliyofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Wengine kulia ni Maofisa wa Tanga Cement.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamal Kassim Ali akikabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika tuzo za za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), mwaka 2021 kwa kwa Mkuu wa wa Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela.

Baadhi ya Maofisa kutoka Tanga Cement wakiwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamali Kassim Ali (kushoto), akikabidhi Tuzo kwa Meneja Mauzo kitaifa wa Kampuni ya Tanga Cement, Mhandisi Leslie Masawe wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ambapo Tanga Cement ilishiriki kwenye maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam, Novemba 30, 2022.

Washindi wa jumla wa tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Washindi wa Kwanza wa tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021 (Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Tanga Cement PLC imeshinda tuzo za NBAA kwa mwaka wa sita mfululizo leo imeshinda Mshindi wa kwanza kipengele cha wazalishaji viwandani katika tuzo za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu (NBAA), ya mwaka 2021 kwa kufuata viwanga stahiki.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAAkilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Tanga Cement imeibuka na mshindi wa kwanza wa jumla katika tuzo za uandaaji na uwasilishaji Bora wa Taarifa za Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu (NBAA), mwaka 2021.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Pieter de Jager amesema tuzowalizopokea Tanga Cement zimetokana na kuendelea kutekeleza miongozo ya uandaaji wa mahesabu iliyowekwa na kuhakikisha kuwa tunaitekeleza ndani ya Tanga Cement.

“Ni kawaida yetu sisi kama Tanga Cement katika kutekeleza miongozo iliyowekwa ya waandaaji wa mahesabu hii tunaifurahia, inatuongezea shauku kubwa ya kuaminika kama wazalishaji bora viwandani.

Tanga Cement imekuwa ikiibuka na ushindi huu kwa mwaka wa sita sasa mfurulizo hii inatupa morali yakuendelea kujiamini pia kuendelea kuzalisha mali ghafi ili watumiaji wetu waendelee kutuamini nakufurahia bidhaa zetu alisema Pieter.

Aidha, Mkuu wa wa Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela amewataka wadau mbalimbali kuitumia Tanga Cement kwani ni vizuri kutambua kuwa kazi inayofanywa na Tanga Cement ni nzuri ndio maana hata imeweza kutwaa ushindi kwa mwaka wa sita mfululizo katika kutoa taarifa zake kwa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu (NBAA).

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mheshimiwa Jamali Kassim Ali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema.

“Kwa mujibu wa Sheria, vigezo vyetu vya ndani na vile vya Kimataifa ili kufanya hesabu zetu ziwe na ubora na watumiaji wake waweze kuzitumia na kufanya maamuzi yaliyosahihi, hilo ndio jambo kubwa ambalo ningependa kuwaasa viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali na zile za binafsi”

“Ukweli ni kwamba nimefurahia kuona washindi walioshinda leo pia niwapongeze kampuni ya Tanga Cement kwakutwaa tuzo ya jumla kwa wazalishaji bora viwandani kwa mwaka wa sita mfululizo hii inaonesha kuwa viwanda vyetu vinafanya vizuri katika uzalishaji pia utoaji wa taarifa za mahesabu.

Hata ukiangalia kwa mujibu wa idadi ya washiriki wa kila kipengele ni kubwa kwaiyo hata kumpata mshindi wa kwanza wa pili na watatu inaonyesha kwamba woteni washindi ila itakuwa ni tofauti ndogo ndogo.

No comments:

Post a Comment