Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Saada Mkuya (katikati), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa katika mkutano aliouandaa akiwashirikisha wakuu wa taasisi mbalimbali za fedha za bara na visiwani kujadili fursa mbalimbali za kifedha zipatikanazo katika kampeni ya uchumi wa buluu iliyoasisiwa na Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi. Uchumi wa Buluu ni dhana inayohusisha uchumi unaojijenga katika Utalii, Uvuvi, Mafuta, gesi na viwanda vinavyotumia malighafi za bahari. |
No comments:
Post a Comment