Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa uhusiano kati ya Serikali na Benki ya Dunia unazidi kuimarika na kwamba watanzania watarajie maendeleo makubwa kupitia ushirikiano huo.
Dkt. Nchemba amesema hayo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kumpokea Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, aliyewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mwaliko wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuisaidia nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu, elimu, afya, mazingira na mingine mingi kupitia mpango wa mikopo nafuu wa dirisha la IDA 19 ambao umemaliza muda wake na pia nchi inatarajia kupata fedha nyingine za kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia dirisha jipya la IDA 20.
Blog Rebranding Teaser_030826
Stanbic Bank Banner_070826
Absa Loan Campaign_160426
Monday, 11 July 2022
BENKI YA DCB YACHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA UCHUMI WA BULUU VISIWANI ZANZIBAR
Friday, 8 July 2022
BENKI YA DCB YAZINDUA KAMPENI KUSHEREHEKEA MIAKA 20 YA MAFANIKIO JIJINI DAR ES SALAAM
Benki ya Biashara ya DCB imezindua kampeni kusherehekea miaka 20 ya mafanikio tokea ilipoanzaishwa huku Mkurugenzi Mtendaji wake, Godfrey Ndalahwa akianisha mambo kadhaa yakiwemo mafanikio na mipango ya baadae akisema yafuatayo akizungumza na waandishi wa habari;
Kama mnavyofahamu benki yetu inasherehekea miaka 20 tokea kuanzishwa kwake kipindi hicho ilipoanzishwa mwaka 2002 ikijulikana kama benki ya Kijamii ya Dar es Salaam (Dar es Salaam Community Bank), kutimiza maono ya Rais wa Awamu ya tatu, Hayati Benjamin William Mkapa kufuatia kilio cha wajasiriamali wakazi wa Dar es Salaam kukosa huduma za kifedha hususani mikopo baada ya kukosa vigezo katika taasisi nyingi za fedha, kwa kipindi hicho benki ilianza na mtaji wa shs bilioni 1.7.
Mafanikio tunayojivunia ni makubwa na ninapenda kuchukua fursa hii kuainisha baadhi ya mafanikio hayo: Ikumbukwe kuwa DCB ilikuwa benki ya kwanza kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) baada ya kutimiza vigezo na masharti ya mamlaka mbalimbali za udhibiti hapa nchini. Kuorodheshwa katika soko la hisa haikuwa tu fursa kwa umma kumiliki benki na kutengeneza faida iliyotokana na gawio pamoja na kuuza na kununua hisa, bali imekuwa fursa kubwa zaidi kwa benki kuongeza mtaji pindi unapohitajika. Niwashukuru sana wanahisa wetu kwa kuendelea kushiriki katika mazoezi ya uuzwaji wa hisa jambo ambalo limesaidia kukuza mtaji wa benki yetu kutoka shilingi bilioni 1.7 hadi kufikia shilingi bilioni 30 hivi sasa. Mtaji huu umeiwezesha benki kukidhi masharti ya benki kuu ya kujiendesha kama benki ya biashara na kuiongezea benki yetu uwezo mkubwa wa kushindana katika soko.
Mwaka 2012 benki yetu ilifanikiwa kuhuisha leseni kutoka kwenye benki ya jamii na kuwa benki kamili ya biashara ambayo imepanua wigo kwa benki yetu kuweza kushindana katika soko ikihudumia wateja wadogo, wa kati na wakubwa. Katika kufanikisha hayo, benki iliweza kufungua matawi 9, na mawakala zaidi ya 700 maeneo tofauti nchini. Benki yetu pia haikuwa nyuma katika kuanzisha mifumo ya kidijitali ambayo kwa sasa ndio ushindani wa soko ulipo, hivyo mnamo mwaka 2016, benki ilianza kutoa huduma za kibenki kwa njia ya simu na mtandao na imeendelea kuboresha huduma hizo kadri teknolojia inavyozidi kubadilika. Huduma hizi za Kidijitali zimewezesha kufikia wateja wengi zaidi kwa muda mfupi hivyo kurahisisha shughuli za utoaji huduma.
BENKI YA NMB YAZINDUA TAWI LA 227, YASAIDIA SERIKALI KUKUSANYA 8.6TRN/-
Akizungumza kabla ya ufunguzi rasmi wa tawi hi hilo Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw. Filbert Mponzi, alisema kati ya mwaka 2019 na 2021, NMB iliisaidia serikai kukusanya mapato yenye thamani ya TZS trilioni 8.6.
Akifafanua mchango wa NMB katika juhudi za maendeleo za serikali, Bw. Mponzi alisema sasa hivi Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) una zaidi ya taasisi 1,100 zilizounga mifumo yake kwenye mifumo ya NMB ya ukusanyaji wa mapato.
Aidha alisema kuwa pamoja na mtandao mpana wa matawi, pia NMB imeendelea kutumia tekinolojia kufikisha huduma zake kwa watanzania wengi zaidi na kulihudumia taifa kwa ujumla.
Bw. Mponzi alisema tawi hilo jipya ambalo ni la 13 mkoani Mwanza na 38 Kanda ya Ziwa, ni tawi kamili lenye huduma zote za kibenki, zikiwemo zile za mikopo kama kuwakopesha wakulima.
NMB imekuwa mstari wa mbele katika jitahada za serikali za kuimarisha kilimo nchini na tayari imetoa mikopo ya kilimo ya TZS bilioni 100 kwa riba nafuu.

Wednesday, 6 July 2022
SBL YAONGOZA VIONGOZI NA WAKAZI WA DODOMA MJINI KWENYE ZOEZI LA UPANDAJI MITI
Dodoma, Julai 6, 2022 – Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa mara ya pili imeungana na viongozi pamoja na wananchi wa eneo la hospitali ya Akili ya Taifa Mirembe mkoani Dodoma katika zoezi la upandaji maelfu ya miti ikiwa ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo wa kukabiliana na ukame.
Katika kuonyesha jitihada za makusudi za kukabiliana na ukame na kutunza mazingira, Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde, Katibu wa Afya Hospital ya Taifa ya Akili Mirembe, Jackson Mjinja, viongozi wa jeshi na magereza ni baadhi ya viongozi walioshiriki katika zoezi hilo la upandaji miti lililoandaliwa na SBL kwa kushirikiana na asasi isiyo ya Kiserikali ya Habari Development Association (HDA).
Akiongea wakati wa zoezi hilo, mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema upandaji miti katika hospitali ya Mirembe ni sehemu ya mkakati endelevu wa kampuni hiyo unaolenga kupanda maelfu ya miti sehemu mbali mbali hapa nchini.
Mkurugenzi huyo alisema mwaka 2019 kampuni ya SBL ilipanda miti katika wilaya za Same Pamoja na Moshi ili kuongeza uotokatika maeneo ya jirani na mlima Kilimanjaro.
“Upandaji miti wa SBL hapa unaendeleza jitihada zingine zilizofanya katika mikoa tofauti nchini na kampuni, ikiwemo wilayani Kongwa mwaka jana, ambapo SBL ilipanda maelfu ya miti” alisema Ocitti.

Tuesday, 5 July 2022
TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKI MAONESHO YA 46 YA BIASHARA SABASABA
Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Joanitha Deogratias (wa pili kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo.
Afisa Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Cornel Mlay (kulia), akizungumza na mmoja ya mteja alietembelea banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo. Katikati ni Afisa Uwendeshaji wa Benki hiyo, Godbright Mlay.
Afisa Uendeshaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Salha Singano (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa mmoja ya mteja alipotembelea Banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo. Kushoto ni Afisa wa Kitengo cha ICT, Joseph Bukuru.
Meneja Uhusiano wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Shilla Senkoro (kushoto), akizungumza na mteja kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo.Akizungumza kwenye maonyesho hayo, Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo wa benki hiyo Joanitha Deogratias alisema benki imejidhatiti katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wengi kwa kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.
“Tunatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na wale wakubwa pia mikopo kwa wastaafu kwa ajili ya kuendeleza shughuli ndogondogo za kiuchumi.
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA TAWI JIPYA BUKOBA
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Moses Machali (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank lililozinduliwa katika Wilaya hiyo hivi karibuni ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuhakikisha inawafikia wateja wake kila kona ya nchi. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial, Sabasaba Moshingi, Mkurugenzi Rasilimali watu, Diana Myonga pamoja na Mkurugenzi wa Mikopo, Henry Bwogi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Benki hiyo lililozinduliwa katika Wilaya ya Bukoba hivi karibuni ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuhakikisha inawafikia wateja wake kila kona ya nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Moses Machali akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Sabasaba Moshingi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Benki hiyo mara baada ya uzinduzi wa Tawi hilo.

PRESIDENT SAMIA CALLS FOR RED TAPE CURE
![]() |
| President Samia Suluhu Hassan witnesses the signing of two contracts, including one for the construction of lot four, Tabora - Isaka Standard Gauge Railway at State House in Dar es Salaam on Monday. |
"In some instances, these legislations take us backward instead of moving us forward. It is high time these laws are reviewed in order to hasten decision making in undertaking investment projects. We should not be slaves of our own laws", President Samia directed.
The Head of State made the directives at State House in Dar es Salaam on Monday, shortly after witnessing the signing of two contracts including one for construction of lot four of Standard Gauge Railway (SGR) stretching 168 kilometres between Tabora and Isaka.
The other contract was between Tanzania Railways Corporation (TRC) and Korea National Railway (KORAIL) for capacity building of Tanzanians, who will be tasked with operating railway services once the SGR is completed.
Construction of the Tabora - Isaka section, which is part of phase one of the SGR between Dar es Salaam and Mwanza covers a total of 1,219 kilometres and will cost 900.1 million US dollars (about 2.094 trillion).
Monday, 4 July 2022
BRANCH KUFIKISHA MIKOPO YA HARAKA KWA WATANZANIA
Branch, kampuni inayoongoza duniani kwa utoaji mikopo kwa watu binafsi kwa njia ya simu za mikononi, imeelezea nia yake thabiti ya kuwafikishia huduma za kifedha za gharama nafuu mamilioni ya Wanzania popote pale walipo.
Tangu kuanzishwa kwake hapa nchini mwaka 2015, Branch tayari imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 73 na kuwafikia zaidi ya watu milioni moja na laki tano walipo sehemu mbali mbali.
Mikopo ainayotolewa na Branch kupitia App yao inaanzia kiasi cha shilingi 5,000 hadi shilingi 1,000,000.
Akiongea na wahariri wa vyombo vya Habari, msimamizi wa huduma kwa wateja kwa Tanzania Reuben Wanyamawi, alisema Branch imejipanga vyema kuwafikishia huduma za mikopo Watanzania popote pale walipo na muda wowote hivyo kuwezesha kutatua changamoto zao zinazohitaji fedha.

MITANANGE AFCON YA WANAWAKE NDANI YA DStv
Soka linaendelea!
Ratiba ya Africa Women Cup Of Nations (AWCON) Jumatatu na Jumanne hii kupitia chaneli za SuperSport.
Mechi hizi zitaruka kupitia @dstvtanzania pekee.
Piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema ufurahie michuano hii.
#DStvEwaaaaah

SPEECH BY THE FIRST FEMALE CHAIRPERSON OF EAST AFRICAN BUSINESS COUNCIL, MS. ANGELINA NGALULA
Our special Guest,
Diplomat, development partners, I wish to recognize the Presence of Mohammed Attaya from the Egyptian embassy, Ms. Neema the country director for TradeMark East Africa and my brother Shammy from TradeMark East Africa.
Members from Government institutions, I recognize the presence of my dear brothers Mr. Masanja Kadogosa – TRC DG, Eric Hamis – TPA DG, Mussa Mbura – TAA DG, Dr. Gift Kweka from AG office, and my sister Anna Haule.
We have our friends from the Parliament; Waheshimiwa Wabunge wadau wa Sekta Binafsi, Mh. Mariam Ditopile and Mh. Catherine Magige.
TPSF Vice Chair – Paul Makanza.
TPSF Board Members.
TPSF & EABC Corporate Members.
EABC Executive Director – Mr. John Bosco.
TPSF Acting Executive Director – Mr. Raphael Laizer.
All invited guests.
I’m so delighted and overwhelmed by showers of love and words of encouragement coming from you and from every angle. I thank you all for spending your quality time with us here today and I also wish to thank TPSF Secretariat for the excellent coordination and my special appreciation the Management of Yatch Club Yatch for allowing TPSF to host this event here.
We could not be here today if it was not for the EABC members who supported and for me voted me and my Colleagues Mr. Paul Makanza CTI Chairman, Dr Jackline Mkindi TAHA CEO and Ali Amour Zanzibar Chamber of Commerce President it has been a blessing to work with you.

Friday, 1 July 2022
VODACOM YAKABIDHI VIFAA KWA SHULE YA WASICHANA
| Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakitoa burudani ya ngoma za asili wakati wa kampuni ya Vodacom walipokwenda shuleni hapo kwa ajili ya kutoa misaada ya vifaa mbalimbali. |
Vodacom Tanzania Yakabidhi Vifaa kwa Shule ya WasichanaVodacom Tanzania Foundation leo imekabidhi vifaa na samani kwa Shule ya Wasichana ya Bethsaida mjini Dar es Salaam ambavyo kampuni ilishinda katika mashindano ya makampuni ya Vodacom duniani.
Akiongea wakati wa makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Vivienne Penessis alisema, “Elimu ni msingi pekee ambao unampatia mtu kianzio cha kujenga miasha bora.
Hii ni kweli zaidi kwa Watoto yatima ambao tegemeo lao ni elimu pekee.”Shule ya Wasichana ya Bethsaida ilichaguliwa kupokea msaada huu kwa kuwa ni moja ya shule chache zinazotoa elimu ya sekondari kwa Watoto yatima wa kike nchini.
Mkurugenzi wa Vodacom pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni waliikabidhi shule hiyo viti 100, vitabu Zaidi ya 300 pamoja na vifaa 20 vya kuzalisha umeme wa jua. Bi penessis alielezea Imani yake kuwa msaada huo utatumika ipasavyo kwani kampuni ya Vodacom ilijiridhisha juu ya utaalam na moyo wa kujitoa wa wafanyakazi wa shule ya Bethsaida.
CRDB, USAID NA DFC KUTOA SHILINGI BILIONI 100 KWENYE SEKTA YA ELIMU, AFYA, BIASHARA NDOGO NA KATI PAMOJA NA SEKTA ZISIZO RASMI TANZANIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) kwa pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright wakionyesha hati za makubaliano ya mikopo ya uwezeshaji yenye thamani ya Bilioni 100 kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC kwa ajili ya kuiwezesha Benki hiyo kukopesha sekta mbalimbali nchini zikiwemo Sekta ya Ujasiriamali, kwa maana ya wajasiriamali wadogo na wakati (MSMEs), Sekta ya Elimu, Sekta ya Afya na biashara zisizo rasmi, muda mfupi baada ya kuzisaini katika hafla fupi iliyofanyika kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam. Picha zote na Othman Michuzi.
Dar es Salaam, Juni 30 2022: Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald J. Wright amethibitisha nia ya Serikali ya Marekani katika kuimarisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia ushirikiano mpya uliosainiwa katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC.
Kupitia ushirikiano huo, Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC yatashirikiana na Benki ya CRDB kuwezesha mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 100 za kItanzania. Ushirikiano huo utaiwezesha Benki ya CRDB kutanua wigo wa uwezeshaji wa mikopo wa wanawake na vijana sambamba na kutoa mikopo zaidi katika sekta za elimu, afya na sekta zisizo rasmi Tanzania nzima.
"Benki ya CRDB inayo furaha kubwa kufanya kazi na USAID na DFC katika kusaidia biashara ndogo nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright wakisaini hati ya makubaliano ya mikopo ya uwezeshaji yenye thamani ya Bilioni 100 kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC kwa ajili ya kuiwezesha Benki hiyo kukopesha sekta mbalimbali nchini zikiwemo Sekta ya Ujasiriamali, kwa maana ya wajasiriamali wadogo na wakati (MSMEs), Sekta ya Elimu, Sekta ya Afya na biashara zisizo rasmi. Hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.
Biashara hizi ndogo na za kati ni muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania na tunaamini ushirikiano huu sio tu utasaidia kutanua wigo wetu wa kukopesha lakini pia kuwawezesha wafanyabiashara kwa kuwashauri na kuhakikisha wanafanya biashara kisasa kwa kutumia teknolojia. Lakini kubwa zaidi katika ushirikiano huu ni nia yetu ya kuwapa motisha wafanyabiashara wanawake na vijana katika safari yao ya ujasiriamali," alisema Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.
"Serikali ya Marekani inatambua kuwa hakuna chombo peke kinachoweza kutatua changamoto za Tanzania hivyo tunafurahi na kusheherekea mikataba hii miwili na Benki ya CRDB ambayo itaongeza ushirikishwaji wa kifedha na uwezeshaji kwa makundi muhimu kama vile wanawake na vijana," alisema Dkt. Donald J. Wright, Balozi wa Marekani nchini Tanzania.
Ushirikiano huu unalenga kuboresha maeneo yafutayo;
Dar es Salaam, Juni 30 2022: Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald J. Wright amethibitisha nia ya Serikali ya Marekani katika kuimarisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia ushirikiano mpya uliosainiwa katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC.
Kupitia ushirikiano huo, Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC yatashirikiana na Benki ya CRDB kuwezesha mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 100 za kItanzania. Ushirikiano huo utaiwezesha Benki ya CRDB kutanua wigo wa uwezeshaji wa mikopo wa wanawake na vijana sambamba na kutoa mikopo zaidi katika sekta za elimu, afya na sekta zisizo rasmi Tanzania nzima.
"Benki ya CRDB inayo furaha kubwa kufanya kazi na USAID na DFC katika kusaidia biashara ndogo nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright wakisaini hati ya makubaliano ya mikopo ya uwezeshaji yenye thamani ya Bilioni 100 kati ya Benki ya CRDB na Mashirika ya Kimarekani ya USAID na DFC kwa ajili ya kuiwezesha Benki hiyo kukopesha sekta mbalimbali nchini zikiwemo Sekta ya Ujasiriamali, kwa maana ya wajasiriamali wadogo na wakati (MSMEs), Sekta ya Elimu, Sekta ya Afya na biashara zisizo rasmi. Hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam."Serikali ya Marekani inatambua kuwa hakuna chombo peke kinachoweza kutatua changamoto za Tanzania hivyo tunafurahi na kusheherekea mikataba hii miwili na Benki ya CRDB ambayo itaongeza ushirikishwaji wa kifedha na uwezeshaji kwa makundi muhimu kama vile wanawake na vijana," alisema Dkt. Donald J. Wright, Balozi wa Marekani nchini Tanzania.
Ushirikiano huu unalenga kuboresha maeneo yafutayo;
- Mikopo katika Sekta ya Afya: Benki itatoa mikopo ya hadi Shilingi Bilioni 20.3 katika sekta ya afya. Mikopo hii itatumika kusaidia katika ujenzi wa mahospitali, vituo vya afya, kliniki, vituo cha uchunguzi wa afya, maduka ya madawa na huduma za uzazi pamoja na ununuzi wa vifaa ya matibabu na ujenzi au ukarabati wa maeneo ya kutolea huduma za afya.
- Mikopo katika Sekta ya Elimu: Benki itatoa mikopo ya hadi Shilingi Bilioni 37.5 katika sekta ya elimu kusaidia katika mnyororo wa thamani wa elimu ikiwemo uanzishwaji wa elimu isiyolenga kupata faida, shule za msingi na sekondari zinazolenga misingi ya imani ya dini ambazo zitahudumia sekta ya elimU sambamba na utoaji mikopo kwa biashara zinazolenga kutoa upatikanaji wa vifaa vya elimu.
- Mikopo kwa Biashara Ndogo na Kati: Benki itatoa hadi Shilingi Bilioni 17.9 katika sekta ya biashara ndogo na kati. Benki itajikita katika biashara za sekta zote za uchumi kusaidia katika mitaji ya uendeshaji, manunuzi ya vifaa, ujenzi na ubadilishwaji wa sehemu za biashara ili kukuza biashara.
- Mikopo kwa Sekta zisizo Rasmi: Benki itatoa hadi Shilingi Bilioni 23.1 kusaidia biashara zisizo rasmi kutoka katika sekta zote za uchumi ambapo kipaumbele kitakua kwenye biashara zinazoendeshwa na vijana na wanawake.
GEITA GOLD MINING LTD. PROMISES TO CONTINUE THE FIGHT AGAINST HIV / AIDS
GGML has also pledged to continue working with the Government through TACAIDS and other stakeholders to advance the fight against HIV and AIDS to achieve the three zeros.
Three zeros targets mean a complete reduction to zero per cent of new infections, zero stigmas as well as zero in AIDS-related deaths.
The statement was made yesterday, June 29, 2022, in Dodoma by GGML Senior Co-operative Manager, Manace Ndoroma, addressing the media about launching the GGM Kili Challenge campaign for 2022.
The statement was made yesterday, June 29, 2022, in Dodoma by GGML Senior Co-operative Manager, Manace Ndoroma, addressing the media about launching the GGM Kili Challenge campaign for 2022.
The campaign, launched by GGML in 2002, aims to fund the fight against HIV and AIDS by raising funds to assist the Tanzanian government in its efforts to achieve the three zeros.
MASKANI POA NDANI YA DStv KILA IJUMAA USIKU
Furahia stori kali kutoka kipindi nambari moja cha Maskani Poa kinacholetwa na baba Levo na Shilole kila siku ya Ijumaa saa 3:00 usiku.
Maskani Poa ni ndani ya Maisha Magic Poa, namba 144 kwa TShs 9,900 tu.
Piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema!
#DStvEwaaaaah
Maskani Poa ni ndani ya Maisha Magic Poa, namba 144 kwa TShs 9,900 tu.
Piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema!
#DStvEwaaaaah
#UsichukuliePoaVituvyaPoa
Subscribe to:
Posts (Atom)

.jpg)